YAH: HOJA YA FOLENI WAKATI WA UJAMAA NA MWALIMU KUOMBA MSAMAHA
ATTENTION: MR.RIGHT, FAIZA FOXY NA WENZENU KATIKA HOJA
Kwanza na awali ya yote, Mr. Right, naomba tuelewane kwamba hapa hatubishani, or at least on my part, tunachofanya ni kujadiliana kwa hoja. kwahiyo hoja kwamba huu ni ubishi baina yangu na wewe naomba uiondoe akili mwako.
Ø Tulijadili hili la Nyerere Versus Free Market Kwa hoja, sio Malumbano.
Pia hili linamhusu Dada yangu Mpendwa, FAIZA, maana hata kwake, suala la foleni wakati wa Mwalimu limekuwa wimbo wa taifa sasa.
Mr Right, Kwanza, nilishaeleza kwa kirefu jinsi gani umaskini Tanzania, Kenya, Nigeria, etc, haujalishi nchi zetu zinafuata Ujamaa au Soko Huru (SOKO HOLELA). Nikauliza, je, Kwa wale wanaosema Ujamaa ulitupotezea muda, kwanini nchi zilizoendelea na soko huru moja kwa moja baada ya uhuru wao, leo wote wapo na sisi kwenye lowest level ya Maendeleo kwa vipimo vya UNDP HDI? According to the UNDP, kuna levels nne za development: (1) Very High; (2) High; (3) Middle; and (4) Low Level. Katika Africa, only one country is in High level (Libya), Middle level zipo nchi kama 7, the rest of the countries in Africa i.e 85% of the continent zipo kwenye LOW LEVEL pamoja na sisi Tanzania. Isitoshe, hata Nigeria, Taifa lililojikita kwenye soko huru tangia uhuru, na la saba duniani kwa uzalishaji wa mafuta, limepitwa na Tanzania in terms of vigezo hivyo vya HDI vinavyoangalia impact of uchumi kupaa (kama wanavyotuimbia wanasiasa wetu) i.e. GDP Growth katika kuboresha maisha ya wananchi literacy levels, educational outcomes, life expectancy, and improved standard of living (quality of life);
Nikauliza, je, haitoshi kutuamsha watanzania wanaomdhihaki Nyerere kwamba mdudu anayetutafuna wote ni mmoja bila ya kujali mfumo wetu ni upi kiuchumi?
Mwalimu aliwahi kusema, uhuru wa kisiasa tumeupata, kazi kubwa iliyopo mbele yenu nayowaachia ni ya kujikomboa kiuchumi. Pia alitamka haya alipoenda USA kwa mwaliko maalum by JFK, White House 1963 (video clip ipo Youtube), aliposema huu ni uhuru wa kisiasa tu, mapambani ndio kwanza yameanza. Ndugu zangu, kinachotumaliza baada ya miaka 50 baada ya uhuru wa Kisiasa,sio kingine bali the unfair integration of our societies into the global capitalist system. Suala la uongozi na sera zetu za nyumbani ni suala secondary. The global current capitalist system ni mfumo ambao unatupokonya uhuru wa kufanya maamuzi yetu ya kiuchumi from the MACRO PERSPECTIVE decisions on where and how to invest, what to produce, how to mobilize savings, exchange rates, employment/unemployment levels, trade movements, inflationary targets etc; jukumu hili wamelipokonya wakubwa World Bank, IMF na WTO ambao wapo kwa ajili ya maslahi ya Nchi Tajiri (G8). Uhuru tulionao kiuchumi sisi ni ule wa MICRO LEVEL households zetu, kwamba leo tule chai na nyanya, ugali na kachumbari, etc. Muundo wa uchumi unaowapa wananchi control ya household decisions (MICRO), huku MACRO ikiwa sio tu nje yao, bali hata serikali yao, ni uchumi Uchwara. Kwa mfumo huo, Maendeleo ya mwananchi yatatokea wapi? Watapenya penya wachache tu kama wewe Mr Right, Faiza na wengineo. Wengi wanaopenya wanapata uwezo wa maisha ambao ni very artificial, sio kutokana na mishahara yao.
Sijui kwanini wengi wetu tunaendeshwa na ushabiki, huku wakubwa wa nje wakitucheka kwani nia yao ni Tanzania na other parts of Africa zibakie kuwa a rural Yard for Europe and North America. Rural Yard kwa maana ya supply of raw materials, minerals
; Wanaofaidi katika mfumo huu ni wachache sana. Kwa kweli hoja kwamba Bora Afrika ije tu kutawaliwa tena na Mkoloni ina mantiki kama watu wa namna yenu ndio walio wengi. Nyerere alijitahidi sana kuzuia huu upuuzi.
Ø Tulitazame suala lako juu ya Nyerere Kukiri kushindwa na Ujamaa
Kama una busara na uelewa wa hali halisi, haitakiwi ubeze Mwalimu kuomba msamaha, bali kumuona shujaa na kuhimiza awe mfano wa kuigwa na viongozi waliomfuatia. Nyerere alikuwa na ujasiri wa ajabu kuthubutu kuwaambia wakubwa wa nje we are a self- determined nation, but ofcourse wakamzidi nguvu; Sasa msamah wa kwamba we wanted to be self determined but we failed ni wa kukejeli jamani? Pia Mwalimu alituacha na warning kuhusu yatakayojiri mbeleni. Ndio haya haya ya GDP growth kuwa na wastani wa 7% kwa miaka zaidi ya kumi sasa, huku Human Development Index inayopima matokeo ya GDP Growth kuboresha maisha ya watanzania kiafya, kielimu etc, ikituweka permanently nafasi ya 150-152 kati ya nchi 187 duniani. Na wanasiasa mnaowashabikia kwamba ndio wamefanya mema chini ya soko huru (SOKO HOLELA) wanapita majukwaani kuisifia hali hiyo, huku nyinyi mkipiga makofi.
Mr Right, ebu tuambie Whats Right:
· JE, unajua ni watanzanai wangapi katika Tanzania ya leo ISIYOKUWA NA FOLENI, wanalala njaa i.e. hawawezi kupata mlo zaidi ya mmoja kwa siku chini ya hilo soko huria, lisilo na foleni?
· JE, ni kiongozi gani chni ya soko huria amewahi kuomba msamaha kwamba sera za soko huria zinawanyima maisha bora wananchi walio wengi pamoja na familia zao?
· JE, ni kiongozi gani wa soko huru amewahi waomba radhi ndugu zetu kule Mwanza na Musoma kwa jinsi gani kemikali za wawekezaji kwenye migodi zinazomwagwa ovyo in the name of soko huria zinawamaliza ndugu zetu?
· JE, ni kiongozi gani wa soko huria amewahi kuomba radhi jinsi gani wananchi wa kanda ya ziwa (Mwanza), ambao walijaliwa na mwenyezi mungu Ziwa Victoria ili liwapatie vitoeo vya samaki, leo hii wanaambulia mapanki?
· JE, nani ambae amewaomba radhi wananchi kwamba, walipigania uhuru kwa ajili ya kurudisha hali ya haki na usawa, only kupigwa virungu na polisi wakidai haki zile walizoahidiwa?
Mr. Right, mambo ya kuombewa radhi ni mengi, lakini hakika, hakuna aliyeombea radhi kwa lolote chini ya soko huruhilo, na sidhani kama yupo atakayethubutu kwani, aliyewajali kwa dhati hatunae tena.
Mr. Right, let us see what is right and what is wrong hapa. Ebu tutazame takwimu zifuatazo ambazo kwa maoni yangu, nazo zinahitaji viongozi waliokuja baada ya Mwalimu, kuwaomba wananchi wa vijijini kwa kuachia soko huru (HOLELA) limalize kabisa matumani yao.
Mmezungumza suala la foleni wakati wa Mwalimu, Mr.Right, Faiza, Je, Tanzania ya Leo ipo nafuu gani bila ya foleni?
· 68% of Tanzanians (milioni kama 30 kati ya jumla ya watu milioni 45) wanaishi chini ya $1.25 a day, hii ni sawa na just about T.sh 2,000 kwa siku. Mr. Right, Fauza, given the current exchange rate (compared na enzi za Mwalimu), unajua mlo mmoja kwa MAMA NTILIE ni shilling ngapi, hata kama mama ntilie wamejaa mitaani na hivyo kutohitaji mtu upange foleni?
· Wangapi wanaweza afford kila ya nyama, unga, sukari kwenye maduka ya kumwaga, ambayo hayahitaji tena foleni?
· Je, mnajua nauli ya basi ya siku nzima ni shillingi ngapi, pamoja na utitiri wa mabasi ambayo hayahitaji watu kupanga tena foleni? Wakati wa Mwalimu kulikuwa na foleni, tena katika kipindi fulani tu, lakini ilitokana na juhudi za Mwalimu kupunguza tatizo la inequity; soko huria limesaidia kina nani sasa compared to Mwalimu?
· Je, mnajua gharama ya umme ni shilling ngapi, umeme ambao hauhitaji foleni kwani unaweza lipia hata kwa M-PESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY?
Ujamaa ulizaa mambo kadhaa ambayo mmeyaweka bayana. Fine, Je, soko huria mbali na kuondoa hizo foleni kama tulivyokwisha ona hapo juu, limezaa nini?
Leo hii, ni mengi ikiwa ni pamoja na yafuatayo:
· Income share held by the highest 10% of the population is 30%;
· Income share held by the highest 20% of the population is 45%;
· Hapa ina maana, 30% of the population wanahodhi 75% of wealth in Tanzania.
· Income share held by the lowest 10% is 7%;
· Income held by the lowest 20% is 3%;
· Hapa ina maana, 30% of the population (wale maskini wa kutupwa), kwa umoja wao wanahodhi only 10% of wealth in Tanzania.
This means the remaining bit, 15% ndio middle Class in Tanzania;
Now, 75% hapo juu PLUS 15% hapo juu, leaves us with 15% to make it 100%; Hii 15% remaining ndio middle class ya Tanzania.
Je, Mr. Right, Dada Faiza, katika Tanzania ya leo isiyokuwa na foleni, mpo kwenye kundi lipi?
Ndugu zangu, with intense concentration of power, wealth and knowledge in the few hands hapa Tanzania, hata mtoto mdogo wa shule might be able to tell kwamba katika mazingira haya hakuna kitu kinatwa free market (let alone demokrasia); kumbukeni: Free Market assumes and requires more or less equal actors in the game, not a few GIANTS living among many DWARFS or MIDGETS. Ndugu zangu, Free Market doesnt count heads, it counts dollars. It favors the rich and powerful, not the miserable many because of their numbers (70% of wanavijiji). Sasa hawa ndio watakuja weka mambo sawa. Nyerere alishawaonyesha njia, lakini safari yao iliyojaa matumaini, ikakatishwa ghafla.