kidadari
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 8,647
- 9,595
SWALI:ZIPI AINA ZA NYUKI NA TABIA ZAO?
JIBU:
Nyuki ni jamii ya wadudu wenye jozi mbili za m zabawa mepesi yenye mishipa laini.Nyuki huishi maisha ya kijamaa.Mwili wa Nyuki umegawanyika katika sehemu kuu tatu;kichwa ,kifua na tumbo(fumbati).Tofauti na wadudu wengine,nyuki hutengeneza na kuhifadhi Asali kwenye masega.
Kuna takribani aina tofauti elfu ishirini(20,000) Duniani.Nyuki hawa wanatofautiana kwa maumbile,ukubwa na tabia,lakini wote wanashahabiana kwa tabia moja ya kutembelea maua ili kukusanya mbochi(maji matamu yanayotengeneza asali) na chavua(unga unaopatikana kwenye maua) kwa ajili ya chakula chao.
Kuna jamii kuu mbili za Nyuki wanaopatikana Tanzania;Nyuki wanaouma na wasiouma.
NYUKI WANAOUMA
Nyuki wanaouma wanaopatikana Tanzania wamegawanyika katika makundi matatu kutegemea mahali wanapoishi.Wapo nyuki wanaoishi;
Sehemu za Mwambao(Pwani) wana umbo dogo na niwakali(Apis mellifera litorea),sehemu kame na tambarare,wana umbo la wastani,wakali kiasi na hutoa asali kwa wingi(Apis mellifera scutellata),sehemu za milimani,(zaidi ya futi 6,000 kutoka usawa wa Bahari) wana umbo kubwa na wapole,jina la kitaalamu wanaitwa Apis mellifera monticola.
NYUKI WASIOUMA
Nyuki wasiouma wanapatikana nchi za tropiki tu kama ilivyo Tanzania.
Nyuki wasiouma wanaishi ndani ya matundu ya miti,chini ya matawi makubwa ya miti,kwenye vichuguu vya mchwa na hata chini ya mapaa ya nyumba,nyuki hawa hu toa asali kidogo kulinganisha na nyuki wanaouma,Nyuki wasiouma wanaweza kutoa hadi lita 5 za asali kwa mwaka kutegemea na ukubwa wa mzinga,aina ,wingi wa nyuki na uwepo wa chakula(maua) cha kutosha.Asali ya Nyuki wasiouma inaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu maradhi mablimbali kuliko asali ya Nyuki wanaouma.
JINSIA YA NYUKI NA MAJUKUMU YAO.
Kama ilivyo kwa viumbe vyote,nyuki nao waa jinsia mbili,nyuki dume na Nyuki Jike.Jinsia hizo ndiyo msingi wa mgawanyo wa majukumu ya kazi katika kundi la Nyuki.
Kundi la Nyuki wanaouma,lina aina tatu za Nyuki ambao ni Nyuki vibarua,malkia na dume.
NYUKI JIKE.
Jinsia hii inamakundi mawili ya nyuki amabyo hutekeleza majukumu mawili tofauti.
a)Nyuki Malkia
Ni nyuki jike ambaye hulelewa kwa kula chakula rasmi(maziwa ya Nyuki) na kupata matunzo maalumu kwa maisha yake yote(tangu hatua ya yai hadi uzee wake wote)Chakula hiki humwezesha kuishi kati ya miaka miwili hadi sita.
Nyuki malkia ni mkubwa kuliko nyuki wengine katika kundi la Nyuki,tumbo lake ni refu lenye rangi ya njano na dhahabu ghafi.
Nyuki Malikia,hutoa kemikali(Pheremones)mwilini mwake kutoa miongozo kwa kundi la Nyuki.Mpangilioo wote na Mgawanyo wa kazi katika kundi la nyuki hutegemea maelekezo yake.Kundi la Nyuki lisilo na Malkia hukosa mwelekeo na huishi kwa kipindi kifupi.
b)Nyuki Vibarua
Nyuki vibarua ni majike ambao maumbile yao hayana uwezo wa kutaga mayai wala kujamiiana na nyuki madume.Kwa kawaida nyuki vibarua ambao hawatagi mayai,ni majike tasaambao hawana uwezo wa wa kutaga mayai.Aidha,hufikia kuishi hadi siku 36.Wanaweza kufikia idadi ya 60,000 au zaidi katika kundi moja.
c)Nyuki dume
Hutokana na mayai ya Malikia yasiyorutubishwa na mbegu za kiumena kuwafanya nyuki hao kuwa na mzazi mmoja tu yaani mama,Nyuki dume ni wakubwa kuliko vibarua lakini wadogo kuliko Malkia.Macho yao ni makubwa na miili yao ina rangi nyeusi,nyuki dume hawana mshale wa sumu kwa ajili ya kujilinda dhidi ya maadui,badala yake wana uume.
Kazi kubwa ya Nyuki dume ni kujamiiana na malkia.Dume mmoja huweza kujamiiana na malikia mara moja katika maisha yake.,Baada ya Tendo la kujamiiana Dume hufa saa chache kutokan na uume wake kukatika wakati wa kujamiiana.
Kwa hali hii hata Nyuki vibarua hawajawai kuwaona baba zao.!
Kazi ya pili ya Nyuki madume ni kurekebisha hali ya hewa ndani ya mzinga kwa kupasha joto kiota hasa wakati wa Usiku kwa kukumbatia juu ya kiota,sehemu ya watoto.Wakati wa upungufu mkubwa wa chakula au kiangazi nyuki madume hutolewa na vibarua nje ya mizinga na baadea hufa kwa njaa au baridi.
Napokea marekebisho!