Offer ya Rostam kwa familia ya Dan Mwakiteleko

Bashe kama MD ametangaza msibani kuwa mjane ataendelea kupokea mshahara wa mumewe kwa miaka mitano,na dependants wawili wa shule ya msingi na wa chuo wataendelea na masomo kwa hisani ya habari cooperation.
RA anaitaji pongezi kwa ilo
Source :ch ten 19hrs news

Utaratibu wa hivyo sijawahi kuusikia mahali popote wala katika sheria yoyote ya kazi au pension. Hata hivyo inaonekana kwa nje kama jambo linalopendeza machoni na kusikika vizuri masikioni, lakini kuna ukweli katika hilo? Je, ni sera ya kampuni inasema hivyo au ni matamshi ya kwenye jukwaa? Je, kuna mkataba utakaosainiwa ili kampuni iweze kuwajibishwa baadaye? Je, kampuni ikifa katika kipindi hicho, nini kitakuwa hatima ya mjane?
 
Rostam sa mambo haya ungefanya nch nzima!walau machungu ya Kagoda yaishe...mnyonge mnyongeni..hongera RA!
 
Baniani m'baya, kiatu chake ni dawa,
Shetani hata afanyaje hageuki malaika,
Na sio kila akuchekea basi anakupenda.
 
Bashe kama MD ametangaza msibani kuwa mjane ataendelea kupokea mshahara wa mumewe kwa miaka mitano,na dependants wawili wa shule ya msingi na wa chuo wataendelea na masomo kwa hisani ya habari cooperation.
RA anaitaji pongezi kwa ilo
Source :ch ten 19hrs news

Utaratibu wa hivyo sijawahi kuusikia mahali popote wala katika sheria yoyote ya kazi au pension. Hata hivyo inaonekana kwa nje kama jambo linalopendeza machoni na kusikika vizuri masikioni, lakini kuna ukweli katika hilo? Je, ni sera ya kampuni inasema hivyo au ni matamshi ya kwenye jukwaa? Je, kuna mkataba utakaosainiwa ili kampuni iweze kuwajibishwa baadaye? Je, kampuni ikifa katika kipindi hicho, nini kitakuwa hatima ya mjane?

isije ikawa ni pr tu hiyo

Bila shaka tunahitaji kuvuta subira kidogo ili kupima utekelezaji wa ahdi hii, sasahivi suala la kutoa ahadi kwa wana magamba ni fasheni, tatizo lao kubwa liko kwenye utekelezaji. Tusubiri kidogo tu "time will tell".
 
mnyonge, mnyongen lakini haki yake mpeni, RA kafanya jambo linalostahili pongezi, nina iman mjane wa mwakiteleko ndo ana nafasi Nzuri ya kulielezea hili
 
wakimnyonga si atakufa?? sasa hiyo haki atapewa saa ngapi? huku akiwa amekufa??
 
Hana lolote huyo,lengo lake siyo kusaidia familia bali ni kujitakasa mbele ya jamii,anataka kupunguza makali ya mabaya aliyoyatenda!
 
Utaratibu wa hivyo sijawahi kuusikia mahali popote wala katika sheria yoyote ya kazi au pension. Hata hivyo inaonekana kwa nje kama jambo linalopendeza machoni na kusikika vizuri masikioni, lakini kuna ukweli katika hilo? Je, ni sera ya kampuni inasema hivyo au ni matamshi ya kwenye jukwaa? Je, kuna mkataba utakaosainiwa ili kampuni iweze kuwajibishwa baadaye? Je, kampuni ikifa katika kipindi hicho, nini kitakuwa hatima ya mjane?

Kwa kuwa umeongea yote niliyotaka kujadili sina haja ya kuongezea....kwa kifupi, ni mtu mwenye kuchukulia mambo kirahisi na kwa wepesi anaweza tu kukubali hizi ngonjera za majukwaani....shuguli sikuzote zipo kwenye utekerezaji tu.
 
Ni jambo jema, binafsi limenifurahisha. Lakini watekeleze ahadi, maana baada ya msiba, watu wengi husahau ahadi na majumuku waliojipangia au kupangiwa.

Tusiwe wepesi kumpongeza kwani kutoa ahadi mbele ya kadamnasi ni rahisi kuliko kuzitekeleza hizo ahadi; mifano mingi tunao ya wanasiasa kutoa ahadi nyingi kwa wanannchi lakini hawazitimizi!! Mmekwisha sahau ahadi za swahiba wake za MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA? Ikumbukwe kwamba wafanyakazi wake wamagazeti huwa wanasota kwa muda mrefu bila kupata mishahara kwahiyo hata hii ahadi itafuata mkumbo huo huo.
 
Mh huyu aliyekufa ni mfanyakazi wa RA alikuwa ? Wengine hatumjui sasa kuleta habari za upande mmoja si safi

Akili za Ma CCM ziko kama uvaaji wa Kofi Olomide ya kuvaa suti bei mbaya chini anavaa raba,juu kofia
umenichekesha sana mkuu kwa hii signature yako.
 
Hana lolote huyo,lengo lake siyo kusaidia familia bali ni kujitakasa mbele ya jamii,anataka kupunguza makali ya mabaya aliyoyatenda!

Acha unafiki!Wewe umesaidi nini famili ya Marehemu!una usafi gani wewe!
 
Akimpongeza mjane ni haki yake, lakini sisi tukimpongeza na kumsifu RA naogopa kusema ubongo wetu utunzao kumbukumbu haiyumkini umekufa! kwa mwenendo huu, ccm watatutesa sana na ikibaki miezi 4 kufanyika uchaguzi 2015 wanafanya mambo ya kupanga ya kiungwana kisha itashinda kwa kishindo!!!! watu wenyewe ndo nyie wakusahau sarakasi za rostam tena ghafla namna hii, kisa mjane, hivi ra ametengeneza watane wangapi tz hii kupitia marichmond yake, marada, mamigodi, mauwekezaji magumashi, watz kibao wanavaa midabwada kisa ra katutapeli, mnakuwa dhalili machoni penu, wake na wato wenu!!!!!
 
Bashe kama MD ametangaza msibani kuwa mjane ataendelea kupokea mshahara wa mumewe kwa miaka mitano,na dependants wawili wa shule ya msingi na wa chuo wataendelea na masomo kwa hisani ya habari cooperation.
RA anaitaji pongezi kwa ilo
Source :ch ten 19hrs news

Nawapongeza Rostam na Habari Corp kwa moyo wa ubinadamu usio na kifani. Mungu awabariki na awazidishie.
 
rostam ana ubinadam gani mkuu, unamuomba mungu amzidishie rostam unajua rostam hupata mengi ya mapato yake kwa kutufix, kwa maana halisi unamuomba mungu atutie ujinga ili ra azidi kuneemeka kwa mali zetu watz, nawa uso wako kisha fikiri upya, ikiwezekana futa maombi yako kwani mungu akikusikia utakuwa umetumaliza.
 
Back
Top Bottom