Ombi maalumu kwa Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi maalumu kwa Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwafrika wa Kike, Oct 13, 2008.

 1. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Mrema,

  Najua kuna wengi watasema kuwa hili haliwezekani au halitakiwi kuwezekana. Najua kuna wengi watakataa kabisa kulipa hili jambo nafasi. Najua kuwa wapo pia wengi ambao watasema kuwa huu ni upotevu wa muda.

  Hii imekuwa kawaida ya wengi wetu kuangalia yasiyowezekana zaidi ya kuwa na muda wa kuangalia yanayowezekana. Wakati nikiwa kitoto kichanga, mama yangu alitumia muda kabla ya kulala kuniambia ni jinsi gani yanayooneka kuwa magumu yanaweza kufanyika. Hajachoka kunikumbusha waliosema kuwa yeye kama Mhaya asingeweza kuolewa na kijana wa kichaga na wakaishi kwa raha na amani maisha yao yote. Maisha yote haya yeye na dadi wamewathibitishia ma-naysayers kuwa mengi sana yanawezekana.

  Mheshimiwa Mrema AKA mzee wa kiraracha AKA mzee wa pilau AKA mzee wa mabomu AKA (tena muhimu sana) mkombozi wa wanawake Tanzania, naomba sana tena sana ufikirie sana ombi langu hili kwako. Kwa miaka yote hii familia yangu imekuwa inakuunga mkono katika juhudi zako za kupigania demokrasia na maendeleo tena. Familia yangu imekuwa nawe katika kutetea masilahi ya wanawake Tanzania. Na zaidi sana, sisi na watanzania wengi sana tumekuwa nawe katika misukosuko yote (ukiwemo ule ambapo mimi na dada zangu wote kwa pamoja tulipigwa mabomu ya machozi na polisi Tanzania bila sababu ya msingi tukihudhuria mkutano wako).

  Mheshimiwa Mrema, mengi umeyafanya kwa ajili ya hii nchi yetu. Wengi hapa watakuita kichaa (kama alivyofanya mkapa na usalama wake wa taifa), chizi, au jina lolote lile watakalopenda. Hata hivyo historia ya Tanzania itakumbuka ulivyomsimamia Mama Siti na wezi wenzake pale Airport ili kuzuia dhahabu na vingine vilivyokuwa tayari kutoroshwa. Wengi tunakukumbuka kwa kupigana na mafisadi wakati ule ambao wengi tukiwa bado tunamuogopa baba wa taifa na kifimbo chake.

  Kwa haya yote na mengine mengi ambayo nimekuwa nayasema hapa, naomba sana ufikirie mwelekeo na hatima ya nchi yetu sasa hivi zaidi kuliko mwaka ule wa 1994 ulivyojiunga rasmi na upinzani na ukaleta nguvu na hamasa kubwa na ya pekee.

  Nakuomba sana uungane nguvu na wadogo zako na watoto wako kina Zitto, Dr Slaa, Mbowe, Mwera, na wapenda maendeleo ambao wanaendeleza yale yote ambayo umekuwa unapigania. Nakuomba ujiunge na CHADEMA ili ujenge chama chenye nguvu zaidi ya kuwaletea watanzania maendeleo. Kuna watu wenye chuki za kikabila watasema kuwa kujiunga kwako na CHADEMA kutakifanya kiwe cha wakasikazini. Jibu la swali hilo liko kwenye speeches za Barack Obama ambazo amekuwa anasema hapa USA kwenye kampeni zake, kama wewe ni mzungu na unazama baharini, je kama akitokea mtu mweusi kwenye boti akakurushia life line ili kuokoa maisha yako, je utaikataa kwa vile tu huyo mwokozi wako ni mweusi? Mama yangu alishalijibu hili swali pale alipokubali kuanza maisha na mchaga. Haijalishi rangi au kabila ya mtu inapokuja kwenye suala la maisha na kifo.

  Haijalishi asili au kabila pale inapokuja kwenye masuala ya maendeleo. Zaidi sana, haitajalisha sana yaliyotokea huko nyuma kama kitakachofanyika sasa hivi ni kitu muhimu sana kwa watanzania wote. Mheshimiwa Mrema, tafadhali sana jiunge na wenzako ili kuongeza nguvu mapambano dhidi ya mafisadi wa Tanzania.

  Asante
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Duh kumbe mrema bado yuko huyu si ameshakufa kisiasa na tumeshamzika jamani ?
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  welcome back Mwafrika wa Kike....I really missed you!
   
 4. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umerudi .....naona watu walikuwa wanakutafuta sana
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Mrema alipotoka CCM, CHADEMA ndio walikuwa wa kwanza kumfata lakini aka-opt kwenda NCCR kwa kuwa alipewa offer ya uenyekiti. Mbowe atakuwa tayari kumpisha huyu?
   
 6. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante Ogah
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Welcome Back!

  You made me log on immediately. I had to double check whether this was today's post, just to make sure i ain't trippin'. Sorry wont talk about Mh. Mrema for now (mods will have to move my post if possible)

  Hapa jamvini, ulituumiza roho wengine unajua... personally i was so worried where you were: https://www.jamiiforums.com/complaints-congrats-advice/9426-wana-jamii-forums-hawa-wako-wapi-currently-most-sought-after-kadampinzan-mwafrika-wa-kike.html, i kept on asking, hamna hata mmoja aliyejua. Daaah, Welcome Back!

  Here is something to get you goin':

  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=qGT0gIY_-jw"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
  SteveD.​
   
  Last edited: Jul 9, 2009
 8. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante SteveD,

  Nimeipenda hiyo nyimbo ya Mase.....

  Asante sana
   
 9. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Yaani Dada angu umekaa huko porini mpaka matukio ya kisiasa ya kakupita ukafikiri bado Mrema ana prevail kwenye anga la siasa???

  Hutakua tofauti na Kijana mmoja aliekaa Ulaya muda mrefu kurudi Bongo anasalimiwa mambo anaitikia WAAA! badala ya POA,SHEGA nk
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mrema ahakikishiwe na CHADEMA atagombea uraisi 2010, atatia timu
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo nadhani ni mentality ya wapinzani. Wengi wanaonekana wanataka kuwa na madaraka kila wanapokwenda. Ushauri wa kumtaka Mrema ajiunge Chadema unaweza kuboreshwa kwa kumtaka aiue TLP na kuiunganisha na Chadema na kuwa na chama kimoja. Ni ushauri mzuri.
  Awali, katika hotuba zake wakati wa ushirikiano wa vyama vinne uliovunjika, Mrema alionyeshsa (kwa maneno) kuwa yupo tayari kutogombea urais ili kumpisha kiongozi mwingine ATAKAYEKUBALIWA na wapinzani. hakusema kuwa yeye hatogombea. Hii inaonyesha kuwa bado ana dhamira ya jambo hilo.
  haiyumkini pia kuwa atakapiongia Chadema hatotaka madaraka huko.
  Lakini ni juu ya Mrema kulifikiria hili ombi na kutoa majibu. Hivi yumo humu?
   
 12. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mimi binafsi sikuwa nakujua,,,, ila kuna mtu alulizia humu Mwafrika wa Kike yuko wapi,,, hata hivyo pia nakukaribisha
  Mrema is no longer in game,,,, anachezea daraja la tano sijui!
  Ila ukimwona sijui anajichubua siku hizi? CCM wamemchoka wamerudi kwa Mtikila sasa. Sisiemu wamegundua kuwa Watanzania wamemchoka wanataka kubadilisha sura ya mchezo kidogo,,,,, MTIKILA aka Mtanganyika, aka Mzee wa Ankara za EPA kwa Rostam, aka mzee wa mawe tarime.
  Welcome back
   
 13. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mrema haeleweki kwa kweli! CHADEMA hawawezi kukubali kupokea garasa!
   
 14. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni kweli amanigk kuwa Mrema anafifia kisiasa (ukichukulia vita kubwa sana aliyopigwa na Mkapa na vijana wa TISS) lakini hekima zake na ujasiri wake ni hazina nzuri inayoweza kutumiwa na vijana wanaochipukia kisiasa CHADEMA na kwingine kote Tanzania.
   
 15. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  asante deny_all...... hiyo avatar yako imetulia sana
   
 16. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bila kusahau 'old is gold' Kama kweli atajitoa publically na kuwaomba wafuasi wake wakubaliane naye ku resolve chama chake ndani a Chadema, si kwamba itamsaidia yeye kumalizia ngwe yake vyema, bali pia itasaidia kutoa hamasa na mwamko mpya ndani ya chama mbadala aka Chadema.

  Usisahau kwamba ukienda hko pembezoni mwa bongo walio pigika na ccm ukiwauliza habari ya uchaguzi wana kiri kweli ccm wamiechoka, mbadala wana kwambia watampa Mrema, kwahiyo bado yumo japo hawavumi sehemu za mijini! kwahiyo yeye akiunga humo atasaidia sana huko sehemu za pembezoni kuinua chama kikubwa kitakacho weza pambana na mafisadi!

  Si hilo tu, hata CUF, wakiendelea kujitofautisha na vibaraka NNCR na wakati wa uchaguzi wakatumia mfumo wa kussupotiana pale wanapo kubalika kati ya CUF na chadema 2010 kitaeleweka sana! I wish mambo yangekuwa hivi
   
 17. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Hahahaha
  Mzee umenichekesha.  .
   
 18. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #18
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mrema ndiye aliyekidhoofisha Chadema mara ya kwanza.

  Chadema ndio chama kilichokuwa na nguvu kuliko vyote vya upinzani kilipoanza.Kilipoanza kikiwa na wanachama Wachaga wengi kibao wenye uwezo mkubwa kifedha na mori wa kutaka mabadiliko.

  Mrema kukataa Chadema na kwenda NCCR nadhani ilikuwa mbinu ya kiakili sana ya kuiua Chadema kiujanja ya kuhamisha wachaga wenye uwezo kutoka CHADEMA wamfuate NCCR kwa kuwa alikuwa mgombea Uraisi Mchaga mwenye nguvu aliyekuwa akielekea kuwa pengine aweza kushinda.Mbinu hiyo ilifanikiwa.

  Alipoamua kugombea uraisi NCCR, kweli wachaga wengi na mali zao walihama CHADEMA wakaenda NCCR kumuunga mkono MREMA.Baada ya wengi kuhama Chadema, CHADEMA ilidhoofika ikawa chama dhaifu kisichokuwa na nguvu kabisa.Chama kikuu cha upinzani kikawa NCCR.

  Alipofika NCCR alikivuruga hicho chama hadi akakisambaratisha na kwenda zake TLP akaendelee na ajenda zake za kusambaratisha.Alipohama NCCR kwenda TLP wachaga wenye uwezo wengi isipokuwa wachache wakagoma kuhama naye kwa kuona hana ajenda zaidi ya kuwapotezea muda na mali zao.Wengine wakaenda CCM,Wengine wakabaki NCCR,Wengine wakarudi CHADEMA na wengine wakaapa hawaji kugusa siasa tena kutokana na mali zao kupotea kwa michango ya chama au kujihusisha na Siasa kulikowaletea misukosuko na dola ya chama tawala kwa biashara zao kuathirika n.k

  Bahati nzuri Mbowe aliposhika uenyekiti akaanza kujenga upya Chadema kwa nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya hadi kukirudisha enzi za utukufu wake na kuzidi hadi kufikisha hapo kwenye ushindi wa Tarime.

  Sasa Utukufu wa Chadema umerudi mtu anasema Mrema aende tena Chadema kufanya nini? …Watu wameshindwa uchaguzi sasa wanataka Mrema aende akaue Chadema!!!
   
 19. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Uliyosema hapa yanawezekana kuwa yote ni ya ukweli mtupu. Hata hivyo, siri kubwa ya mafanikio katika siasa, ni watu wenye muelekeo na mawazo yenye kufanana, kusahau uadui na utofauti wao na kujenga future yenye nguvu.

  Hapa US, Mama Clinton na Obama walipambana na kutoleana maneno mengi sana wakati wa primaries. Sasa hivi wameungana na kuweka tofauti zao zote pembeni ili kujenga umoja wenye nguvu. Ombi langu ni kwa mrema kujiunga na Chadema (na sio kwa mrema kujiunga ili awe kiongozi wa Chadema).

  Hata hivyo nimependa pia your point of view kwenye hili.
   
 20. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mrema alikuwa mchapa kazi alipokuwa CCM.

  Akitaka 'kufanikiwa' kisiasa arudi CCM, maana CCM ndio mambo yote ndani ya yote hapa Tanzania.

  Kidumu Chama Cha Mapinduzi

  Kidumu Chama Tawala
   
Loading...