Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,935
- 6,844
Swala hapa isiwe kwa nini. Serikali ina jukumu la kuwajengea makazi bora raia wake wawe wafanyakazi wa benki, makarani au wakulima etc. Makazi bora kwa wananchi wote, hili ni jukumu ambalo lilianza tulipopata uhuru kama unakumbuka NHC ndio walipewa jukumu la kujenga nyumba na idara yoyote ya serikali ikihitaji nyumba wanakwenda kwa wataalamu wao ambao wamepewa hilo jukumu.
Si jukumu la serikali kuwajengea raia wake makazi bora. Jukumu la serikali ni kuweka mazingira ambayo yatawawezesha raia wake kupata( Kujenga au kupanga) makazi bora. Dhana ya kuwapatia wafanyakazi au raia wake makazi ndiyo iliyotufikisha hapa.
Amandla.......