Waberoya:
Nashukuru kwa mchango wako mzuri. Nianze kwa kukiri kwamba ni kweli, makala yangu ilikuwa ndefu sana, kitu ambacho nilishaiombea msamaha hapo awali.
Baada ya kusema hayo, ningependa nianze kwa kukumbushia tu kwamba makala yangu haikuwa inalenga kumpigia Nyerere debe awe nominated kuwa BABA WA TAIFA; Makala yangu haifananii na hekaheka za kumpigia mtu debe ili apate heshima au cheo ambacho bado hana au bado hajatuzwa bado, mfano kama tunavyoona juhudi mbali mbali za makundi mbali mbali za kupigia debe watu fulani fulani kwamba ndio wanafaa kuwa wagombea wa nafasi ya uRais (CCM) uchaguzi wa mwaka 2015. Kama ulisoma kwa makini, makala yangu imezaliwa katika mazingira ambayo tayari kuna mtu anayetambulika kama BABA WA TAIFA, ambae ni Mwalimu Nyerere, heshima ambayo imeshakuwa conferred, at least customarily, na inatumika ndani ya chombo cha kutunga sheria BUNGE, katika mijadala mbali mbali, na na pia katika kutunga sheria nyingine mbalimbali za kuipa nguvu heshima hiyo kwa Mwalimu, mfano rejea hoja yangu juu ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ACT ya mwaka 2005. Kwahiyo naomba tuwe on par level hapa kwamba makala yangu haikuwa kampeni for Mwalimu apate heshima, bali, recognition on heshima iliyopo, na kwanini mimi binafsi naona alistahili, na kwanini bado anastahili heshima hiyo kwa vigezo nilivyovieleza.
Baadae nikashauri kwamba malumbano juu ya Heshima kwa Mwalimu, hayawe tupeleka popote zaidi ya kupotezeana muda katika mazingira haya magumu aambapo miaka 50 baada ya uhuru, mwanakijiji bado ana hali ileile ya zamani, if not worse. Tuna kazi muhimu zaidi ya kujenga taifa letu katika mazingira hayo hayo unayoyasema ya MODERNITY, na mjadala juu ya Nyerere na ubaba wa taifa, una manufaa pale tu kama tutakuwa tunalenga zaidi kuchota hekima yake iliyompelekea kupata heshima hiyo, ili tuitumie kujanga taifa hili. Nikatoa mawazo kwamba ni vyema zaidi tujitahidi kushirikiana na viongozi wetu wa sasa na wa baadae ili na sisi Tanzania tupate our Abraham Lincolns, Thomas Jeffersons, Joachim Chissanos, na hata ikiwezekana, Nobel Laureates na Good Governance Awards recipients (from Mohamed Ibrahim Foundation), na haijalishi kama viongozi hao watatokea CCM, CHADEMA, CUF, vyama vingine 14 vilivyopo, au hata Mgombea binafsi, kama katiba itaruhusu.
Kuhusu makosa ya Mwalimu Kiutendaji, nakubaliana na wewe, yapo mengi sana kwani it is obvious, just like in any newly independent country AT THAT PERIOD, Under Mwalimu, THERE WERE SOME THINGS THAT WENT RIGHT but also THERE WERE SOME THINGS THAT WENT WRONG. Lakini lazima tukubaliane kwamba katika nchi nyingine, hali zilikuwa mbaya sana, coups, vita vya wenyewe kwa wenyewe, wizi wa kupindukia wa mali za taifa na wanasiasa, political assassinations ambazo zina ushahidi wa wazi, mauaji ya halaiki kidini, kikabila, kwa makusudi kabisa, n.k.. Kwa Tanzania kwa kweli things were very calm in comparison. Otherwise, nimewahi kuyataja mapungufu ya Mwalimu from time to time, na nipo tayari kuendelea kuyajadili. Lakini as already mentioned, hiyo haikuwa focus ya makala yangu.
Baada ya kusema hayo yote, makosa ya kiongozi katika utendaji/sera, in my humble opinion, sio kigezo to disqualify heshima yake kama BABA WA TAIFA. Vinginevyo, I agree kuna mambo mengi hayakwenda sawa chini ya Mwalimu kiutendaji na kimtazamo, and I am ready to debate that lakini as long as lengo letu liwe to determine how we should move forward na kurekesbisha mambo kadhaa, hususan yale ndani ya Azimio la Arusha, pamoja na mawazo mengine mapya yenye lengo la kuwainua ndugu zetu milioni zaidi ya 30 huko vijijini. Otherwise kama focus ya mjadala juu ya Mwalimu itaishia kuwa nani kashinda au kushindwa kwa hoja, haitatujenga au kutusaidia kupelekea nchi yetu mbele, especially kupunguza umaskini vijijini na sehemu za mijini.
Kuhusu Nyerere kwamba hakuleta uhuru kwa sababu ambazo umeziweka bayana kama vile hoja yako kwamba tuliendeleza mfumo wa kigeni, utamaduni, lugha n.k, now this is where it gets very interesting. It can be a very stimulating debate intellectually, kwani kama unaleta hiyo variable kwenye equation ya uhuru kama moja ya disqualifications za ubaba wa taifa, ina maana hata kina Samora Machell ambae nchi yake lugha kuu ni Kireno, Kenyatta ambae taifa lake linatawaliwa na lugha ya Kiswahili na kiingereza, na wengine wengi, wote hawa kwa hoja yako UBABA WAO WA TAIFA ni wa mashaka. Lakini angalau wakati tunajiandaa na mjadala huo, tumpe Mwalimu credit basi ya kutuunganisha na lugha moja ya Kiswahili, lugha ambayo tayari ilikuwa spoken widely, hivyo akaona ni njia rahisi kutuunganisha katika ujenzi wa taifa kupitia lugha ambayo wengi wali relate nayo kama siyo ya kigeni kwa kuletewa bali ya kigeni kutokana na interactions na jamii za kiarabu, kireno, Kiswahili, miaka mingi sana kabla ya uhuru.
Pia tumpe Mwalimu angalau credit kwa kuanzisha vyuo vya sanaa na utamaduni, kuwa na maafisa utamaduni wa mikoa na wilaya nchi nzima kukuza utamaduni wetu, na mambo kama hayo. Kwa taarifa niliyonayo, mambo mengi ya sanaa yametupwa, hata Jumba la Sanaa Dar-es-salaam linabadilishwa na kuwa moja ya maeneo ya uwekezaji wa magorofa marefu ya vioo ambayo mtanzania ambae alikuwa na uwezo wa kuingia miaka ya nyuma, hata kama ni fukara mwenye mwili ulioodhofika kwa njaa, na mavazi ya kimaskini, jingo lile pale jipya mtu huyo hatothubutu tena kusogea kwani ataweza itwa mwizi.
Lakini inanisikitisha sana kwamba, anything ambacho mnakiona aliharibu, anapewa lawama yeye kama Nyerere, lakini anything ambacho mnakubali alifanya vizuri, mnasema lazima kiwe shared na wengine katika mazingira ya founding fathers. Ndugu zangu, mnasimama wapi???
All that said, mjadala kuhusu father of the nation versus founding fathers, ni mjadala mzuri, and as you rightly said, kila mtu yupo huru kuwa na mtazamo anaodhania ni sahihi kwake, akiwa kama sehemu ya taifa hili. Lakini, as I said kwenye my original post, mpaka tufikie huko, tumpe Mwalimu heshima yake ambayo tayari anayo ndani na nje ya nchi kama BABA WA TAIFA. Ni heshima aliyonayo tayari na hawezi pokonywa; kama mjadala ni kwamba wapo wengine wanaostahili, that is debatable, lakini haina maana kwamba heshima hiyo basi Mwalimu apokonywe. Hilo haliwezekani, na nina uhakika mkubwa tu kwamba hatutafika huko.
Pia naomba uelewe kwamba mimi sijalenga rais au kiongozi yoyote specifically aliyemfuatia Mwalimu after 1985, ninachokifanya ni kuongelea wote kwa ujumla wao, focus ikiwa utawala chini ya soko huria VS Ujamaa under Mwalimu. Ukiona nataja kiongozi huyu au yule hapa na pale, ni katika kujibu tu hoja kadhaa au kuomba ufafanuzi, vinginevyo kutaja viongozi fulani, watoto wao, na familia zao, mimi lengo langu sio hilo, lengo langu katika mijadala ya namna hiyo huwa ni Ujamaa (Nyerere) VS Soko Huru (Mwinyi, Mkapa, Kikwete);
Baada ya kusema hayo, ningependa kusikia juu ya mtazamo wako: Kwa Tanzania, ni vigezo gani vingekuwa sahihi kwa Nyerere kuitwa FATHER OF THE NATION na ni Vigezo gani ni sahihi kwa sasa kutumia Neno FOUNDING FATHERS?
Ni matumainu yangu kwamba nimegusia maeneo yote muhimu ambayo yanahitaji majibu yangu ya haraka, mengine tutaendelea kujadili kadri tunavyopata nafasi.