Ata ukimaliza urubani basi ushatumia mamilioni mia mia ivi ndio uwe na uwezo wa kurusha ndege na kupakia abiria. Hatua ya kwanza tu, unakata kama milioni 40 ivi, unapewa private license huwezi kurusha ndege kwa malipo yoyote na tena hapo unarusha cessna 152/172 ambayo umesomeshwa nayo. Hatua ya pili ya kukupatia leseni ya kurusha ndege na kulipwa tena ukate mamilioni kadhaa, na hapo bado hupati kazi, ukienda kama precision kuomba kazi, ambao wana operate ATR planes, unatakiwa ukasomee kitu inaitwa type rating, yaani ukaisomee hio ndege ambayo unataka kurusha sasa, hapa ndio unakwenda kuchoma tena pesa nyingi tu. Yaani mpaka unamaliza walau milioni 150 ivi umewekeza.ukisomea urubani mambo ya kuzunguka na bahasha kusaka ajira hayapo,ajira zinakufata zenyewe hadi mlangoni....hii ndo faida ya kusomea vitu vya "watu wachache"
Sasa baada ya kuchoma izo kabla ya kupata kazi, makampuni yanataka uwe na minimum hours hii inategemeana na kampuni matakwa yao. Lakini kwa mtu mjanja, ambae hajafikia hayo masaa, anashinda airport, kwa vile anakuwa anajulikana kama mhitimu, huwa zinatokea fursa unapewa upeleke abiria sehemu, hulipwi mshahara unapewa posho tu. Sio noma, kwa sababu wewe unapata kurikodi masaa yako mpaka yakifikia yale yanayohitajika, inakuwa rahisi kupata ajira (ikiwa nafasi zipo). Ukipata ajira, zile hela ulizochoma zote, utaona kuwa it was worth it. Maana mshahara huwa mnono na benefits zinategemeana na kampuni.
Tatizo vijana wanataka wakimaliza kusoma na kuwa na masaa kadhaa wanataka ajira direct, wakati kumbe angekubali kufanya kazi bure tu na kujipatia posho uku anajenga masaa yake ambayo later on yatamuwezesha kupata kazi kirahisi.