One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

Zitto hivi ukiwa unafanya siasa unawachukuliaje watanzania. Je unawaona kama ni watu wajinga wakuambiwa na kukubali chochote tu? Kaa utafakali kwa kina sana watanzania leo wanauwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kumpima mtu na kujua shamiri ya mtu huyo. Ni dhairi kabisa zitto una ajenda ya siri imejificha nyuma ya act ukatae muda si mrefu utaumbuliwa na matendo yako. Ni maajabu mpinzani wa kweli kutwa kucha anasifiwa na chama tawala hiyo ni ishara tosha kuwa kuna kitu mnashare na ccm unaweza kubisha lakini kuuficha ukweli ni sawa na kuzuia jua lisionekane. Act dhamira yake kubwa ni kuvuruga upinzani kwa maana nyingine ni wakala la CCM bisha kataa lakini ukweli utadhihiri muda utakapofika.
 
Kimweri,

Kinachonitatiza mimi ni viongozi wa vyama vyote vya Upinzani kushindwa kujieleza ama kujibu maswala muhimu yanayohusu chama, Itikadi zao na sera zao, sasa sijui wanategemea wananchi ni wajinga kiasi gani ama hawapaswi kujua malengo yao. Wote sasa kwa pamoja wametumia siasa za lazima CCM itoke madarakani na wanapigania nani atashika kiti cha juu.

UKAWA ikiongozwa na CDM ndio kabisaa kazi ni kutafuta WASALITI wanaopingana na maamuzi ya viongozi juu ya Utawala na sii lengo la pamoja halafu wanategemea nguvu ya Umoja huo itatokana na mawazo ya wachache wenye madaraka ya vyama. Na Shida zetu ndizo zimekuwa ahadi kubwa za siasa za vyama vyote iwe Elimu, Afya, Maji, Umeme, vifo vya watoto, wenye Ulemavu wa ngozi yaani tumerudi nyuma katika siasa za KUPIGANIA UHURU, wamesahau kabisa kama kuna Demokrasia ambayo ni wananchi ndio wenye nguvu na ridhaa ya wawapa vyama mamlaka ya kuongoza.

Na ndio maana siasa za sasa wanajitokeza kina Che Guevala. Wenye akili saana za kumuondoa CCM madarakani pasipo kutumia mtutu wa bunduki ila kwa kupitia sanduku la Kura. Halafu wakija shindwa Uchaguzi itakuwa lawama kwa wananchi, ni wajinga na wapumbavu kuendelea kuichagua CCM. Alaa kumbe vita sio yenu ila ni ya wananchi?. Viongozi wameshindwa kuelewa kwamba wananchi wenyewe ndio silaha, ndio wenye maamuzi na sii Mbowe wala Zitto anamtaka nani na nani awe naye ktk kundi lake.

Hizi siasa za majitaka hazitawasaidia Chadema wala ACT kama watashindwa kuwashawishi wananchi mrengo wao, sera zao, ilani zao na hata kujifafanua juu yao maana nimeuliza tu juu ya Azimio la Arusha na ACT wamekimbia wote ilihali Azimio la Arusha liliundwa kwa sababu CCM ilikuwa chama tawala na misingi yote ya Miiko na Maadili iliwekwa kwa kutazama nafasi ya CCM kama chama Tawala. Niliuliza makusudi kuelewa kama kweli chama hiki wanajua wanachokitaka na watafuata misingi hiyo.

Hivyo nilitegemea pengine viongozi wa ACT wangenambia wao wanalifuata Azimio Hilo sii kwa muundo wa chama ama masharti kwa viongozi wa Chama maana wametenganisha uongozi wa chama na Kitaifa. na kwamba miiko na maadili ya viongozi ni kwa viongozi wa NCHI, yaani kama wakipewa ridhaa ya kuongoza nchi basi Chama kitahakikisha kila kiongozi wake hataruhusiwa kuwa na nyumba ya kupangisha, mishahara miwli na kadhalika.

- Wameshindwa..
 
Zitto asitufanye mambulula humu;
Vitendo huongea zaidi kuliko maneno.Ushahidi wa kimazingira unaonesha wazi kuwa ACT imekuja kuvuruga upinzani,
PERIOD!!!!
 
Last edited by a moderator:
Huwa najizuia sana kuchangia threads kama hizi lakini wakati mwingine unalazimika. Issue siyo kwamba Zitto hajui anachofanya, anajua sana. Tatizo ni pale anapodhani watanzania hawana akili. Zitto ameanza usaliti 2006, watanzania wanajua. Kama amekuwa msaliti miaka 9 anahitaji zaidi ya miaka 10 kuwaaminisha watanzania anachotaka waamini.

Hatuwezi kudharau anachofanya lakini ajue kazi si rahisi kama anavyodhani. Anaweza kupata wabunge hata watatu hata wanne, lakini naamini ACT itakufa hata ukitaka kuweka kiberiti niweke nyumba.
 
Nini maana ya MSALITI?
 
haya bwana zito sisi wananchi wazalendo ambao chama chako kinatulenga tunakusubiri utufungue hii minyororo....Comrade
 
Zito nakukumbuka zaid nikikumbuka mapinduzi yako hadi Nyerere lecture theaters zikajengwa UDSM.
pia nakukumbuka zaid kwamba wewe kwenye uanzishwaji wa bodi ya mikopo SLB na yaliyotokea.

kwahaya yote nakupongeza kwaqsabb kwanza ulikuwa hueleweki lkn mwishoni sana umekuja kueleweka kwa njia ngumu sana

naomba nikwambie jambo moja kubwa ambalo ni mapungufu uliyo nayo, mie kwa mtazamo wangu naona kwamba huwa unatumia njia ngumu sana kufundisha watu na kwa njia hii huwa unajichumia maadui zaid kuliko marafiki.

kutokana na hali hiyo kwenye siasa hsa za chama kichanga mtadondokea pua. Unatakiwa ujimudu uweze kufanya siasa lkn kwa njia ambayo inaeleweka/ itaeleweka miongoni mwa walio wengi hata kama sio wote. mfano mzuri leo hii ACT inaonekana kama ni mwiba kwa upinzani na hii ni kutokana na mbinu zako unazotumia.

kwaalaiye wahi kuwa na wewe kwenye siasa zile za miaka ile nafkiri watu kama akina Ruge watakuelewa sana ama watu kama akina Flaviana lkn sio watu wagen kwako. hebu jaribu kurekebisha hali hii ili usomeke mapema zaid kwa mifano rahisi zaid
 
Nini maana ya MSALITI?

CDM msaliti ni yeyote asiyesikilizana na Mbowe na Slaa, au yoyote mwenye mtazamo tofauti,mambo ya ajabu kabisa.

CDM tuliyokuwa tunaipa sapoti ya nguvu humu circa 2006-7 sio hii ya leo iliyojaa watoto wasiojua hata kuunga sentensi mbili za kiswahili. Nasikitishwa sana na hii hali, sijui kwanini uongozi wa CDM waliacha hali ikafikia kwenye hatua hii bila wao kufanya damage control.

Sasa hivi imekuwa haiwezekaniki kujadili mada na vijana wa CDM kabla hawajaanza kutoa lugha za maudhi na kero.Yani kila akiandika sentensi mbili, anaanza wewe msaliti, wewe msaliti.yani hopeless kabisa.
 
Kamwe, Never hatuwezi kuiondoa ccm madarakani kwakuanzisha vyama kiholela. Tunahitaji kuunganisha nguvu za upinzani. Siasa sio kigodoro kwamba ukiweka taarabu mzuriiiii ndo utajaza watu kwenye unyago wako.

Sio kweli, Uingereza kwa miaka mingi sana Consevatives na Labour wamekuwa wakihodhi madaraka, na as long as chama kimoja kilikuw ana uhakika wa kushinda kutokana na umaarufu wa sera za kwa kipindi hicho, basi matakwa ya wananchi hayakusikilizwa, sasa hivi imekuwa tofauti baada ya kuja vyama mbadala ambavyo vimekuwa na kufikia hatua ya kubadilisha maamuzi ya chaguzi kuu,sasa hivi kina Cameron hawakon complacent tena.

Demokrasia za vyama viwili kama amrekani ni mbovu kuliko kuwa na chama kimoja, kwani kunakuwa na illusion of choice, Kama CDM wanaogopa uwepo wa vyama vingi kuipinga CCM, mbona hawakuwahi kulalamika uwepo wao,wakati wao wakiwa sio chama kikuu cha upinzani?ingekuwa busara wangeungana na CUF 2000 au 2005 wakati huo ngangari ngangari kweli. CUF walikaa kimya wakati CDM walivyokuja juu na kupoka umaarufu wao,na mimi binafsi nilishukuru kwa kuwa aina ya siasa zilizokuwa zinaendeshwa na CUF hazikuwa inclusive kwa baadhi ya Jamii.

Kuhusu ACT, mie nawashauri CDM mkipuuze, kama hawana hoja watakufa kifo cha mende muda si mrefu, kama hoja zao ni nzito na wananchi wakawapenda na kuwapa ushirikiano, basi mkubali hizo ndio siasa za ushindani. Mnachokifanya sasa hivi ni sawa na mwanariadha anayetaka kushindanishwa na mtu wa pili peke yake, kwa kuwa hataki wa-3 kurudi nyuma nao washiriki,hai-make sense. Kama mnaamini kasi ya CDM,ACT wataendelea kuwa nyuma yenu milele.

Mnasema wanakuja kugawa kura za upinzani, watagawaje kura za upinzani, wakati ACT ni chama chenye sera za Ujamaa?sera ambazo, mabaki yake mengi yako CCM? CDM haijawahi kuweka wazi ni chama cha mrengo upi, ingawa ukitazama ni kama kimeegemea ubepari kiasi, kwa kuwatazama viongozi wake n.k

wekeni sera za CDM wazi, iteni wananchi wanaowafuata kwa kufuata sera zenu. Period.

Acheni kulalama kama watoto wadogo. Mkue, ili hata ukiitishwa mdahalo wa Kitaifa viongozi wa vyama waongee kuhusu sera za vyama vyao,sio flani msaliti wa hiki na kile, ni upuuuzi kujadili siasa za kjinga kwa nchi masikini kama TZ.
 
CDM msaliti ni yeyote asiyesikilizana na Mbowe na Slaa, au yoyote mwenye mtazamo tofauti,mambo ya ajabu kabisa.

CDM tuliyokuwa tunaipa sapoti ya nguvu humu circa 2006-7 sio hii ya leo iliyojaa watoto wasiojua hata kuunga sentensi mbili za kiswahili. Nasikitishwa sana na hii hali, sijui kwanini uongozi wa CDM waliacha hali ikafikia kwenye hatua hii bila wao kufanya damage control.

Sasa hivi imekuwa haiwezekaniki kujadili mada na vijana wa CDM kabla hawajaanza kutoa lugha za maudhi na kero.Yani kila akiandika sentensi mbili, anaanza wewe msaliti, wewe msaliti.yani hopeless kabisa.

Tukana upendavyo...Lakini hawa vijana wa Chadema unaowatukana hapa ndiyo wapiga kura wenyewe.Ndiyo wameifanya Chadema kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.Ndiyo wameipa Chadema wajumbe wengi wa mitaa na vijiji...

Tuwaone nyie mnaojifanya wasomi uchwara na chama chenu cha usaliti mtafika wapi.
 
Tunacholaani sisi ni CCM kuanzisha matawi yake kuhujumu upinzani kama walivyofadhili uanzishwaji wa ACT
 
Na hapa ndipo Chadema inapokosa mwongozo maana USALITI wa CDM sasa hivi umepachikwa kuwa Usaliti wa TAIFA. Ukipingana na Chadema kwa lolote lile wewe ni msaliti wa TAIFA kana kwamba Chadema ndio mwongozo wa nchi na imenisikitisha hadi viongozi wanatumia lugha hii. Wewe unaomba ridhaa ya wananchi leo unakuwa mstari wa mbele kuhukumu wengineo ambao wana haki sawa na wewe Kidemokrasia!.

Na kibaya zaidi kama nilivyoeleza huko nyuma, kama kweli kuna Usaliti basi Mzee Mtei alikuwa Msaliti maana hakukubaliana na Nyerere, msaliti alikuwa Mzee Malechela ambaye hakukubaliana na CCM juu ya Serikali 3. Msaliti alikuwa Mrema, Seif Sharrif na hata Lowassa ambaye leo anagombea Urais. Wasaliti ni Ukawa maana hawakubaliani na katiba iliyopo na wakaendelea kuitumia kudai uongozi.

Lakini huu Usaliti umekuja onekana kwa kina Kitila tu kwa sababu za Kichama. Na mijinga imeingizwa katika ushirikina huu maana uchawi sio lazima utumie tunguli, mifupa na manyanga bali Uchawi ni dhamira na roho mbaya inayowatakia maafa wengine - Adui yako muombee kifo, na ndio maana mimi husema - Uchawi upo!
 
Naona msaliti Zitto kalala mbele,
Bro kwa upepo wa maswali tu ya hapa JF kwako pima mwenyewe.Kiukweli una wakati mgumu saaaaana na ACT yako.!!!!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Tunacholaani sisi ni CCM kuanzisha matawi yake kuhujumu upinzani kama walivyofadhili uanzishwaji wa ACT

Unalaani kitu gani sasa?kama ngoma inachezwa na CCM nyie CDM inawahusu vipi? Kinachoonekana hapa ni ukosekanaji wa focus. Kama mnachoongea kina ukweli wa kimantiki, kwa nini na nyie msianzishe matawi ya CDM ndani ya CCM?

Je mnafikiria kwa kuchokonoa wanachokifanya CCM wananchi ndio wataridhika na CDM?kazi ya CDM ni kuchokonoa matendo ya CCM au kuwaeleza wananchi wa TZ mbadala wa kisera na aina ya Tanzania mara baada ya CDM kupewa nchi?
 
Tukana upendavyo...Lakini hawa vijana wa Chadema unaowatukana hapa ndiyo wapiga kura wenyewe.Ndiyo wameifanya Chadema kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.Ndiyo wameipa Chadema wajumbe wengi wa mitaa na vijiji...

Tuwaone nyie mnaojifanya wasomi uchwara na chama chenu cha usaliti mtafika wapi.

Moja, mimi sio mwanachama wa ACT, wala sijawahi kuwa mwanachama wa CDM, may be niliwahi kuwa mwanachama wa CCM miaka hiyo enzi za nyerere by default.

Acha kuchanganya mambo, jibu hoja sio kukimbilia kufunua personality ya Kimweri ni nani.

Hakuna Tusi hata moja nililoandika, acha kuhamaki na kuweweseka,

Tafuta Tusi kwenye nilichoandika, ukilikosa jua umeishiwa hoja.

--- Nilichokiandika kabla ----

CDM msaliti ni yeyote asiyesikilizana na Mbowe na Slaa, au yoyote mwenye mtazamo tofauti,mambo ya ajabu kabisa.

CDM tuliyokuwa tunaipa sapoti ya nguvu humu circa 2006-7 sio hii ya leo iliyojaa watoto wasiojua hata kuunga sentensi mbili za kiswahili. Nasikitishwa sana na hii hali, sijui kwanini uongozi wa CDM waliacha hali ikafikia kwenye hatua hii bila wao kufanya damage control.

Sasa hivi imekuwa haiwezekaniki kujadili mada na vijana wa CDM kabla hawajaanza kutoa lugha za maudhi na kero.Yani kila akiandika sentensi mbili, anaanza wewe msaliti, wewe msaliti.yani hopeless kabisa.
 
Unalaani kitu gani sasa?kama ngoma inachezwa na CCM nyie CDM inawahusu vipi? Kinachoonekana hapa ni ukosekanaji wa focus. Kama mnachoongea kina ukweli wa kimantiki, kwa nini na nyie msianzishe matawi ya CDM ndani ya CCM?

Je mnafikiria kwa kuchokonoa wanachokifanya CCM wananchi ndio wataridhika na CDM?kazi ya CDM ni kuchokonoa matendo ya CCM au kuwaeleza wananchi wa TZ mbadala wa kisera na aina ya Tanzania mara baada ya CDM kupewa nchi?

ukiulizwa sera ya tanzania kwa kipindi cha 2005-15 utajibuje arawa
 
Unalaani kitu gani sasa?kama ngoma inachezwa na CCM nyie CDM inawahusu vipi? Kinachoonekana hapa ni ukosekanaji wa focus. Kama mnachoongea kina ukweli wa kimantiki, kwa nini na nyie msianzishe matawi ya CDM ndani ya CCM?

Je mnafikiria kwa kuchokonoa wanachokifanya CCM wananchi ndio wataridhika na CDM?kazi ya CDM ni kuchokonoa matendo ya CCM au kuwaeleza wananchi wa TZ mbadala wa kisera na aina ya Tanzania mara baada ya CDM kupewa nchi?

CDM kwa sasa tunapambana na CCM na vibaraka wake wote.Hatuwezi kucheka na vibaraka wa CCM huku tukitarajia kukomboa wananchi..

Siku zote tunaamini kupambana na CCM ni pamoja na kuwaanika wale mawakala wake popote pale walipo ili wananchi wajue adui yuko wapi..
 
Kwa hiyo mnaamini kwa dhati kabisa kuwa vyama vya upinzanin vyenye sera zenye mtazamo tofauti na CDM na vile visivyokubaliana na watakavyo viiongozi wa CDM ni maadui wa CDM?unaamini huu ndio msimamo wa kiongozi yoyote mwenye weledi ndani ya CDM?au ni kelele unapiga shabiki?

Kwa hiyo na CUF circa 2005 walitakiwa wapambane na CDM sio, na NCCR Mageuzi Circa 1995-2000 walitakiwa wapambane na CDM na CUF maana ndio walikuwa wapinzani wakuu.

Vitu unavyoandika havina mantiki, havina hoja wala havina mashiko. Unaandika vitu based on paranoia.

Huwezi kumkomboa mtanzania kabla hujamweleza una nini tofauti cha kumpatia. leo hii nikikuuliza CDM itafanya nini tofauti kukuza demokrasia ndani ya Taifa mara kikiwa chama tawala utajibu nini? Naomba jibu la hili.
 
Back
Top Bottom