Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,253
- 44,595
Nyuki wamechachamaa, Nyuki wameshacharuka,
Hasira kama kichaa, kichwani zimewashika,
Hawana cha msamaha, zamu yao imefika,
Nyuki wamechachamaa, Kingo wamekasirika!
Hawa nyuki wa asali, nyuki wanaosifika,
Wanauliza maswali, yapo yasotamkika,
Si moja au mawili, ni mengi ya uhakika,

Asali twatengeneza, mbona bado maskini,
Na ngambo tunaiuza, inauzwa hata ndani,
Kingo ndio wapendeza, sisi tumekosa nini

Asali yetu ni bora, mfano wake hakuna,
Mtwara hadi Tabora, mizinga imejazana,
Kingo wanavyotupora, wanetu kula hakuna,

Wageni wanatujia, kuja kurina asali,
Wanakuja kwa mamia, toka masafa ya mbali,
Kingo wanatuambia, ni wawekezaji mahili,

Mikataba waingia, kingo wanashangilia,
Mizinga wanagaia, nyuki tunaangalia,
Miaka inakimbia, mizinga yakaukia,

Mzinga ukiishia, mwingine wanahamia,
Wenyewe tunajifia, huku tunajililia,
Twafa tunaangalia, wapi tutakimbilia,
Nyuki wamechachamaa, Kingo wamekasirika
Kingo walishazoea , kula asali kwa zamu,
Hakuna wa kufokea, wanajilia kwa hamu,
Mabingwa wa kubobea, wamegeuka walimu,

Wanakula na masega, masega yanye asali!
Mizinga toka Nzega, kwa sahani na bakuli,
Wanakula na kumwaga, nyuki tunalikubali?
Nyuki Wamechachamaa, Kingo wamekasirika!
Sasa nyuki kimewaka, kingo wanataharuki!
Wamezindukazinduka, lahaullah hawa nyuki!
Kingo wanatetemeka, wamezidiwa mikiki!

Wanaleta na polisi, kupiga mkwara nyuki,
Nyuki wanazidi kasi, wala hawababaiki,
Wanapigwa na risasi, nyuki chini haanguki,

Toka Arusha na Mtwara, Tanga hadi Newala,
Na nyuki toka Tabora, wa Iringa, na Ukala
Utadhani Tora Bora, Kingo wanashindwa kula!
Nyuki wamechachamaa kingo wamekasirika!
Nyuki wametuma neno, asali haitoki tena,
Haitoki kwa maneno, au vitisho vya jana,
Kingo wakosa unono, wageni waulizana,
Nyuki wamechachama, kingo wamekasirika!
Tushikamane nyuki, asali hiyo ni yetu,
Ya kwenu tena ya haki, yenu na ya wanetu!
Kingo wakae na nyuki, asali itufae petu!
Nyuki wamechachamaa, kingo wamekasirika!
Ninalo neno kwa kingo, kingo walamba asali,
Mmetawala kwa uongo, mkikimbia maswali,
Ahadi za mlolongo, mkipindisha kauli!

Kukasirika kwa kingo, hakuwasumbui nyuki!
Hata waje na magongo, huyu nyuki hatishiki,
Umeporomoka wongo, umekoma uzandiki!

Nyuki wameshaamka, kulala tena hakuna,
Na lindo wamelishika, hawatoachia tena,
Zamu yenu kugeuka, kingo ngondo mwaona,
Nyuki wamechachamaa, kingo wamekasirika
Beti zangu zinakoma, ninafunga kwa nukta,
Wakijiji natuwama, heshima zangu wapata,
Nyuki wameshasimama, hawa kingo watajuta!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Kwa heshima ya Marehemu Saadan Abdul Kandoro na Shairi lake la Siafu Wamekazana