SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,803
- 25,444
- Thread starter
- #221
*NYUMA YAKO (MSIMU WA TATU) -- 28 & 29*
*Simulizi za series*
“Aaahmm … hapana. Sema tu sikukutaraji. Si unajua. It is more than a surprise.”
“Nilihisi utahitaji kuniona ama sivyo?”
Kelly akacheka kiuongo. Aliporudisha macho yake akamkuta Marshall akiwa anamtazama kwa macho ya mkazo. Kidogo akahofia.
“Yah! Sijakuona muda, Marshall. Tangu mahakamani.”
“Ni kweli. Naomba basi unipatie maji ya kunywa. Nimengoja uniulize lakini nimeona kimya.”
Kelly akatabasamu.
Alikuwa amekalia bunduki.
Ni kivipi angesimama?
ENDELEA
Basi akawaza na kuwazua ndani ya muda wake mchache na punde akavuta mto uliokuwepo karibu na kuzuga kuushikashika.
“Ungependelea maji gani Marshall, baridi ama moto?”
“Naomba ya baridi.”
“Yasiwe na ladha yoyote?”
“Hapana. Maji kama maji tu.”
Basi Kelly akanyanyuka upesi na kusogeza mto wake pale alipokuwa ameketi. Kisha akaendaze kufuata jokofu na kuthoa maji humo kuyamimina ndani ya glasi na kwenda nayo sebuleni kumpa Marshall.
“Niambie Marshall. Maisha yamekwendaje? Ni muda mrefu sasa na umepitia mengi hapa karibuni.”
**
“Una uhakika?” sauti iliuliza ndani ya simu.
“Ndio, nina uhakika. Kwa macho yangu nimemwona,” akasema mwanaume mnene aliyevalia shati limembana. Mwanaume huyo alikuwa ana pipi ya kijiti mdomoni, kofia kaigeuzia nyuma.
Tumbo lake lilikuwa kubwa kiasi kwamba shati halikuwa linamtosha. Jeans yake ilikuwa imepauka na viatu vyake havikuwa inaridhisha.
“... ameingia ndani ya jengo muda si mrefu. Kwa macho yangu kabisa nimemtambua. Ndiye yeye!”
“Sawa tunakuja!” sauti ikasema kimamlaka. Bwana huyo kabla hajakata simu, akauliza, “na vipi kuhusu pesa yangu?”
“Utapata pesa punde tutakampotia mkononi kwa kutumia taarifa yako.”
Baada ya hapo simu ikakata akibakia mwenye hamu. Alitoa pipi yake mdomoni akajaribu kupiga tena lakini hakupokelewa. Akalaani akiwa amekunja ndita.
Kwasababu za madai, akakaa kando kungoja wana usalama watakaokuja ili basi apate kuonana nao na kuwadai pesa yake.
**
Kelly alicheka akiwa ameziba kinywa chake. Alitengenezea nywele zake vema kisha akamtazama Marshall. “Nadhani utakuwa unatania.”
“Hapana,” Marshall akatikisa kichwa. “Nipo serious kabisa.”
Basi Kelly akalifinya tabasamu lake la uongo na kusema, “sijui unachokiongelea, Marshall. Kabisa.”
“Kwenu ni wapi Kelly?” Marshall akauliza. “Usiniambie New Zealand maana ni wongo.”
Kelly akamtazama kwanza Marshall. Kuna kitu alikuwa anakiwaza kichwani mwake.
“Kwanini waniuliza vivyo, Marshall? Unadhani nilikudanganya?”
“Sidhani bali ni kweli ulinidanganya.”
“Kwanini?”
“Sijajua kwasababu gani, Kelly. Labda uniambie lengo lako ni nini haswa? Kuna mtu alikutuma kunifuatilia tangu kule Hong Kong?”
Kelly akaduwaa. Akatabasamu kiuongo kabla hajatikisa kichwa chake na kutengenezea nywele zake kichwani.
“Nani amekutuma Kelly. Niambie kweli na sitafanya jambo. Nitakuachia huru uende zako.”
“Marshall, nimeshasema hapo awali. Sijui unachokiongea. Nilikutana na wewe Hongkong wote tukiwa kwenye utalii. Tumekutana tena Marekani sababu nimekuja kusoma. Hivyo vitu viwili ndo’ vimekufanya uunganishe matukio kiasi hicho?”
Marshall akazamisha mkono wake kwenye mfuko wa koti alafu akatoa picha aliyoirushia mezani. Kelly akadaka picha hiyo na kuitazama. Ilikuwa ya Keen!
Hapo mapigo yake ya moyo yakachumpa kabla ya kukimbia. Alihisi mambo mengi sasa. Kwa kufupisha, alijiona hayupo salama tena.
Akatoa macho yake kwenye picha na kumtazama Marshall, wakakutana macho kwa macho. Kuna kitu kilikuwa kinanenwa japo vinywa vilikuwa kimya.
Kelly akarejesha macho yake kwenye picha lakini sasa mawazo yake yakiwa mbali. Alikuwa anawaza namna ya kujikomboa ama kummaliza Marshall.
Kulikuwa kuna kaukimya ka ufu kwa muda kidogo.
Punde ukimya huo ukavunjwa na mlio wa king’ora cha polisi huko nje. Kila mtu alishtuka. Walitazamana na upesi kila mmoja akatoa silaha yake kumwonyeshea mwenzake. Tendo hilo lilichukua kama sekunde moja tu!
“Weka silaha chini!” Marshall akafoka, Kelly akabinua mdomo wake na kutikisa kichwa, “weka wewe silaha chini , Marshall,” akasema kwa sauti ya pole.
Wakiendelea kujibizana, wakasikia sauti za watu zikiwa zinajongea karibu, na zaidi zikiwa zinakwea ngazi.
Walitazamana kwa tahadhari na kidogo tu wakahisi watu wapo mlangoni.
Mwanaume mmoja aliyevalia sare za kikosi cha kupambana na majanga na maswahiba ya wepesi, alitazama wenzake wanne na kuwapatia ishara. Walikuwa wamebebelea bunduki na vifua vyao vimekingwa na ‘bulletproof’. mmoja kati yao alikuwa amebebelea gogo la chuma kwa ajili ya kuvunjia mlango.
Wakahesabu moja, mbili, tatu wakavunja mlango na kuzama ndani wakiwa wamenyooshea midomo yao ya bunduki sebuleni. Hawakuona kitu. Wakatoa macho kuangaza na punde yule mmoja wao, captain, akawaagiza wenzake watawanyike kusaka maeneo mbalimbali humo ndani.
Walisaka kwa kama dakika tatu, hawakupata kitu!
“Hamna kitu, cap!” alisema bwana mmoja. Captain akatazama dirisha na kugundua lilikuwa wazi. Akasonga na kulitazama, hapo kwenye kingo za dirisha akaona kukiwa kumebonyea.
Alipotazama kwenda juu, akaona bomba kubwa likielekea kwenye paa ya ghorofa, upesi akawaambia wenzake waelekee juu ya paa kwani mlengwa wao yupo huko.
Basi haraka kwa kutumia ngazi wakakwea na kukwea mpaka huko juu. Wakatazama wasione kitu.
“Atakuwa ameelekea wapi?”
Maghorofa yalikuwa mengi sana papo. Ukiyatazama kwa juu ni kana kwamba miti ndani ya misitu. Waliwaza itakuwa mlengwa karukia maghorofa na kupotelea kusikojulikana, lakini sasa kwenda upande upi?
“Cap, kuna suspect upande wa magharibi mtaa wa tatu. Wapo wawili wanakimbia!” sauti ilimeta kwenye kifaa cha mawasiliano cha Cap.
Basi upesi mabwana hao wakashuka tena toka walipo waende huko wanapoelekezwa.
Ilikuwa ni tukio la upesi sana. Hakukuwa na muda wa kupoteza. Walishuka ngazi wakiendelea kuwasiliana zaidi na zaidi.
Walipofika chini, bwana yule mnene aliyetoa taarifa akatokea na kusimama mbele yao,
“Subiri! Subiri!” alinyoosha mikono yake yote miwili. “Naombeni kwanza pesa yangu. Ni mimi ndiye niliwapa taarifa!”
Mabwana hao hawakutia neno, captain alimpiga kumbo zito akadondokea kando kama kiroba, kisha wakaendelea na safari yao kwenda huko walipokuwa wanaelekezwa.
Kulikuwa na magari mawili chini. Moja likafyatuka kuondoka kwa kasi sana. Kwa ndani lilikuwa na maafisa wawili. Wengine walikuwa wameshawahi kwenda eneo la tukio!
Mabwana hawa wanne wakiwa wanatumia miguu, wakakimbia sana, muda si mrefu wakawasili eneo la tukio na kukuta hapo magari mawili. Moja lilikuwa ni lile lililotoka mapema zaidi na jingine ndo’ lile lililofyatuka baada ya wao kushuka chini.
Walipotazama ndaniye, wakakuta watu wote wakiwa wamelala chini. Majeruhi wanaomimina damu lukuki!
“Shit!” captain akalaani akibonda gari.
“Tumempoteza mlengwa … tumempoteza mlengwa!” akanena kwenye kifaa chake cha mawasiliano kabla hajakitupa kunining’inia kifuani.
**
"So uko wapi? Akauliza Danielle. Uso wake ulikuwa umeparamiwa na hofu kiasi. Baada ya punde akanyanyuka upesi na kufuata gari yake.
Majira yalikuwa ni jioni ya mapema.
Alijikwea kwenye gari na kuelekea mahali anapopajua yeye kichwani. Aliendesha kwa kasi sana na baada ya kama dakika arobaini na tano akawa amefika kwenye eneo tulivu, hapo akaegesha gari na kuangaza.
Ilikuwa ni katikati ya jiji pia. Hakuwa anajua atakuwapo hapo kwa muda gani. Alitazama 'side mirrors' zake kuhakikisha usalama, punde akaona gari moja likijiegesha nyuma kwa mbali kidogo.
Hakulitilia maanani, magari kadhaa yalikuwapo hapo. Akaendelea kuangazaangaza akiwa anajiuliza. Punde akatumiwa ujumbe, "nakuja!"
Alipotoa macho yake kwenye simu akamwona mtu karibu na gari, punde mtu huyo akafungua mlango na kuzama ndani. Alikuwa ni Marshall!
Alikuwa anahema kwanguvu akiwa ameshikilia mkono wake wa kushoto chini kidogo ya kiwiko.
"Twende!"
Danielle akatia moto na gari likahepa.
"Tuwafuate!" Alisema mwanaume ndani ya gari. Gari lile ambalo lilipaki nyuma ya mbali ya la Danielle. Kumbe walikuwa wanamfuatilia mwanamke huyo.
"Hamna haja ya kuwafuata," akasema mwingine. "Tulichokuwa tunakitafuta, tumekipata."
Ndani ya gari hilo alikuwa ameketi bwana James na Smith. James alikuwa amekalia usukani huku mwenzake akikaa pembeni yake.
Bwana James alikuwa ameshikilia kamera ambayo anaipekua kutazama picha zake. Kwenye picha hizo Marshall alikuwa anaonekana akitazama chini akitembea mpaka alipozama kwenye gari.
James akatabasamu.
"Hatimaye. Marshall na Danielle!"
Kisha akacheka cheko kubwa na kumtazama Smith aliyekuwa amekaa kando.
"Sasa umenielewa sio?"
"Hakika!"
"Nilikuambia tuliza munkari. Ile ishu ilivyotangazwa, tumuwahi na tumtazame Danielle. Yeye atatupa ramani wapi twende."
Smith akasafisha koo. "Lakini tulikuwa tumeshamaliza kila kitu. Mbona tukawaacha waende?"
"Smith!" James akaita. "Mimi ndiye nimekupanga katika yote haya. Najua ninachokifanya. Trust the process. Hamna haja ya kutumia nguvu sana. Tutaharibu."
Kukawa kimya kidogo.
"Mbu akitua kwenye korodani, utaelewa si kila jambo lahitaji nguvu," akahitimisha James kabla hajawasha gari na kuondoka huku Smith akiwa hoi kwa kucheka.
Maneno ya James yalimkuna.
**
Saa mbili usiku ...
Marshall alibandua bandeji aliyokuwa nayo mwanzoni kisha akaiweka kando na kupachikwa nyingine na Danielle. Wote walikuwa wamekaa kwenye kiti kimoja ingali Jack akiwa amejitenga kidogo.
Yeye alikuwa ameketi kwenye kiti kingine uso wake ukiwa umemezwa na mawazo. Alikuwa anatazama chini muda wote.
Kichwani mwake alikuwa anatafakari mambo kadhaa, haswa kumhusu Kelly ambaye mbivu zake ametoka kuzifahamu muda si mwingi toka kwa Marshall.
"Nilikuwa mpumbavu sana," akasema kwa sauti ya chini. Kauli yake hiyo ikafanya wote wamtazame. "Niliruhusu mapenzi yakawa upofu. Nakiri kukosa, nisameheni."
"Usijali, Jack," Marshall akamsihi. "It's not a big deal. Kingetokea tu."
"Hapana!" Jack akakanusha. "Nilipaswa kuhusisha akili yangu kwenye hili."
"Nafahamu. Haukupata muda wa kutulia tangu uachane na Vio. Ulifanya maamuzi kwa upesi."
"Ni kweli. Moyo wangu ulihitaji kupoa kwa upesi, matokeo yake ukaumizwa zaidi!"
Kukawa kimya kidogo. Danielle alimalizia kumfunga Marshall bandeji mwanaume huyo akajiveka nguo yake vema kuficha kifua.
"Kelly si mwanamke wa kawaida," akasema Marshall. "Ni mwanamke mwerevu, mwepesi wa kufanya maamuzi. Lakini pia mwenye uwezo wa kupambana."
Aliposema hivyo akaweka kituo. Alikuwa anavuta kumbukumbu fulani.
"Nimeshindwa kumweka nguvuni. Polisi waliharibu kila kitu. Badala ya kufanya kilichonipeleka, nikabaki kufanya namna ya kutoroka salama.
Na pengine nilimshusha sana adui wangu. Sikutaraji."