On Ndulu: The "Guardian" must be kidding me!

grrrrrrrrrrrr!!! Mimi ningependa hiyo nyumba ipigwe mnada tuone kama itauzika kwa bei hiyo! si bado mpya?

nchi ilivyojaa mifisadi,utaona kin aJeetu,Manji et al wanavyoigombania kwa offer za $2-$3M kusave face za washirika wao!

hii nchi ni michezo ya kuigiza everywhere..,
 
We say the said expenditure was a pretext because available evidence indicates that, based on the annual rent of 113 million/- BoT had been paying for the governor’s accommodation in rented premises, the expenditure of 1.4 billion/- for the official residence represents a payback period of 12 years while also affording the bank an official residence befitting its CEO’s status.

So it is based on this, then a 1.4bn hse for governor is justified!!!! Nadhani tukiletewa matumizi ya muungwana na safari zake inajustfy kumnunulia customized B747 the like of Airforce one...........

Is this the guardian we know? What a foolish justification!?! Mzee Mengi please do something otherwise we will never read your paper.
 
Hii ndo Wadanganyika bana, sehemu ya kunawa, watu wanaamua kuoga kabisa
Ndio maana wanangangania uongozi, Nchi hii inaongozwa na Mabosi wa umma wala sio watumishi wa umma.
 
unajua watanzania wengi ni mandumila kuwili na wapaka mafuta wazuri (kukusifu kumbe huku wanakumaliza) kimsingi sijashangaa utumbo uliozungumziwa hapa na na wala sitoshangaa.

Kuna matatizo mawili yaliyopo la kwanza BOT ni chombo gani? na Pili ni akina nani wahusika wa chombo yaani wamiliki wake kina nani. Tukiweza kujibu maswali haya ndio tutaweza kutatua matatizo ya uongozi mbovu hapo BOT. BOT ni institution entrusted for the function of regulating our financial system. Sasa tunapomlinganisha gavana na CEO wa microsoft i think si sahihi kwasababu CEO wa microsoft ana malengo ambayo tofauti na gavana hivyo basi malipo atakayolipwa yatakuwa tofauti na gavana.

Tuje kwenye nani wamiliki wa BOT ni mimi na wewe ( sasa inakuwaje tunalipa mtu kwa kazi ambayo haionekani???) To me this is pathetic and distortion. Gavana analipwa $15,000 wakati uchumi umejaa madudu inflation wanadai 12% but nimeenda Tanzania inflation is more than 100% sasa what is this???. Wanadai watu waliokuwa employed ni 16 million but ukiangalia the real environment more than half of the adults who are graduated and capable of working are unemployed (ndio ufanisi huo). Interest rate katika borrowing ipo 20%-25% mtanzania gani ana biashara ya kulipa mkopo huo je unadhani watu wataweza vp kujiajiri? unbankable individuals wapo wengi na ndio majority banks wameconcentrate kwa hao wachache vibopa je uchumi unakua (kukopesha wachache eti wanafaa kukopeshwa ndio maana umaskini unanuka tanzania) Profesa wetu amekaa katika kiyoyozi hata kufikiria kuwawezesha maskini tanzania hana mpango huo.

Kiufupi bwana Tanzania tunaenda kubaya tena sana mungu ibariki tu!!!!
 
jengo la hadhi ya Gavana! you must be kidding me! Unafikiri kwa "hadhi" yake jengo hilo linatosha? Kuna vitu vingine twaweza kumpatia ili viandane na hadhi yake? Twaweza kumpa msafara wa magari, na mabodyguards, vipi kuhusu kumjengea nyumba nyingine kijijini kwao? Je watoto wake wana magari (maana hatuwezi kuwa na watoto wa gavana wanaopanda madaladala!), Je wajukuu zake wanasoma Tanzania shule za serikali au za binafsi?


+ Tumjengee 'underground tunnel Home office' asikumbane na foleni...
 
It is clear that those who previously profited through corruption and other foul play at the central bank are a vastly disgruntled lot with Prof Ndulu in the saddle and will not go down without a fight.


Pamoja na kuikosoa editorial hii, kuna jambo muhimu hapa ambalo tunaelekea kutolitilia maanani. Ni kwamba kuna kampeni inayoongozwa na mafisadi kutaka kumng'oa Gavana Ndulu na kumpachika mtu wao, kama walivyofanya sehemu nyingine nyeti. Hapa lazima tuwe macho, tusije tukaingia kwenye mtego wa mafisadi wa kumuona Ndulu ni fisadi kama wao na hivyo kuhalalisha kung'olewa kwake. Tuwe macho! Na bila shaka The Guardian wameliona hilo ndio maana wametwanga editorial hii kumsafisha.
 
Kwa speed hii! Bus lazima lipinduke! Halafu na shangaa sana nchi hii watu wanavyolindana! Kuna ganzi gani kwenye vichwa vyetu jamani! Scandle kama ingekuwa kwingineko kama US au UK ungeona an immediate response kutoka serikalini ama kweli ni hujuma au uwongo! Lakini kwetu mshikaji ana batasamu tu! May be ndivyo tulivyo! Eti kuna haja gani ya kujilinganisha na USA wakati sisi ni Tz! Do whatever u want! there will kelele kidogo! halafu watasahau! Ndiyo!!! that is how it is! Kesi za Gray, PesaMoja ziko wapi? Juzi kapewa sijui uenyekiti wa TANROAD wakati ana kesi pending mahakamani ya ufujaji na matumizi mabaya ya sirkali! Sasa najiuliza tumepigwa nusu kaputi!!!!!!!!!!? unaweza fikiri nchi hii ina watu wangapi wachapa kazi ambao wangeweza kuifanya hiyo kazi badala ya kuchukua huyu mtuhumiwa! tena wa uhujumu uchumi!
 
Katika maisha yangu sijawahi kuona jitihada yeyoye ya makusudi imewahi chukuliwa na serikali ya waChukua Chao Mapema kusaidia chochote Tanzania, mambo yote ni kwa neema tu! Business as usual Leo hii Bongo paamoja na umasikini wetu mkubwa ndio tunaoongoza kwa kuwa na gharama za juu za umeme, simu! Riba katika mabank ziko juu! kwa sababu u can do whatever you want in Tz kama una pesa! Jamaa aliulizwa mtafanya nini na hii economic crisis! BIG SMILE! halafu Kwaza kabisa tutawashinikiza wahisani waendelee...............Honestly nashidwa kujua tunakoenda!
Mheshimiwa JK STOP saying everythig is OK! Things are NOT OK! Kuna mafisadi? YES WAPO! Wameathiri uchumi, maisha ya mtanzania mlipa kodi! and we know them! What do we do! Hold them responsible!
Mungu Ibariki Tanzania!
 
taifa la watu wasio na uwezo wa kuhoji kamwe usitegemee maendeleo
 
Maswali ya kujiuliza,

1. Kwa nini bado tuna utamaduni wa mashirika, taasisi na Serikali kujengea wafanyakazi nyumba? Kwa nini wasijihudumie wao wenyewe kwa kutumia mishahara yao?

2. Kwa nini Benki Kuu kama mdhibiti wa Uchumi wa Tanzania ilikubali kujengewa nyumba kwa gharama za juu kiasi hiki, ukizingatia kuwa sekta ya Ujenzi inajipangia bei zake kiholelea na hakuna udhibiti wa mfumuko wa bei za viwanja na malighafi (vifaa vya ujenzi) unaofanyiwa uratibu na Serikali?

3. Kama Benki kuu inaazimia kuwa bei hizi ni sawa (si kwa sababu ya bajeti) kutokana na hali halisi ya sekta ya ujenzi na nyumba Tanzania, je Uchumi wa Tanzania na safari ya Watanzania kuwezakujitegemea na kujijengea nyumba bora itafanikiwa vipi ikiwa kila siku kuna mfumuko wa bei za viwanja, hakuna sheria madhubuti za ardhi, na gharama za vifaa vya ujenzi na wajenzi ni kubwa kuliko sehemu nyingi duniani na ukipima uwiano wa umahiri wa Sarafu yetu?

4 Je nyumba hizi zimejengwa kuwa kutumia malighafi na Rasilimali ambazo zinazalishwa Tanzania? Kama sivyo, ni kwa nini BOT ambayo inatakiwa kuchochea uzalishaji wa mali na kukuza uchumi wetu ilikubali mkandarasi alieagiza mbao kutoka Malaysia, huku tuna mbao nyingi kule Mufindi? Je udongo ulaya, misumari, fito, madirisha, samani, nyaya na hata udongo vilitoka nje ya nchi na hivyo kuongeza gharama za ujenzi?

5. Je Benki Kuu pamoja na kuwa hizi pesa zilitengwa awali, je kulikuwa na ulazima wa kuingia gharama na kuzijenga nyumba hizi wakati huu ambao Uchumi si wa Tanzania tuu bali wa Dunia ni mbaya na hivyo matumizi haya yalifanyiwa maamuzi na kuidhinishwa bila kutumia busara? Je Ndulu na wenzake walikuwa wanakaa wapi kabla ya kuwa Gavana wa Benki?

Oh by the way, Tanzania's budget is in extra extra large red, and we still showe Ndullu with praises? I have not heard from his mouth or his policy aboutt frugality or kupunguza matumizi. All I hear is tumepata misaada and lete kama tulivyo tuzitumbue!

If our DEFICT is soaring, how can one dare to say Ndullu is doing an outstanding job?
 
laiti ningekuwa ni mimi gavana Ndulu ningehakikisha BOT inatoa walau vibilioni viwili kwa waathirika wa mafuriko kule kilosa na kwa kiasi hicho zaidi ya familia 400 wangepata makazi ya kudumu. huu ni upuuzi kwa nchi masikini kama yetu kutumia zaidi ya i.3billion kujenge nyumba kwa makazi ya familia moja huku mamia ya wananchi wakilala nje>

mungu atusaidie tuendelee kuwa wapumbavu!
 
araway said:
laiti ningekuwa ni mimi gavana Ndulu ningehakikisha BOT inatoa walau vibilioni viwili kwa waathirika wa mafuriko kule kilosa na kwa kiasi hicho zaidi ya familia 400 wangepata makazi ya kudumu. huu ni upuuzi kwa nchi masikini kama yetu kutumia zaidi ya i.3billion kujenge nyumba kwa makazi ya familia moja huku mamia ya wananchi wakilala nje.

araway,

..sijui kama unafahamu, lakini Prof.Ndulu ana asili ya Ulanga-Kilombero.

..sasa wakati yeye anastarehe kwenye jumba la thamani ya mabilioni, ndugu zake wanataabika kwa mafuriko na kupata msaada kiduchu toka serikalini.
 
Ndullu anajua kwa muda huu ndo wa kupiga mambo. Wajanga watakumbuka mambo ya Keenja wakati alipokabidhiwa kuliongoza kwa mpito Jiji la Dar, aliweka safi pale wananchi walipokuwa wakipigia kelele lakini ni katika kipindi hicho hicho Charles Keenja (MP) aliweza pia kujikusannya zile zilizomwezesha kugombea Ubungo wa Ubungo.
Acha matusi wewe, unahitaji kiasi gani ili uweze kugombea ubunge?
Kama hujui unalosema huna haja ya kulisema. Watu watakushangaa bure tu.

Hivi unaamini kuwa lazima uibe ili uweze kugombea Ubunge?
 
Maswali ya kujiuliza,
4 Je nyumba hizi zimejengwa kuwa kutumia malighafi na Rasilimali ambazo zinazalishwa Tanzania? Kama sivyo, ni kwa nini BOT ambayo inatakiwa kuchochea uzalishaji wa mali na kukuza uchumi wetu ilikubali mkandarasi alieagiza mbao kutoka Malaysia, huku tuna mbao nyingi kule Mufindi? Je udongo ulaya, misumari, fito, madirisha, samani, nyaya na hata udongo vilitoka nje ya nchi na hivyo kuongeza gharama za ujenzi?

Rev. Kishoka, swali hili, nimeliona very objective. Kutafuta na reasons behind any move/action/uamuzi hatimaye hutufikisha kwenye justification ya whatever is done/has been done. Baada ya kelele za Twin tower, mpaka leo ripoti ya value for money haijatolewa ili kuestablish genuine expenditure ni kiasi gani na ulaji ni kiasi gani.

Nliyaona hayo majengo, sakafu na kuta zote ni granite, hakuna tofali, wamemwaga zege ya foam tangu chini mpaka juu, wametumia japanese technology ya skyscrepers za kule kwa kutumia nondo za titanium ili hata likitokea tetemeko, jengo litaswing up to 45 degrees bila kubomoka. Wameweka fire resistant materials kwenye kila kuta ili moto ukitokea chumba kimoja, unaishia hapo hapo. Ndani wametumia light wood ili kupunguza uzito, hoja eti finishing ya cyprus yetu, haiwi smooth enough, na mbao ya Iringa ni too heavy and too expensive to process. Mambo mengine ni security issues kama bullet proof windows etc. etc.

Pamoja na vikolokolo vyote hivyo, sio justification ya lavish spending.

Kama Balali aliidhinisha ujenzi wa vikolokolo hivyo na bodi ikaridhia, naamini ndicho walichokifanya kwenye nyumba ya gavana, wameimimina zege tupu kama Ubalozi wa Marekani, Bomb proof as if Gavana anawindwa, hata Ikulu yet sio fotress kihivyo.

Watu huweza kufanya yote kutokana na preferences na purchasing power. Wakati saa ya kawaida Dar inaanzia Sh. 500 ya kibongo, kuna mtu anavaa saa ya mwaka 1933 gold Patek Phillipe kwa $11 million au hii 1 – $25 million – 201-carat Chopard iko sokoni na watu watafika bei, what for?. There must be a reason!.

Wakati brand new mobile phone ya kawaida ndani ya bongo, inaanzia Shiling 15,000! kuna watu wananunua mobile phone ya Goldvish "Le million" au Vertu Signature Cobra, au Sony Ericsson Black Diamond na kutumia kwa $1,000,000, ambayo ni sawa na nyumba ya Gavana!. What for?. Its for a reason.

No matter what, yes we can't justify such spending, but at least we should get the reasons behind ili tujustify at least what BOT Board were thinking about.
Tikisha pata hiyo justification yao, then tupige makombara kisawasawa to hit the target.

Japo siungi mkono hiyo PR Capaign ya Guardian, lakini niko curious kujua what a big deal ya hiyo nyumba ya 1.4 Bil. Baada ya kina Mramba, Yona na Mgonja kutiwa ndani, Ndugu jamaa na marafiki wa Mgonja na Mramba, walichangishana kupata thamana. Yona alijidhamini mwenyewe na miongoni mwa dhamana zake ni nyumba yake ya Makongo Juu, 1.2 Bilion. What's so big deal kuhusu hii ya 1.4 kabla hatujapata what are reasons behind justifying it.
 
Mzee Mwanakijiji, I don't justify lavish spending in whatever the reasons might be, lakini lazimas tufike mahali tuukubali ukweli kuwa we have to deserve the best that money can buy...

....Kwa mlio nje, Tanzania ya leo ioneni hivyo hivyo ilivyo, au isikieni tuu, lakini the reality hiyo spending ya bilions kwenye nyumba ya gavana, is nothing compared to billions and billions zinakuwa spend on good for nothing issues......

...Baada ya kele za Twin Tower, nilipata bahati ya kuiona hilo Jengo inside out, nothing of its kind in Tanzania in terms of technology and security. This does not justify the spending, lakini value for money ifanye kwanza ndipo tujue kick back ni ngapi watu waliopoket kushibisha matumbo yao, na sio kukimbilia mahakami kumtoa kafara Liyumba, kwa mashitaka ya full value as if nothing has been done..

...Kama speaker anakodiwa nyumba kwa milioni 10 kwa mwezi ili kuishi kwenye nyumba ya hadhi ya speker, hebu fanyeni utafiti, hilo hekalu lenye hadhi ya spika litagharimu kiasi gani?. Kama spika ana haki ya kuspend such an ammount to please his ego, jee gavana anastahili hadhi gani?

...Dar kuna kuanzia kulala nje kwenye pavement (homeless) vibanda vya maboksi, vibanda vya mbao, vijumna vya udogo, makuti, bati za madebe, nyumba za kawaida, majumba mpaka mahekalu ya kama peponi. Hivi huyu gavana wetu anastahili hadhi gani?

..Sina idadi ya askari polisi wanaokuwa duty every week-end mkulu anapokwenda Mlingotini, kila barabara inayoingia mainroad tangu Magogoni mpaka Mlingotini, wanawekwa askari two hours before. Mbona marais wa nchi za wenzetu hawafanyi hivyo. How much do we spend for nothing?

..Naelewa shida ya umasikini uliotopea kwa Watanzania, mashule yasiyo na waalimu, mahospitali yasiyo na dawa, wakulima wapinda migongo kwa jembe la mkono lisilo tija, wanafunzi wanaonyimwa mikopo kuendelea na elimu, matatizo ni mengi, lakini ndio iwe sababu Gavana asipate makazi bora sababu ya shida zetu?

...Hizo bilioni nadhani kama ziara moja tuu ya raisi nje ya nchi. Kama kweli viongozi wa nchi yetu wanauchungu na nchi hii, wangeshafanya wakipasacho kufanywa long ago. Tuungane kwa kauli moja, October tuseme Basi na nyumba ya gavana tutampa Mnyika!.

Pasco mara nyingi nakubaliana sana na insights zako,lakini pia huwa unanichanganya sana mara nyingi,Sasa haufagilii lavish spending lakini hapo hapo unataka tuwe na the best money can buy?
Sehemu zote posting imetulia kasoro hapo tu....Na ndio maana nimetoa sanks lakini nikiwa critical kwenye red highlights.
 
Tunaendelea kuisafisha BoT – Gavana
Rajab Mkasaba, Zanzibar
Daily News; Friday,February 22, 2008 @05:25

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, amesema taasisi yake bado inaendelea na kazi ya kujisafisha na kurejesha imani ya wananchi.

Akizungumza na Rais Amani Karume wakati alipokwenda kumtembelea Ikulu leo, Profesa Ndulu alisema amefarijika na jinsi wananchi walivyoonyesha imani kwake tangu ateuliwe na akaahidi kuendelea kuiimarisha benki hiyo sambamba na kuondoa upungufu uliokuwapo.

Katika maelezo yake, Profesa Ndulu, ambaye alifuatana na uongozi mpya wa BoT alimweleza Rais Karume kuwa miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika uongozi huo tangu kuteuliwa kwake, ni kurudisha imani kwa wananchi.

"Kwa msaada wa viongozi wetu, ukiwamo Rais Karume tutajitahidi kufanya yale ambayo yatatusaidia katika kufikia lengo lililokusudiwa kwani wananchi wana matarajio makubwa," alisema Profesa Ndulu.

Alimweleza Rais Karume kuwa uongozi wa benki hiyo upo tayari kukabiliana na changamoto zote katika ufanyaji wake wa kazi ukiwa na malengo na madhumuni yaliyokusudiwa.

Akitaja changamoto nyingine, Profesa Ndulu alisema kuwa ni pamoja na kuimarisha utengamano wa bei za bidhaa na huduma, kulinda mafanikio yaliyokwisha patikana katika kudhibiti mfumko wa bei na kuimarisha mfumo wa usimamizi wa benki na kuhakikisha usalama kati ya mfumo wa sekta ya fedha.

Gavana Ndulu alisema BoT ina mpango wa kuwapa nafasi vijana wenye uwezo katika utendaji kwenye masuala ya Kibenki ili waje kuwa watendaji wazuri wa hapo baadaye.

Rais Karume aliupongeza uongozi wa BoT kwa namna ya maendeleo yaliyopatikana katika kipindi kifupi na kusema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa benki hiyo inapata mafanikio zaidi.
 
Maswali ya kujiuliza,

1. Kwa nini bado tuna utamaduni wa mashirika, taasisi na Serikali kujengea wafanyakazi nyumba? Kwa nini wasijihudumie wao wenyewe kwa kutumia mishahara yao?

2. Kwa nini Benki Kuu kama mdhibiti wa Uchumi wa Tanzania ilikubali kujengewa nyumba kwa gharama za juu kiasi hiki, ukizingatia kuwa sekta ya Ujenzi inajipangia bei zake kiholelea na hakuna udhibiti wa mfumuko wa bei za viwanja na malighafi (vifaa vya ujenzi) unaofanyiwa uratibu na Serikali?

3. Kama Benki kuu inaazimia kuwa bei hizi ni sawa (si kwa sababu ya bajeti) kutokana na hali halisi ya sekta ya ujenzi na nyumba Tanzania, je Uchumi wa Tanzania na safari ya Watanzania kuwezakujitegemea na kujijengea nyumba bora itafanikiwa vipi ikiwa kila siku kuna mfumuko wa bei za viwanja, hakuna sheria madhubuti za ardhi, na gharama za vifaa vya ujenzi na wajenzi ni kubwa kuliko sehemu nyingi duniani na ukipima uwiano wa umahiri wa Sarafu yetu?

4 Je nyumba hizi zimejengwa kuwa kutumia malighafi na Rasilimali ambazo zinazalishwa Tanzania? Kama sivyo, ni kwa nini BOT ambayo inatakiwa kuchochea uzalishaji wa mali na kukuza uchumi wetu ilikubali mkandarasi alieagiza mbao kutoka Malaysia, huku tuna mbao nyingi kule Mufindi? Je udongo ulaya, misumari, fito, madirisha, samani, nyaya na hata udongo vilitoka nje ya nchi na hivyo kuongeza gharama za ujenzi?

5. Je Benki Kuu pamoja na kuwa hizi pesa zilitengwa awali, je kulikuwa na ulazima wa kuingia gharama na kuzijenga nyumba hizi wakati huu ambao Uchumi si wa Tanzania tuu bali wa Dunia ni mbaya na hivyo matumizi haya yalifanyiwa maamuzi na kuidhinishwa bila kutumia busara? Je Ndulu na wenzake walikuwa wanakaa wapi kabla ya kuwa Gavana wa Benki?

Oh by the way, Tanzania's budget is in extra extra large red, and we still showe Ndullu with praises? I have not heard from his mouth or his policy aboutt frugality or kupunguza matumizi. All I hear is tumepata misaada and lete kama tulivyo tuzitumbue!

If our DEFICT is soaring, how can one dare to say Ndullu is doing an outstanding job?


Swala hapa isiwe kwa nini. Serikali ina jukumu la kuwajengea makazi bora raia wake wawe wafanyakazi wa benki, makarani au wakulima etc. Makazi bora kwa wananchi wote, hili ni jukumu ambalo lilianza tulipopata uhuru kama unakumbuka NHC ndio walipewa jukumu la kujenga nyumba na idara yoyote ya serikali ikihitaji nyumba wanakwenda kwa wataalamu wao ambao wamepewa hilo jukumu.

Kwa nini basi serikali na mashirika mbali mbali yanakaidi kutumia NHC ni kwa sababu ya wizi wa mchana kweupe na ukaidi wa waliopewa dhamana kuchukua hatua zozote. Haiwezekani uwe na wizara ambayo inashughulikia ujenzi wa makazi bora halafu kila uchwao nyumba za serikali zinajengwa na matapeli bila kupitia kwa wasomi wake.
 
Nliyaona hayo majengo, sakafu na kuta zote ni granite, hakuna tofali, wamemwaga zege ya foam tangu chini mpaka juu, wametumia japanese technology ya skyscrepers za kule kwa kutumia nondo za titanium ili hata likitokea tetemeko, jengo litaswing up to 45 degrees bila kubomoka. Wameweka fire resistant materials kwenye kila kuta ili moto ukitokea chumba kimoja, unaishia hapo hapo. Ndani wametumia light wood ili kupunguza uzito, hoja eti finishing ya cyprus yetu, haiwi smooth enough, na mbao ya Iringa ni too heavy and too expensive to process. Mambo mengine ni security issues kama bullet proof windows etc. etc.

Pasco. Nenda taratibu, mbona unataka kutufanya wote limbukeni?

Hauwezi kutumia titanium kama nondo. Hata huko japan hawatumii. Titanium quality zake hazikidhi mahitaji. Titanium inatumika zaidi katika kufunika jengo na sio kwenye zege.

Hakuna kitu kama Japanese technology ya kujengea skyscraper. Ujuzi ni ule ule. Hesabu za structure ni zile zile. Ubunifu ni kwa watu binafsi na sio kwa taifa, Kwanza skyscrapers nyingi hazijengwi kwa zege. Ni chuma mtindo mmoja.

Light wood ndio nini? Kupunguza uzito kwenye nini? Unaweka sakafu na kuta za granite halafu unaogopa uzito!

Bullet proof windows za nini? Hivi wao wasiwasi wao ni watu kupigwa risasi au jengo kulipuliwa? Hizi ndiyo specification za kipuuzi.

Naona aliyekutembeza amekuingiza mkenge. Ukweli ni kuwa kwenye lile jengo hakuna value for money ya aina yeyote.

Amandla.......
 
Back
Top Bottom