Ombi maalumu kwa Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema

MWK Karibu tena...Tume kumiss kwa sana tu...Nadhani hata MJKK atakiri hilo.

Kwa upande wa hoja...Ni wazi Mrema ni mmoja wa mashujaa wetu hilo liko wazi kabisa...Hata majambazi wengi wamefurahia baada ya kuanza kupata sapoti ya wale waliopewa nguvu za ziada za unyanyasaji ili kuwalinda mafisadi...Mahita na wengineo ni mfano hai.

Toka wamuite kichaa kwa kuigeuka system ya kifisadi na kupoteza maslahi yake...Kuhatarisha maisha yake na hata bila kujali hayo wengi wetu hapa wanayoyaita maslahi kwa kudai eti ajiuzulu ili ale pension.

Angebaki ndani ya chama cha mafisadi hiyo pension nyie mngekuwa na haja ya kumwuliza ama mngekuwa mnamwita mzee wa vijisenti?

Haya wengi wetu waliyoyasema ni kama matusi kwa mtu aliyejitolea kama Mrema.

Kazi aliyofanya ni ngumu na kila alipokwenda ccm walimfuata kwa kuwahonga watu ndani ya chama ama kuwanunua baadhi ya wanasiasa wenye ushawishi ndani ya chama.

Hata yaliyowakumba chadema mnayajuwa.....Hayo hayo ya ccm kuingilia issue kwa undani ndani ya vyama kwa kupenyeza rupia....Ni jambo la busara kama Mrema atapewa nafasi katika vita hii kwani ni wazi bado wale watanzania wenye kujuwa historia kamili ya upinzani, watakubaliana na mimi kuwa Mrema bado ni factor kwani kazi aliyoianza imepata wapiganaji wengi zaidi na uzoefu waliokwisha upata sasa wanaweza kuja pamoja na kufanya mambo yanayotakiwa.

Ni muhimu sana tukapata chama mbadala chenye nguvu ili tuwe na demokrasia pevu yenye siasa safi za kuwatumikia wananchi na si kuwapora na kuwauwa kwa umasikini, maradhi na njaa...Bila kusahahu ujinga.

Mungu na aendelee kumlinda mzee wetu Mrema na iko siku Mungu atamlipa fadhila kwani pundits and cynists dont count to the powerful politics of common sense.
 
Mrema alikuwa mchapa kazi alipokuwa CCM.

Akitaka 'kufanikiwa' kisiasa arudi CCM, maana CCM ndio mambo yote ndani ya yote hapa Tanzania.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Tawala

Akitaka kufanikiwa kisiasa aende CHADEMA, maana CHADEMA ndio mambo yote ndani ya yote hapa Tanzania.

Kidumu cham cha CHADEMA

Kidumu chama Tawala kuanzia TARIME SASA ,NA TANZANIA YOTE 2010

waberoya
 
Yaani Dada angu umekaa huko porini mpaka matukio ya kisiasa ya kakupita ukafikiri bado Mrema ana prevail kwenye anga la siasa???

Hutakua tofauti na Kijana mmoja aliekaa Ulaya muda mrefu kurudi Bongo anasalimiwa mambo anaitikia WAAA! badala ya POA,SHEGA nk

Una maana kuwa sasa hivi ikipigwa muziki wa bakurutu aka zilipendwa hapo Tanzania vijana hawachezi????
 
Akitaka kufanikiwa kisiasa aende CHADEMA, maana CHADEMA ndio mambo yote ndani ya yote hapa Tanzania.

Kidumu cham cha CHADEMA

Kidumu chama Tawala kuanzia TARIME SASA ,NA TANZANIA YOTE 2010

waberoya

Hahahahaaaaaaa kwi kwi kwi kwi ... ... ...

Acha 'kudesa' mkuu.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Kidumu Chama Tawala
(Kiendelee kutawala hadi mwaka 2100).
 
Mwafirika,Nimependa mawazo yako but For sure Mzee wa kiraracha hawezi kuja na jipya.
 
Huenda amepotea ktk ramani maana hana ushauri wako wa karibu; njoo umsaidie; ila ukweli hayuko tena katk ramani ya siasa; kaungana na Mbatia ( Msaliti wa upinzani) kutoa tamko ambalo mwisho wake limewaaibisha akina NCCR kabisa; wanavamia Tarime bila kufanya tathmini; sisa mufilisi za Mbatia ndio tatizo kubwa kabisa NCCR inafutika kabla ya 2010, huenda tukawa na Democrats(Chadema) vs Republican (CCM) muda si mrefu tena baada ya uchaguzi 2010 hiyo ndio ndoto yangu na Watanzania sasa watapumua maana NCCR/DP/etc vyote vitakuwa sana na green party etc visivyo na ushawishi wa kutawala nchi ila kusindikiza tu
 
Muungwana Kithuku,

Unajua viongozi wetu hawana utamaduni wa kuandika historia yao kwenye vitabu kwa kizazi kijacho.

Mtu kama Lyatonga kaifanyia mengi sana nchi yetu na anaifahamu sana system yetu. NAAMINI ingekuwa wakati muafaka kwa upande wake kukaa chini na kuandika kitabu, atupe historia ya nchi yetu..Imagine jamaa amekaa usalama wa taifa, mambo ya ndani, very powerful deputy Prime Minister, wizara ya kazi na baadaye akawa very powerful opposition leader ambaye almanusura aing`oe serikali ya ccm Madarakani. Si mtu mdogo huyo...From the staunchest supporter of the CCM status quo to archy enemy of the system he faithfully worked hard to create and defend.

MWK kama ni ushauri, mwambieni mzee Mrema akae chini aandike kitabu..anayo mengi sana ya kuwaachia watanzania..who knows? na wengine tunaweza kujifunza kutoka kwenye uelewa wake. Kama ni kula atakula mrahaba wa kitabu chake! Thats the best of all the possible world for him.

Kwa sasa siasa haimfai tena Mrema. akitulia atapewa heshima ya mzee wa busara au mzee wa chama kama Mzee Mtei na wale wenye moyo na uwezo wa kupigania mabadiliko na demokrasia ya kweli katika nchi yetu.

Masanja,

Well said Masanja, I admire your advise!!! Bravo!!
 
Mwafrika wa Kike,
Mrema ni mzigo sasa hivi hana tena sauti wala ubavu wa kuweza kuisaidia Chadema isipokuwa kuipunguza nguvu zaidi. NI Mrema aliyeendesha kampeni kali kichini chini kuwashutumu Chadema na uongozi wake kuhusiana na msiba wa Wangwe...
Ni Mrema na Cheyo walioendesha kampeni za utengano pindi tu ilipoonekana nafasi ya wao kuchukua Tarime wakabakia msibani kufanya kampeni zao za kichini chini...Opportunist! - Mtu kama huyu hakuna haja ya kumwamini wala kumweka karibu.
Kifupi Mrema kisha laaniwa (cursed) ktk maswala ya Utawala!.. Amini maneno yangu, labda siku atakayo weza kutubu madhambi yake ya nyuma ndio anaweza funguliwa ukurasa mpya wa maisha yake.. he has blood in his hands!

Please explain this: "he has blood in his hands"; are you referring to Mwinyi tenure as a president; I can't see where he spilled blood; we understand Mr. Mkapa had one in Zanzzibar in 2001 January. I take Mrema as an opportunists like all of us (you and I), he made a gamble in politics: For his life. Think in other way if he was a hypocrite like others who survive in the jungle of politics; he could be a billionaire!! Give him a B+
 
Mrema akijiunga na Chadema itakuwa ndiyo mwanzo wa safari yake ( Chadema sio yeye) kwenda kaburini. Angalia track record yake! NCCR-Mageuzi kaiyumbisha na hadi sasa haija-recover. TLP nayo hivyo hivyo. Ni opportunist, populist na mpenda makuu. Ataisaidia nchi kama ataamua kustaafu badala ya kubaki na ndoto ya kuingia Ikulu.

Mkuu nakubaliana na wewe,,,ila kuna moja labda tutafakari!

Mrema alikuwa usalama wa Taifa,,,, Mabere anamjua sana (X and Y) kesi ya Mac Gee
Ni kada aliyesomea siasa pale Kigamboni na hata Bulgaria alienda,,,,,

Akaja kuwa mbunge wa huko Moshi Vijijini,,, baadae Waziri ambaye utendaji na ubabe wake ulitishia hata Rais wa nji hii (nchi hii). Naibu Waziri Mkuu ati,,,, unashangaa ndiyo! Na alipoondoka cheo chake akaondoka nacho.

Sisiemu wakamtuma kazi maalumu,,,, kuangamiza upinzani. Linganisha moja ya kauli za Mwalimu na hapa nanukuu "mpinzani wa kweli atatoka CCM" mwisho wa nukuu. Wapinzani wakaamini kuwa mpinzani wa kweli ni Lyatonga kwa sababu Mwalimu alisema! Ila tuangalie, Mrema alingana na wa usalama wa Taifa mwenzake Mabere na Masumbuko (Masumbuko alicheza mchezo asoujua) Wakajiunga na NCCR-Mageuzi. Tuliona vile chama kilivyokuwa machachari. Mara karibu na uchaguzi,,,, vurugu! Wewe ondoka,,,, siondoki mara mmoja huyooooooo TLP. Mzee akaukwaa Uenyekiti,,,, haya chama hiiichooo chama,,,, hadithi ikawa ile ile,,,, vurugu tupu. TLP haina kitu,,,,iko hoi ICU. Ni nani asiyejua hilo...Kampeni zilizopita aliwalaani Watanzania kuwa atalia na Mungu wasipomchagua. Mrema bado yuko sisiemu! Ndivyo niaminivyo bwana.

Mrema huyu huyu ametoa matamshi ya kumkashifu Baba wa Taifa kama alivyofanya Mtikila,,,,,Mrema hata Keko hakuiona ila Mtikila huyooooo Segerea.

Hakuna siku hata moja Mrema amewahi kuona mlango wa Gereza,,,, ana nini huyu? Anajua Sheria sana za nchi hii? Eti anaulizwa kwa nini hukuja mahakamani tarehe ya kesi yako,,,, anajibu nilipata lifti ya ndege kwenda kuangalia afya yangu kule KCMC! Hakimu anaridhika! Loh! ni sababu kweli hii?

Wengine wakipigwa mabomu na kupelekwa Gereza la Karanga kule Moshi,,, yeye sukari imepanda yuko Kitandani KCMC na ulinzi wa uhakika. Usalama wa Taifa hauachwi kiholela namna hiyo! Yaliyomkuta Kombe tunayajua. Jamani Agustino Lyatonga ni pandikizi la CCM na si vinginevyo! nataka niamini hivyo,,, simlazimishi mtu kuamini ila mimi ninaamini hivyo.
 
with all due respect to mwafrika wa kike naomba niseme kuwa una dhumuni la kuiua chadema!

mimi si mwanachama wa chama chochote ila naangalia tu maslahi ya watanzania kwa ujumla, kwa kweli tunaitaji upinzani wenye nguvu na currently ni chadema na cuf.

tukiangalia historia, kila chama alichoingia Mrema baada ya kutoka ccm kilikufa kisisasa, sasa kumuomba aingie chadema ni kukuia chadema bila ubishi.

kwanza afadhali angeingia zamani, sasa hivi ndio hafai kabisa, abaki hukohuko!
 
with all due respect to mwafrika wa kike naomba niseme kuwa una dhumuni la kuiua chadema!

mimi si mwanachama wa chama chochote ila naangalia tu maslahi ya watanzania kwa ujumla, kwa kweli tunaitaji upinzani wenye nguvu na currently ni chadema na cuf.

tukiangalia historia, kila chama alichoingia Mrema baada ya kutoka ccm kilikufa kisisasa, sasa kumuomba aingie chadema ni kukuia chadema bila ubishi.

kwanza afadhali angeingia zamani, sasa hivi ndio hafai kabisa, abaki hukohuko!
Karibu sana JF, nakubaliana na wewe Mrema is a moving corpse kisiasa!
 
Mwafrika wa Kike,
Mrema ni mzigo sasa hivi hana tena sauti wala ubavu wa kuweza kuisaidia Chadema isipokuwa kuipunguza nguvu zaidi. NI Mrema aliyeendesha kampeni kali kichini chini kuwashutumu Chadema na uongozi wake kuhusiana na msiba wa Wangwe...
Ni Mrema na Cheyo walioendesha kampeni za utengano pindi tu ilipoonekana nafasi ya wao kuchukua Tarime wakabakia msibani kufanya kampeni zao za kichini chini...Opportunist! - Mtu kama huyu hakuna haja ya kumwamini wala kumweka karibu.
Kifupi Mrema kisha laaniwa (cursed) ktk maswala ya Utawala!.. Amini maneno yangu, labda siku atakayo weza kutubu madhambi yake ya nyuma ndio anaweza funguliwa ukurasa mpya wa maisha yake.. he has blood in his hands!

Mkandara,

Inaonekana dhambi aliyofanya Mrema haitokuwa rahisi kusameheka hasa pia ukichukulia majibu ya wachangiaji hapa. Na kama Mrema amelaaniwa (na yule aliyemlaani ameshakufa) basi kuna kazi kweli kweli.

Inawezekena yote yanayosemwa hapa juu yake ni kweli lakini pia aliyofanya Mrema kwa nchi hii yanafahamika pia. Mimi nimeshauri kuwa Mrema ajiunge na CHADEMA. Sikusema kuwa apewe uongozi ndani ya chama ila anaweza kuwa kama mshauri au mzee wa baraza wakati huo huo akiwapa moyo vijana wote wanaochipukia ndani ya CHADEMA.

Huu ni mtizamo wangu, ninaamini kuwa binadamu wanaweza kuweka hisia na tofauti zao mbali na wakajenga umoja mzuri (kama mama clinton na Obama). Ila pia kama inaonekana ni vigumu kiasi hiki basi ni vizuri mzee wa kiraracha na mkombozi wa wanawake akastaafu sasa kuliko kuendeleza kambi nyingine ya upinzani na kudhoofisha upinzani.

Hawa kina Mbatia, Mvungi na Mtikila ndio hivyo wamejichimbia kaburi lao la kisiasa na sioni namna ya kuwasaidia hapa. Nimekuwa namsapoti Mrema kwa miaka mingi sana na probably nitaendelea kumpenda na kumheshimu huyu baba kwa yote aliyoifanyia Tanzania. Wakati ambapo sasa ninamove on na a new kid in town - CHADEMA, nilitaka kuhakikisha kuwa Mrema anapata ride kwenye hii fast moving train.

Otherwise, kuhusu bash ya motor city - ni proposal tu ilitolewa jana na mkjj na mimi nikaiunga mkono. Kama ikipata wahusika wengi basi utapata message mzee bila wasiwasi yoyote. Kwa wengine wote -mushi, mtanzania na wengine wote, nashukuru kukaribishwa. Life iko bize lakini kwa kadri iwezekanavyo kila mara tutaendeleza mijadala hapa na struggle hii kwa ajili ya future ya nchi hii na watoto na vijukuu vyetu.
 
Mkuu JMUSH!,

Sina cha kuongezea bro. Mangi umeteta!
Shukran Mkuu..Cha kushangaza hapa, Wale wote wanaodai kuwa MremA KESHAKUFA ni wana ccm...Hapa jamvini hao wote wanaopinga hili la Mrema si wapinzani...Hapo sasa utaona pili pili wasiyoila still inawawasha.

Toka lini hao wana ccm wawe na nia nzuri na upinzani eti kuwashauri kuwa Mrema si mpinzani mwenzao?

Kuna member hapa ambao ni chadema na wao wataleta maoni yao....Cha msingi hapa ni heshima ya Mrema ambayo ni wazi kuwa utovu wa fadhila uliobobea na utovu wa nidhamu uliokubuhu ndiyo reflection sahihi ya wale wenye kudai eti Mrema hafai na ajiuzulu ale pensheni...Kazi bado haijaisha na Mzee wa Kiraracha bado tunamuhitaji...Kama wanataka kushinda ni lazima waje pamoja.
 
Mheshimiwa Mrema,
Nakuomba sana uungane nguvu na wadogo zako na watoto wako kina Zitto, Dr Slaa, Mbowe, Mwera, na wapenda maendeleo ambao wanaendeleza yale yote ambayo umekuwa unapigania. Nakuomba ujiunge na CHADEMA ili ujenge chama chenye nguvu zaidi ya kuwaletea watanzania maendeleo. Kuna watu wenye chuki za kikabila watasema kuwa kujiunga kwako na CHADEMA kutakifanya kiwe cha wakasikazini. Jibu la swali hilo liko kwenye speeches za Barack Obama ambazo amekuwa anasema hapa USA kwenye kampeni zake, kama wewe ni mzungu na unazama baharini, je kama akitokea mtu mweusi kwenye boti akakurushia life line ili kuokoa maisha yako, je utaikataa kwa vile tu huyo mwokozi wako ni mweusi? Mama yangu alishalijibu hili swali pale alipokubali kuanza maisha na mchaga. Haijalishi rangi au kabila ya mtu inapokuja kwenye suala la maisha na kifo.
Asante

I mean, seriously: this is a very terrible idea! CHADEMA wanachotakiwa kufanya sasa hivi ni kulikuruti wasomi vijana wenye mvuto wa kupendwa na wananchi wa kawaida. Tumia pesa za ruzuku kuzunguka mashule, vyuoni, na hata nje ya nchi kuwalikuruti watanzania wenye nguvu ya kushawishi umma ili wajiunge na CHADEMA. Now is no time for old faces like Mrema or Marando or Ramwai. Kuzikaribisha hizi faces ndani ya CHADEMA ni kukaribisha drama ndani ya chama, hence kukiua chama.
 
with all due respect to mwafrika wa kike naomba niseme kuwa una dhumuni la kuiua chadema!

mimi si mwanachama wa chama chochote ila naangalia tu maslahi ya watanzania kwa ujumla, kwa kweli tunaitaji upinzani wenye nguvu na currently ni chadema na cuf.

tukiangalia historia, kila chama alichoingia Mrema baada ya kutoka ccm kilikufa kisisasa, sasa kumuomba aingie chadema ni kukuia chadema bila ubishi.

kwanza afadhali angeingia zamani, sasa hivi ndio hafai kabisa, abaki hukohuko!


Hapo sawa, unapotaja CHADEMA na CUF.

Sidhani kama Mrema ana ubavu wa kuiua CHADEMA. Huko alikovurunda ilitokea hivyo kwa sababu walimruhusu. Kama ana madhara yoyote, CHADEMA wanalitambua hilo na wala hawatamkaribisha chumbani, ataishia sebuleni tu kama sio barazani.


Si kwamba aende kuongeza nguvu huko CHADEMA, la hasha. Kama inavyosemwa hapa, pamoja na mapungufu yake, Mrema ni alama muhimu. Labda mtu anithibitishie vinginevyo, mimi bado namwona kama mpiganaji na kielelezo katika kupigania haki ya mnyonge. Tumsome vizuri tujue angependa kutumikaje katika umri wake huu. He can indeed be very useful!




.
 
Mrema alikuwa mchapa kazi alipokuwa CCM.

Akitaka 'kufanikiwa' kisiasa arudi CCM, maana CCM ndio mambo yote ndani ya yote hapa Tanzania.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Tawala

Kwa taarifa tu alishawahi kufanya mazungumzo na CCM kuhusiana na hilo. Bei yake ilikuwa ni kuachiwa jimbo la Vunjo ili amalizie maisha yake ya kisiasa huko, sijafuatilia kujua hatma ya mazungumzo haya ilikuwa nini
 
Sawa Mkuu,

Watukanaji wameshanitukana na mods wakakaa kimya.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Tawala.


Mkuu wakati mwingie unawachokoza, umeisha sisikika

Kigumu Chama Cha Mapinduzi

Kigumu Chama Tawala na Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti
....sasa mkuu wewe huchangii hoja una kuja kila wakati na chorus yako, bila shaka unatafuta matusi mengine

ushi
 
Back
Top Bottom