Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Defiant Gaddafi vows to fight on

In televised speech, Libyan leader blames youths inspired by regional events for uprising and vows to die a 'martyr'. ( 23-Feb-2011 )

SWALI HUMU: UTAMADUNI WA KURITHISHA WATOTO WA WAKUBWA
UKUBWA TANZANIA CHANZO CHAKE NI WAPI???

Nani anayejua hasa darasa la huyu King of Kings?

Kwa mtaji wa hutuba aliyoitao hivi majuzi ni mara mia angjinyamazia tu hivyo tungeendelea kumfikiria mstaarabu fulani hivi. Kwa kujiunga kwake jeshini akiwa na umri wa miaka 12 (child soldier) wala hatuhitaji kuuliza kama 'ALIONEWA SANA YEYE', 'AKADHALILISHWA SANA GADDAFI' hivyo kuja kupata kamwanya wa kuongoza nchi kwa mtindo wake mwenyewe hivi sasa anarudishia ngumi kwa jamii nzima ya Libya.

Tujifunze kitu basi na sisi hapa kwamba wale tuliowahi kuwaondoa kwenye nyadhifa fulani hapa nyumbani kufuatia kashfa iliyogoma kwisha katikati yetu hadi leo, nao wakija tu kupata urais wa nchi hii mtindo wao wenyewe na tusifikirie matendo yao kutofautiana sana na ya huyu nduli hapa.

Hakika shule iliomuingia mtu na kutulia ndani mwake ni muhimu zaidi tena sana kuliko shule ya kupitia hata kama madarasa yako ni mengi kimahesabu vidoleni.

Kanali Gaddafi ajikaanga kwa ulimi wake mwenyewe. Na watoto wake , masikini ya Mungu, ndio kabisaa wanaamini taifa zima la Libya ni kama shamba binafsi la ukoo kwa baba yao.

Nikitazama ya Ben Ali wa Tunisia, nikamgeukia Hosni Mubarak wa Misri na kumtaza mzee huyu ambaye kimawazo ni 'chipukizi' tu, na mwenendo mzima wa ushiriki wa familia zao katika mambo ya utawala wa nchi, Wa-Tanzania wenzangu NAPATA MAJIBU KUBWA SANA HAPA HAPA NYUMBANI kwamba ni kwa nini kati ya marais wetu wote wanne ni wawili tu kati yao ambao waonekana kupenda saana KUWARITHISHA UKUBWA WA TAIFA HILI kimtindo!!

Endapo Hussein Mwinyi hatojiuzulu ya Gongolamboto kwa kiburi tu kama ya watoto wa marais niliotangulia kuwataja kaskazini mwa bara hili basi huenda hata UKUBWA WA ZANZIBAR unaotazamiwa kwake ukagoma lakini ya Muungano ndio kabisaaaa wa kusikia tu redioni.

Katika hili tayari Vijana wa Tanzania TUMEWASOMA MCHEZO MZIMA na majibu tunayo!!!​
 
Nimesikitishwa na hoja mfu ambayo mtu aliyeanzisha mada hii ametoa. Kusema Nyerere hakufanya mambo ya maana katika nchi yetu ni matusi kwa wale ambao wanaelewa nchi yetu ilikuwa wapi na nini kilisababisha uchumi wetu kudorora mwaka 1979-hadi miaka ya tisini. Niliona upungufu mkubwa wa uelewa wa historia ya nchi yetu pale tulipokuwa tukijadili uamuzi wa Mwalimu kuitambua Biafra na kwa kweli wale ambao wanapima maendeleo kwa wingi wa vitu ambavyo wachache wanavyo na si jinsi ambavyo wengi wanavyo.

Je, ni nani asiyefahamu kuwa hadi mwaka 1978 nchi yetu ilikuwa na uchumi mzuri sana hadi IMF walidai kuwa Tanzania lazima itumie akiba yake ya nje na ibakie isiyozidi miezi sita hapo mwaka 1977? Najua mbumbumbu wanaotoa hoja mfu humu ndani watakuwa hawajui hilo. Je, ni nani asiyejua kuwa nchi yetu ililazimika kutumia dola milioni moja kila siku katika vita ya Uganda na kuwa vita hiyo ndiyo iliyofilisi nchi yetu? Mbumbumbu wa historia na uchumi watang'aka kama watu waliofumwa ugoni? Je, ni nani asiyejua kuwa mnamo mwaka 1979-80 bei ya mafuta ilipanda sana duniani na nchi yetu ambayo tayari ilikuwa imefilisika kwa vita haikuwa na fedha za kuweza kuendesha uchumi wake? Mazezeta wa historia na uchumi hilo halipo vichwani mwao kwani hawajui na wala hawajawahi kujishughulisha kujua hilo?
Je, ni nani asiyejua mataifa yanayotoka katika vita na ambayo uchumi wake umeyumbishwa navyo yanahitaji msaada/mikopo kutegemeza chumi zao? Watoa majibu ya kijiweni hawajui hilo kwani hawajawahi kujiuliza kuwa historia ya dunia imeonyesha hivyo kwani hata mataifa ya Ulaya yalipata msaada huo kutoka kwa Marekani katika Mpango wa Marshal. Na suala la mgawo na foleni za chakula na bidhaa baada ya vita je wamewahi kujiuliza kuwa Waingereza walikaa katika mgawo kwa miaka saba na siku waliporuhusiwa kula mayai mawili ni siku ambapo Malkia Elizabeth alisimikwa?

Ninaweza kuendelea kuuliza maswali mengi cha muhimu ni kusema kuwa Mwalimu alikuwa na makosa aliyoyafanya lakini huwezi ukaniambia kuwa eti aliporomosha uchumi kwa siasa za Ujamaa bali kukataa kwake masharti ya kijinga ya IMF na Benki ya Dunia yaliyodai eti serikali yake ilikuwa imeshindwa kuendesha uchumi vizuri ni uongo mtupu. Nilikuwepo wakati ule na nilipanga foleni ya sukari, sabuni na vitu vingine na kwa kweli kama kuna wakati serikali iliwahi kutoa sababu za ukweli kuhusiana hali ya uchumi ni wakati ule. Kama mtu aliyepata nafasi ya kusoma si tu sheria bali uchumi na siasa za taasisi za kimataifa za pesa ninathibitisha kuwa hali mbaya ya uchumi ilichangiwa kwa sehemu kubwa na sababu za nje na si za ndani. Kwa bahati mbaya watu wenye kupenda majibu mepesi na kwa kweli ya kijiweni ndio wako mstari wa mbele kupotosha ukweli na kutaka kutufanya kuwa sisi tu mazezeta wasio na uwezo wa kuchambua mambo. Chuki zao kwa Mwalimu kwa kweli huwezi ukazieleza vizuri kwani mtu ambaye alidiriki hata kutaifisha taasisi za kidini na kuzifanya za watu wote hivi sasa anaonekana kuwa alikuwa na ajenda ya kupendelea watu wa madhehebu fulani? Hivi hii kweli inaingia akilini?

Ninamalizia kusema kuwa maamuzi ya Mwalimu mengi yalilenga ustawi wa watu na si wa kutaka kujinufaisha na kama alikuwa mtu aliyependa watu wasisome je si huyu aliyetaifisha shule ili watu wa dini na makabila yote wasome? Je si huyu aliyeanzisha elimu ya watu wazima na kusababisha kiwango cha kujua kusoma na kuandika kupanda na kuwa asilimia 95? Si huyu aliyejenga miundo mbinu kama Tazara na viwanda vingi ambavyo mafisadi wamevigawa bure? Si huyu aliyeweza kushinda mbinu za benki za nje kuua NBC pale ilipotaifishwa? Si huyu ambaye hakutumia madaraka yake ya uraisi kujitarisha na hata watoto wake hali zake ni zinakaribia za Watanzania wengine.

Inanisikitisha sana kuona haya yote lakini watu wenye ajenda ovu ndivyo walivyo na hawatachoka kupotosha historia ili nia zao ovu zifanikiwe. Napenda kusema kuwa watashindwa kwani wale wenye uelewa mzuri wa mambo tutasimama imara kupangua hoja zao mfu.

Thanks Rugemeleza!!
Unajua kwa sisi tulioishi na kusoma enzi za mwalimu, maelezo yako yanaweza kututoa machozi na hapa nilipo nina hasira wala sijui nifanyeje! yaani kuna watu wanadiriki kumdhihaki Mwalimu Nyerere? anyway hata Jesus alisalitiwa sembuse Nyerere acha tu watukane. kuna watu wa ajabu nchi hii sijapata kuona. Mimi ndiyo maana kila siku nasema Dr. Slaa awe mwangalifu sasa hivi kila mtu anavyo mchekea wacha siku aingie Ikulu atalijua jiji maana wakati mwili wa Mwl. Nyerere umerudishwa nchini almost kila mtanzania alilia labda huyu jamaa alikua ananyonya kwani kama alikuwa na akili zake na bado anaandika huu upuuzi na cha ajabu ana pata support toka kwa baadhi JF members. TZ we still have a very long way to go!!
 
Ametunyima elimu. Ana dhambi kubwa sana huyu mzee. Na ndio maana mpaka leo Mitanzania inaongoza duniani kwa ujinga
Kufikia Mwaka 1985 wakati Nyerere anaondoka madarakani; Tanzania literacy rate yake ilikuwa zaidi ya 90%. Na Elimu ilitolewa kwa rika zote tena Bure!!!!!. Kulikuwa na Elimu ya Watu wazima nk. Leo hii takribani miaka 26 baada ya kuondoka madarakani na Miaka 11 baada ya kifo chake niambie literacy kwa sasa ni 72%; Mwaka 1992 kwa watu wa umri zaidi ya miaka 13 ilikuwa 84% ; Tena baada ya kufukua Madini aliyowachia na kuuza mashirika na kila kitu alichowaachia. Pia baada ya Kukaribisha wanaoitwa wawekezaji. Sasa unalalama nini?
http://www.dailynews.co.tz/home/?n=14831&cat=home
 
Nimesikitishwa na hoja mfu ambayo mtu aliyeanzisha mada hii ametoa. Kusema Nyerere hakufanya mambo ya maana katika nchi yetu ni matusi kwa wale ambao wanaelewa nchi yetu ilikuwa wapi na nini kilisababisha uchumi wetu kudorora mwaka 1979-hadi miaka ya tisini. Niliona upungufu mkubwa wa uelewa wa historia ya nchi yetu pale tulipokuwa tukijadili uamuzi wa Mwalimu kuitambua Biafra na kwa kweli wale ambao wanapima maendeleo kwa wingi wa vitu ambavyo wachache wanavyo na si jinsi ambavyo wengi wanavyo.

Je, ni nani asiyefahamu kuwa hadi mwaka 1978 nchi yetu ilikuwa na uchumi mzuri sana hadi IMF walidai kuwa Tanzania lazima itumie akiba yake ya nje na ibakie isiyozidi miezi sita hapo mwaka 1977? Najua mbumbumbu wanaotoa hoja mfu humu ndani watakuwa hawajui hilo. Je, ni nani asiyejua kuwa nchi yetu ililazimika kutumia dola milioni moja kila siku katika vita ya Uganda na kuwa vita hiyo ndiyo iliyofilisi nchi yetu? Mbumbumbu wa historia na uchumi watang'aka kama watu waliofumwa ugoni? Je, ni nani asiyejua kuwa mnamo mwaka 1979-80 bei ya mafuta ilipanda sana duniani na nchi yetu ambayo tayari ilikuwa imefilisika kwa vita haikuwa na fedha za kuweza kuendesha uchumi wake? Mazezeta wa historia na uchumi hilo halipo vichwani mwao kwani hawajui na wala hawajawahi kujishughulisha kujua hilo?
Je, ni nani asiyejua mataifa yanayotoka katika vita na ambayo uchumi wake umeyumbishwa navyo yanahitaji msaada/mikopo kutegemeza chumi zao? Watoa majibu ya kijiweni hawajui hilo kwani hawajawahi kujiuliza kuwa historia ya dunia imeonyesha hivyo kwani hata mataifa ya Ulaya yalipata msaada huo kutoka kwa Marekani katika Mpango wa Marshal. Na suala la mgawo na foleni za chakula na bidhaa baada ya vita je wamewahi kujiuliza kuwa Waingereza walikaa katika mgawo kwa miaka saba na siku waliporuhusiwa kula mayai mawili ni siku ambapo Malkia Elizabeth alisimikwa?

Ninaweza kuendelea kuuliza maswali mengi cha muhimu ni kusema kuwa Mwalimu alikuwa na makosa aliyoyafanya lakini huwezi ukaniambia kuwa eti aliporomosha uchumi kwa siasa za Ujamaa bali kukataa kwake masharti ya kijinga ya IMF na Benki ya Dunia yaliyodai eti serikali yake ilikuwa imeshindwa kuendesha uchumi vizuri ni uongo mtupu. Nilikuwepo wakati ule na nilipanga foleni ya sukari, sabuni na vitu vingine na kwa kweli kama kuna wakati serikali iliwahi kutoa sababu za ukweli kuhusiana hali ya uchumi ni wakati ule. Kama mtu aliyepata nafasi ya kusoma si tu sheria bali uchumi na siasa za taasisi za kimataifa za pesa ninathibitisha kuwa hali mbaya ya uchumi ilichangiwa kwa sehemu kubwa na sababu za nje na si za ndani. Kwa bahati mbaya watu wenye kupenda majibu mepesi na kwa kweli ya kijiweni ndio wako mstari wa mbele kupotosha ukweli na kutaka kutufanya kuwa sisi tu mazezeta wasio na uwezo wa kuchambua mambo. Chuki zao kwa Mwalimu kwa kweli huwezi ukazieleza vizuri kwani mtu ambaye alidiriki hata kutaifisha taasisi za kidini na kuzifanya za watu wote hivi sasa anaonekana kuwa alikuwa na ajenda ya kupendelea watu wa madhehebu fulani? Hivi hii kweli inaingia akilini?

Ninamalizia kusema kuwa maamuzi ya Mwalimu mengi yalilenga ustawi wa watu na si wa kutaka kujinufaisha na kama alikuwa mtu aliyependa watu wasisome je si huyu aliyetaifisha shule ili watu wa dini na makabila yote wasome? Je si huyu aliyeanzisha elimu ya watu wazima na kusababisha kiwango cha kujua kusoma na kuandika kupanda na kuwa asilimia 95? Si huyu aliyejenga miundo mbinu kama Tazara na viwanda vingi ambavyo mafisadi wamevigawa bure? Si huyu aliyeweza kushinda mbinu za benki za nje kuua NBC pale ilipotaifishwa? Si huyu ambaye hakutumia madaraka yake ya uraisi kujitarisha na hata watoto wake hali zake ni zinakaribia za Watanzania wengine.

Inanisikitisha sana kuona haya yote lakini watu wenye ajenda ovu ndivyo walivyo na hawatachoka kupotosha historia ili nia zao ovu zifanikiwe. Napenda kusema kuwa watashindwa kwani wale wenye uelewa mzuri wa mambo tutasimama imara kupangua hoja zao mfu.

Rugemaliza umeongea mengi sana. Kwa Nyerere kufanya yote hayo haimuondolei udikteta wake na ubaya wake. Hata Adolf Hitler dikteta wa Ujerumani alipenda sana wananchi wake. Nenda Leo Ujerumani, barabara zote kubwa na imara katika miji ya Cologne, Berlin nk ambazo leo zinasifika kama barabara bora kabisa duniani zilijengwa na Hitler.

Wana historia watakubaliana na mimi kuwa Adolf Hitler alikuwa na machungu makubwa kila alipoona Mdachi masikini. Baada ya kubaini kuwa wadachi ni masikini na utajiri mwingi wa Ujerumani upo mikononi mwa waserbia na wayahudi ndipo alipoanza sera za kutaifisha mali zao na kuwakabidhi wajerumani. Pamoja na mapenzi hayo kwa watu wake bado haimuondolei udikteta.

Nyerere ni dikteta, tupende tusipende. Na kwa wale wanaomchukulia kama ni SI UNIT wanakosea(kwa maoni yangu).

Nilipoweka rangi nyekundu nimepapenda sana. Uchumi wa Tanzania ni kweli uliporomoka baada ya vita ya Kagera. Kwanza vita ya Kagera ilikuwa haituhusu sisi. Ni vita vya kujitakia. Nyerere aliingiza nchi vitani kwa lengo la kumsaidia dikteta mwenzake Milton Obote baada ya kupinduliwa na Idd Amini Dada. Ingawa alifanikiwa kumrudisha madarakani alipinduliwa tena na Museveni. Kwa msingi huo, ni Nyerere aliyeporomosha uchumi wetu kwa kujiingiza ktk mambo ya ndani ya nchi huru.

Nyerere hakung'atuka kwa mapenzi yake. Ni baada ya kuona mambo yanenda mrama na wananchi wanaishi maisha duni vibaya. Nakumbuka mwaka 1983, tukiwa RUA JKT mkoani Rukwa, nilishuhudia watu wakiwa wamevaa mifuko ya mbolea(ambayo sasa tunawekea unga). Kipindi hicho mtu kuwa na chumvi na anasa.

Ni Nyerere aliyejaza ndugu zake ikulu. Mfano wao ni Joseph Butiku na Joseph Warioba. Ni yeye aliyewapa vyeo vikubwa ndugu zake mfano ni General Msuguri.

All in All, anayemsifu Dikteta Nyerere inawezekana anamjua upande mmoja tu. Upande wa pili hamjui.
 
Kwa kila mwanasiasa wa Tanzania anaetaka kuungwa mkono na wananchi wengi amekuwa akijitahidi kujionesha kuwa ni mfuasi wa Rais wa kwanza wa Tzania Mwl Nyerere. Anasifiwa kwa kila kitu lakini kwangu mimi simkubali kabisa Mwl Nyerere. Siamini kama alikuwa na kipaji cha uongozi. Alikuwa ni dikteta. Alifinya uhuru wa habari, aliwafunga wapinzani wake, alileta umasikini mkubwa kwa taifa na wananchi wa Tzania. Si kwamba alikuwa anapendwa bali alikuwa anaongoza wananchi wengi wasiojua dunia inakwendaje"wajinga".

Huyo ndio Nyerere. Kwa miwani yangu namuona kuwa ana mabaya mengi kuliko mazuri kama tunavyolazimishwa kuamini. Kutojilimbikizia mali au kutoa huduma za jamii bure si kigezo cha kutokuwa dikteta maana hata Pinnochet, Hitler na Mussolin walikuwa wanatoa huduma za jamii bora na bure kabisa kwa watu wao.

Uzuri wa hapa JF ni kuwa kila mtu yuko entitled to their opinion...mwanzisha thread hii included. Safi sana!

Ila mi mwenzenu jamani....natamani kweli Mwl angekuwa hai leo hii ili huyu Mwarabu wa Dowans ashikishwe adabu na atambue kuwa TZ ni sovereign state na si duka la groceries la Rostam!!
 
Rugemaliza umeongea mengi sana. Kwa Nyerere kufanya yote hayo haimuondolei udikteta wake na ubaya wake. Hata Adolf Hitler dikteta wa Ujerumani alipenda sana wananchi wake. Nenda Leo Ujerumani, barabara zote kubwa na imara katika miji ya Cologne, Berlin nk ambazo leo zinasifika kama barabara bora kabisa duniani zilijengwa na Hitler.

Wana historia watakubaliana na mimi kuwa Adolf Hitler alikuwa na machungu makubwa kila alipoona Mdachi masikini. Baada ya kubaini kuwa wadachi ni masikini na utajiri mwingi wa Ujerumani upo mikononi mwa waserbia na wayahudi ndipo alipoanza sera za kutaifisha mali zao na kuwakabidhi wajerumani. Pamoja na mapenzi hayo kwa watu wake bado haimuondolei udikteta.

Nyerere ni dikteta, tupende tusipende. Na kwa wale wanaomchukulia kama ni SI UNIT wanakosea(kwa maoni yangu).

Nilipoweka rangi nyekundu nimepapenda sana. Uchumi wa Tanzania ni kweli uliporomoka baada ya vita ya Kagera. Kwanza vita ya Kagera ilikuwa haituhusu sisi. Ni vita vya kujitakia. Nyerere aliingiza nchi vitani kwa lengo la kumsaidia dikteta mwenzake Milton Obote baada ya kupinduliwa na Idd Amini Dada. Ingawa alifanikiwa kumrudisha madarakani alipinduliwa tena na Museveni. Kwa msingi huo, ni Nyerere aliyeporomosha uchumi wetu kwa kujiingiza ktk mambo ya ndani ya nchi huru.

Nyerere hakung'atuka kwa mapenzi yake. Ni baada ya kuona mambo yanenda mrama na wananchi wanaishi maisha duni vibaya. Nakumbuka mwaka 1983, tukiwa RUA JKT mkoani Rukwa, nilishuhudia watu wakiwa wamevaa mifuko ya mbolea(ambayo sasa tunawekea unga). Kipindi hicho mtu kuwa na chumvi na anasa.

Ni Nyerere aliyejaza ndugu zake ikulu. Mfano wao ni Joseph Butiku na Joseph Warioba. Ni yeye aliyewapa vyeo vikubwa ndugu zake mfano ni General Msuguri.

All in All, anayemsifu Dikteta Nyerere inawezekana anamjua upande mmoja tu. Upande wa pili hamjui.

Ni vigumu kuzungumza na mtu aliye na ajenda ya siri. Hivi ni kweli unaamini kuwa vita ya Uganda ilikuwa ya kujitakia? Je, ni Tanzania iliyovamia Uganda mnamno tarehe 27 Oktoba, 1978? Je, Tanzania baada ya kuvamiwa ilitakiwa ifumbate mikono na kusema hewala kwa Amini? Bila hata aibu unamlinganisha Nyerere na Hitler? Je, Nyerere aliua watu milioni sita Ujerumani na kusabaisha mauaji ya Warusi Milioni 27 na wazungu wengine zaidi ya milioni 10? Kutokana na mfano huo nadhani siwezi kujadiliana nawe kwani uelewa wako wa historia na ukweli haupo. Kwa imani yoyote ile ninakuomba utubu kwani umejichumia dhambi kutokana na si tu kwa kusema uongo bali kupotosha ukweli na kuwalaghai wengi.
 
Mkuu mbona unajichanganya na hizo data zako? unasema mwaka 1978 uchumi wetu ulikuwa mzuri sana hadi IMF walidai kuwa lazima itumie akiba yake yake ya nje ibakie isiozidi miezi sita hapo mwaka 1977, hapa kuna vitu viwili umechanganya miaka na umechukuwa data za IMF kama ushahidi, hapo hapo utaki tena kuzitumia data za IMF baada ya kumwambia serikali yake imeshindwa kuendesha uchumi unasema ni uongo mtupu, kuhusu vita Tanzania wamepewa misaada mingi tu kutoka China, Ujerumani,Uingereza,Malawi,Kenya,nchi za Scandnavia nazo zilitoa msaada wakati wa vita na Uganda, hivo vita vyenyewe vilichukuwa miezi minane tena vita kamili vya kupigana na vya miezi mitatu, ndio Tanzania tukafirisika?
Nadhani huelewi nilichokisema na unataka kusema nilijichanganya. Nitajbiu hoja zao baadae kidogo kwani nina shughuli hapa Chuoni.
 
Mitanzania ikiwemo na wewe!

TZ during Mwalimu's era was 2nd to Cuba when it came to literate rates. Hiyo ilianza kuanguka wakati wa Mwinyi,then Mkapa kisha mkwere ndo amefanya wewe na hao unaowaita mitanzania,muwe wajinga!

You are right again. By 1986 Tanzania ilikuwa inafuata kwa CUba katika Literacy rate. Leo hata Kenya imetupita?????????? Aibu!!!!! eti watu wazima na akili zao wanaona leo maisha ni Bora kuliko wakati wa Mwalimu!!!!!!!!!!Ona List of countries by literacy rate - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Rugemaliza umeongea mengi sana. Kwa Nyerere kufanya yote hayo haimuondolei udikteta wake na ubaya wake. Hata Adolf Hitler dikteta wa Ujerumani alipenda sana wananchi wake. Nenda Leo Ujerumani, barabara zote kubwa na imara katika miji ya Cologne, Berlin nk ambazo leo zinasifika kama barabara bora kabisa duniani zilijengwa na Hitler.

Wana historia watakubaliana na mimi kuwa Adolf Hitler alikuwa na machungu makubwa kila alipoona Mdachi masikini. Baada ya kubaini kuwa wadachi ni masikini na utajiri mwingi wa Ujerumani upo mikononi mwa waserbia na wayahudi ndipo alipoanza sera za kutaifisha mali zao na kuwakabidhi wajerumani. Pamoja na mapenzi hayo kwa watu wake bado haimuondolei udikteta.

Nyerere ni dikteta, tupende tusipende. Na kwa wale wanaomchukulia kama ni SI UNIT wanakosea(kwa maoni yangu).

Nilipoweka rangi nyekundu nimepapenda sana. Uchumi wa Tanzania ni kweli uliporomoka baada ya vita ya Kagera. Kwanza vita ya Kagera ilikuwa haituhusu sisi. Ni vita vya kujitakia. Nyerere aliingiza nchi vitani kwa lengo la kumsaidia dikteta mwenzake Milton Obote baada ya kupinduliwa na Idd Amini Dada. Ingawa alifanikiwa kumrudisha madarakani alipinduliwa tena na Museveni. Kwa msingi huo, ni Nyerere aliyeporomosha uchumi wetu kwa kujiingiza ktk mambo ya ndani ya nchi huru.

Nyerere hakung'atuka kwa mapenzi yake. Ni baada ya kuona mambo yanenda mrama na wananchi wanaishi maisha duni vibaya. Nakumbuka mwaka 1983, tukiwa RUA JKT mkoani Rukwa, nilishuhudia watu wakiwa wamevaa mifuko ya mbolea(ambayo sasa tunawekea unga). Kipindi hicho mtu kuwa na chumvi na anasa.

Ni Nyerere aliyejaza ndugu zake ikulu. Mfano wao ni Joseph Butiku na Joseph Warioba. Ni yeye aliyewapa vyeo vikubwa ndugu zake mfano ni General Msuguri.

All in All, anayemsifu Dikteta Nyerere inawezekana anamjua upande mmoja tu. Upande wa pili hamjui.

Anayemuita Nyerere Dictator ni Hao kundi la Mafisadi ambao Nyerere hakuwaonea aibu. Ni haki yao walie. Lakini fahamu kuwa ipo siku tutawatoa mkuku. Tunasema siku zenu zinahesabika. Tumechoka kuibiwa na Kudhulumiwa raslimali za Taifa. Tunahitaji Kiongozi wa aina na aiba ya Nyerere asiyewaonea aibu mafisadi na vibaraka wao. Hao makuadi wenu na mabwana zao watakiona cha Moto. Nashukuru kuwa sasa mnaaza kujipambanua maana watu aina ya Nyerere mnafahamu hawapo tena. Mmehodhi madaraka ya Umma na kutumia mwanya huo kujilimbikizia mali. Make mkijua tumeishawashutukia na tuko tayari kupambana nanyi. Aluta continua.
 
Ni vigumu kuzungumza na mtu aliye na ajenda ya siri. Hivi ni kweli unaamini kuwa vita ya Uganda ilikuwa ya kujitakia? Je, ni Tanzania iliyovamia Uganda mnamno tarehe 27 Oktoba, 1978? Je, Tanzania baada ya kuvamiwa ilitakiwa ifumbate mikono na kusema hewala kwa Amini? Bila hata aibu unamlinganisha Nyerere na Hitler? Je, Nyerere aliua watu milioni sita Ujerumani na kusabaisha mauaji ya Warusi Milioni 27 na wazungu wengine zaidi ya milioni 10? Kutokana na mfano huo nadhani siwezi kujadiliana nawe kwani uelewa wako wa historia na ukweli haupo. Kwa imani yoyote ile ninakuomba utubu kwani umejichumia dhambi kutokana na si tu kwa kusema uongo bali kupotosha ukweli na kuwalaghai wengi.

Vita ya Uganda ilikuwa ya kujitakia, tatizo ni kwamba umesikiliza sana propaganda za vyombo vya habari vya Tzania ambavyo kwa namna yoyote ile visingeweza kusema ukweli.

Unaweza kujiuliza maswali machache sana. Ni kwa nini Amini aliivamia Tanzania miaka 6 mbele baada ya kumpindua Obote? Ni kwa nini Iddi Amini alipewa uenyekiti wa OAU trh 28.7.1975 na hakuna karipio lolote alilopewa na OAU?
 
Ni kweli nyerere hakupigania uhuru bali alipewa tuu. Hata babaako kama angekuwa mstari wa mbele ktk chama angepewa huo uhuru. Kumbukeni kuwa kipindi hicho tulikuwa chini ya himaya ya waingereza baada ya mjerumani kushindwa ww2. Mkumbuke pia kuwa alikwenda UNO kwenye mkutano miaka ya 1958 akisindikizwa na baadhi ya wahindi (waliosponsor safari yake huko) . Maadhimio ya mkutano huo yalikuwa kwamba watanganyika wasubiri kidogo hadi 1961 ndo watapewa huo uhuru wanaodai. Kwa wale mtakaokumbuka, nyerere alipokuwa anarejea toka yuno akiwa eapot alikuwa ameshikilia bango lenye ujumbe wa kuwa "uhuru 1961'. Kwa hiyo ni kweli kabisa nyerere hakupigania uhuru. Kumbukeni kuwa wakati wa mkoloni kulikuwa na matabaka yaani wazungu(tabaka la juu) waasia(kati) na weusi(chini).

Yaani hapa ndio tuna tatizo mnageuza kabisa historia ili kujenga hoja inayofuata hapa chini na mnataka tukubali kuwa ndivyo uhuru ulivyopatikana. Kwanini Nyerere aliacha kufundisha Pugu? Alipokuwa Makerere alikuwa kiongozi wa nini na kwanini? Unayajua maandishi ya Mwalimu alipokuwa Uingereza masomoni na ni kitu gani alikuwa anakifanya au unataka tuamini tu alikuja akakaa na wahindi (wanaojua sana kulobby) na wakasema nenda kachukue uhuru!?

Kwa maan hiyo
waasia(wahindi) walikuwa wanaloby namna ambavyo watakuwa tabaka la juu na ndio maana walishadadia sana na kusupport move yote ya kuomba uhuru. Mtakubaliana na mimi kwamba wahindi ni wataalamu wa lobying.mtakubaliana na mimi pia kuwa katika wageni wote waliokuwapo enzi za ukoloni, ni wahindi pekee ndo hawakufukuzwa na ndo hadi sasa wako wanamiliki biashara nyingi na kuishi katika maeneo prime ya miji yetu mikubwa. Watu kama akina mtikira ndo maana walikuwa wanamchukia sana nyerere kwa kuwabeba "magabachori'

Hatukubaliani na wewe! kwanza unapotosha hoja kuwa "wahindi pekee ndo hawakufukuzwa" nani alifukuzwa mgeni?

Kwa maana nyingine ni sawa na sasa ambapo matajiri (akina rostam na wengineo) wananyenyekewa kwa sababu ya kusupport chama. Hata enzi za mwalimu walikuwepo. Ninachoweza kusema ni kuwa Nyerere alikuwa na "stupidity innocense". Mkumbuke kuwa amepewa nchi akiwa a mere guy, hajui mambo ya uchumi,hana chochote yaani hakuwa na experience yoyote ya uongozi pamoja na kuwa kiongozi wa TAA na baadae Tanu.

yaani, hata huoni self-contradiction humo humo!! What is "mere guy"? Kwanini hawakumpata mtu mwingine ambaye alikuwa "a mere guy". Mnasema hakuwa anajua mambo ya uchumi - yaani mtu anashahada ya pili ya uchumi mnasema alikuwa hajuii mambo ya uchumi?

Ujinga na uppuuzi wake unakuja pale alipokuwa hataki ushauri toka kwa watu wataalamu kama akina mtei, kolimba nk. Mjue pia kuwa ndo maana uongozi wa Nyerere ulijaa viongozi ambao noi ma yes men/women. Yeyote aliyeonekana kuchallenge aliwekwa kizuizini au kupelekwa mbali mfano kuwa balozi.

Na hawa waliokubali ushauri wa mawaziri wao wa fedha (basil Mramba) na kina Mgonja na wengine "upuuzi wao na ujinga wao" uko wapi? Yaani, mnaamini kabisa kuwa kama Nyerere angekubali hoja zote za Mtei nchi isingekuwa hapa ilipo? Really? Mtei si yupo hai hadi leo hii kwanini serikali haijaa kumuuliza ushauri wake na tuone kama wataufanyia kazi? Mtei si ameandika mara kadhaa na kutoa ushauri hata hadharani amesikilizwa na nani?

Na kama wengine mnapotosha ukweli ati "yeyote aliyeonekana kumchallenge" aliwekwa kizuizini? Really? Embu tutajieni watu waliowekwa kizuizini kwa kumchallenge Nyererer. Na kupelekwa Ubalozini kuwa balozi ni adhabu? ! Hivi mnajua madikteta wa kweli hufanya nini na watu wanaowachallenge kiukweli - mnioneshe dikteta aliyempa mtu kazi ya kuwakilisha taifa lake nje baada ya kumpinga na mimi nikutaonesha waliowasindikiza makaburini waliowapinga!

Ukiangalia uchumi wa Tanganyika na baadae Tanzania utagundua kuwa wakoloni walituacha pazuri sana. Baada ya kupewa uhuru nyerere na wenzake walikuwa wakisherehekea tangu hiyo 61 hadi kuungana na zanzibar. Miaka yote hiyo no production at all. Kilichokuwa kinafanyika ni kuchukua kwenye hivyo viwanda. Kuja kutahamaki uchumi unaanza kuyumba na yeye kuja na arusha declaration(ujamaa na kujitegemea-african socialism) kama suluhisho la kurevive uchumi.

Yaani hadi najihisi mzee! ati Wakoloni walituachia uchumi mzuri? TAfuta takwimu za uchumi wetu kati ya miaka kumi baada ya uhuru (1961 -1971) na ulinganisha na miaka 50 kabla ya Uhuru! Halafu utuambie ni upi ulkuwa bora.

Lakini kwa sababu ya mipango mibovu inashindwa. Come 1972 anakuja na villagilization anahamisha watu mahali ambapo walizoea kulima( kwa maana wanajua majira ya mwaka, udongo nk) na kupelekwa sehemu ngeni.

Hapa ndio inaonekana watu hata hamjui historia yetu. Swali la kuuliza ni kwanini ulikuja mpango wa kutengeneza vijijini vipya na kuachana na vile vya asili? Leo hii kama nilivyosema hapo nyuma Tanzania imeundwa na vijiji vilivyoundwa wakati wa Nyerere na vichache ambavyo viliachwa. Ikumbukwe si vijiji vyote vilihamishwa kulikuwa na sababu za kiutawala, usalama na huduma ambazo ililazimisha kuleta watu karibu. Lakini vile vile watu wanachukulikia kirahisi rahisi tu kujenga taifa. Hivi, mnafikiri Marekani ya leo watu walijikuta tu wanahamia kwenye miji ya kisasa? Hivi mnafikiri China ya leo isingetengenezwa na kina Mao (kwa gharama kubwa sana) ingekuwa na nguvu tunayoiona nayo leo?

Kati ya vitu ambavyo historia itamhukumu Nyerere vizuri zaidi ni kuleta wananchi pamoja katika muundo wa vijiji vya kisasa. Tatizo kubwa ambalo leo tunajua vizuri kwanini ni kuwa hakukuwa na mfumo mzuri wa kusimamia na kama tatizo la watendaji wa leo ambao ni wasomi sana tunaliona katika mambo mbalimbali fikiria mwaka 1972 watendaji wetu walikuwa na elimu na uzoefu gani kukamilisha mradi ule mkubwa.

Matokeo yake watanzania wakawa stranded. Hawajui cha kufanya. Unapita msimu wa kwanza na wapili kwani hawajui ni zao gani walime na majira hawayajui. Baati mbaya ukame unaikumba nchi miaka ya 1975 na kuleta disaster ya njaa. Kumbuka kuwa tangu 1972 uzalishaji wa chakula unayumba kwa sababu ya vilagisation, ukame unaikumba nchi, matokeo yake ni njaa. Kama mnakumbuka enzi za unga wa Yanga kama msaada toka marekani. 1978 vita ya kagera ambayo inaigharimu tanzania mamilioni ya shilingi. Kwa hiyo tanzania ikawa haina pesa hata kidogo.

Tatizo unataka kukwepa historia; matatizo ya mwanzoni ya miaka ya sabini ilikuwa ni pamoja na kuyumba kwa uchumi wa dunia na vile vile bei ya mafuta kupanda sana mwaka 1970. Kama tunavyoona leo hii baada ya kuyumba uchumi wa dunia jinsi gani hata mataifa yaliyokuwa yako yamesimama yaliyoumba. Sisi tuliyumba kidogo lakini guess what? Nyerere hakuona aibu kuomba msaada wa chakula na baadaye kuhakikisha tunalima chakula cha kutosha sana. Hata leo hii miaka karibu 40 tangu wakati ule Tanzania bado inahangaika na tatizo la njaa! Kama tatizo lilikuwa Nyerere kwanini leo bado watawala wetu wameshindwa kulitatua tatizo hilo?

Kuna tetesi kuwa baada ya vita na I'd amin nyerere alitaka kung'atuka lakini intellijensia ikamshauri asubiri na akaamua kusogea hadi hiyo 1985. Alipong'atuka na kuwa nje ya uwanja ndo akaanza kuhisi madudu aliyofanya na kuwa kama mshauri wa serikali.

Haikuwa tetesi, Nyerere alitaka kustaafu mapema zaidi. Na siyo alitaka tu alishawahi kujiuzulu uongozi serikalini (na kumuachia Kawawa)! Lakini upotoshaji mwingine wa historia ni kudai kuwa ni baada ya "kuwa nje ya uwanja ndo akaanza kuhisi madudu". HIili nalo si kweli. Labda tafuta kijitabu kiitwacho "Tujisahihishe" utaona kuwa Nyerere alifanya kitu ambacho hakuna Rais mwingine wa Tanzania amewahi kukifanya nacho kujiangalia kiuongozi na kusahihisha makosa! Hakusubiri atoke madarakani kama Mwinyi, au Mkapa walivyofanya.

haya mengine ni recent histori nitawaachia wengine.

I stand to be corrected.

and corrected you are.
 
Vita ya Uganda ilikuwa ya kujitakia, tatizo ni kwamba umesikiliza sana propaganda za vyombo vya habari vya Tzania ambavyo kwa namna yoyote ile visingeweza kusema ukweli.

Unaweza kujiuliza maswali machache sana. Ni kwa nini Amini aliivamia Tanzania miaka 6 mbele baada ya kumpindua Obote? Ni kwa nini Iddi Amini alipewa uenyekiti wa OAU trh 28.7.1975 na hakuna karipio lolote alilopewa na OAU?

jamani.. si zipo video toka Uganda za wakati ule kwani ni siri?
 
mie wana jf nauliza tu kitu kimoja wamepita marais wnne tangu tupate uhuru(kwa tanzania bara) katika hawa wnne nani aneweza kuthubutu kusimama nakusema kwamba sikuibiia serekali, sijawai kufuja mali ya umma, na nililinda kwanza utaifa ubinafsi nyuma na ninai katika hwa marais wanne ni mzalendo? (and then we can start kumponda mwalimu).
 
Kutokana na uhuru wa kuongea tulionao na haki ya kusema jambo lolota ilimradi usivunje sheria basi kila mtu aseme awezavyo kusema mawazo yake na pia mawazo yake tunapaswa kuyaheshimu.
kwa upande wangu pamoja na mapungufu ya ki ubinadam aliyokuwa nayo kuna mazuri kafanya na mabaya pia yapo... hivyo tunapaswa kuiga mazuri na kuacha mabaya,, tatizo letu sisi watanzania mabaya hatuyataki hata mazuri pia hatuyataki.... nyerere alikuwa na sauti akisema kitu watu wanamsikiliza hata ndani ya chama chao akisema john malecela hugombei kweli hagombei,,, lakini leo nani anaweza kumwambia mwenzake usigombeee? maana huyo alieambiwa asigombee nae atahoji kwa nini nisigombee kama sababu ni ufusadi basi atasema mbona na wewe ni fisadi?
kwa mtazamo wangu nyerere ni jembe katika awamu zote nne,, wengine hawa ni wasanii tu:rain:
 
bradha umesoma vitabu vya nyerere? umesoma azimio la Arusha na kujua nyerere alikuwa na lengo gani kwa taifa? hutamkubali Nyerere mpaka utakapomkubali
 
I once said you have to be like 'crazy' to defend Nyerere in this world! tena mtapandwa na pressure is better to ignore maana Nyerere anabaki kama Nyerere.

Tatizo hapa si kuwa Nyerere alikosea au hakukosea ila alikuwa na malengo gani, ubaya na udikteta wa Nyerere unaonekana kwenye

1. Kuondoa vyama vingi
2. Kutoshaurika
3. Kunyima fursa kwa wapinzani wake
4. Kufanya chaguzi zisizozingatia haki na akili timamu!

However, justifiable reasons za why he did that is

1. He was eager to see Tanzania is developing within one year!
2. Hakuwa mroho wa madaraka na aliacha ngazi mapema..this is not easy
3.Hakuwa mroho wa mali, this confirms that he did what he did for good intention though he failed badly!

wengi watetezi wa Nyerere huwa hawana hoja za kumtetea Nyerere ila ni kulazimisha tu which is very wrong.

Nyerere anabaki kuwa kiongozi bora kabisa kupata kutokea kwa sababu alikuwa na malengo, mipango na visions, ali-fail kama mtu mwingine yeyote na VIONGOZI WALIOKUJA BAADAYE WALITAKIWA KUANZIA PALE GARI LA NYERERE LILIPOISHIA na sio kuwa kama sasa hivi.Rais JK leo hii hata kusoma kitabu page 2 tu hawezi! is he philosopher? hell no! Nyerere was and is philosophical ideas are still valid but only for sound minded people!
 
Ni kweli Nyerere alikuwa dikteta! Lakini alikuwa na dhamira ya ukweli kutuendeleza ni kweli dhana ya ujamaa na kujitegemea aliyoitegemea ilishindwa ktk ubebari! Lakini unaposema Nyerere hafai ww uliyemuona anayefaa baada ya Nyerere ni nani? Mwalimu alikuwa anamaanisha anachosema na ukimuona usoni unajua anamaanisha anachosema tatizo alikosea ku base kwenye ujamaa na hakujua kuwa ubepari ndo deal, licha ya hayo alituachia misingi mizuri pamoja na mapungufu yake na alisema "tumefanya mazuri mengi na mabaya pia, tatizo la viongozi wa sasa wanachukua mabaya wanaacha mazuri!" mwinyi, mkapa, mkwere hawatoshi kuwafananisha na Mwalimu hata kidogo wanajari maslahi yao binafsi kuliko ya wa tz kwa hilo Nyerere alikuwa excellent, ni ideology ya ujamaa iliyompoteza lakini angetokea mtu makini na kupokea kijiti kama china unadhani ingekuwaje? Hata kama watu waliumia in china na wanaendelea kuumia lakini angalia wanavyoendelea TAFAKARI kabla hujaanzisha thread, mkwere kakufanyia nini ndo la msingi hii miaka 10 anayopewa
 
Hayo yote wanayozungumza wanaompinga nyerere ndio hayo yanayozungumzwa misiktini,kwenye mihadhara ya dini ya kiislamu,kwenye magazeti kama alnuur na radio imani.Sasa wanaosema haya mambo yapuuzwe ndo wajue kuwa sumu zimewaingia waislamu wengi na wamezimeza bila hata kufikiri.

Mnapopita kwenye magazeti basi angalieni hata vichwa vya habari kwenye magazeti yao na mtaona hayo anayosema mtoa mada.Wamefikia hatua wanasema historia ya nchi ibadilishwe.
 
Back
Top Bottom