One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

One Struggle, Many Fronts. Forward ever, Backward Never... Tumeamua kuangalia mbele!

Kwi kwi kwi kwi siku zote huna hoja wewe, haya pita lumumba ukakinge mkono kupokea bakshishi yako. Aliyekwambia neno msaliti linawaacha wengine ni nani? Usibadili maneno banaa nimekwambia huu uzi ni unamhusu msaliti Zitto unataka kumjadili Mtei fungua uzi wa Mtei.

Alaa ime ku touch eeeh, Tafsiri ya neno inatumika mahala pote mkuu haichagui Zitto ikawaacha wengine..
 
Kwi kwi kwi kwi siku zote huna hoja wewe, haya pita lumumba ukakinge mkono kupokea bakshishi yako. Aliyekwambia neno msaliti linawaacha wengine ni nani? Usibadili maneno banaa nimekwambia huu uzi ni unamhusu msaliti Zitto unataka kumjadili Mtei fungua uzi wa Mtei.
Alaaah mbona Zitto mwenyewe kayasema haya usimwambie asiwalete kina Mtei? Uzi kauanzisha Zitto na kawasema hao, unataka ikomee kwa Zitto tu. Hayo ya Lumumba unayajua wewe, japo wewe Ufipa wapaona kanisani basi wengine tusiseme.
 
Hebu tutafutie msaliti Zitto arudi hapa jamvini kuja kujibu maswali chungu nzima aliyoulizwa likiwemo hili, na ache ubaradhuli wa kuja hapa na watu wakimuuliza maswali anakimbia bila kuyajibu.

Kama hujawahi kufanya usaliti wowote ilikuwaje December 2012 ukaanzisha thread hapa jamvini ya kuwaomba radhi wanachama wa CHADEMA na kuahidi mwaka mpya wa 2013 kubadilika na kuongeza ushirikiano na viongozi wenzio ili kuhakikisha mshikamano ndani ya CHADEMA?

Je, ile radhi ambayo ulikuwa unawaomba wanachama wa CHADEMA ilihusiana na kitu/vitu gani ulichokifanya/ulivyovifanya kama mwanachama na kiongozi wa CHADEMA kilichokusukuma/vilivyokusukuma mpaka uanzishe uzi kama ule!? Bahati mbaya sana uzi ule ulifutwa bila sababu zozote zile za msingi.

Swali la nyongeza ule uzi ulitaka wewe ufutwe au ulifutwa na wamiliki wa JF? Kama ni wewe ulitaka ufutwe ni kwa sababu zipi hukutaka ule uzi uendelee kuwepo hapa jamvini?



Alaaah mbona Zitto mwenyewe kayasema haya usimwambie asiwalete kina Mtei? Uzi kauanzisha Zitto na kawasema hao, unataka ikomee kwa Zitto tu. Hayo ya Lumumba unayajua wewe japo wewe Ufipa wapaona ni kanisani.
 
Nafukir unatatizo la uelewa,tatizo lako moja tu unafikir indirectly!!!unaongozwa na falsafa za kimapokeo katika kujenga hoja mithili ya wafuasi wa Stallin waliotenda kwa kusikia!!Vyovyote mtakavyomtetea!Zitto amebreak trust kwa watu wenye fikra pevu kinyume chake ndio wanaomwamini.Zitto is opportuniste politician who dont walk on his words/speech.Anaamini wte wajinga na wepesi wa kusau!!!!Ni bingwa wa kujenga hoja zenye lengo la kuseek public empathy!!!its realy awkward to believe in him!!


Shida yako unafikira namtetea Zitto, bada ya kushindwa kujibu hoja unaanza kuni-attack mimi kama mimi, am not surprised, kwa kuwa ndicho mnachoweza kukifanya kwa ufanisi.

Hujui naongozwa na falsafa gani, kunitungia ninachoamini kunakuelezea wewe sio mie. Jenga hoja, acha kurukia watu usiowajua wala kujua wanachoamini, kama hujui uliza, utajibiwa.
 
Makala hii iliandikwa na Samson Mwigamba tar 9//12/2009 NAKUHURUMIA ZITTO KABWE MHESHIMIWA Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, salaam. Awali ya yote naomba kama nianze kwa kutangaza mgongano wa kimaslahi kama ilivyo kawaida kwa wabunge kufuatana na Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la Mwaka 2007. Mgongano wa kimaslahi ni kwamba ninakuandikia waraka huu nikitaka kujadili machache juu ya mwenendo wa mambo ndani ya CHADEMA, mambo ambayo yanakugusa kila wakati nikitaka kujaribu, kwa faida ya wasomaji, kuangalia kulikoni na wakati huohuo nikijua kwamba wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na ambaye tumekuwa pamoja tukikubaliana kwa mambo karibu yote, wakati wote. Mheshimiwa unajua urafiki wetu ni wa muda mrefu na kwa kweli nilikupenda kabla wewe hujanifahamu; nikakuhesabu kama rafiki kabla hujanifahamu na kwa bahati nzuri sana uliponifahamu ukakubali kuwa rafiki yangu. Nimekuunga mkono katika matukio, maamuzi na hata mitazamo yako mingi kwa muda mrefu. Nilikuwa upande wako katika kupiga vita ufisadi na hata uliposimamishwa ubunge wakati wa hoja ya Buzwagi nilikuwa upande wako. Nilikuwa upande wako ulipotoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga utaratibu wa kuwachagua wabunge wa Afrika Mashariki na hata katika kile ulichokiita ‘bifu’ kati yako na Spika wa Bunge, lililotokana na hatua yako ya kutoka nje ya ukumbi wa bunge na maneno uliyoyatoa nje ya ukumbi huo kuhusu uwezo wa spika kusimamia kanuni za Bunge. Nilikuwa pia upande wako uliposimama kumtetea Spika kuhusu hoja iliyotolewa na mwandishi mmoja akipinga uwepo wa Kamati ya Bunge ya Kutunga Sheria katika kanuni mpya za Bunge. Nilikuwa upande wako pale ulipounga mkono maelezo ya kitaalam ya TANESCO kununua mitambo ya Dowans na hili unalifahamu zaidi maana tulikuwa tukiwasiliana sana na huenda mimi na Absalom Kibanda ni miongoni mwa waandishi wachache sana tuliodiriki kusema waziwazi kupitia kalamu zetu kwamba tunaunga mkono msimamo wako wa kununua mitambo ya Dowans. Utakumbuka pia siku moja tulipishana mtazamo tulipokuwa tukichangia kwenye mtandao mmoja wa intaneti hoja ya utafiti wa taasisi moja iliyoonyesha kwamba bado Kikwete na CCM ni maarufu kuliko vyama vya upinzani kwa mbali sana. Unakumbuka kwamba mimi nilitofautiana na wewe kwa hoja za kitaalam zinazohusu utafiti. Lakini baada ya kutoa hoja zako na mimi nikatoa hoja zangu na wewe ukazijibu nilikubaliana na wewe na hatimaye nikawa upande wako. Lakini katika siku za karibuni nimejikuta nikiwa katika mfululizo wa matukio, mitazamo na maamuzi ya mimi kutokubaliana na wewe. Utakumbuka nilianza kutokubaliana na wewe kuhusu uamuzi wako wa kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa taifa wa CHADEMA. Nilikutumia barua pepe ndefu sana nikipinga uamuzi huo na kukuomba kwamba ujitoe kwa hoja nyingi ambazo najua unazikumbuka vema. Kwa bahati mbaya hukujibu ile barua pepe, lakini sikukata tamaa, nikaambiwa nipitie kwa msaidizi wako David Kafulila. Nikafanya hivyo na Kafulila akanihakikishia kwamba kila tunachoongea anakufikishia na kwamba unampa majibu ya kunipatia. Lakini mheshimiwa unakumbuka kwamba mwishoni kabisa majibu yako yalikuwa ni kwamba hoja zangu zote ulikuwa unazikubali lakini ulishazizingatia kabla hujaamua kujitosa kwenye kugombea uenyekiti na hivyo usingejitoa. Nashukuru kwamba baadaye uliamua kujitoa japo ulikuwa umechelewa. Mheshimiwa Zitto, nilitofautiana na wewe pia kwa kauli zako ulizokuwa unazitumia kutaka kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla ya kujiondoa. Katika moja ya taarifa za habari ulinukuliwa ukisema unatofautiana na Mbowe kwa sababu wewe ni mjamaa wakati yeye ni bepari. Nikawaza na kukumbuka kwamba Agosti 13, 2006 wakati chama chenu kinazinduliwa upya ulikuwepo na ninaamini ulishiriki kikamilifu katika kufanya utafiti, kuchambua na hatimaye kuja na katiba mpya iliyowasilishwa kwenye mkutano mkuu siku hiyo na kupitishwa kuwa katiba mpya ya chama hicho. Na kwamba maneno haya yanayosomeka kwenye utangulizi wa katiba hiyo mpya ya CHADEMA yakiwa yametamkwa kwa kunyanyua mikono na wajumbe wa mkutano huo mkuu, basi yalikuwa ni yako pia: “Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika Agosti 13, 2006, mjini Dar es Salaam, tumeamua kuifanyia mabadiliko Katiba ya 2004 ya Chama chetu cha siasa kitanachoitwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya Nguvu na Mamlaka ya Umma na Dira na Dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea. “Kuanzia sasa CHADEMA, kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitavyotungwa kwa mujibu wa Katiba ili kuimarisha kutetea, kudumisha, na kuendeleza Demokrasia ya kweli na hatimaye kuweza kuleta maendeleo ya kweli ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa jamii nzima ya taifa la Tanzania.” Kama na wewe ni miongoni mwa wana CHADEMA waliotamka maneno hayo siku hiyo kwamba: “Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitakavyotungwa kwa mujibu wa Katiba hii” nilitegemea uwe umeisoma katiba yenyewe na kuona kwamba ibara ya 3 ya katiba hiyo, ibara ndogo ya 3.B. kifungu cha 3.1.1 kinasema “CHADEMA ni chama cha itikadi ya Mrengo wa kati (center party)”. Hata kwa elimu ndogo tu maelezo haya yanatosha kuonyesha kwamba chama hiki kinaongozwa kwa itikadi iliyoandikwa ndani ya katiba ambayo ni Mrengo wa Kati na wala si itikadi binafsi ya Mbowe ya ubepari ama ya Zitto. Kwa imani niliyokuwa nayo kwako na nikizingatia elimu kubwa uliyokuwa nayo, nafsi yangu ikanituma kufikiria kwamba labda ‘wamekunukuu vibaya’. Nilihudhuria mkutano wenu na waandishi wa habari uliokusudia kuzika tofauti zenu na Mbowe na kusonga mbele kama chama. Pale ulipoulizwa swali na mwandishi mmoja kwamba utawezaje kufanya kazi na Mbowe wakati wewe ni mjamaa na yeye ni bepari; ukajibu kwa namna ambayo haikukata kiu yangu ndipo nikaamini kwamba kumbe hukunukuliwa vibaya bali ni kweli ulisema maneno hayo. Nilipingana na wewe pia pale ulipoamua kupinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA). Unakumbuka kwamba nilialikwa katika uchaguzi huo miongoni mwa wageni wachache wanafunzi, wanahabari, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali walioalikwa kushuhudia uchaguzi ule. Wakati wa uchaguzi wenyewe utakumbuka mimi na wewe tulikaa meza moja na tulitenganishwa na mtu mmoja tu (Mkurugenzi wa Uenezi Taifa wa CHADEMA, Erasto Tumbo). Nilitegemea mambo yasiyoendana na sera na kauli mbiu za chama chenu ambazo zinatangazwa hata katika jina la chama (DEMOKRASIA na MAENDELEO) ambayo yalifanyika pale ukumbini uliyaona. Najua jioni wakati wa kutangaza matokeo hukuwepo lakini nategemea ulipata taarifa za kauli za vijana mbalimbali walizotoa pale wakitaja waziwazi majina ya watu walioharibu uchaguzi ule. Sikutarajia kama Naibu Katibu Mkuu wa chama upinge hatua ile iliyochukuliwa na msimamizi wa uchaguzi pamoja na kikao kingine chochote cha juu ya msimamizi wa uchaguzi eti kwa sababu tu rafiki yako Kafulila alikuwa anaongoza. Hilo lilinipa taabu kubwa na naomba uniwie radhi rafiki yangu lakini nasema ukweli wa nafsi yangu kwamba nilifikia kujiuliza mara mbilimbili kama ungechaguliwa wewe kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, hali ingekuwaje? Na mwisho nilipingana na wewe pale ulipopinga kwenye vyombo vya habari kuvuliwa wadhifa kwa David Kafulila. Kwanza ulionekana umeweka ubaguzi kwa sababu katika maneno yote uliyonukuliwa ulisisitiza juu ya Kafulila peke yake na hukumgusia kabisa Danda Juju wakati wote walivuliwa kwa sababu zinazofanana. Lakini kwa sababu Kafulila ni rafiki yako sana, umemwandaa kuwa mbunge na unamuunga mkono katika harakati zake, na ni mbunge mtarajiwa kwa kuwa anakubalika sana jimboni basi ukamtetea na kumsahau ‘mhanga’ mwenzake. Hilo tu linafanya tutofautiane na zaidi sana tunatofautiana kwa kupinga maamuzi ya Katibu Mkuu wako nje ya vikao, maamuzi aliyoyachukua kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo. Najua yote haya umeamua kuwa kimya hujayatolea kauli yako ikiwa ni pamoja na yale ya kumfadhili Kafulila kwenda Kigoma kuichafua vizuri CHADEMA. Lakini kama ni kweli, napingana na wewe na kama unaendelea kukaa kimya nitaamini kwamba ni kweli. Sasa limeibuka la kusema kwamba unatembea na barua ya kujiuzulu nyadhifa zako zote ndani ya CHADEMA ikiwa ni pamoja na ubunge. Bado pia sijapata kauli yako, narudia kusema kwa kuendelea kunyamaza unanifanya niamini kuwa ni kweli. Na kama ni kweli, nakuhurumia sana Zitto Kabwe. Sasa naona kile nilichokuambia wakati nikikushauri ujitoe kugombea uenyekiti kinatimia. Nilikuambia ujitoe haraka tena kimyakimya kwa kumweleza tu Katibu Mkuu aweke fomu yako pembeni lakini hukutaka kunisikia. Lakini utakumbuka moja ya sentesi zangu ilikuonya kwamba ukingang’ania kugombea iwe umeshinda uenyekiti ama umeshindwa utapata shida kubwa. Nilikueleza kwamba hutaaminika tena na Watanzania na kila kitu utakachofanya utaonekana kama ulikuwa ni mamluki ndani ya chama. Ni kwa bahati kwamba umetokea kuwa na viongozi wenye busara sana kina Freeman Mbowe na kina Dk. Wilbrod Slaa wakisaidiwa na hekima na kamati ya wazee. Hawa wakaamua kukurejesha kwenye unaibu katibu mkuu. Nilishuhudia siku ile wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA walivyoshangilia uteuzi wako na wa Dk. Slaa na Hamad Yusuph kama wakuu wa Sekretarieti ya chama. Nilidhani sasa ungetulia na kufanya kazi ya kujenga chama chenu na kusonga mbele lakini haikuwa hivyo. Baada ya kushauriana sana wakati ule ulipotaka kugombea uenyekiti niliamua kutafuta habari za kiuchunguzi ndani ya CHADEMA. Nimeongea na viongozi mbalimbali na maofisa wa CHADEMA makao makuu, nimeongea sana na David Kafulila na hata niliwahi kumsikiliza mama yako mzazi akiongea na watu ambao sikuwafahamu. Nimegundua kitu kimoja tu: kwamba kama mambo haya huyafanyi kwa makusudi na kwa malengo maalumu, basi watu uliowaamini sana ndani ya CHADEMA hata kama walikuwa na nyadhifa ndogo, walikubali kutumiwa ili wakutumie wewe kuimaliza CHADEMA na wewe ukaingia mkenge. Ukakubali kugombanishwa na viongozi wenzako wa ngazi za juu hasa Mwenyekiti Freeman Mbowe ili malengo ya watu hao yatimie. Sasa nakuonea huruma. Nakuonea huruma kwa sababu kama ni malengo ya hao watu kukutumia kukimaliza chama hawatafanikiwa na badala yake watakumaliza wewe bure na utakuja kushtuka ukiwa umekwisha kisiasa. Kama ni malengo yako kwa utashi wako umeamua kutumika kukimaliza chama, nakuhurumia kwa sababu utajimaliza wewe na CHADEMA itaendelea kuimarika bila wewe wala Kafulila. Ukitaka kujua ninachokisema, tuulize sisi waandishi tunaopata mawazo ya Watanzania moja kwa moja. Kwa kuanzia muulize tu Edward Kinabo kwamba Jumatano iliyopita alipoandika makala ya “Simwelewi Zitto Kabwe” aliungwa mkono na wasomaji wangapi na walikuwa na mawazo gani juu yako. Hapo ndipo utakapoelewa kile ninachokisema. Namalizia kwa ujumbe wa msomaji wangu mmoja tu kati ya wengi. Huyu aliniambia anaitwa Meshack na yuko Korogwe. Aliniambia, “Sisi tulishajua kwamba Zitto anaondoka CHADEMA na kwamba anachosubiri tu ni pensheni yake ya ubunge ambayo huwa inatolewa baada ya Bunge kuvunjwa. Naomba Mwigamba kwa sababu unaweza kuongea na viongozi wakuu wa CHADEMA, waambie kwamba wasije wakafanya kosa la kumvua Zitto uongozi wala kumvua uanachama. Sisi hatutaki apate kisingizio cha kuondoka CHADEMA. Waambie wamuache tu mpaka atakapoondoka mwenyewe ili Watanzania wazidi kumfahamu,” mwisho wa kunukuu. Tafakari mwenyewe ulikofika, uamue cha kufanya. Kumbuka uamuzi wa mwisho ni wako wengine tunakueleza tu maana tumejiapiza kuzungumza ukweli hata katikati ya ugomvi. Kama utaamua kuondoka CHADEMA ama kujivua tu nyadhifa zako. katika yote nakutakia kila heri! Kwa hisani ya Mu-sir
Inonyesha jinsi gani huyu jamaa anahang hewani km katuni,wakati anarealize kuwa anaanguka ndio anaanza kimbia hewani kurudi palipo na pa kukanyagia ila inakuw atoo late.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hebu tutafutie msaliti Zitto arudi hapa jamvini kuja kujibu maswali chungu nzima aliyoulizwa likiwemo hili, na ache ubaradhuli wa kuja hapa na watu wakimuuliza maswali anakimbia bila kuyajibu.

Kama hujawahi kufanya usaliti wowote ilikuwaje December 2012 ukaanzisha thread hapa jamvini ya kuwaomba radhi wanachama wa CHADEMA na kuahidi mwaka mpya wa 2013 kubadilika na kuongeza ushirikiano na viongozi wenzio ili kuhakikisha mshikamano ndani ya CHADEMA?

Je, ile radhi ambayo ulikuwa unawaomba wanachama wa CHADEMA ilihusiana na kitu/vitu gani ulichokifanya/ulivyovifanya kama mwanachama na kiongozi wa CHADEMA kilichokusukuma/vilivyokusukuma mpaka uanzishe uzi kama ule!? Bahati mbaya sana uzi ule ulifutwa bila sababu zozote zile za msingi.

Swali la nyongeza ule uzi ulitaka wewe ufutwe au ulifutwa na wamiliki wa JF? Kama ni wewe ulitaka ufutwe ni kwa sababu zipi hukutaka ule uzi uendelee kuwepo hapa jamvini?
Unaona sasa kigeugeu nani? ya Kaizali mpelekee Kaizali, wewe unajadiliana na mimi sio Zitto wala sipo hapa kama sauti yake wala wewe sauti ya Mbowe. Hata Hivyo maana ya mimi kusema haya ilikuwa kwamba tofauti zao Nyerere na Mtei zilitupa picha halisi ya kuwepo njia nyingineyo. na hivo Tofauti baina ya Zitto na Chadema au Mbowe inatupa picha halisi ya kuwepo tofauti za kiitikadi baina ya wanachama wa Chadema. A good thing to realise..

Hivyo kuna kheri yake maana sasa tunajua Chadema ni chama cha Mrengo wa kati Kulia, na wanachama wake lazima wakubaliane na mrengo huo na Zitto na ACT yake ni Wajamaa na watu wenye kukubaliana na mrengo huo wajikate toka vyama vyote na sio CDM pekee. Binafsi nadhani huu ni mwanzo mzuri sana katika siasa za Tanzania na simtazami Zitto kama Msaliti kama nilivyomtazama Mzee Mtei miaka ile. Sikukubaliana naye lakini hakuwa mkosa ila alituonenyesha njia nyingine ya kuondokana na umaskini.
Hivyo ukinisoma kwa makini simlaumu Mtu kati yao na nawapongeza kwa tofauti zao maana kutofautiana kiitikadi ndio hasa maana ya SIASA.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
We acha tu Mkuu Nicholas katika huo uzi wake aliowaomba wana CHADEMA samahani kwa matendo yake aliulizwa maswali mengi na alijaribu kuyajibu baadhi lakini akaishia kujikanyaga vibaya sana na kisha kuukimbia uzi na siku chache baadaye nadhani akataka ufutwe na ukafutwa. Huu nao sidhani kama una maisha marefu hapa jamvini, utapotea muda si mrefu ujao. Na baadhi ya michango mingi ya wanachama mbali mbali katika uzi huu imeshafutwa.

Inonyesha jinsi gani huyu jamaa anahang hewani km katuni,wakati anarealize kuwa anaanguka ndio anaanza kimbia hewani kurudi palipo na pa kukanyagia ila inakuw atoo late.
 
Last edited by a moderator:
We acha tu Mkuu Nicholas katika huo uzi wake aliowaomba wana CHADEMA samahani kwa matendo yake aliulizwa maswali mengi na alijaribu kuyajibu baadhi lakini akaishia kujikanyaga vibaya sana na kisha kuukimbia uzi na siku chache baadaye nadhani akataka ufutwe na ukafutwa. Huu nao sidhani kama una maisha marefu hapa jamvini, utapotea muda si mrefu ujao. Na baadhi ya michango mingi ya wanachama mbali mbali katika uzi huu imeshafutwa.
ZItto na wengine wanasahau sana kuna mafanikio yanahitaji kuwa safi ktk mambo mengi sana,na kufanya mambo sahihi ktk muda sahihi.hayo ndio yanaongeza nafasi za mafanikio na uwezo wakulinda mafanikio...

Watu wa aina ya zitto wapo wengi ktk miji wanauza nyumba na viwanja mabilion na bado hayatosha kuwa mtaji,wakati aliyenunua babake aliuza ng`ombe na kumpa nauli ya kwenda mjini au alipiwe ada..akachagua nauli ya kwenda mjini...na akapokelewa na watu waliomdharau na kumchukia kwa kabila ila sasa ndio wanatoa mabilioni kuwahamisha waliojenga na kumiliki hivyo viwanja na majumba kwa vizazi.

Zitto ni plunderer , hakuna kitu kinaweza kuwa mtaji kwake, naibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani bado haoni kuwa ni mtaji analia km mtu asiye hata na kadi ya chama km act? Mamilioni aliyopoteza kupeleka wasanii kigoma, kununua magari ya kununu utu mbele ya Mbowe, na baadae akaja na thread eti baada ya mbowe kupata ride alisena ni gari ya kifahari kweli na baadae akaachana nayo kwa kuona yana gharama kubwa sana..Yaani alinunua magari bila haya kuyajua au kufikiri km mchumi?

Niliuliza hili swali ,tena nikamuuliza mkandala bado hakuwa na majibu na hadi leo wanalikwepa km hawalioni kwa vile wanajua niliwauliza ..akipewa nafasi ktk nchi atafanya vipi tofauti ktk miradi na issue nyingine kwa hela kidgo iliyopo ktk taifa?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
BAK, Kama huo ndio Usaliti kuna tofauti gani kati ya Zitto na Mzee Mtei?, weka pia maelezo juu yao maana Mtei alikuwa Bepari na Nyerere Mjamaa na mwisho wao haukuwa mzuri pia, lakini hakuna aloitwa Msaliti. Hivi sii kweli kuwa viongozi wanaotofautiana Mrengo hawawezi kuwa chama kimoja na wala haitakiwi!. Kwa maana hizi ukinambia Zitto ni Msaliti wa UBEPARI nitakubaliana nawe.. Kisha mnatumia neno Msaliti kwa Watanzania lihali kila ushahidi mnaotoa ni kwa Chadema kwani Chadema inawakilisha Watanzania wote? Kwa nini mnapenda sana kuwahadaa wananchi? leo na Katiba ya wananchi wakati kumbe mmeona Uchaguzi wa ubunge kupata millioni 12 kwa mwezi kwa miaka mitano ni muhimu kuliko kuipata Katiba Mpya ambayo ndiyo mwongozo na kitu kikubwa sana kwa wananchi?.
Mukandala ulisema kwamba Zitto ni wamwisho kuondoka CDM mbona kawa wa kwanza?
 
Mukandala ulisema kwamba Zitto ni wamwisho kuondoka CDM mbona kawa wa kwanza?
Zitto kafukuzwa hakuondoka!...Labda kaondoka bungeni sii mlisema Zitto ni Mbunge wa Mahakama au leo imebadilika! Na tafadhali jina langu Mkandara fanya heshima kidogo tutaelewana..
 
Kwa kifupi Zitto alikuwa na bright future CHADEMA lakini umimi, kiburi, tamaa, kujiona yeye ndiyo yeye, kutokuwa mwaminifu kwa viongozi wenzie na dharau kubwa hivi vyote vimechangia sana katika kumshushia hadhi yake aliyokuwa nayo ndani ya CHADEMA na kwa Watanzania wengi. Sijui kama ataligundua hili na kuamua kubadilika.

ZItto na wengine wanasahau sana kuna mafanikio yanahitaji kuwa safi ktk mambo mengi sana,na kufanya mambo sahihi ktk muda sahihi.hayo ndio yanaongeza nafasi za mafanikio na uwezo wakulinda mafanikio...watu wa aina ya zitto wapo wengi ktk miji wanauza nyumba na viwanja mabilion na bado hayatosha kuwa mtaji,wakati aliyenunua babake aliuza ng`ombe na kumpa nauli ya kwenda mjini au alipiwe ada..akachagua nauli ya kwenda mjini...na akapokelewa na watu waliomdharau na kumchukia kwa kabila ila sasa ndio wanatoa mabilioni kuwahamisha waliojenga na kumiliki hivyo viwanja na majumba kwa vizazi.Zitto ni plunderer , hakuna kitu kinaweza kuwa mtaji kwake, naibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani bado haoni kuwa ni mtaji analia km mtu asiye hata na kadi ya chama km act?Mamilioni aliyopoteza kupeleka wasanii kigoma, kununua magari ya kununu utu mbele ya Mbowe, na baadae akaja na thread eti baada ya mbowe kupata ride alisena ni gari ya kifahari kweli na baadae akaachana nayo kwa kuona yana gharama kubwa sana..Yaani alinunua magari bila haya kuyajua au kufikiri km mchumi?Niliuliza hili swali ,tena nikamuuliza mkandala bado hakuwa na majibu na hadi leo wanalikwepa km hawalioni kwa vile wanajua niliwauliza ..akipewa nafasi ktk nchi atafanya vipi tofauti ktk miradi na issue nyingine kwa hela kidgo iliyopo ktk taifa?
 
Kwa kifupi Zitto alikuwa na bright future CHADEMA lakini umimi, kiburi, tamaa, kujiona yeye ndiyo yeye, kutokuwa mwaminifu kwa viongozi wenzie na dharau kubwa hivi vyote vimechangia sana katika kumshushia hadhi yake aliyokuwa nayo ndani ya CHADEMA na kwa Watanzania wengi. Sijui kama ataligundua hili na kuamua kubadilika.
Ndio hivyo waafrica wengi hata akina tyson, diof, na wengine wakishaafika juu hawawezi baki juu au kuendelea kuwa juu..hawana malezi sana.Km huyu dogo alilelewa na kaipa ponda na kila mara visingio zilimponya,na mara nyingine kujifanya victim na kupata huruma kulimpeleka mbele,then huko mbele ni ngumu sana kila mtu kumlinda au kukubalina na huo upuuzi ,life lazima ianze kuwa ngumu.Km mamake alimkabidhi kwa baregu ni wazi kuwa huyu mama boy alimsumbua sana ***** kwa kujiliza na kuchezea huruma ya mama.
 
Mhe. Zitto jiungeni UKAWA kama kweli ni one struggle many fronts. Umoja wa upinzani ndio utakuwa nguvu yenu!
 
Last edited by a moderator:
Zitto kafukuzwa hakuondoka!...Labda kaondoka bungeni sii mlisema Zitto ni Mbunge wa Mahakama au leo imebadilika! Na tafadhali jina langu Mkandara fanya heshima kidogo tutaelewana..
well ,said nilidhani ungesema tofauti kwa vile ktk ubishi wa kipindi kile ukiandika ...CHADEMA WAKIFANYA HIZI USHINDI NI WAO..tulibishana sana nilipokuambia hajui afanyalo na niliwahi kuuliza alitaka apate Nafasi gani Zaidi ya unaibu katibu Mkuu,na nafasi nyingine ili asijifiche ktk hila za sijui udini,sijui kutoka familia masikini,sijui ukanda.....ambazo ni dalili za mtu kupwaya ktk nafasi.Ulmteteta sana kujua alichokuwa kaifanya na ulifikia sema kuwa akitoka cdm inavunjika, etc .Sasa unakiri kuwa alifukuzwa na si kujitoa na akatoa wa kwanza?
 
Unaona sasa kigeugeu nani? ya Kaizali mpelekee Kaizali, wewe unajadiliana na mimi sio Zitto wala sipo hapa kama sauti yake wala wewe sauti ya Mbowe. Hata Hivyo maana ya mimi kusema haya ilikuwa kwamba tofauti zao Nyerere na Mtei zilitupa picha halisi ya kuwepo njia nyingineyo. na hivo Tofauti baina ya Zitto na Chadema au Mbowe inatupa picha halisi ya kuwepo tofauti za kiitikadi baina ya wanachama wa Chadema. A good thing to realise..

Hivyo kuna kheri yake maana sasa tunajua Chadema ni chama cha Mrengo wa kati Kulia, na wanachama wake lazima wakubaliane na mrengo huo na Zitto na ACT yake ni Wajamaa na watu wenye kukubaliana na mrengo huo wajikate toka vyama vyote na sio CDM pekee. Binafsi nadhani huu ni mwanzo mzuri sana katika siasa za Tanzania na simtazami Zitto kama Msaliti kama nilivyomtazama Mzee Mtei miaka ile. Sikukubaliana naye lakini hakuwa mkosa ila alituonenyesha njia nyingine ya kuondokana na umaskini.
Hivyo ukinisoma kwa makini simlaumu Mtu kati yao na nawapongeza kwa tofauti zao maana kutofautiana kiitikadi ndio hasa maana ya SIASA.


HUu ni upotoshaji.
 
Mhe. Zitto jiungeni UKAWA kama kweli ni one struggle many fronts. Umoja wa upinzani ndio utakuwa nguvu yenu!

Soma hapa halafu ungansiha DOTI.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...muhimu-kuliko-katiba-mpya-2.html#post12374492

Mkuu kwa kauli hizi za Kibaraka wake Mkuu humu Mkandara Zitto hawezi kujiunga na UKAWA, maana ukawa wanaamini katika serekali tatu huku ACT wakiamini katika Serekali mbili zilizo Nyuishwa(Kumbuka CCM wansema Zilizoboreshwa)
kwahiyo kw avyovyote ACT ni CCM iliyo Nyuishwa au Kuboreshwa.
 
Last edited by a moderator:
Soma hapa halafu ungansiha DOTI.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...muhimu-kuliko-katiba-mpya-2.html#post12374492

Mkuu kwa kauli hizi za Kibaraka wake Mkuu humu Mkandara Zitto hawezi kujiunga na UKAWA, maana ukawa wanaamini katika serekali tatu huku ACT wakiamini katika Serekali mbili zilizo Nyuishwa(Kumbuka CCM wansema Zilizoboreshwa)
kwahiyo kw avyovyote ACT ni CCM iliyo Nyuishwa au Kuboreshwa.

Kwani kuna ulazima wa watu wote kufikiri kama wewe unavyofikiri?
hata ndani ya chama ni lazma pawe nabfikira huru ili muweze kujenga chama kwa misingi thabiti.
mkiwaza sawa hamtaweza kutatua changamoto mpya zinapofika!
Naunga mkono fikira huru za watu bila kujali wanatoka katika mlengo upi..kinachotakiwa ni hoja zenye mantiki tu za kujenga tanzania tunayoitaka!
 
Last edited by a moderator:
ACT ni kigenge cha wahuni wachache wasiozidi kumi, ili wapige hela za CCM yapata kama 500 Mil. Zilizotengwa kuidhoofisha Chadema. Wengine wanaobwabwaja humu ni wapiga makelele tupu tu!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom