Offer ya Rostam kwa familia ya Dan Mwakiteleko

Offer ya Rostam kwa familia ya Dan Mwakiteleko

Hivi mshahara wa miaka 20 wa huyu mfanyakazi ilikuwa ni kiasi gani? Je alikuwa anafanya kazi gani? Mazingara ya kifo chake yakoje? Mwenye kujua anaweza kutujuza ili na sisi tuwe na mwanga japo kiduchu.

BTW hiyo offer ya RA ni ya shillingi / dollar ngapi maana bongo hawajachacha kwa kutumia forex.
 
huu uzushi....wafanyakazi hawalipwi mshahara huu ni unafiki. hata nssf hawapeleki michango
 
kwani wafanyakazi wa New Habari Corporation hawana pension?
Mkuu, hizi rambirambi ambazo hazipo kwenye HR Manual sio za kushabikia.Hiyo ni rambirambi, sio stahili kwa mujibu wa terms za kazi yake.Sio kwamba akifa dereva wa habari coperation basi mjane wake atapewa kama alivyopewa mhariri, and to me that is stupid.
 
Kwa ili Rostam, Congrats!
I still object!Sioni mantiki coz anatakiwa kuwa na mpango wa kuwasaidia wafanyakazi wake, ambao upo documented, badala ya bashe kumpigia rostam cm na kuamua tu huyo tumpe kiasi hiki.
 
Mlitegemea nini RA asitoe chochote na huyu alikuwa mstari wa mbele kumsafisha RA na EL, huoni kamandi nzima ya mafisadi ilikuweko kutoa rambirambi mpaka na Mr ma-rope pia.
 
Bashe kama MD ametangaza msibani kuwa mjane ataendelea kupokea mshahara wa mumewe kwa miaka mitano,na dependants wawili wa shule ya msingi na wa chuo wataendelea na masomo kwa hisani ya habari cooperation.
RA anaitaji pongezi kwa ilo
Source :ch ten 19hrs news

Ok tumpongeze lakini
Hiyo ni favour kwa kwa mtu mmja tu au ndio muundo wa utumishi habari corporation ulivyo? vitu kama hivi vinaeleza jinsi watanzania tunavyopima watu hasa wanasiasa kwa mambo madogo madogo.
 
Offer ya Rostam kwa familia ya hayati Dan Mwakiteleko ni mfano wa kuigwa na waajiri. Ni ishara dhahiri kwamba mchango wake katika majukumu aliyokabidhiwa yamethaminiwa na bado angali kioo cha utendaji kwenye stuff aliyoiacha.

Nimeongea mara kadhaa hatuchukii mtu tunachukia hoja au matendo maovu, kwani mtu anaweza kubadilika ila tendo likishatendeka huwa halibadiliki sawa na kumwaga maji mchangani. Pamoja na mengi yaliyotendeka ndani ya serikali Rostam akitazamwa na wengi kama ndiye mbunifu lakini inakuja fahamikia uzao nao una taabu, maana kuna wenye makosa makubwa zaidi ya rostam na tunaona movie inavyoendelea.

Rostam tunashukuru kwa utu na uungwana wako, kosa ni kibinadamu lakini kurudia kosa ndio ubaya.
 
Mkuu, hizi rambirambi ambazo hazipo kwenye HR Manual sio za kushabikia.Hiyo ni rambirambi, sio stahili kwa mujibu wa terms za kazi yake.Sio kwamba akifa dereva wa habari coperation basi mjane wake atapewa kama alivyopewa mhariri, and to me that is stupid.

Ok tumpongeze lakini
Hiyo ni favour kwa kwa mtu mmja tu au ndio muundo wa utumishi habari corporation ulivyo? vitu kama hivi vinaeleza jinsi watanzania tunavyopima watu hasa wanasiasa kwa mambo madogo madogo.
Ndio maana nilisema hapa hamna kitu, ni chezo tu la kupumbaza watu
Penye uzia penyeza rupia, hebu waulize watumishi waliopo hapo habari corp ndio utapata picha kamili
 
Kama Muuaji kama Kagame mwenye damu mkononi kwake amejirekebisha na anaiendesha na kuiendeleza vizuri Rwanda

Kwanini Rostam ambaye ni Mwizi lakini anatoa kusaidi familia iliyoondokewa na baba yao as a bread winner tusipongeze? Ni bora kumkumbatia Mwizi kuliko Muuaji Mwenye Damu Mikononi Mwake.
 
Ndio maana nilisema hapa hamna kitu, ni chezo tu la kupumbaza watu
Penye uzia penyeza rupia, hebu waulize watumishi waliopo hapo habari corp ndio utapata picha kamili

Watanzania tuwe na mtazamo mpana, upendo na simanzi ya Rostam kwa familia ya marehemu inaonjeka na kuwa mwango wenye mapenzi mema. Achaneni na chuki, kwani chuki huzaa uadui, upendo huzaa amani na utulivu. Mnataka hata kumfikilisi Rostam agaiwie mapesa kwa kila mtu kwa kiwango gani? Sina maana ya kutetea ya Rostam ila tuwe na fikra pana, lakini kubeza kila chema si kustaarabika, anapofanya mazuri tumpongeze ndio ukomavu. Ninyi ndio wale wanaochukua siasa za jukwaani na kuzihusisha na maisha ya kawaida. Tukishateremka Jukwaani tunaendelea na maisha ya kijamii pamoja bila chuki.

Nadhani wengine wanajicho tofauti na jinsi Mbowe anavyohudhuiria maziko ya ndugu wa viongozi waaandamizi wa Chama cha Mapindizi, huku ndiko kukomaa si kuchukia mtu na watu ila tunapingana hoja.
 
Tusiwe wepesi kumpongeza kwani kutoa ahadi mbele ya kadamnasi ni rahisi kuliko kuzitekeleza hizo ahadi; mifano mingi tunao ya wanasiasa kutoa ahadi nyingi kwa wanannchi lakini hawazitimizi!! Mmekwisha sahau ahadi za swahiba wake za MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA? Ikumbukwe kwamba wafanyakazi wake wamagazeti huwa wanasota kwa muda mrefu bila kupata mishahara kwahiyo hata hii ahadi itafuata mkumbo huo huo.

...Kila ninaposoma maandiko/maandishi, natafuta neno "lakini", hapo ndipo ujumbe mahsusi unapokuwa umewekwa. The rest is just water to push a bitter pill!
 
JAMBO JEMA!!

Can u imagine kama marehemu wakati wa uhai wake angejua hili litatokea angefanya nini?
 
Watanzania tuwe na mtazamo mpana, upendo na simanzi ya Rostam kwa familia ya marehemu inaonjeka na kuwa mwango wenye mapenzi mema. Achaneni na chuki, kwani chuki huzaa uadui, upendo huzaa amani na utulivu. Mnataka hata kumfikilisi Rostam agaiwie mapesa kwa kila mtu kwa kiwango gani? Sina maana ya kutetea ya Rostam ila tuwe na fikra pana, lakini kubeza kila chema si kustaarabika, anapofanya mazuri tumpongeze ndio ukomavu. Ninyi ndio wale wanaochukua siasa za jukwaani na kuzihusisha na maisha ya kawaida. Tukishateremka Jukwaani tunaendelea na maisha ya kijamii pamoja bila chuki.

Nadhani wengine wanajicho tofauti na jinsi Mbowe anavyohudhuiria maziko ya ndugu wa viongozi waaandamizi wa Chama cha Mapindizi, huku ndiko kukomaa si kuchukia mtu na watu ila tunapingana hoja.
Mkuu siasa ni mchezo wa kucheza na kadamnasi na upepo ukoje, nakuhakikishia hapo kabla wameisha fariki wafanyakazi wa Habari corp kabla na wapo wenye matatatizo makubwa na wapo watakao fariki baadae je Mh alifanya/atafanya nini? kama alivyo mfanyia huyu?
Kifo cha mwandishi huyu kimevuta masikio na macho ya watu wengi kwa wanasiasa kama Rostam huu ni wakati wao wa kupenyeza rupia kwenye uzia kutafuta sympathy kwa jamii.
Anyway hukatazwi kupongeza lakini unapaswa kuchambua mambo zaidi ya uavyo yaona na kuyasikia
 
Ni jambo jema wakuu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Upande wa 2 wa shilingi tunajiuliza huo ni mwanzo kwa mwingine atakayepatwa na masahibu ndani ya Habari Kooperesheni au ndo imeishia hapo? Na je mpango huuu atauendeleza kwaenye makampuni yake mengine hadi huko chanel 10 na Caspian? (just to mentionn few). Hiyo ndio changamoto iliyopo mbele yake walau arudishe hata asilimia moja ya kagoda,richmond nk......
 
Naaaaaaam SHOW OFF TIME.Ukweli Taifa limepoteza Muungwana kwenye sekta ya habari,lakini hofu yangu mjane huyu na familia yake watatumika kisiasa kama ambavyo tayari baadhi wameonyesha kuwa wanajali.Time Will Tell.Jamii itakapo anza kupoteza taswira ya muungwana huyu aliyetangulia mbele za haki MAKUCHA YA UKWELI ya WANAOITUMIA FAMILIA HIYO YATAANZA KUJITOKEZA NA SI AJBU KUSIKIA CHOCHOTE TOKA KWA MJANE.
 
Hapa kuna watu wa habari cooperation, ni jukumu lao kufuatilia ahadi hii maana isije ikawa danganya toto ya kujitutumua msibani.
Pia ni lazima kuwe na utaratibu ambao hiyo familia itaendelea kufaidika na hiyo ahadi hata kama kutakuwa na mabadiliko. miaka mitano ni mingi na hulka ya binadamu ni kuwasahau wafu mapema.
 
Back
Top Bottom