Nzega: Risasi zatumika kumuokoa Mbunge Kigwangalla

Nzega: Risasi zatumika kumuokoa Mbunge Kigwangalla

Nilikuwa nashangaa kwa huyo so called Kigwandalla kusema polisi wamemdhalilisha. Walipokuwa wanakamatwa wabunge wa CHADEMA, kutiwa korokoroni, kubambikwa kesi zisizokuwa na kichwa wala vidole, kudhalilishwa si kwa wabunge peke yao, hata wananchi wasiokuwa na hatia....Kigwandalla hayuko kwenye rekodi kukemea tabia hiyo ya polisi. Sasa kuwa yeye amekuwa one of the victims ndo anaanza kulialia. Welcome bro, ukombozi hauji kwa mteremko kama ulivyofikiri....muulize Mbowe, Zitto, Kiwanga, Lissu, Lema na watu wengineo ambao walikumbana na kadhia hiyo.
Kwa makamanda wa kweli kulala sero ni sawa na kulala Hilton, Sheraton au any other 4 or 5 Star Hotel. Jichunguze na kujiangalia vyema ni upande upi unapenda kusimamia.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Mbunge mwingine CCM afikishwa mahakamani
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 24 October 2011 20:37 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

kigwangala.jpg
Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla,


Mwandishi wetu, Nzega
MBUNGE wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla, amekamatwa na kuswekwa rumande kisha kufikishwa mahakamani jana kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

Habari zimeeleza kuwa mbunge huyo alikamatwa juzi jioni na kuwekwa mahabusu ya polisi katika Kituo cha Nzega ambako alilala hadi jana asubuhi alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Nzega kujibu tuhuma hizo.

Alikamatwa pamoja na watu wengine watatu, Mrisho Hamisi, Mathew Dotto na Mwanja Mwandu, wote wakiwa wakazi wa kata ya Nata ambao ni wachimbaji wadogo, waliodaiwa kushiriki vurugu zilizotokea juzi katika kijiji cha Mwabangu.

Wakisomewa mashtaka yao jana mbele ya hakimu Ajali Mlanzi waendesha mashtaka wa polisi, Merito Ukingoji na Joseph Mbwana, walisema kwa pamoja watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali Oktoba 23 mwaka huu, katika mgodi mdogo wa wachimbaji wadogo uliopo kijijini hapo.

Waendesha mashtaka hao waliieleza mahakama kuwa mbali na kufanya mkusanyiko usiokuwa wa halali, watuhumiwa hao pia, waliingia katika mgodi huo mdogo unaomilikiwa na wawekezaji bila idhini ya wamiliki na kuvamia Kituo cha Polisi cha Nzega.

Waendesha mashitaka hao, walisema washtakiwa hao pia wanatuhumiwa kufanya njama katika ofisi ya wilaya ya CCM na kufanya maandamano kisha kuvamia kituo cha polisi.

Dk Kigwangalla na Mwandu pia wanakabiliwa na shitaka la kupiga na kujeruhi. Waendesha mashtaka hao waliwataja waliopigwa katika tukio hilo kuwa ni Moses Kichambi na Ferdinald Yusuph.

Hata hivyo watuhumiwa wote wanne walikana shtaka na wako nje kwa dhamana baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa bado unahitaji muda kuendelea na upepelezi wa tukio hilo.

Mbali na hakimu Mlanzi kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 18 mwaka huu, amemzuia mbunge huyo kufika katika eneo la mgodi huo ili kuondoa uwekezakano wa kutokea kwa machafuko mapya.

"Mahakama inatambua kuwa ni wewe (Kigwangalla) ni mbunge wa jimbo na unapaswa kutembelea wananchi wako lakini kwa sababu suala hilo sasa liko mahakamani, hutakiwi kufika kwenye eneo la mgodi huo," alisema hakimu Mlanzi.

Adai rumande imemdhalilisha

Dk Kigwangalla aliliambia gazeti hili nje ya mahakama kuwa hakujua kama angehusishwa kwenye kesi hiyo na kuswekwa rumande kwani alifika kituoni hapo kwa nia ya kuwadhamini wenzake.

Dk Kigwangalla alisema kuwa baada ya kuwatuliza wananchi ambao walikuwa wakielekea kwenye Kituo cha Polisi Nzega Mjini, aliwaweka kchini katika ofisi ya CCM wilaya na kuwataka wamsubiri aende kuwawekea dhamana wenzake waliokamatwa.

"Tulipokuwa tunaelekea kituoni, askari wakawa wanazungumza kwa jazba na kusema mimi ndiye niliyeanzisha vurugu na nilipofika kituoni ghafla nikaambiwa nivue viatu na kuelezwa nitalala rumande," alisema Dk Kigwangalla.

"Leo (jana) wamenitoa rumande na kunipeleka mahakamani nikiwa nimefungwa pingu na watu wengine niliokuwa nimeenda kuwadhamini," alisema Dk Kigwangalla.

"Nilikataa kutoa maelezo nilipokuwa kituoni lakini (leo) jana nilipelekwa Mahakamani na kufunguliwa mashtaka kama nane hivi, moja likiwa kujeruhi na mengine ya jinai," alisema Dk Kigwangalla.

Dk Kigwangalla alilalamika "Nimedhalilishwa sana na hawa polisi kwa kuninyima hata nafasi ya kupiga simu kwa mtu yeyote kabla sijawekwa rumande."

"Nimeshangazwa na polisi hasa OCD, kunibambikia makosa ambayo hayana ukweli na kunidhalilisha kwa kunipiga vibao kama mtoto mdogo na dhihaka mbalimbali kwa wananchi wangu ambao walikuwa wakidai haki yao ya msingi. Hii si haki, sikutendewa haki katika hili ni uonevu mtupu!’’alilalamika Dk Kigwangalla.

Kilufi naye afikishwa tena kortini

Wakati huohuo Brandy Nelson anaripoti kutoka Mbeya kuwa
mashahidi watatu katika kesi inayomkabili Mbunge wa Mbarali kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Modestus Dickson Kilufi jana walianza kutoa ushahidi katika kesi hiyo ya kutishia kuua kwa maneno.

Kesi hiyo inayoendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, jana ilianza kusikilizwa kwa shahidi wa kwanza Jordan Masweve, ambaye ndiye mlalakaji kumwambia Hakimu Mkazi Michael Mteite kuwa, Machi 16 mwaka huu, aliongozana na diwani wa kata yake, Alex Paulo kwenda katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Alieleza kuwa akiwa katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, ofisi tatu tofauti na alipomaliza shida zake alirejea kwenye gari tayari kwa kurejea nyumbani, alipofika kwenye gari, alikuta simu ya Diwani Paulo ikiita wakati mwenyewe akiwa mbali. Alisema wakati huo diwani huyo alikuwa akizungumza na Mbunge Kilufi.

”Nilichukua simu hiyo kwa lengo la kumpelekea diwani kabla sijafika katika eneo walilokuwepo Mbunge Kilufi alinipa tahadhari kuwa nisifike kwenye eneo hilo na kunitaka niende nikajisalimishe kwake ndani ya wiki mbili,”alisema na kuongeza:

“ Huku akijisifu kuwa nisipojisalimisha atanionyesha kwa kuwa ana marafiki wengi ambao ni watu wakubwa serikalini akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria.”

Alisema baada ya kuambiwa hivyo aliamua kuondoka, lakini Kilufi alianza kumrushia matusi kwa kumwambia kuwa yeye (Jordan) ni mpumbavu na kwamba baada ya kitendo hicho aliamua kwenda katika kituo cha Polisi kwa ajili ya kufungua jalada kwa kitendo hicho alichofanyiwa na Mbunge huyo.

Shahidi wa pili, Alex Paulo ambaye ni diwani wa Kata ya Rwiwa aliiambia mahakama kuwa wakati wakiendelea na maongezi na Mbunge Kilufi, alisikia mbunge huyo akijibizana na Masweve, akimtaka aondoe kesi mahakamani na kama asipofanya hivyo atamtoa roho.

Alisema baada ya kutolewa vitisho hivyo, aliongozana na Masweve kwenda kumweleza Mkurugenzi wa Wilaya, George Kagomba, ambaye aliwashauri kwenda kuripoti suala hilo polisi.

Baada ya upande wa mashahidi kumaliza kutoa ushahidi wao, Hakimu Mteite alimtaka Mbunge Kilufi aanze kujitetea, lakini mawakili wa Serikali walipinga kwa madai kuwa walikuwa hawajajiandaa kwa ajili ya kusikiliza upande wa utetezi.

Hakimu Mteite aliamua kuiahirisha kesi hiyo hadi leo siku ambapo Kilufi ataanza kujitetea.

Wabunge wengine walioonja rumande

Mzimu wa kulala rumande umewaandama wabunge kadhaa wa bunge la sasa katika siku za karibuni kutokana na visa na mikasa mbalimbali.

Waliofikwa na balaa hilo ni Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na mwenzake wa Moshi Mjini Philemoni Ndesamburo waliosekwa rumande mwishoni mwaka jana kutokana na kasheshe la uchaguzi wa udiwani Arusha. Mwingine aliyefikwa na balaa hilo, ni Mbunge wa Chadema, Arusha Godbless Lema.

Wengine ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) kwenye vurugu za Tarime, Mbunge wa CUF Viti Maalumu Mkoa wa Tabora , Magdalena Sakaya naye alijikuta akilala mahabusu kwenye sakata la wafugaji Tabora .

Susan Kiwanga Viti Maalumu Chadema na Sylivester Kasulumbai (Chadema- Maswa Mashariki) hawa walionja rumande kwenye sakata la uchaguzi wa Igunga uliomalizika hivi karibuni
source :mwananchi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Hapo atakuwa kama jusi joto ya jiwe kwisa jua, Siku zote wamekuwa wakiwatuhumu CDM kwa kesi za kubambikwa na kunyanyaswa na wao wanashangilia sasa mkuki kwa nguruwe kwa binaadam mchungu
 
Zambi ya kubambikiza kesi ni kama kula nyama za watu ukishaanza ni lazma utaendelea huwezi kuacha na wakiisha wa kuwabambikiza unjikuta unajibabambikizia mwenyewe.
chama cha majambazi aka ccM ndio kazi yao hyo na bado mpaka wabakane hadharani
 
Kigwangala una kichwa kigumu kwani usichoelewa nini? Kila siku wao wanasema CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo wao yaani Top layer na watoto wao kama akina Ritz1, sasa wewe jina kama mlio wa kalai limeanguka kwenye kokoto nani anakutambua kwa ukigogo wa baba yako? Utajuta kuzaliwa mpaka utatia akili, ulikuwa unafurahia watanzania wanavyonyanyaswa na Polisi, leo zamu yako-nyea debe kwanza ukipata akili utajiunga na Airtel.
 
Ahsanteni wanaJF wazalendo na wale wote makuwadi wa ufisadi na dhulma, na hata wale washabiki wa vyama mliopofushwa na itikadi za vyama vyenu na kusahau uzalendo.

Naomba nikiri sikuwahi kuonewa namna hii na polisi hata siku moja ila safari hii nimeshuhudia dhulma na ukandamizaji wa hali ya juu unaofanywa na watu waliotumwa kazi ya kutoa huduma na CCM! Kwa hakika ili CCM iendelee kushika dola huko tuendako ni 'lazima' ifanye mabadiliko ya ukweli ya muundo wa kuwadhibiti watumishi wake iliyowapa kazi ya kuendesha nchi...narudia tena ni lazima! Hili suala si la mjadala kabisa. Wananchi, hata wale wa vijijini, wamebadilika sana na wanauona ukweli...sasa wananchi wamedhulumiwa ardhi yao halali - kwa leseni feki, wamefuatilia bila mafanikio - mfumo mbovu wa kujibu barua na malalamiko ya wananchi umetamalaki na wananchi wanashuhudia Mbunge wao wanayetegemea awasaidie kufuatilia suala lao anapigwa mawe na muwekezaji na wafanyakazi wake, gari yake inavunjwa vioo na kuharibiwa sura, na kisha Mbunge wao na viongozi wengine wa serikali yao wanawekwa ndani kwa dharau na udhalilishaji mkubwa kiasi hiki...kwa hakika uvumilivu utawashinda tu wananzega...ukiona mkanda wa mahojiano ya wanahabari na wananchi utashangaa kusikia kauli zinazotolewa. Akina mama wazee wakilia na kuongea kwa hasira kiasi cha kushangaza kabisa. Machozi yalinilengalenga na nilishindwa kusimama kuwasikia!

Regards,
HK.
Yule mbunge wa CUF aliposimama kidete kuwatetea wanachi waliodhurumiwa alikamatwa na polisi akapata kipigo cha kutosha, akawekwa mahabusu na wanamme bila kujali kama yeye ni wakike, alikataliwa dhamana akaa huko mahabusu kwa siku zakutosha. Mh. Kigwangala ulikaa kimya, wala hatukusikia sauti yako ya kulaani vitendo vya hovyo vya kumdhalilisha mbunge mwenzako!
Unatutaka tukuonee huruma wewe unayejidai unajua kutetea haki za wanyonge! Juzi tu polisi wenu na vijana wenzako wa CCM wamefanya vitendo vya hovyo sana kule Igunga, hatukusikia ukipaza sauti kulaani unyama na uovyo ule. Sasa nakusihi funga domo lako chafu, hakuna chochote cha maana unacholaani hapa, huo ni unafiki na ubaradhuri tu. Nenda kawambie vijana mwenzako Nape na Bashe huenda watakuelewa lakini sio watanzania makini wanaofutatilia uozo wako na chama chako. Kwanza Polisi wamekustahi sana mpaka wamekuruhusu ujidhamini. Mbona yule mbunge wa mbalali alinyea debe muda mrefu tu, mbona wale wabunge wa CHADEMA walipelekwa Tabora kutoka Igunga bila dhamana?
 
Ila amejitahidi kuwa mkweli badala ya kukana kama magamba wengine. kuna magamba kama Nape hata akivunjwa mguu na polisi bado anaweza akakataa kuwa hajapigwa na polisi.

Kigwangala acha apate hicho kichapo maana malipo ni hapa hapa duniani maana makamanda wakilalamika yeye anawadhihaki kuwa nchi hii inaongozwa kwa mjibu wa sheria.
 
Kigwangala una kichwa kigumu kwani usichoelewa nini? Kila siku wao wanasema CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo wao yaani Top layer na watoto wao kama akina Ritz1, sasa wewe jina kama mlio wa kalai limeanguka kwenye kokoto nani anakutambua kwa ukigogo wa baba yako? Utajuta kuzaliwa mpaka utatia akili, ulikuwa unafurahia watanzania wanavyonyanyaswa na Polisi, leo zamu yako-nyea debe kwanza ukipata akili utajiunga na Airtel.
Umenikumbusha yule bosi aliyeinunuwa Uda ambae ni rafiki wa mtoto wa mkulu,wakati wa uchaguzi wa ubunge mwaka jana kwenye lile jimbo la Shibuda alimpiga ngwala OCD na hakufanywa lolote na alikuwa ni mgombea tu,jiulize sasa ww mbunge unatetea wananchi wako unalambwa vibao,can u imagine?Kigwangala hii nchi kiwango cha uonevu kinatisha na uzuri na ww umeonja machungu yake.Sasatunakutuma kwa hao maboss wako ccm waambie wasijidanganye huku mtaani kimenuka,tunataka KATIBA MPYA na tunajuwa ndio mkombozi wetu wala hatuwabembelezi,ni haki yetu.
 
kumbe neno kubambikiziwa analijua? Huyu bwana ana bifu na md wa habari corp na mmiliki wake RA.Sasa akiingia anga zao wanamfix
Kaka, jamaa anachezea very thin line... CCM wamemchoka, na wapinzani alishawatukana na kuwadhalilisha sana. it is rare, lakini shepu za akina hamisi huishia kuwa political orphans au kurudi walipotoka

Kituko zaidi, kesi itafutwa na utamkuta bunge lijalo akisifia sana polisi na kukandya wapinzani kwa kukurupuka kudai haki bila kufuata taratibu

he has four very long years to survive
 
Ahsanteni wanaJF wazalendo na wale wote makuwadi wa ufisadi na dhulma, na hata wale washabiki wa vyama mliopofushwa na itikadi za vyama vyenu na kusahau uzalendo.
Regards,
HK.

Kweli Nyani haoni kundule!!!
 
Haijapita hata mwezi ulikuwa unashabikia udhalimu zaidi hata ya uliyotendewa, ukawa unashabikia mauaji ya Igunga kwa kisingizio eti Slaa alishawahi kutamka nchi haitatawalika jisome mwenyewe hapa chini. Halafu leo unakuja kulia lia humu. Muwe mnaona aibu sometimes, mjifunze kuheshimu utu!

Dr. Hamisi A. Kigwangalla
Hayo ya siku za nyuma tuyaache, tuongee ya leo kule Igunga. Nilikuwepo na
nilishuhudia jinsi gani CDM walijipanga kufanya vurugu...

Na nimekuwa nikimsikia Slaa anavyohamasisha vurugu kwa kauli yake maarufu ya
'nchi haitotawalika'...sijui alidhani ni lelemama nchi kutotawalika? Hizi ni
dalili tu, mvua yenyewe bado haijanyesha. Leo kafa wa CDM, kumekuwa vilio na
kila mtu anasema CCM wamemuua, siku CDM walipombaka binti wa miaka 12, na
kumkata panga babaake mliona sawa, siku kijana wa CCM alipomwagiwa tindikali
mliona sawa, siku DC alivyonyanyaswa mliona sawa...wote hawa walikuwa na
haki zao, na zilinyang'anywa...sikuona haya malalamiko hata kidogo!

Hata hivyo, hivi kuna ushahidi gani kuwa Marehemu aliuliwa na CCM? Na kwa
mujibu wa maelezo ya waliomuona maiti wanasema ameuawa siku chache kabla ya
kugundulika, hivi kampeni si zilikuwa zimeisha? Huyu bwana alikuwa na
wanaCCM wapi hao kwa muda wote huu toka uchaguzi uishe?

HK.
raha ya uongo uwe na kumbukumbu
 
Jikaze mtoto wa kiume,
Hao polisi mbona wako kazini kama wewe,
Ukilialia wenzako watakunyang'anya uheshimiwa,
Ukirudi bungeni mtafute Sakaya na Lissu wakupe uzoefu
 
hivi dr. Ni mwanaume au mwana mke?

Maana kama ni mtoto wa kiume kapigwa makofi analalamika ni aibu sana sasa ikija vita si utakimbilia
nje ya nchi..
 
Heshima yenu wakubwa,
Mbunge wa Nzege, kupitia ccm, Dr H. Kingwangala baada ya kusota Rumande kwa siku kadhaa kutokana na mapambano yake amewashtua mamia ya wananchi wake kwa kuwaeleza kuwa anawezakujizulu ubunge wakati wo wote kama serikali haitasaidia harakati za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hilo.
kingwangala alipoulizwa, alimthibitishia mwandishi wa mwanahalisi kwa kujibu,

Ndiyo, Nimewaambia wananchi kuwa kama serikali haitanisikiliza ktk juhudi za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hili, nitajiuzulu.
Ubunge si kazi, ni utumishi, huwezi kung'ang'ania kama hupati fursa ya kwatumikia wananchi waliokuchagua.
Nilishasema kwamba ktk matatizo yanayowahusu wananchi, nitasimama na wananchi.

Dr Kingwangala alitoa kauli hiyo baada ya mahakama mjini Nzega kumwachia kwa dhamana yeye pamoja na watu wengine 3, kutokana na tafrani iliyotokea ktk mgodi wa dhahabu ulioko jimboni humo.

My take,
Mwanzo wa mwisho wa ccm umefika?
 
CCM hawaha kalcha ya kujiuzulu

watch this space
 
Back
Top Bottom