Faiza,1) Nyerere kajenga barabara ipi zaidi ya Dar-Tunduma?
Haukumsikia kipenzi chako, JMK, kwenye hotuba ile ya miaka 50 ya uhuru juu ya barabara?
Faiza,1) Nyerere kajenga barabara ipi zaidi ya Dar-Tunduma?
Ndiyo maana nimekuambia kwamba upo OFF topic. Mkandara alikuwa anazungumzia issue ya mwaka 1980 na wewe unaleta takwimu za mwaka 2011!!
Nimempa sababu zinazosababisha price ni Supply na Demand, yeye akawa ananiambia mambo ya wanunuzi kwamba walitaka kununua kwa bei ndogo. Sasa mnunuzi atataka kununua bei ndogo bila kuona Supply kubwa?
Ukiwa na bidhaa ikizidi excess of supply basi ujue mnunuzi lazima atataka kukupangia bei. Kwa sababu anajua atapata sehemu nyengine. Ndiyo maana nikamjibu changing in price ni kati ya Supply na Demand.
Ile barabara ya Mwanza-Musoma ilijengwa mwaka gani vile? Baadhi yetu humu lawama kwa Mwalimu ni ili tujifunze zaidi. Kwa kuwa enzi za Mwalimu hapakuwa na Tv na vyombo vingi vya habari kama ilivyo sasa, mengi aliyoyafanya hayafahamiki kwa watu kama Faiza ambao kwa mila na desturi za Pwani na DINI yao walijifungia ndani muda mwingi tu na walipotoka walielekea Uarabuni ambako masharti kwa wanawake ni magumu zaidi. Natumaini mmefunguka si haba!Barabara zote, tena zilikuwa zinapitika bila lami, kiangazi au masika. Zilikuwepo kabla ya Nyerere.
Nyerere hakuleta barabara mpya wakati wake zaidi ya vichochoro vya Sinza, Manzese na Buguruni. Na hata hivyo vilikuiwa havipitiki kabla ya yeye kuondoka.
Morogoro- Dodoma
Bw, Mkubwa... Hakuna mtz aliyezaliwa kumchukia Nyerere, kama kukosolewa kwakwe ,kwako wewe ni sawa na chuki ,hiyo juu yako na kasumba zako. Nyerere anavuna alicho panda (lima). Wapo waliopoteza ndugu zao wakati wa Udikteta wake na kamwe hawatakaa kimya . Mnae muuabudu fanyeni hivyo kwa maslahi yenu binafsi.
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa kama malengo ya awali ya kusaidia landlock countries hayapo, kwanini Tanzania istumie kipande cha Dar hadi Mbeya kwa usafiri wa abiria na mizigo.
Treni ndio usafiri unaochukua bidhaa nyingi kwa wakati mmoja na kwa bei rahisi sana. Inasikitisha mahindi yanaoza Sumbawanga halafu kuna mtu anakufa njaa Monduli. Yaani reli ipo hata maarifa ya kuweka injini na mabehewa hayapo.
Nakumbuka Tazara ilivyokuwa ukombozi kwetu kule Mang'ula, Mlimba, Ifakara, Kisaki n.k. Sisi wa Mtimbira na Kidogobasi tukikumbuka tunabubujikwa na machozi.
Uwepo wa reli ungesaidia kuongeza muda wa maisha ya bara bara za lami.
Nchi zote zilizoendelea, marekani, Uingereza, Canada, Japan watu wanatumia reli. Margareth Thatcher alipoanza kuiongelea reli kuhusu ubinafsishaji waingereza wakamwambia ampishe mwingine number 10 Down street.
Huyo Nyerere anayeitwa kila majina ya uovu, akiondoka ikulu reli zilikuwa na mabehewa na injini. Nakumbuka wakati huo ukisikia Injini ya Mcanada (Bombardier) basi uelewe behewa 40 zimefunga, Mwanza, Tabora, Kigoma n.k zinahamia Dar.
Waliofuata wakawaalika matapeli wakang'oa reli kama vyuma chakavu. Hawa ndio tunaaminishwa wamejenga reli na kuweka lami. Hii imani kama si upuuzi ni nini. Ni hawa ndio tunaambiwa wameleta Internet huku nchi ikirudi miaka 20 nyuma. Kuna wenzetu wanaamini Pipi na Big za Pakistan ni maendeleo! poor friends.
Katika jamii ya wenzetu Waislaam hasa misikiti ya hapa Dar wamefaulu kwa kiasi fulani. Umesikia bila shaka yale maandamano ya kupinga MoU ya makanisa na serikali. Agenda yake ni pana zaidi. Na haya hayaonekani kama ni uchochezi isipokuwa makala ya Mwigamba kwenye Tanzania Daima.Dada Faiza na Wenzako katika Hoja,
Juhudi zenu to minimize Nyerere's prominence kwa vizazi vijavyo ibakie kuwa kama ya Kina Kinjeketile na Chifu Mkwawa, hazitawezekana. At least not when some of us are still breathing.
Ile barabara ya Mwanza-Musoma ilijengwa mwaka gani vile? Baadhi yetu humu lawama kwa Mwalimu ni ili tujifunze zaidi. Kwa kuwa enzi za Mwalimu hapakuwa na Tv na vyombo vingi vya habari kama ilivyo sasa, mengi aliyoyafanya hayafahamiki kwa watu kama Faiza ambao kwa mila na desturi za Pwani na DINI yao walijifungia ndani muda mwingi tu na walipotoka walielekea Uarabuni ambako masharti kwa wanawake ni magumu zaidi. Natumaini mmefunguka si haba!
Unapotosha kusema barabara ya Mwanza- Musoma, sema Magu- Musoma..
Kutoka Mwanza Mjini mpaka Nyanguge ilikuwa mashimo matupu wakati wa Nyerere..
Imejengwa wakati wa Mwinyi pamoja na barabara zote za Mwanza mjini..
Bila shaka kulikuwa na lami kati ya Nyanguge na Mwanza mjini ambayo baadae iligeuka ikawa mashimo. Historia haiandikwi upya wala kurekebishwa.Unapotosha kusema barabara ya Mwanza- Musoma, sema Magu- Musoma..
Kutoka Mwanza Mjini mpaka Nyanguge ilikuwa mashimo matupu wakati wa Nyerere..
Imejengwa wakati wa Mwinyi pamoja na barabara zote za Mwanza mjini..
Bila shaka kulikuwa na lami kati ya Nyanguge na Mwanza mjini ambayo baadae iligeuka ikawa mashimo. Historia haiandikwi upya wala kurekebishwa.
Umeona eenh! kuna mijitu kichwa ngumu bila bakora haiendi. wewe huoni wazee wa Kiswahili bakora mikononi haziwatoki wanajua bila bakora hawataelewana!!Pamoja na kazi yoooote ya uchambuzi alofanya Mchambuzi haya ndio majibu.
Sasa naelewa kwa nini walimu wetu wakati mwingine wanatembeza bakora.........
Hakuna lawama dhidi ya Nyerere, upo uzushi unaoundwa na kikundi cha watu wachache kama Takashi ambao hawana hoja, data wala ukweli. Wamejazwa hadi akili haziwezi kubaini kati ya kudanganya au kudanganywa.
Nimeweka maswali hapo juu hakuna anayejibu, bali tunaona watu wakibadili mada na kuleta udikteta, Zimbabwe, unit n.k.
Nikuulize wewe Takashi unayedhani huna chuki mdomoni lakini moyoni ni mweusi. Maswali ni haya:
1. Mwinyi, Mkapa, Kikwete wamejenga bara bara gani kwa pamoja kushinda Nyerere. Sio kuweka lami uelewe!
2. Watatu hao wamewekeza kiasi gani katika 'energy' kuliko Nyerere
3. Ni kitu gani kinafanyika sasa hivi ambacho hakina msingi alioweka Nyerere
Ukijibu maswali hayo nitajua upo kwa mjadala, usipojibu kaa kimya chuki itafaune nafasi yako.
Bw,Nguruvi3, mimi siko hapa kumfananisha Nyerere na waliofatia baada yake. Wote hao wana kasoro zao . Ninacho kipinga na nitaendelea kukipinga ni zile sifa na utukufu anaopewa Nyerere .Hakuwa matakatifi, wala innocent , he was as all dictator are...Kama alijenga bararbara kutoka tz hadi south Africa kwangu mimi haibadilishi kitu.
Hilo kundi lenu lenye kumuabudu Nyerere, tunajua mnafanya hivo kwa maslahi yenu binafsi. Hivi yule mzee angekua bado yupo madarakani , JF ingekuwepo? Hivi angeruhusu wa Tz wawe na mijadala ya wazi kuhusu masula ya nchi yao? Aliwanyima hata TV kwa kuhofia wa Tz watafungua macho mapema.