Ufugaji nyuki wa kisasa

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Natamani kumshauri mwanangu akasomee utaalamu wa kufuga nyuki chuo kikuu. Ninachojiuliza ni kuwa je, ni vyepesi kiasi gani au ni ngumu kiasi gani mtu kujiajiri kwenye ufugaji nyuki ukiwa na utaalam wako mwenyewe?

Je, ni gharama na changamoto zipi kwa mtu kujiajiri kwenye ufugaji wa nyuki?

Je ni lazima kufugia nyuki porini?

========
Mbinu za ufugaji nyuki

MBINU ZA UFUGAJI NYUKI
Mbinu za ufugaji nyuki : Nyuki ni wadudu wadogo ambao hutengeneza na kula asali. Nyuki huishi na kufanya kazi kijamaa, Utendaji wao wa kazi hutegemeana na umri na mahitaji ya kundi husika. Kuna aina tatu za nyuki katika kundi moja la nyuki. Kundi huwa na Malkia madume na vibarua.

Kuzaliana
Nyuki huzaliana kwa msimu maalum, unapofika msimu huo, kundi husika huzalisha madume ya kutosha na baadaye malkia wachache ambao wanapopevuka hujamiiana na madume.

Kundi la vibarua huwa la nyuki majike ambao sehemu zao za kike hazifanyi kazi. Hawa ndiyo watendaji wa takribani shughuli zote katika kundi.

Miongoni mwa shughuli zinazotendwa na vibarua ni kuzalisha chakula cha mabuu au malkia, ulinzi wa kundi kwa kutumia sumu inayotunga katika mwili wake.

Mara sumu hii inapokuwa tayari hufanya kazi ya kwenda kutafuta maji na chakula kwenye maua. Na inapofika wakati ambao kundi huhitaji masega basi vibarua huanza kujenga masega.

NAMNA MIZINGA YA NYUKI INAVYOKUA NA KUNING'INIZWA KWENYE MITI

Namna mizinga ya nyuki inavyokua na kuning’inizwa kwenye miti

Mbinu za ufugaji
Kutokana na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa nyuki kuhusu namna anavyozalisha asali, mbinu mbalimbali zimependekezwa za namna ya kufuga nyuki.

Mbinu hizi zimelenga kumfanya nyuki azalishe asali zaidi kwa matumizi ya binaadamu na sio kwa manufaa yao (nyuki) wenyewe ambao lengo lao la kutengeneza asali ni kujiwekea chakula cha akiba kwa ajili ya wakati wa njaa.

Mara nyuki atengenezapo asali humpa changamoto mwanadamu kuamini kwamba anahitaji jitihada zaidi ili aweze kujaza nafasi inayoonekana tupu kwenye mzinga kabla ya msimu wa maua haujamalizika.

Ili uweze kupata mafanikio katika ufugaji wa nyuki inapasa kuzingatia mambo yafuatayo:
• Kwanza ni vyema kufahamu mazingira ya mahali unapotaka kufugia nyuki wako na ni muhimu ni kuhakikisha kuwapo kwa;

• Mimea itoayo maua ya kutosha ili nyuki wako wasipoteze muda na nishati kubwa kutafuta chakula.

• Pawepo na majike karibu na iwapo hayapo basi wawekee kisima kidogo na kutumbukiza vijiti.

• Pawe na kivuli cha kutosha ili nyuki wasipoteze muda mrefu kupooza kiota chao badala ya kwenda kutafuta chakula.

• Pasiwe na njia kuu kwa vile nyuki hawapendi kelele na harufu mbaya kama moshi wa mashine, moto nakadhalika.

• Pasiwe mahali penye tindikali la madawa kwani huweza kuwaua nyuki wakati wakisaka chakula na maji.

• Baada ya kuijua mimea itoayo maua vilevile ni muhimu kujua wakati au msimu ambao mimea hiyo hutoa maua. Kwa kawaida maua hutoka baada ya mvua za masika na vuli. Kwa kawaida msimu mkubwa huwa baada ya mvua za masika na wakati huo hujulikana kama msimu wa asali.

• Mara baada ya maua haya ya msimu wa asali yanapoanza kupuputika asali huanza kuiva kwenye mizinga au kiota. Nyuki huwa tayari wametengeneza asali na kuifunika kwa nta nyororo ili isiweze kunyonya maji (moisture) kwenye hewa.

• Wakati mvua zinapokaribia kuimalizika makundi ya nyuki huanza kuzaa watoto wengi ili wapatikane nyuki wengi wa kukusanya chakula, hivyo ni vyema kuzuia kujigawa kwa nyuki wakati huo.

NAMNA YA KUJIKINGA NA MASHAMBULIZI YA NYUKI

Namna ya kujikinga na mashambulizi ya nyuki

Mfugaji akishaelewa mazingira ya ufugaji nyuki, inapasa aamue mahali pa kufugia nyuki na muda na kitu gani anatakiwa kufanya.

Muhimu kuzingatia
• Mfugaji nyuki lazima ajue jinsi ya kuweka mizinga ili nyuki waweze kuingia kwenye mzinga yake. Mara nyingi nyuki wanapoanza kuzaana mfugaji nyuki asafishe mizinga yake na kuweka chambo ili waingie wenyewe.

Ulinaji wa asali
• Mfugaji anashauriwa kuwa na kinga ya miiba ya nyuki. Nyuki huwa wanauma na sumu yao ni kali na yenye maumivu. Kinga zinazopendekezwa ni kama vile ovaroli la mikono mirefu lenye rangi ya khaki, nyeupe au maziwa (usitumie lenye rangi nyeusi au nyekundu), tumia pia wavu wa usoni (Bee veil), mipira ya mikononi (Bee gloves), na viatu (Gum boots).

MCHAKATO WA ULINAJI ASALI

Mchakato wa ulinaji asali

• Ni vema kutumia bomba la moshi (Bee smoker). Bomba hili huwekwa kipande cha gunia au nguo ili ule moshi uweze kupulizwa kwenye nyuki na kuwafanya watulie.

Nyuki wanapoona moshi au moto jambo la kwanza hufikiria kukimbia au kuhama lakini kabla ya kukimbia ni lazima ale asali ashibe ndio aondoke.

Wakati akijishughulisha kula asali kwenye masega mfugaji anaweza kufanya kazi yake bila nyuki kumshambulia au kumghasi. Vifaa hivi vinapatikana kwenye ofisi za idara za misitu na nyuki.

• Nyuki wa kiafrika wa kusini mwa ukanda wa Sahara (Apis Mellifera Scullelata) huwa ni wakali kupita kiasi, hivyo baadhi ya wafugaji wa nyuki hulazimika kuchoma aina fulani ya majani (Ocinum) au aina fulani za uyoga (Puff balls) inayomea kwenye magamba ya miti iliyooza wakati wa mvua kujikinga dhidi ya mashambulizi ya nyuki wakati wa kulina asali. Wengine huchovya gunia dawa ijulikanayo kama Ammonium nitrate na linapokauka huchomwa ndani ya bomba la moshi.

Vyote hivi huwafanya nyuki kulewa na kupumbaa hivyo kumwezesha mfugaji kushughulika bila wasiwasi na nyuki wake kwenye mzinga na bila kuwathiri nyuki.

• Hata hivyo mfugaji anatakiwa kupata ushauri zaidi toka idara ya misitu na nyuki ili aweze kufuga nyuki kwa ubora na mafanikio zaidi.

=======
Michango ya wadau
Inawezekana kujiajiri kupitia ufugaji nyuki ikiwa unamtaji wa kutosha. vitu vya msingi ili uweze kujihusisha na ufugaji nyuki ni;

1. Utaalamu: Kwa maana ya elimu na ujuzi wa ufugaji nyuki ambao utaweza kuupata chuoni au kwa wataalamu wa ufugaji nyuki.

2. Eneo la kufugia: Unatakiwa uwe na eneo kubwa la kutosha ambalo lina chakula cha nyuki kama vile maji matamu matamu ya kwenye maua na unga unga (necta na pollen). eneo hilo liwe umbali wa km 7 kutoka kwenye makazi ya watu na mashamba yanayotumia viuatilifu, liwe na maji ya kutosha, lisiwe na upepo mkali, lisiwe na maadui wa nyuki (simba wa nyuki, nyegere na ndege wala nyuki n.k).

3. Mizinga: mizinga utakayoanzia kufugia inategemea na ukubwa wa mtaji ulionao. Mizinga ipo ya jadi na ya kisasa. mizinga ya kisasa pia ipo mizinga ya kati ya kitanzania na biashara. kama utakuwa na mtaji mdogo unaweza kuanza kutumia mizinga ya jadi (ya magogo), ila endapo mtaji ni wa kutosha unaweza kutumia mizinga ya kisasa mfano mzinga wa kati wa kitanzania(transitional hive) au mzinga wa kibiashara wa kitanzania (commercial hive).

4. Vifaa vya kinga (protective gears): katika ufugaji nyuki utahitajika kuwa na vifaa vya kinga kwa ajili ya kujikinga na nyuki wasikushambulie haswa kipindi cha kurina asali. Vifaa utakavyohitajika kuwa navyo ni overrol, taji la uso (bee veil), mipira ya mikono (gloves), viatu virefu (gumboot), kofia, bomba la moshi (bee smoker) na kisu cha mzinga (hive tool).

Gharama kubwa za ufugaji nyuki zimejikita haswa katika upatikanaji eneo na mizinga ya nyuki nazo zinategemea na mahala ulipo. kwa mfano huku kanda ya kaskazini mzinga wa jadi ni kiasi cha sh 20,000/=, mzinga wa kisasa ni kuanzia 80,000/= hadi 120,000/=. vifaa vya kujikinga seti moja ya vifaa ni sh.150,000/=.

Eneo lolote kubwa lenye sifa nilizoziainisha hapo juu na lililo mbali na makazi ya watu linafaa kwa ufugaji wa nyuki na siyo lazima iwe porini. Kwenye ufugaji nyuki unaweza kutumia mabanda yalijengwa kwa miti au matofali ( bee cage or bee house).
---
Habari.
Unahitaji shamba la miti yenye maua kwaajili ya kuwavutia nyuki au kama miti haina maua unaweza kupanda mazao yenye maua umbali usiozidi km 5 kutoka mizinga ilipo.
Unahitaji mizinga bora
Nta
Na vifaa vitakavyokusaidia kipindi cha kilimo chako kama vile mavazi ya uvunaji asali.

Gharama kwa mzinga mmoja.
Mzinga 70000
Nta 1 kg 15000
Kundi la nyuki 30000 (hii ni kwa ufugaji wa kisasa huitaji kusubiri nyuki waje wenyewe)
Hapo utakua umeanza ufugaji.
-----
Ahsante,

1. Matumizi ya Chavua na Jeli ya Kufalme ni mengi sana katika afya za binadamu, jama kinga na tiba ya magonjwa mengi sana. Mada hii nitaiongelea baadae.

2. Ni muhimu sana Kutambua aina ya miti na aina ya maua yanayopatikana eneo husika. Utatakiwa kujua Msimu wa hio miti kutoa maua ili kuhakikisha kwamba maua yanakuepo kwa muda wote au kipindi kirefu.
Tafafhali hudhuria Mafunzo ili kupata hii elimu.

3. Kuhusu idadi ya mizinga inayotosha kawika chumba, itategemea na mambo kadha wa kadha;
i. Aina ya nyuki
ii. Aina ya mazao ambayo unataka kuvuna

Sent using Jamii Forums mobile app
----

Nyuki huwa wana athiriwa sana na dawa za kuuwa wadudu zinazopuliziwa kwenye mimea mbali mbali ya mazao ya biashara.

Kumbuka nyuki anapokuwa anatafuta material ya kutengeneza asali huwa anapapasa karibu kila mmea. Kwa bahati mbaya hii mimea ya kisasa huwa inapuliziwa dawa za kuuwa wadudu waharibifu ambazo hizi dawa huwa ni sumu hat kwa mwanadamu.

Nyuki wanapopita especially maeneo yenye hiyo mimea na kuigusa, huwa wanarejea na ile sumu katika mikono yao na wanaingia nayo kwenye mzinga bila kujua madhara yake. Na inapotokea wakawa wengi na wakaisambaza, ikamfikia hadi malkia ndipo hapo huwa ni mwisho wa hilo koroni.

Hii tafiti niliifanya miaka mitatu iliyopita kwa kutazama video za kimazingira huko YouTube. Na nilishaizungumza kipindi fulani kuwa haya madawa na mbegu za kibiashara zitakuja kuwa na madhara kwenye mazingira siku zijazo, ila sikupata ushirikiano mzuri nikaonekana kama mtu anayejifanya mjuaji.

Leo huyu mwenzetu ameshaanza kuona madhara.....

Kama unabisha nenda katazame mizinga iliyopo kwenye misitu au maporini, uone kama inakutwa na hili tatizo.
[/QUOTE
----
Habari Mkuu, Pole sana kwa kasumba ya kupoteza nyuki wako mara mara...

Kwa kawaida Nyuki wa asali hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya kuambukizwa ambayo husababishwa na bakteria, fangasi, protozoan, virusi na mara chache hushambuliwa na predator na sumu...

Pia magonjwa haya huenezwa kutoka kundi moja kwenda lingine kwa nyuki wakubwa, kwa kutumia mzinga ulio na vimelea, waangalizi wa mizinga, vifaa vinavyotumika katika kulina asali, na pia nta kutoka katika mimea ambapo nyuki hufuata nta kwa ajili ya kutengenezea asali...

Magonjwa ni mengi mno, kwa maelezo siwezi kusema moja kwa moja ni ugonjwa gani unaowasibu nyuki wako hadi kupelekea wao kufa kwa wingi hivyo. Ingawa kwenye industry yetu hii tunapoona vifo vya ghafla na kwa wingi zaidi huwa moja kwa moja huwa ugonjwa husika husababishwa na virusi...

Hivyo, ningependa kujua unafugia katika mazingira gani? upo peke yako au umepakana na mashamba husika?

Pia, vifo hivyo ni kwa nyuki wakubwa tu au hadi wale nyuki watoto ambao hupatikana katika masega?

Na hali husika katika masega yapoje? hapa nataka kujua rangi ya sega la nyuki lina rangi gani? au kuna mabadiliko yoyote ya rangi?

Nataka kujua hayo ili kuweza ku narrow diagnosis mkuu..

Ahsante...
----
Yap ni kweli kabisa nyuki kama viumbe vingine vinaweza kuzalishwa kwa wingi,kama ilivyo kwa mifugo kama kuku nyuki huweza kuzalishwa kwa wingi zaidi,na wataalamu wabobezi wa nyuki hushauri ni vyema ukazalisha nyuki wako wenyewe ambao wanasifa za kuresist magonjwa kuwa na uwezo wa kuzalisha asali kwa wingi،wafugaji wengi wa nyuki hawajui tasnia nzima ya ufugaji wa nyuki kwa undani na kudhani ufugaji wa nyuki ni jambo LA kawaida na kupata asali ni bahati,kimsingi kinachodhalishwa ni malkia wa nyuki,huyu ndio kiwanda cha nyuki wote kwenye mzinga.sio kazi nyepesi kumdhalisha malkia ,lakini ukiamua in rahisi sana,ikumbukwe malkia hutaga mayai yanayoweza kuwa workers au queen,kama unahitaji malkia basi kuna namna ya kufanya mayai yaliotagwa kutoa malkia tu,kuna chakula spesho unatakiwa kuwawekea malarva ili wawe malkia ,na hivyo kuwa na malkia wengi ambao utawapandikiza kwenye mizinga mipya na hivyo kuongeza uzalishaji wa nyuki

sio rahisi kueleza mchakato mzima hapa,lakini ukipenda ntaleta somo lote lijulikanalo kama "practical queen rearing"

kingine kwa wafugaji wa nyuki hawajui kuwa kupata asali kidogo husababishwa na drone kuwa wengi kwenye mzinga,na hivyo kula asali yote,embu fikiri unafuga kuku halafu majogoo wako 100 mitetea 20,tarajis kupata hasara kwa sababu majogoo watakula Shea ya chakula nyingi huku wakiwa hawana faida ukulinganisha na mitetea,kitaalamu jogoo mmoja kwa mitetea mitano mpaka nane،ndivyo ilivyo kwa nyuki inabidi ukontrol idadi ya nyuki dume dhidi ya nyuki jike, nyuki dume wanahitajika wachache sana kwenye mzinga،kazi yao ni kumpanda malkia tu.

wakiwa wengi hutafuna asali sana na kusababisha mfugaji kupata mavuno kiduchu unapaswa kijifunza namna ya kuwapunguza nyuki ,mzinga unapaswa kuwa na nyuki jike wengi zaidi,kwa sababu ndio huzalisha asali

udhalishaji wa nyuki unahitiji kujitoa kwelikweli kama unajaribu acha kabisa
udhalishaji wa malikia unahitaji vifaa maalumu,mizinga inayotumika kudhalisha malkia inapaswa kutengenezwa kitaalamu na inapaswa kuwa karibu na mfugaji 24 hours wakati wa kupandika mayai kuwa malkia,

ikumbukwe tunadhalisha malkia kwa kuwa ndio kiongozi mzalishaji wa asali
malkia anapopandwa na nyuki dume kutaga mayai yanadestinate kuwa workers na Queen asipopandwa hutaga mayai yanayokuwa drone pekee
 
Ni rahisi kujibiwa maswali hayo kama utampata mtu mwenye fani hiyo. Ila kuanzisha ufugaji wa kisasa wa nyuki ni gharama lakini italipa.

Gharama kubwa ni kuhakikisha una maji muda wote hivyo utawachimbia kisima.utakuwa na uhakika kukaa nao muda wote.

Pia kuwekeza kwenye mizinga ya kisasa ya kibiashara. Kuhusu kufugia porini inategemea ni aina gani ya nyuki ya nyuki.

Je ni nyuki wakubwa au nyuki wadogo. Katika uvunaji na uandaaji wa bidhaa yako kwa kuwa sasa watu wanaofanya hiyo ni wengi lenga kupata nembo ya ubora ya TBS ili uweze kuuza soko la kimataifa.

Hivyo vikiria kitu ambacho kitakuwa ni international. Ni jambo linalohitaji uwekezaji wa kutosha ili kupata mafanikio makubwa. Ukidhamiria kufika hatua hiyo utakuwa mbali sana.
 
Kuongezea pia, Nyuki wadogo soko lipo zuri na ushindani sio mkubwa. Ila utapata fedha zaidi kama utaweza kupata nembo ya ubora ya bidhaa zako.
 
Gharama ni manunuzi ya mizinga na mazingira yenye usalama. Kuna siku niliona mizinga ya kisasa kabisa pale Njiro Arusha.

Kwa kweli iko vizuri kabisa ambayo unaweza ukaiweka porini nyuki wakiingia unafunga na kupeleka kwenye maeneo unayotaka. Tatizo bei yake sasa.
 
Inawezekana kujiajiri kupitia ufugaji nyuki ikiwa unamtaji wa kutosha. vitu vya msingi ili uweze kujihusisha na ufugaji nyuki ni;

1. Utaalamu: Kwa maana ya elimu na ujuzi wa ufugaji nyuki ambao utaweza kuupata chuoni au kwa wataalamu wa ufugaji nyuki.

2. Eneo la kufugia: Unatakiwa uwe na eneo kubwa la kutosha ambalo lina chakula cha nyuki kama vile maji matamu matamu ya kwenye maua na unga unga (necta na pollen). eneo hilo liwe umbali wa km 7 kutoka kwenye makazi ya watu na mashamba yanayotumia viuatilifu, liwe na maji ya kutosha, lisiwe na upepo mkali, lisiwe na maadui wa nyuki (simba wa nyuki, nyegere na ndege wala nyuki n.k).

3. Mizinga: mizinga utakayoanzia kufugia inategemea na ukubwa wa mtaji ulionao. Mizinga ipo ya jadi na ya kisasa. mizinga ya kisasa pia ipo mizinga ya kati ya kitanzania na biashara. kama utakuwa na mtaji mdogo unaweza kuanza kutumia mizinga ya jadi (ya magogo), ila endapo mtaji ni wa kutosha unaweza kutumia mizinga ya kisasa mfano mzinga wa kati wa kitanzania(transitional hive) au mzinga wa kibiashara wa kitanzania (commercial hive).

4. Vifaa vya kinga (protective gears): katika ufugaji nyuki utahitajika kuwa na vifaa vya kinga kwa ajili ya kujikinga na nyuki wasikushambulie haswa kipindi cha kurina asali. Vifaa utakavyohitajika kuwa navyo ni overrol, taji la uso (bee veil), mipira ya mikono (gloves), viatu virefu (gumboot), kofia, bomba la moshi (bee smoker) na kisu cha mzinga (hive tool).

Gharama kubwa za ufugaji nyuki zimejikita haswa katika upatikanaji eneo na mizinga ya nyuki nazo zinategemea na mahala ulipo. kwa mfano huku kanda ya kaskazini mzinga wa jadi ni kiasi cha sh 20,000/=, mzinga wa kisasa ni kuanzia 80,000/= hadi 120,000/=. vifaa vya kujikinga seti moja ya vifaa ni sh.150,000/=.

Eneo lolote kubwa lenye sifa nilizoziainisha hapo juu na lililo mbali na makazi ya watu linafaa kwa ufugaji wa nyuki na siyo lazima iwe porini. Kwenye ufugaji nyuki unaweza kutumia mabanda yalijengwa kwa miti au matofali ( bee cage or bee house).
 
Inawezekana kujiajiri kupitia ufugaji nyuki ikiwa unamtaji wa kutosha. vitu vya msingi ili uweze kujihusisha na ufugaji nyuki ni;
1. Utaalamu: Kwa maana ya elimu na ujuzi wa ufugaji nyuki ambao utaweza kuupata chuoni au kwa wataalamu wa ufugaji nyuki.

2. Eneo la kufugia: Unatakiwa uwe na eneo kubwa la kutosha ambalo lina chakula cha nyuki kama vile maji matamu matamu ya kwenye maua na unga unga (necta na pollen). eneo hilo liwe umbali wa km 7 kutoka kwenye makazi ya watu na mashamba yanayotumia viuatilifu, liwe na maji ya kutosha, lisiwe na upepo mkali, lisiwe na maadui wa nyuki (simba wa nyuki, nyegere na ndege wala nyuki n.k).

3. Mizinga: mizinga utakayoanzia kufugia inategemea na ukubwa wa mtaji ulionao. Mizinga ipo ya jadi na ya kisasa. mizinga ya kisasa pia ipo mizinga ya kati ya kitanzania na biashara. kama utakuwa na mtaji mdogo unaweza kuanza kutumia mizinga ya jadi (ya magogo), ila endapo mtaji ni wa kutosha unaweza kutumia mizinga ya kisasa mfano mzinga wa kati wa kitanzania(transitional hive) au mzinga wa kibiashara wa kitanzania (commercial hive).

4. Vifaa vya kinga (protective gears): katika ufugaji nyuki utahitajika kuwa na vifaa vya kinga kwa ajili ya kujikinga na nyuki wasikushambulie haswa kipindi cha kurina asali. Vifaa utakavyohitajika kuwa navyo ni overrol, taji la uso (bee veil), mipira ya mikono (gloves), viatu virefu (gumboot), kofia, bomba la moshi (bee smoker) na kisu cha mzinga (hive tool).

Gharama kubwa za ufugaji nyuki zimejikita haswa katika upatikanaji eneo na mizinga ya nyuki nazo zinategemea na mahala ulipo. kwa mfano huku kanda ya kaskazini mzinga wa jadi ni kiasi cha sh 20,000/=, mzinga wa kisasa ni kuanzia 80,000/= hadi 120,000/=. vifaa vya kujikinga seti moja ya vifaa ni sh.150,000/=.
Eneo lolote kubwa lenye sifa nilizoziainisha hapo juu na lililo mbali na makazi ya watu linafaa kwa ufugaji wa nyuki na siyo lazima iwe porini. Kwenye ufugaji nyuki unaweza kutumia mabanda yalijengwa kwa miti au matofali ( bee cage or bee house).
Wewe ni mfugaji nyuki??
 
Je, kuna tofauti katika masoko kwa asali iliyotokana na mizinga ya jadi na ile ya mizinga ya kisasa....pia lita 1 ya asali inauzwaje??.....
 
Habari ndugu zangu, Naomba msaada wa kimawazo kwenye ufugaji wa nyuki nimekuwa nikiwaza sana hii kazi lakini nabaki njia panda pia ufugaji huu utakuwa mbali namimi kwani ninakazi nyingine, Asanteni sana.
 
Jaribu kuwasiliana na chuo cha nyuki Tabora wanaweza kukupa msaada zaidi. Kingine ni kuwa hizi mada zimejadiliwa sana humu. Jaribu kusearch utapata majibu.
 
Habarini za mchana wapendwa, natumaini kuwa mu wazima wa afya njema kabisa,
niende moja kwa moja kwenye maada;-

Nahitaji kufanya biashara ya ufugaji wa nyuki kwa kuanza na mizinga 100, kutokana na ufinyu wa eneo nililo nalo pamoja na mtaji nilio nao na hapa kuna mtaalamu wa kutengeneza mizinga pamoja na kuita nyuki ameshapatikana.

Kwa kuwa sina elimu yoyote ya ufugaji wa nyuki nimekuja kwenu kuomba ushauri kwa yeyote mwenye utaalamu kuhusiana na biashara hii anisaidie hatua ninazotakiwa kuzifuata ili niweze kufanya biashara hii kihalali.
 
Mkuu si ushasema mtaalam wa mizinga na kuvuta nyuki umempata? Sasa utaalam gani tena unataka? Any way nakushauri angalia YouTube utajifunza mengi.

Ukishaanza nitakuja kujifunza. Uko mkoa gani Mkuu?
 
Mkuu huyu mtu yeye ni wa kutengeneza na kuita nyuki tu zaidi yeye ni wa kienyeji, mambo ya kitaalam hajui, binafsi nilitaka kufahamu kama kuna mambo ya vibali au taratibu za kisheria kutoka serikalini ili nisije kuzuiwa mbeleni, Shamba liko Handeni Tanga.
 
Nahitaji kufanya ufugaji wa nyuki {wakubwa na wadogo} .... Naomba mchanganuo na mazingira ya ufugaji huo.......... Wataalam karibun.....
 
Nahitaji kufanya ufugaji huo pia mwenye uzoefu wa taratibu au hatua za kufuata (hata guide jornal pdf hivi) tupia hapa.
 
Nahitaji kufanya ufugaji wa nyuki {wakubwa na wadogo} .... Naomba mchanganuo na mazingira ya ufugaji huo.......... Wataalam karibun.....
Habari.
Unahitaji shamba la miti yenye maua kwaajili ya kuwavutia nyuki au kama miti haina maua unaweza kupanda mazao yenye maua umbali usiozidi km 5 kutoka mizinga ilipo.
Unahitaji mizinga bora
Nta
Na vifaa vitakavyokusaidia kipindi cha kilimo chako kama vile mavazi ya uvunaji asali.

Gharama kwa mzinga mmoja.
Mzinga 70000
Nta 1 kg 15000
Kundi la nyuki 30000 (hii ni kwa ufugaji wa kisasa huitaji kusubiri nyuki waje wenyewe)
Hapo utakua umeanza ufugaji.
 
Mkuu kama upo ndani ya Dar karibu nikupatie maandiko kadha wa kadha pia unaweza kwenda pale jengo la mali asili ukapata elimu yakukufaa.
 
mkuu ka upo ndani ya dar karibu nikupatie maandiko kadha wa kadha pia unaweza enda pale jengo la mali asili ukapata elimu yakukufaa
Asanteee muungwanaaa kwasasa nipo Moshi ila ntakuja Dar soon mana kila kitu business, ukitaka kujifunza business.. Uuh! ............ Unatokea Uchira nini!??.... Mana mimi napandia Kawawa road (Moshi huku).... Joking...
 
Back
Top Bottom