Ofisi ya Kata wanashirikiana na baba yangu mzazi kuninyima haki yangu ya mali

Kabisa Mkuu ila mimi sidhani kama mzazi ananafasi ya kulaumiwa hapa labda tulaumu chuo alikopata hiyo degree.

Mzazi kacheza part yake kumsomesha ni wachache wanapata fursa hiyo,

Imagine kwa umri huo bado jamaa linamshitaki baba ake likidai mgao eti ni haki yake.

Na watoto yatima wako mitaani waseme aje, asipoangalia tamaa na ujinga utamjaa kisha atamtoa kafara mzee wake.
Mzee lazima aingie kwenye lawama maana hajakuza vizuri ile spirit ya uchapaji kazi hakuiingiza ndani ya mwanae uyo ndio maana ana lilia mali.

Trust me Malezi yanachangia big time kumshape mtoto. Kama asifiwavyo mzazi pale mwanae afanyapo mazuri basi vice versa is true lawama ziende kwao kokote waliko
 
Ungekuwa chini ya miaka 18 ungesaidiwa
usipoteze mda ndio nyie mnaua wazazi mpate uridhi mikono si unayo ungekuwa mlemavu sawa
 
Ni Kikohozi kweli kweli!
Mwenye mali anauza mali yake kuna mtu si mali yake anataka mgao utani huu.
Unatakiwa kupigwa na bomba la kufungulia tairi kichwani maana huna faida yoyote, labda uwe unafanya mzaha.
 
Ulivyoandika wengi hawajakuelewa, Mimi binafsi nimehangaika na familia ya Baba yangu, nimepoteza muda mwingi kuwahangaikia wadogo zangu na kaka zangu, nimewatafutia kazi wote, sasa hivi wana maisha mazuri sana. Lakini wote wamenitosa , hata kuwaona watoto wangu tu hawataki wanasema kila mtu ahangaike na mzigo iiiii
 
Ila Mungu mkubwa, sasa hivi wenyewe ndio wanakuja kuniomba msaada, nawaangalia tu, ila nawasidia ingawaje wanajisikia aibu. Mali za Baba nilisha waachia walinipa kadri walivyopenda.
Ila maisha yangu yanasonga kwa kiwango cha sgr
 
Mzee lazima aingie kwenye lawama maana hajakuza vizuri ile spirit ya uchapaji kazi hakuiingiza ndani ya mwanae uyo ndio maana ana lilia mali.

Trust me Malezi yanachangia big time kumshape mtoto. Kama asiwavyo mzazi pale mwanae afanyapo mazuri basi vice versa is true lawama ziende kwao kokote waliko
Nakubaliana na wewe mkuu malezi yanachangia pakubwa kumshape mtu tabia.
 
Ni Kikohozi kweli kweli!
Mwenye mali anauza mali yake kuna mtu si mali yake anataka mgao utani huu.
Unatakiwa kupigwa na bomba la kufungulia tairi kichwani maana huna faida yoyote, labda uwe unafanya mzaha.
Mkuu, nilichogundua kwa mtoa mada ni kwamba amechangia pakubwa kuendeleza familia, ila kuna baadhi ya ndugu hawana shughuli yoyote wameamua kumtenga kwa maana yeye ana uwezo. Ni shida moja mbaya sana.
 
Wewe jamaa nilikuambia kwenye thread ya mwanzo mambo ya msingi sana, kama unaweza naomba urudi ukasome. Usiposikia haya unayoambiwa, kuna siku utakuja kujuta sana.
Mind yako inakudanganya sana, utakuja kumchukia mzazi wako bure au kufanya kitendo kibaya zaidi kama kwenda kwa waganga au kumuua mzee wako. Wanaokushauri uendelee na unachofanya hawakutakii mema.
 
Kwa majibu ambayo mtoa mada aliyapata kwenye thread yake ya awali, sikutarajia kama angeandika uzi unaofanana na wa awali.

Kwa umri huo hata uende mahakama kuu, watasikiliza tu halafu waendelee na mengine. Huwezi pata chochote,maana haingii akilini udai mali ambazo sio zako. Ukizingatia mwenye mali yupo na afya tele.
 
Habarini ndugu zangu, pole na majukumu ya hapa na pale niende moja kwa moja kwenye maada usika, mimi ni Kijana mwenye umri wa miaka 42 (nimetimiza mwaka huu mwezi wa 1, tarehe 6 nashukuru Mungu nimeona mwaka na kuongeza mwaka),

Yapata week 3 sasa tangu nilete uzi wangu hapa kuwa baba yangu ameuza nyumba yake na hataki kunipatia japo pesa kidogo mimi mtoto wake nikaanze maisha, na nilikuja kwenu kuomba ushauri, baada ya kupata baadhi ya ushauri mzuri na mwingine wa kejeri na maneno makali, nikaamua nifanye yafuatayo.

Nikaenda kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa kumueleza ili suala nikaona mwenyekiti wa Serikali za mtaa nae kama anataka kunizunguka, maana baada ya kumueleza mwenyekiti akaniambia atalishughulikia badala yake wakati naondoka akampigia mzee simu na kumueleza kuwa nimeenda kuripoti kwake ili nipate mgao. Nikaona huyu mwenyekiti hatokuwa na msaada kwangu, nikapanda kwa maboss wake ambao ni ofisi ya kata

Baada ya kufika ofisi ya kata nikaelezea mkasa mzima wa baba yangu kuuza nyumba yake na hataki kunipa mgao wa hela mimi mtoto wake ambaye natakiwa nipate haki yangu nikaanze maisha yangu, ofisi ya kata walisikitika sana na kuahidi kunisaidia kwa hali na mali, na kuniambia watamuandikia barua baba angu ili aweze kufika na kueleza kwanini ananipa manyanyaso mimi mtoto wake kwenye mali ambazo na mimi nastahili mgao.

Leo asubuhi nimeitwa kwenye ofisi ya kata mimi na baba, tumefika pale cha kushangaza ofisi ya kata wote wanaanza kunishambulia mimi kwa maneno makali sana, ndugu zangu nimeumia sana na mimewaeleza nitapanda ngazi za juu zaidi ili niweze kupata haki yangu Ikiwezekana hata mahakamni nitafika haiwezekani mimi mtoto niwe naagaika hivi wakati baba yangu pesa anayo tena ni kubwa tu. Na nimepata wasiwasi mkubwa watu wote wanasimama na baba ni kwasababu ana pesa huenda wanataka pesa zake ndio maana wanaona mimi sina hela.

WanaJamiiForums nisaidieni niweze kupata mali kutoka kwa baba yangu, najua kuna wanasheria humu ndani.

Naumia sana kwa haya manyanyaso ninayopitia ukilinganisha mimi ndio mtoto ambaye nina elimu kubwa sana kupita wote pale nyumbani (nina Bcom in marketing ) kutoka chuo kikuu cha DAR ES SALAAM-UDBS, pia nina Basic Certificate ya computer application natakiwa nipewe kipaumbele kwa kila kitu kwenye kuendeleza mali za mzee.
Kisheria,Mali hizo no A babako na mamako. Hats ukienda mahakama gani hautapata chochote. Acha uvivu,tafuta vya kwako.
 
Miaka 42 una mke bado unalilia mali ya baba??.uyo mwanamke nae bado anakuvumilia tu
Kwani mkuu limesema lina mke? Kwanza miaka 42 siyo kijana huyo! Halafu inakuwaje miaka 42 bado linajambia makochi ya mzee tu? Mimi ningekuwa ndiye babake na hili tutusa ningelipeleka kwanza kupima DNA huenda siyo kitoto langu!
 
Nilianza kujitegemea mara tu nilipomaliza chuo bila kujalisha sina ajira na niwashukuru wazazi kwa urithi sahihi wa elimu walionipa.

Nakosa nikushauri nini ila unaidhalilisha elimu ya UDSM kwa upofu wa nawazo. Pambana kutafuta mali zako kaka acha uboya huo. Miaka 42 eti kijana?? Wewe ni mzee usie jielewa. Kwenye kuna shida sana hapa bongo
 
Pole sana baba ako anayo roho mbaya sana amepata zaidi ya milioni mia anashindwa hata kukupa milioni 2 kweli lakini inawezekana baba ako analishwa maneno na mtu wake wa karibu kama mama yako ni wakambo basi tegemea ndugu kukosa kabisa.kwa kweli ni aibu sana
 
Back
Top Bottom