Nzega: Risasi zatumika kumuokoa Mbunge Kigwangalla

Huyu Dr kingwa anafanya maandalizi ya kwenda India nyie subirini...
 
Kigwa kwani ana msaada gani na wana nzega?kama ubunge niwakupewa dhambi ya dhuluma inamuangaisha tu ana lolote.
 
Mh kigwangala namfahamu, wakati nipo 1st year pale Muhimbili yeye alikuwa ni intern pale nakumbuka yeye ndo alikuwa kiongozi wa mgomo ule uliotikisa Taifa wa Madaktari 2005: kwahiyo uanaharakati haukuanza jana ila alinza zamani. Na mpaka sasa madr tunanunafuu kidogo ukilinganisha na kipindi kile. Mwaka 2005 Dr alikuwa analipwa laki 200 mshahara baada ya ule mgomo mshahara ulipanda kwa 100% ingawa bado ulikuwa mdogo. Toka hapo umeendelea kupanda. Then kwa mabadiliko ya kipindi kile yaiongozwa na yeye na waliongoza pia kumtoa mkurugenzi wa MNH kipindi kile aliyeitwa Tregonin pia wakisaidiana na MAT nilishuhudia waziri mkuu kipindi kile Sumaye akigomewa live na madaktari na manesi wakimzomea. Kwa hiyo tusimbeze ameanza zamani uanaharakati na kashaleta mabadiliko ambayo tunayakumbuka sekta ya afya. Baada ya ule mgomo yeye pamoja na mkti wa kipindi kile alikuwa wa mbeya simkumbuki jina walifungiwa leseni zao na walikaa miezi kadhaa bila kazi na baadaye iliwapelekea kwenda kwa Mh. Sumaye na kuomba msamaha na walionyeshwa na television ya taifa enzi hizo TvT na baadaye wakasamehewa na kuendelea kuhudumia jamii. Mi naomba tusimbeze sana sema baada ya hapo alienda kuibukia ccm ambako sikuona kama ni sahihi sana kwake hasa ktk kipindi hiki cha mageuizi naomba tumuunge mkono na akiweza ajiuzulu ili tutetee haki za wananchi vema. Nipo tayari kurekebishwa mi sina uhusiano wowote na Kigwangala zaidi ya kuwa tumesoma chuo kimoja na tupo chini ya wizara moja.

umenena vema kama ulilosema ni kweli,ubarikiwe
 
Heshima yenu wakubwa,
Mbunge wa Nzege, kupitia ccm, Dr H. Kingwangala baada ya kusota Rumande kwa siku kadhaa kutokana na mapambano yake amewashtua mamia ya wananchi wake kwa kuwaeleza kuwa anawezakujizulu ubunge wakati wo wote kama serikali haitasaidia harakati za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hilo.
kingwangala alipoulizwa, alimthibitishia mwandishi wa mwanahalisi kwa kujibu,

Ndiyo, Nimewaambia wananchi kuwa kama serikali haitanisikiliza ktk juhudi za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hili, nitajiuzulu.
Ubunge si kazi, ni utumishi, huwezi kung'ang'ania kama hupati fursa ya kwatumikia wananchi waliokuchagua.
Nilishasema kwamba ktk matatizo yanayowahusu wananchi, nitasimama na wananchi.

Dr Kingwangala alitoa kauli hiyo baada ya mahakama mjini Nzega kumwachia kwa dhamana yeye pamoja na watu wengine 3, kutokana na tafrani iliyotokea ktk mgodi wa dhahabu ulioko jimboni humo.

My take,
Mwanzo wa mwisho wa ccm umefika?
..................Jamani kama ni single tu CCCCCM wamevunja rekodi, kila kukicha, mara ooh magamba, sijui hatukukutana uchochoroni, maamuzi magumu na sasa hii iliyopo sokoni saivi ndo issue kama vile Bw. Misosi nitoke vipi! TOKA LINI CCCCCM WAMEANZA KUJIUZULU? Yale yale ya Kibanga kampiga Mkoloni........
 
Mh kigwangala namfahamu, wakati nipo 1st year pale Muhimbili yeye alikuwa ni intern pale nakumbuka yeye ndo alikuwa kiongozi wa mgomo ule uliotikisa Taifa wa Madaktari 2005: kwahiyo uanaharakati haukuanza jana ila alinza zamani. Na mpaka sasa madr tunanunafuu kidogo ukilinganisha na kipindi kile. Mwaka 2005 Dr alikuwa analipwa laki 200 mshahara baada ya ule mgomo mshahara ulipanda kwa 100% ingawa bado ulikuwa mdogo. Toka hapo umeendelea kupanda. Then kwa mabadiliko ya kipindi kile yaiongozwa na yeye na waliongoza pia kumtoa mkurugenzi wa MNH kipindi kile aliyeitwa Tregonin pia wakisaidiana na MAT nilishuhudia waziri mkuu kipindi kile Sumaye akigomewa live na madaktari na manesi wakimzomea. Kwa hiyo tusimbeze ameanza zamani uanaharakati na kashaleta mabadiliko ambayo tunayakumbuka sekta ya afya. Baada ya ule mgomo yeye pamoja na mkti wa kipindi kile alikuwa wa mbeya simkumbuki jina walifungiwa leseni zao na walikaa miezi kadhaa bila kazi na baadaye iliwapelekea kwenda kwa Mh. Sumaye na kuomba msamaha na walionyeshwa na television ya taifa enzi hizo TvT na baadaye wakasamehewa na kuendelea kuhudumia jamii. Mi naomba tusimbeze sana sema baada ya hapo alienda kuibukia ccm ambako sikuona kama ni sahihi sana kwake hasa ktk kipindi hiki cha mageuizi naomba tumuunge mkono na akiweza ajiuzulu ili tutetee haki za wananchi vema. Nipo tayari kurekebishwa mi sina uhusiano wowote na Kigwangala zaidi ya kuwa tumesoma chuo kimoja na tupo chini ya wizara moja.

Haya yote uliyoelezea yaliyo fanywa na huyu dr hapo muhimbili na anayo yafanya sasa ni desa la package of lies, swali hapo muhimbili wanasoma hayo au ali google akapata taaluma yake ili imsaidie kuendesha maisha yake?
 
Jamani tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili. Magamba hawana tabia hyo wameshindwa walikuja na kauli mbiu ya kujivua gamba lakini je imeishia wapi? Bora wawe wanakaa kimya kabisa
 
Heshima yenu wakubwa,
Mbunge wa Nzege, kupitia ccm, Dr H. Kingwangala baada ya kusota Rumande kwa siku kadhaa kutokana na mapambano yake amewashtua mamia ya wananchi wake kwa kuwaeleza kuwa anawezakujizulu ubunge wakati wo wote kama serikali haitasaidia harakati za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hilo.
kingwangala alipoulizwa, alimthibitishia mwandishi wa mwanahalisi kwa kujibu,

Ndiyo, Nimewaambia wananchi kuwa kama serikali haitanisikiliza ktk juhudi za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hili, nitajiuzulu.
Ubunge si kazi, ni utumishi, huwezi kung'ang'ania kama hupati fursa ya kwatumikia wananchi waliokuchagua.
Nilishasema kwamba ktk matatizo yanayowahusu wananchi, nitasimama na wananchi.

Dr Kingwangala alitoa kauli hiyo baada ya mahakama mjini Nzega kumwachia kwa dhamana yeye pamoja na watu wengine 3, kutokana na tafrani iliyotokea ktk mgodi wa dhahabu ulioko jimboni humo.

My take,
Mwanzo wa mwisho wa ccm umefika?

Uungwana ni vitendo. Ngoja tumsubiri!
 
Kujiuzulu siyo ufumbuzi wa matatizo, ajenge hoja apambane tuone matunda yake. Anatangaza kushindwa hata mapambano hayajaanza !!!!
The problem I see with the dear Doctor is lack of INTEGRITY AND MORAL AUTHORITY TO LEAD THE CAUSE...EVERY MOVE HE MAKES IS A DRAMA.
 
Daktari uliyemsahau anaitwa Dr ulimboka sijui siku hizi yupo wapi? yeye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa ma intern.
 
Kwanza msimpe shavu kubwa yeye ni Dk. na sio Dr.
Afanye haraka kwani hajui serikali ya CCM ni kiziwi?
 
Yaani huyo bwana mdogo sio wa kumuamini hata kidogo, kishatumbukia humu JF just a day baada ya kutoka selo with aliases as usual and the beat is just the same as before. Anachotafuta ni platform na free airtyme!!!!!
 
Heshima yenu wakubwa,
Mbunge wa Nzege, kupitia ccm, Dr H. Kingwangala baada ya kusota Rumande kwa siku kadhaa kutokana na mapambano yake amewashtua mamia ya wananchi wake kwa kuwaeleza kuwa anawezakujizulu ubunge wakati wo wote kama serikali haitasaidia harakati za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hilo.
kingwangala alipoulizwa, alimthibitishia mwandishi wa mwanahalisi kwa kujibu,

Ndiyo, Nimewaambia wananchi kuwa kama serikali haitanisikiliza ktk juhudi za kuwatetea wananchi wanyonge ktk jimbo hili, nitajiuzulu.
Ubunge si kazi, ni utumishi, huwezi kung'ang'ania kama hupati fursa ya kwatumikia wananchi waliokuchagua.
Nilishasema kwamba ktk matatizo yanayowahusu wananchi, nitasimama na wananchi.

Dr Kingwangala alitoa kauli hiyo baada ya mahakama mjini Nzega kumwachia kwa dhamana yeye pamoja na watu wengine 3, kutokana na tafrani iliyotokea ktk mgodi wa dhahabu ulioko jimboni humo.

My take,
Mwanzo wa mwisho wa ccm umefika?

Mkuu kamaanisha kufutiwa kesi au wananchi hasa wale ambao yeye nui mbunge wao ? Anaipa serikali muda gani kabla hajaamua ?
 
Back
Top Bottom