Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,060
- 22,755
Mimi naomba tu kumjibu anayejiita Pasco kama ifuatavyo. Prof. Ndulu siye wa kwanza kushutumiwa kwa matumizi ya kifisadi. Wengi tu wamesemwa humu JF na hata pale ilipoonekana kuwa shutuma zina chembe za ukweli watuhumiwa hawakuwahi kukosa watetezi - tukianzia juu - Mkulu au Mkapa, katikati - Ndulu au Idris hadi chini kabisa kwa akina Londa na wengineo.
Kikubwa ni kuwa tunapiga kelele na siku zote tutaendelea kupiga kelele. Swali la kwanza ni je, kelele zetu zimeweza kuwanyima usingizi ? Jibu nafikiri liko wazi kuwa si tu wanakosa usingzii bali wangetamani angalau hata wapate mahali pa kuzificha nyuso zao, lakini wapi - ufisadi wao umewaganda kama shati lililoloweshwa na aina ya gundi inayoijulikana kama magic glue.
Wote wanajuta, kama anavyojuta Ndulu hivi sasa, laiti angejua litakalofuata asingefanya hilo alilolifanya. Swali la pili ni je hili linatoa fundisho lolote kwa wengine watakaofuata ? Pamoja na jibu kutokuwa rahisi lakini somo kubwa hapa ni kuwa ukifanya madudu ukae tu ukijua kuwa vyombo kama JF vipo na havitakupa free pass kama ilivyozoeleka zamani, vitakuandama kama nyuki.
Wangekuwa hawajuti, utetezi wa kijinga kama huu wa Guardian haungepata nafasi. Hizi ni dalili za kutapatapa, lakini tunao tu.