Maswali magumu kwa hussein bashe kuhusu kifo cha mwakiteleko. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali magumu kwa hussein bashe kuhusu kifo cha mwakiteleko.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfu Lela Ulela, Jul 26, 2011.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jana nimepata taarifa kupitia vyombo vya habari (Chanel Ten-taarifa ya saa 1jioni na TBC-kwny usiku wa habari), kuhusu mpango wa NEW HABARI CORPORATION kuisaidia familia ya aliyekuwa mhariri msaidizi wa gazeti la RAI marehemu Dany Mwakiteleko.

  Miongoni mwa ahadi alizotoa Bashe ni kumlipa mke wa Dany mshahara wa mumewe kwa miaka mitano, na kusomesha watoto wawili wa Dany pamoja na other two depandants hadi level ya University.

  Lakini kabla sijapongeza hatua hiyo naomba kumuuliza Bashe maswali kadhaa ya msingi ambayo majibu yake yatatupa taswira ya alichosema jana.

  Kwanza,
  je kwa mshahara wa miaka mitano atakaolipwa mkewe, inamaanisha kuwa atapoteza stahili zake nyingine alizokuwa nazo Dany kama mwajiriwa? Mbona hatujasikia suala ka pension ya Dany?

  Pili,
  Je Dany ni mwajiriwa wa kwanza wa NEW HABARI kufariki? Ikiwa sivyo, je aliyemtangulia Dany alifanyiwa hivyo? Kama hakufanyiwa, je ni vigezo gani vimetumika kumpa Dany offer hiyo?

  Tatu,
  Je utaratibu huu ni kwa Dany pekee au ni wafanyakazi wote wa NEW HABARI? Je akifa mwingine utaratibu utakuwa huohuo?

  Nne,
  Je mshahara atakaolipwa mkewe Dany utakuwa ukipanda kila mwaka au atalipwa mshahara Dany aliostaafia kwa miaka yote mitano?

  Sita,
  mtoto mdogo wa Dany yuko darasa la sita. Ameahidiwa kusomeshwa hadi chuo kikuu, je kampuni itakuwepo kwa kipindi chote hicho?
  Vipi ikiwa kampuni itakufa mwakani?

  Saba,
  nani atasimamia utekelezaji wa ahadi hizo?

  NB:Ikumbukwe ahadi zilizotolewa ni hisani (courtesy). Hisani hailazimishwi kulipwa. Hakuna mkataba familia ya Dany imesaini ili hayo yaliyoahidiwa yasipotekelezwa familia ichukue hatua.So utekekezaji wake utategemea kudra za NEW HABARI, na Bashe kama MD.

  Mwisho natoa rai kwa media houses nyingine (hasa za Reginald Mengi) kuiga mfano waliounesha NEW HABARI.

  Mungu ibariki tasnia adhimu ya habari,
  Mungu ibariki TZ.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  danny alimtumikia vizuri sana ROSTAM na LOWASA,
   
 3. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hizo ni ahadi kama za kwenye michango ya harusi . yaani ni favour. Mjumbe hata kama alsema atatoa laki mbili asipotoa au akatoa robo huna la kumfanya.

  Zaidi ni mjumbe atakuwa amepata sifa mbele ya kikako
   
 4. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,405
  Trophy Points: 280

  Kwenye nyekundu humo mna maswali ya msingi sana.
   
 5. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuna v2 vya msingi mf.. penye red.....
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  sijaiona hiyo habari lakini umeuliza maswali ya msingi.
   
 7. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na hilo ndilo lililonipa wasiwasi na kulazimika kuhoji. Isije ikawa RA na Bashe wakajipatia ujiko mbele ya jamii then ahadi zikaishia kuwa story za tom na jerry.
   
 8. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Tuyuku nashukuru kwa kuliona hilo.
   
 9. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  thanx for your concern sir!
   
 10. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeuliza maswali mazuri sana,i hope the message is delivered and read...
   
 11. c

  chaArusha Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Wataka sifa tu hao. Mbona wafanyakazi wengi wa New Habari hadi leo wanadai mishahara yao ya Agosti, Septemba na Oktoba? Hata wale waliocha kazi hawajalipiwa mafao yao ya NSSF, PPF. Hapo Rostam na Bashe wametaka cheap popularity ya kisiasa. Si ulimuona Lowassa msibani?
   
 12. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I apprrecite your concern. Hope the msg delivered!
   
 13. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Umenifurahsha sana,umeuliza vitu makini sana..You speak my Language!!Ila Mungu anisamehe!ila Danny Alimsafisha sana Lowasa na RA....Mpaka Mtanzania na Rai zikawa kama Uhuru na Mzalendo...Lakn hakuna mwenye hak mbele za bwana,wote tu wadhambi!Mwenyez Mungu ampokee
   
 14. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mtu mwenye akili Timamu,.. Hayo maswali yajibiwe si kwa maneno tu, bali kwenye maandishi tena advocate awepo na wahusika wasaini mbele yake na hayo mafaili kopi kwa kampuni, kopi nyingine kwa advocate na familia ipewe original kopi...
   
 15. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu hayo ni maswali ya msingi ambayo kila mtanzania lazima ajiulize,
  kwangu mimi namwona huyo msomali anataka ubunge kwa nguvu
  jamani tumechoka na wageni kutuongoza msikubali hilo
   
 16. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unanifurahisha mkuu,ama kuhusu ubunge it might be true.!
   
 17. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,405
  Trophy Points: 280
  ahsante sana ndugu
   
 18. n

  nndondo JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Nimesoma hiki kichekesho. Kwa bahati. Mbaya hawa wsanii hawajashikishwa adobe kujua kuheshimu mambo yasiyo ya utani. Tatizo lingine ni ujinga wa haw a wasanii wa aina ya Bashe ya kutokujua kwamba it is only pension funds na BIMA sinazowewza kufanya hilo wanalosema. Kama wanaubavu wangemkatia Danny na wafqnyakazi wq aina yake bima ama kuwaingiza kwenye mifuko ya pension ambayo mpaka wanafariki ama hawajaandikishwa AMA moaka Leo makato yao hayajawakilishwa mpaka Leo. Bashe asijaribu hat a Kidogo kutaka kuidhalilisha familia ya Danny kwa kujaribu kufivhq makucha yao ya namna walivyoshindwa kuwjibika katika kuwatayarishia watumishi wake maisha ya baadae si tu kwa kifo, bali hat a ajali na mambo yanayofnana na hayo. Pamoja na nia njema ya Bashe na kampuni yake, hii ahadi ni BATILI, ni ajabu kuona wadanganyika wakishusha lundo la pongezi humu. Familia ya Mwakiteleko haihitji usanii kwa sasa, wanachohitaji ni counseling na kujiweka saw a kwa maisha bila bread earner, maisha sustainable sio upumbavu wa hadithi za wakina Bashe ambao hat a wao hatima yao na hiyo kampuni yao haieleweki. Hawajua watanzania wanafikiria nini juu ya hatma yao katika nchi ugenini.
   
 19. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  You are absolutely correct mkuu. Japokuwa hatuwezi wala hatupaswi kuhukumu, lakini ni ukweli ulio wazi kuwa Dany alimtumikia RA kwa moyo na akili yake yote.Hata katika mazingira mengine alikiuka maadili ya kazi yake ili kumfurahisha his master (RA). Kwa kushirikiana na Bashe pamoja na Manyerere Jackton waliyafanya magazeti ya RAI na MTANZANIA kupoteza hadhi kabisa mbele ya wanajamii (hasa wasomi).Binafsi nimewahi kuingia nao kwenye mgogoro baada ya kuhoji issue fulani, waliyotoa kwenye Mtanzamia (December last year) bila kuwa na ushahidi.Katika taarifa ile hakukuwa na objectivity wala fairness maana tuhuma zilitolewa bila kufanya attribution kwa mtuhumiwa.Nilipompigia Jacton alishindwa kudhibitisha but after some minutes wakanitext kuwa natumiwa na CHADEMA.Nilishangaa kuwa wao wanaotumiwa na RA hawajioni, wanabaki kugase wengine. Nikajaribu kuwaelewesha kuwa im arguing on proffesionalism b'se i also posses degree of the same proffesion but hawakunielewa tukaishia kulumbana.So it is true kuwa Dany na wenzake walimtumikia RA for their all energy hata wakati mwingine kupindisha ukweli. Hatupaswi kuhukumu but to be honest Dany alipaswa kuiomba jamii radhi kabla hajatwaliwa ktk haya mavumbi.Sina hakika kama alitubu kwa Mungu wake, lakini nina hakika hakutubu kwa WATANZANIA. Nasikitika amekufa na deni hilo. Eeeh Mungu mrehemu Daniel Mwakiteleko apumzike kwa amani.
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Maswali yako ni ya muhimu lakini umeyaweka pasipo, sijui unategemea nini au bangi?

  Nakushauri mwandikie Bashe Barua na copy ndio uteletee hapa JF kama upo serious na hayo maswali.
   
Loading...