SIKU YA MKOSI - Riwaya Mpya ya Kusisimua...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
16508961_10154240531236156_8570951480949413950_n.jpg

SURA YA KWANZA

Na. M. M. Mwanakijiji

Siku ya mkosi haiji na mmoja. Siku yangu ilianza kwa jina langu kuwa miongoni mwa majina yaliyotajwa kama waliotumbuliwa na Waziri mara baada ya serikali mpya kuingia madarakani. Nilipolala jana yake nilikuwa miongoni mwa watu wazito kwenye mojawapo ya taasisi nyeti zilizo chini ya Wizara ya Fedha; unaweza kuniita kuwa nilikuwa miongoni mwa ‘vigogo’ au ‘vingunge’. Usiku ule ulikuwa ni kama siku nyingine zilizopita; nilienda kulala nikiwa na mipango yangu mingine mingi tu ya kazi na ya kutumia nafasi mbalimbali zilizokuwa zinajitokeza pale kazini kuendeleza maisha yangu, ya ndugu zangu na rafiki zangu. Nililala nikiwa na furaha na maisha yangu yakiendelea kung’ara. Sikutarajia kuwa asubuhi yake na siku nzima iliyofuatia ingekuwa ni siku ya kukumbukwa katika maisha yangu.

Asubuhi ya siku ile ya Jumatatu ilianza kwa dalili fulani hivi. Kwa vile sikuwa mtu wa kuamini sana katika mambo ya ushirikina baadhi ya dalili hizo nilizipuuzia kwani niliona kama bahati mbaya tu. Kwanza, niliamka na kukuta jenereta la umeme linaunguruma kuashirikia kuwa umeme wa TANESCO ambao tulikuwa tunaukopa Watanzania wengi ulikuwa umechukuliwa na wenyewe. Wakijisikia kuurudisha wataurudisha tu, nilijiambia. Hilo halikunisumbua kwani pale nyumbani sikujali sana umeme huo. Ukiwepo nashukuru ukikosekana nasonga mbele.

Nilimuacha mchumba wangu Rita akiwa kitandani; alikuwa amechoka kwa kunichosha usiku uliopita. Labda na mimi nilikuwa nimemchosha pia; maana hayakuwa mapenzi yale ya usiku ilikuwa ni vurugu mechi. Nilijiona kama miongoni mwa watu wenye bahati sana duniani. Rita alikuwa ni mtoto wa Balozi wa Tanzania nchini China Dkt. Rose Kitangile Ericsson. Baba yake alikuwa ni Msweden aliyekuwa amefanya kazi Tanzania kama Mkurugenzi Mkazi wa SIDA miaka ya themanini na baadaye kuamua kuishi Tanzania baada ya mkataba wake kuisha. Aliomba uraia wa Tanzania miaka michache baadaye. Walizaliwa wawili tu kwenye familia yake; yeye mkubwa na mdogo wake wa kike Marieta ambaye alikuwa anasoma huko Sweden.

Wakati naamka kitandani nilimuangalia Rita alivyolala na kujipongeza moyoni kuwa kwa hakika nilikuwa nimeopoa kweli kweli. Mtoto alikuwa ameumbwa akaumbika na kama mbinguni kuna malaika basi nina uhakika mmoja wao alitupwa duniani kama zawadi kwangu. Alikuwa amelala akiwa mtupu kabisa kajifunika shuka nyepesi ambayo ilimfanya aonekane kama picha nzuri ya kuchora ambayo mtu angeweza kuitundika ukutani kwa fahari. Ningekuwa mtu wa kuendekeza mambo hayo kwa kweli ningepiga simu kutokwenda kazini niendelee na sarakasi zangu. Kuna watu wanasema kiporo kitamu.

Kwa kawaida sikuwa napata chakula cha asubuhi nyumbani kwani muda niliokuwa ninatoka nyumbani kwenda kazini ni mapema sana; nikishapiga mswaki na kuoga na kuvaa kujiandaa kwenda kazini nilikuwa nachukua glasi ya maji ya moto na kunywa kushtua tumbo kidogo. Siku hiyo hata hivyo, nilipochukua glasi kabatini kabla sijaishika vizuri iliteleza mkononi na kuanguka sakafuni; tena sakafu ya marumaru. Ilivunjika vipande vikubwa vitatu; na vipande vingine vidogo vidogo. Nilifyonza na kutukana kwa kimombo na kusikilizia kama nimemshtua Rita huko juu ghorofani. Sikusikia kitu. Nilichukua ufagio na kwa haraka nikafagia fagia na kuokota vipande vile vikubwa kuvitupa kwenye pipa dogo la takataka nikiwa nimefunga kwenye mfuko. Niliandika ujumbe mdogo na kuacha kwenye mlango wa jokofu kumtaarifu Rita kuwa ahakikisha anatumia mashine ya kuvuta vumbi kwani kulikuwa na vipande vidogo vidogo vya glasi pale chini.

Sikutaka kuchukua glasi nyingine; nilichukua ufunguo wa gari langu na mkoba wangu wa kazini ambao ulikuwa na nyaraka mbalimbali pamoja na Ipad yangu. Niliharakisha kutoka ndani ya nyumba yangu huku mawazoni nikianza kupanga siku yangu itakavyokuwa pindi nikifika kazini. Kabla sijavuka kabisa mlango nikakumbuka nimeacha simu yangu juu pembeni ya kitanda; nikaamua kuharakisha kwenda kuichukua. Na kama vile kulikuwa na njama imepangwa katika haraka yangu nikashindwa kukanyaga vizuri ngazi ya kwanza; nikateleza na kama nisingekuwa makini ningevunja pua hivi hivi. Nilijiwahi kushika chini na kujizuia kuumia. Nikashika kingo za ngazi vizuri na kupanda kwa heshima zote; na hata wakati wa kurudi nilidhamiria kuwa makini zaidi.

Niliingia kwenye gari langu wakati mlinzi akifungua geti kuniruhusu nitoke nyumbani kwangu. Mawazo yangu yalihamia barabarani wakati nakanyaga mafuta kuelekea kazini. Nilikuwa naishi Masaki nyuma kidogo ya ofisi za Water Aid upande wa barabara ya Haile Selasie. Niliposhika barabara ya Haile Selasie sikufikiria kitu kingine chochote isipokuwa kusikiliza kipindi cha asubuhi kutoka EFM Radio.

>>>>>>

Nilipofika ofisini sikuhisi jambo lolote baya au kuwa na hisia yoyote kuwa kuna jambo baya linakuja. Ukiondoa Mkurugenzi Mkuu mimi nilikuwa ni mtu wa pili kufika ofisini siku ile. Kwa kawaida nilikuwa mtu wa kwanza kufika ofisini kila asubuhi. Ukiondoa sababu ya kukwepa foleni ya magari nilipenda kufika mapema ili kuweza kufanya kazi nyingi mapema ili mchana niweze kufanya mambo yangu mengine. Nilishakuwa na kawaida ya kutoka kazini majira ya saa nane hivi kuendelea na shughuli zangu; hakukuwa na mtu wa kuniuliza kwani nilikuwa msaidizi mkubwa wa Mkurugenzi lakini pia nilikuwa na watu chini yangu ambao walikuwa wanatekeleza majukumu mbalimbali pale ofisini.

Nimesahau kusema; nilikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu kwenye moja nyeti chini ya Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango. Nilianza kupitia kazi mbalimbali ambazo nilikuwa nimeacha jana ikiwemo kupitia mafaili ya nidhamu ambayo yalihitaji kufikishwa kwa Katibu Mkuu baada ya Mkurugenzi Mkuu kuyapitia. Kulikuwa na baadhi ya maombi ya kusafiri kwenda nje ambayo nayo yalihitaji kupitiwa ili hatimaye tuweze kuyaombea kibali Ikulu. Niliendelea kuchambua na kuandika mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya Mkurugenzi Mkuu ili baadaye niweze kuyapitisha. Pamoja na hayo nilipitia taarifa mbalimbali za matumizi ya fedha kwa ajili ya hatimaye kuidhinisha madai mbalimbali ya watumishi ili wenye kustahili waweze kulipwa.

“Bosi, habari za asubuhi?” ilinishtua sauti ya Clara baada tu ya kufungua mlango. Japo nilikuwa natarajia wakati wowote angetokea lakini nilikuwa nimezama sana kwenye kazi zangu hata sikumsikia alipoingia ofisini. Clara alikuwa ni Katibu Muhtasi wangu na kabla ya mimi kuhamishiwa hapo kutoka Mwanza miaka mitatu nyuma alikuwa pia ni Katibu Muhtasi wa mtangulizi wangu.

“Nzuri tu Dada Clara” nilimjibu huku nami nikimjulia hali. Aliniambia tu kuwa amechelewa kidogo sababu ya mvua barabarani na mimi nilimwambia kuwa na mimi ilipiga vizuri tu wakati naelekea kazini. Alitaka kujua kama nilihitaji chai au kahawa asubuhi ile. Nilimwambia kahawa itatosha maana nilikuwa nataka nichangamke kidogo. Alienda sehemu yenye birika la umeme la kutengenezea kahawa na kufanya vitu vyake. Dakika chache baadaye harufu ya kahawa ilimtangulia alipoileta ofisini. Nilishukuru na nikampa maagizo kidogo ya vitu ambavyo nilitaka ashughulikie mapema kwani nilihitaji kumpatia Mkurugenzi ripoti saa nne kamili asubuhi. Niliendelea na kazi huku nikinywa kahawa yangu kavu taratibu.

Muda haukupita kwani ilipofika saa mbili hivi ofisi ilikuwa imeshachangamka na karibu kila mtumishi alikuwa tayari ofisini; japo wachache walikuwa wameanza kazi. Wapo ambao walikuwa wanapiga soga kidogo huku wakiwa wamekaa kwenye sehemu zao na wengine wakiwa nao wanakunywa chai. Miezi michache nyuma ilikuwa ni kawaida kwa lundo la wafanyakazi baada ya kujionesha kuwa wamekuja kazini walikuwa wanakimbia chini ambapo kuna migahawa kununua ‘chochote’ kabla ya kurudi kazini. Kazi hasa ilikuwa inaanza karibu saa nne asubuhi. Wengine walitumia muda mwingi wakiwa kwenye mitandao ya kijamii. Lakini tangu serikali mpya iingie madarakani hali ilikuwa inaendelea kubadilika taratibu; watu walikuwa wanaonesha kuheshimu kazi zaidi na hata labda kujionesha wanaheshimu kazi.

Nilitoka kwenye ofisi yangu na kutembea kidogo kusalimia baadhi ya wafanyakazi na ikawa kama ishara kwao kwamba ni muda wa kazi. Kila aliyeniona alijifanya anajishughulisha. Nilirudi ofisini kwangu. Kama saa tatu hivi na nusu Clara alichungulia kutoka kwenye ofisi yake ambayo inapakana moja kwa moja na yangu na kuniuliza kama nilikuwa na mpango wa kutoka.

“Hapana sitoki saa hivi hadi mchana” nilimuambia na kumuuliza “kwani vipi?”

“Hapana DG aliulizia tu”

Hilo lilinishtua kidogo, haikuwa kawaida kwa Mkurugenzi Mkuu kuniuliza kwani akitaka kujua nipo au vipi aliweza kunipigia extension yangu ya simu moja kwa moja.

“Kwani vipi?” nilijaribu kudadisi. Clara alinyanyua mabega yake juu kuashiria kuwa na yeye hajui.

Akili yangu ikaniambia labda ni kuhusiana na ripoti ambayo nilikuwa niwasilishe kwake au labda kuna kitu kingine maana wiki hizi tangu JPM aingie madarakani ofisi imekuwa hakukaliki. Niliangalia ripoti zangu zilikuwa safi, na mambo mengine ya mitkasi yangu nayo nilijua iko salama.

Hazikupita dakika chache simu yangu iliita na ilikuwa inaonesha ni kutoka ofisini kwa bosi.

“Vicent, acha yote unayofanya sasa hivi tunaitwa ofisini kwa Katibu Mkuu” alisema.

Moyo ulishtuka; kwa muda wote ambao nilikuwa pale ofisini nimekutana na Katibu Mkuu kama mara mbili hivi na mara zote hizo ilikuwa ni vikao vilivyopangwa. Lakini kuitwa moja kwa moja na Katibu Mkuu kulinifanya nishtuke.

“Sawa bosi, on my away” nilisema huku nikizungumza kwa sauti ambayo ilionesha kujiamini na kuwa sijali sana nani alikuwa ananiita. Nilifunga tai yangu vizuri na kuchukua jaketi langu nililokuwa nimeliweka nyuma ya kiti changu. Nilimuaga Clara kuwa nimeitwa kwa Katibu Mkuu pamoja na DG na Wakurugenzi wengine watatu. Moyo ulianza kunienda mbio.

SURA YA PILI

Nilikuwa nimelowa jasho; mwili bado ulikuwa unatetemeka. Kila nilivyofikiria moyo ulinilipuka. Koo lilikuwa limekauka nikiwa na kiu ya pipa la maji. Nilikuwa nimetembea kwa mwendo wa haraka sana toka pale ofisini hadi makutano ya Barabara ya Maktaba na Bibi Titi Mohammed. Sikuwahi kutembea kwa haraka namna hiyo kama nilivyotembea hivyo tangu nilipokuwa shule ya Msingi Nyanguge miaka ile. Nilitamani kukaa chini kupumzika lakini sikuamini kama nilikuwa na muda wa kufanya hivyo. Toka ofisini barabara ya Madaraka hadi nilipokuwepo nilikuwa nimetembea kwa muda mfupi sana. Sikutaka kusimama pale; mfukoni nilikuwa na shilingi elfu ishirini tu. Nilikuwa na mamilioni benki na nikapata wazo la kwenda ATM yoyote iliyokuwa karibu nichukue hela kidogo kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Nilikata kushoto kuelekea barabara ya Morogoro. Nilikuwa na akaunti yangu mojawapo kwenye benki ya Barclays na lilikuwa ni kusudio langu kufika pale mara moja. Kelele za magari yaliyokuwa yanaenda huku na kule sikuzijali; mara mbili hivi nilijikuta narushiwa matusi na makonda wa daladala kwa sababu walinikosakosa.

Akili yangu ilikuwa inazunguka kuliko pia; bado nilikuwa katika hali ya kutoamini kwani yaliyotokea kama saa moja kabla niliona kama ni ndoto fulani ambayo ningeweza kuzinduka. Kwa kadiri nilivyokuwa natembea ndivyo nilivyojua kuwa sikuwa ndotoni; nilikuwa kwenye tukio lililokuwa linaendelea kutokea wakati ule.

Nilipoingia pale benki kitu cha kwanza niliomba chupa ya maji. Kabla sijaenda kwenye kaunta kujaribu kutoa hela kidogo. Nilitumia tai yangu iliyokuwa mfukoni kujipangusa uso wakati nakunywa maji. Nilisogea mbele ya kaunta ya dada wa benki na kumkabidhi kitambulisho changu pamoja na fomu ya rangi ya njano ya kuchukulia fedha. Alichukua vyote hivyo na kuanza kuingia kwenye mtandao wao kuangalia akaunti yangu na kunipatia fedha zangu.

Nilikuwa nimezama kwenye mawazo hata sikumuuona dada yule alipoondoka pale dirishani. Niligundua kuwa hakuwepo wakati namuona akija pale dirisha la kuchukulia fedha na mtu ambaye nilimtambua kuwa ni menewa wa tawi lile la benki.

“Vipi kuna tatizo” niliwawahi kabla hawajasema kitu

“Samahani Vicent, kuna tatizo kidogo katika kuifungua akaunti yako” alisema Meneja ambaye nilikuwa nafahamiana naye kwa muda mrefu tangu nifungue akaunti yangu pale.

“Iddi, kuna shida gani ni kwa akaunti zote au yangu tu?” niliuliza kwa udadisi.

“Sasa hivi ni akaunti yako tu” alisema Iddi Mchonde. Mchonde alikuwa ni mtu wa makamu ambaye alikuwa amenyoa nywele zake zote kipara. Alikuwa mfupi na mwenye kitambi kidogo ambacho kama kitaachwa kinaweza kuwa ni shida mbele ya safari. Alivyonipa jibu hilo niliuma midomo yangu kutafakari kwa sekunde chache. Kabla sijasema lolote aliniwahi.

“Naomba uje ofisini ili tuweze kufuatilia makao makuu kugundua kuna tatizo gani” alisema.

Nilipiga hesabu za haraka haraka nikaona kuna mtego hapo. Nilishaona filamu nyingi ambazo zinatoa mafunzo ya vitu kama hivi; mara nyingi hakuna jema hapo. Mawazo yangu yalikatishwa ghafla baada ya kuona gari la polisi likiingia katika eneo la benki ile; meneja hakuweza kuona kwani ilikuwa upande ambao alikuwa ameupa mgongo.

Niliamua kumshukuru na kumwambia kuna mahali ninaenda nitarudi tena baadaye labda tatizo litakuwa limetatuliwa. Sikutaka kupoteza muda nilibeba chupa yangu ya maji macho yangu yakiwa yanaelekea upande wa lile gari la polisi. Sikujua lilikuwa linafuata nini pale na sikutaka kujua lakini akili yangu yote ilikuwa inapiga ving’ora vya tahadhari. Nilitoka kwenye eneo la benki na mara moja kuchepukia upande mwingine wa jengo lile kuelekea barabarani ambako nilikuwa nimetokea. Nikashika tena barabara ya Bi Titi Mohammed kuelekea makutano yake na mtaa wa Uhuru.

Nilipofika kituo cha basi cha Baridi pale nikadandia kibajaji kuelekea mtaa wa Uhuru. Nilimuambia yule kijana anipeleke hadi tawi la NBC mtaa wa Samora. Akili yangu ilikuwa inaenda kasi sana; sikuwa nafikiria kitu kingine chochote isipokuwa uwezekano kuwa akaunti zako zote zinaweza kuwa zimepigwa stop na kama ni hivyo wapi nitaweza kupata fedha. Nilikuwa na kiasi kikubwa cha fedha taslimu nyumbani. Akaunti yangu nyingine iliyokuwa na fedha za Kitanzania ilikuwa pale; niliombea tu kuwa kilichonikuta kule Barclays kisirudie na kuwa ilikuwa ni bahati mbaya tu ya mifumo yao na siyo kitu kingine chochote.

Dakika chache za kupishana na mabasi na magari ya kila namna nilifika pale NBC. Jambo la kwanza lililonishtua ni uwepo wa magari mawili ya polisi. Nilitembea mbali na pale benki nikiwa ninaangalia kwa machale. Kengele zangu za tahadhari ziliendelea kupiga kelele. Inawezekana hakikuwa kitu chochote lakini sikutaka kujaribisha kuona; nilijua natafutwa na wanaonitafuta wameamua kubana kila kinachoweza kubanwa kikabana.

Nilimwomba dereva wa bodaboda kuniteremsha makutano ya Azikiwe na Samora. Nilikuwa najisikia njaa maana tangu ile asubuhi nilipopata kifungua kinywa sikuwa nimekula chakula chochote na nilihitaji muda wa kufikiria vizuri nini cha kufanya. Hela kidogo niliyokuwa nayo mfukoni ingenitosha kwa chakula na labda ikibidi hata kujilaza kwenye hoteli mahali fulani. Lakini nilihitaji hela na mahali pekee nilipojua kwa uhakika palikuwa na hela taslimu ni nyumbani kwangu. Nilifikiria kuwa kama polisi walikuwa wananitafuta kwa hakika watakuwa wameshafika nyumbani kwangu au wananitegea nifike.

Katika kutafakari nini cha kufanya kati ya kumpigia simu Rita au mwenyewe kwenda pale nyumbani niliona lililokuwa salama zaidi ni kupiga simu nijue hali ilivyo pale nyumbani kuliko kwenda na kujikuta nimejiingiza mwenyewe mtegoni hasa baada ya yale matukio ya mapema mchana kwenye benki. Nilikuwa nafahamku kuwa polisi na vyombo vya usalama wanaweza kumfuatilia mtu kwa kutumia simu yake ya mkononi kwani teknolojia ya GPS ambayo simu zinatumia kuelekeza mahali inaweza pia kutumiwa kujua simu ya mtu iko wapi.

Nilitembea baada ya kushuka kutoka kwenye mtaa wa Samora hadi nilipofika Diamond Plaza; kulikuwa na mgahawa mmoja pale ambao nilikuwa napenda kwenda wakati wa mchana nikaingia kimya kimya kuagiza chakula wakati napanga mkakato wa nini la kufanya. Wakati nasubiria chakula nilichomoa simu yangu na kutoa sim card yangu pamoja na memory card nyingine ambayo ilikuwa na picha na video mbalimbali. Nilitoa betri kutoka kwenye simu kuhakikisha kuwa imezimika kweli. Nilifanya hivyo bila kuonekana na mtu yeyote na nilipomaliza kula tu nikaenda kutupa simu yenyewe kwenye pipa la takataka lililokuwa pale nje ya mgahawa; nilitupa betri baada ya kuvuka upande wa pili mtaa wa Mirambo kuelekea Barabara ya Sokoine. Nilitembea kwa muda kuelekea barabara ya Sokoine lakini muda wote ule akili yangu ilikuwa inazunguka kama pia kichwani mwangu, nilikuwa nahema, nimechoka lakini pia nikiwa nashuku kila gari lililopita karibu karibu yangu. Sikutaka kusimama hadi nifike kwenye kituo cha mabasi Mwendokasi pale Mirambo inapokutana na ile ya Kivukoni. Sikuwahi kutembea maisha yangu yote kama nilivyotembea siku hiyo.

Sijui ni kitu gani kilininong’oneza kuangalia upande wa pili wa barabara. Inawezekana ni mizimu, hisia ya machale au ni bahati tu; macho yangu yalimuona mtu ambaye ni kama nilikuwa nimemuona mara nyingi siku ile na sikumtilia maanani. Hata hivyo, kumuona tena pale kulinifanya moyo ushtuke kidogo. Alikuwa ni kijana hivi labda kama miaka ishirini na tano lakini siyo wa kuzidi miaka thelathini. Alikuwa amevaa suruali ya jeans na viatu vya raba za Nike. Alikuwa amevaa tsheti nyeusi na miwani ya jua. Kilichonifanya nimuangalie ni kuwa mtu huyo huyo nilimuona mara ya kwanza wakati nakimbia kutoka ofisini baada ya kufukuzwa kazi. Nilimuona tena wakati natoka benki ya ya Barclays na baadaye nina uhakika wa asilimia mia moja alikuwa mbele yangu wakati bajaji inanishusha pale Azikiwe na Samora. Lakini kumuona kwangu tena umbali wa kama mita hamsini tu kulitokea si kwa bahati mbaya; macho yetu yaligongana kwa sekunde kadhaa na mara moja niligundua kuwa alikuwa ananitazama mimi.

Nilipoepusha macho yangu kujaribu kufikiria nifanye nini nilishtushwa na mlio wa gari lililofunga breki mbele yangu kabisa. Nilirudka pembeni kujaribu kujiepusha nalo nikidhani limekosea njia. Kilichofuatia kilitokea kwa haraka, sikupata hata muda wa kuufanya ubongo wangu ufuatilie kwa makini kwani pamoja na kukutwa na hofu ya ghafla, wazo la kuwa naelekea kufa lilinijia kwa ghafla vile vile. Sikujua ni nini kilitokea. Ninachokumbuka ni kuwa baada ya lile gari kufunga breki kitu pekee nilichoweza kukiona ni kuwa lilikuwa ni gari aina ya Toyota Landcruiser mpya kabisa ikiwa na vioo vilivyotiwa giza.

Mlango wa mbele wa abiria na ule wa nyuma wa upande wa kushoto ilifunga kwa wakati mmoja; watu wawili ambao walikuwa ni mapandakizi ya watu walitokea kwenye kila mlango na kabla sijajua nini kinafuatia mmoja alikuja nyuma yangu na mara moja nikahisi mdomo wa bastola.

“Ingia kwenye gari!” aliniamuru. Niliangalia kama kuna mtu yeyote ameona. Sidhani kama watu waliokuwepo pale walielewa nini kinatokea.

“Nimefanya nini kwani” nilijaribu kuuliza huku nikijizuia kuingia kwenye lile gari. Ndipo yule mtu mwingine alipokuja mbele yangu na kunipiga ngumi tumboni iliyonifanya niiname kwa maumivu makali. Nilijihisi kutapika kwa ghafla. Kabla sijainuka wote wawili walinusukuma mzoba mzoba kuingia kwenye mlango wa nyuma wa abiria na mmoja akaingia upande wa kushoto kwangu. Wakati huo huo mlango ule wa abiria upande wa kulia nyuma ya dereva ulifungulia na yule jamaa niliyekuwa nimemuona mwanzoni; aliyekuwa amevaa suruali ya jeans na tsheti nyeusi aliingia na kufunga mlango. Jamaa mwingine aliyetoka upande wa mbele wa abiria naye aliingia kwenye kiti chake na mtu mwingine aliyekuwa dereva nilimuona akiondoa mguu wake kwenye breki.

Kabla sijafungua mdomo wangu; jamaa mwenye tsheti nyeusi alinichomeka sindano shingoni na mara moja nilihisi usingizi mzito ukinijia. Nilijaribu kufungua mdomo kupiga kelele sikuweza. Nilijaribu kujifurugusa sikuweza. Niiliishiwa nguvu. Nilijikuta napiga kelele moyoni tu.

“Mungu nisaidie”
http://www.zamampya.com/stories/riwaya-siku-ya-mkosi-1/

INAENDELEA HAPA
 
Mkuu Mbona hujaandika haifai kusomwa na watoto chini ya miaka 18?
"Kuchoshana jana usiku" haifai kumeza watoto bwana.
Ila yote tisa hongera sana, nimeipenda hii Riwaya.
 
16508961_10154240531236156_8570951480949413950_n.jpg

SURA YA 1
Siku ya mkosi haiji na mmoja. Siku yangu ilianza kwa jina langu kuwa miongoni mwa majina yaliyotajwa kama waliotumbuliwa na Waziri mara baada ya serikali mpya kuingia madarakani. Nilipolala jana yake nilikuwa miongoni mwa watu wazito kwenye mojawapo ya taasisi nyeti zilizo chini ya Wizara ya Fedha; unaweza kuniita kuwa nilikuwa miongoni mwa ‘vigogo’ au ‘vingunge’. Usiku ule ulikuwa ni kama siku nyingine zilizopita; nilienda kulala nikiwa na mipango yangu mingine mingi tu ya kazi na ya kutumia nafasi mbalimbali zilizokuwa zinajitokeza pale kazini kuendeleza maisha yangu, ya ndugu zangu na rafiki zangu. Nililala nikiwa na furaha na maisha yangu yakiendelea kung’ara. Sikutarajia kuwa asubuhi yake na siku nzima iliyofuatia ingekuwa ni siku ya kukumbukwa katika maisha yangu.

Asubuhi ya siku ile ya Jumatatu ilianza kwa dalili fulani hivi. Kwa vile sikuwa mtu wa kuamini sana katika mambo ya ushirikina baadhi ya dalili hizo nilizipuuzia kwani niliona kama bahati mbaya tu. Kwanza, niliamka na kukuta jenereta la umeme linaunguruma kuashirikia kuwa umeme wa TANESCO ambao tulikuwa tunaukopa Watanzania wengi ulikuwa umechukuliwa na wenyewe. Wakijisikia kuurudisha wataurudisha tu, nilijiambia. Hilo halikunisumbua kwani pale nyumbani sikujali sana umeme huo. Ukiwepo nashukuru ukikosekana nasonga mbele.

Nilimuacha mchumba wangu Rita akiwa kitandani; alikuwa amechoka kwa kunichosha usiku uliopita. Labda na mimi nilikuwa nimemchosha pia; maana hayakuwa mapenzi yale ya usiku ilikuwa ni vurugu mechi. Nilijiona kama miongoni mwa watu wenye bahati sana duniani. Rita alikuwa ni mtoto wa Balozi wa Tanzania nchini China Dkt. Rose Kitangile Ericsson. Baba yake alikuwa ni Msweden aliyekuwa amefanya kazi Tanzania kama Mkurugenzi Mkazi wa SIDA miaka ya themanini na baadaye kuamua kuishi Tanzania baada ya mkataba wake kuisha. Aliomba uraia wa Tanzania miaka michache baadaye. Walizaliwa wawili tu kwenye familia yake; yeye mkubwa na mdogo wake wa kike Marieta ambaye alikuwa anasoma huko Sweden.

Wakati naamka kitandani nilimuangalia Rita alivyolala na kujipongeza moyoni kuwa kwa hakika nilikuwa nimeopoa kweli kweli. Mtoto alikuwa ameumbwa akaumbika na kama mbinguni kuna malaika basi nina uhakika mmoja wao alitupwa duniani kama zawadi kwangu. Alikuwa amelala akiwa mtupu kabisa kajifunika shuka nyepesi ambayo ilimfanya aonekane kama picha nzuri ya kuchora ambayo mtu angeweza kuitundika ukutani kwa fahari. Ningekuwa mtu wa kuendekeza mambo hayo kwa kweli ningepiga simu kutokwenda kazini niendelee na sarakasi zangu. Kuna watu wanasema kiporo kitamu.

INAENDELEA HAPA

Mzee naona umeirudia fani.

Safi sana.

Majeruhi wa Mapenzi iliwahi kunipatia mchumba...na kuniingizia hasara ya 20,000 pale duka la Scholastic....Mlimani City:D
 
Mzee naona umeirudia fani.

Safi sana.

Majeruhi wa Mapenzi iliwahi kunipatia mchumba...na kuniingizia hasara ya 20,000 pale duka la Scholastic....Mlimani City:D
hahahahaha aisee nakumbuka; sasa wanataka kuitengeneza movie aisee.. finger crossed. Nasubiria nione script kwanza.
 
Mkuu Mbona hujaandika haifai kusomwa na watoto chini ya miaka 18?
"Kuchoshana jana usiku" haifai kumeza watoto bwana.
Ila yote tisa hongera sana, nimeipenda hii Riwaya.

Sasa si mtu mzima tu ataelewa nimemaanisha nini; ningetaka kuwa more graphic ningesema maneno mengine ya ajabu.. mtoto akikuuliza "kuchoshana" ni nini itabidi iutafute maelezo mepesi..
 
16508961_10154240531236156_8570951480949413950_n.jpg

SURA YA 1
Siku ya mkosi haiji na mmoja. Siku yangu ilianza kwa jina langu kuwa miongoni mwa majina yaliyotajwa kama waliotumbuliwa na Waziri mara baada ya serikali mpya kuingia madarakani. Nilipolala jana yake nilikuwa miongoni mwa watu wazito kwenye mojawapo ya taasisi nyeti zilizo chini ya Wizara ya Fedha; unaweza kuniita kuwa nilikuwa miongoni mwa ‘vigogo’ au ‘vingunge’. Usiku ule ulikuwa ni kama siku nyingine zilizopita; nilienda kulala nikiwa na mipango yangu mingine mingi tu ya kazi na ya kutumia nafasi mbalimbali zilizokuwa zinajitokeza pale kazini kuendeleza maisha yangu, ya ndugu zangu na rafiki zangu. Nililala nikiwa na furaha na maisha yangu yakiendelea kung’ara. Sikutarajia kuwa asubuhi yake na siku nzima iliyofuatia ingekuwa ni siku ya kukumbukwa katika maisha yangu.

Asubuhi ya siku ile ya Jumatatu ilianza kwa dalili fulani hivi. Kwa vile sikuwa mtu wa kuamini sana katika mambo ya ushirikina baadhi ya dalili hizo nilizipuuzia kwani niliona kama bahati mbaya tu. Kwanza, niliamka na kukuta jenereta la umeme linaunguruma kuashirikia kuwa umeme wa TANESCO ambao tulikuwa tunaukopa Watanzania wengi ulikuwa umechukuliwa na wenyewe. Wakijisikia kuurudisha wataurudisha tu, nilijiambia. Hilo halikunisumbua kwani pale nyumbani sikujali sana umeme huo. Ukiwepo nashukuru ukikosekana nasonga mbele.

Nilimuacha mchumba wangu Rita akiwa kitandani; alikuwa amechoka kwa kunichosha usiku uliopita. Labda na mimi nilikuwa nimemchosha pia; maana hayakuwa mapenzi yale ya usiku ilikuwa ni vurugu mechi. Nilijiona kama miongoni mwa watu wenye bahati sana duniani. Rita alikuwa ni mtoto wa Balozi wa Tanzania nchini China Dkt. Rose Kitangile Ericsson. Baba yake alikuwa ni Msweden aliyekuwa amefanya kazi Tanzania kama Mkurugenzi Mkazi wa SIDA miaka ya themanini na baadaye kuamua kuishi Tanzania baada ya mkataba wake kuisha. Aliomba uraia wa Tanzania miaka michache baadaye. Walizaliwa wawili tu kwenye familia yake; yeye mkubwa na mdogo wake wa kike Marieta ambaye alikuwa anasoma huko Sweden.

Wakati naamka kitandani nilimuangalia Rita alivyolala na kujipongeza moyoni kuwa kwa hakika nilikuwa nimeopoa kweli kweli. Mtoto alikuwa ameumbwa akaumbika na kama mbinguni kuna malaika basi nina uhakika mmoja wao alitupwa duniani kama zawadi kwangu. Alikuwa amelala akiwa mtupu kabisa kajifunika shuka nyepesi ambayo ilimfanya aonekane kama picha nzuri ya kuchora ambayo mtu angeweza kuitundika ukutani kwa fahari. Ningekuwa mtu wa kuendekeza mambo hayo kwa kweli ningepiga simu kutokwenda kazini niendelee na sarakasi zangu. Kuna watu wanasema kiporo kitamu.

INAENDELEA HAPA
Ln xx itaendelea?
 
Back
Top Bottom