SOBY
JF-Expert Member
- Sep 19, 2011
- 1,268
- 459
Kwanza kabisa population dynamics zinaifanya hiyo 60,000 kuwa less than 46,000.Hili la baba wa taifa tuachane nao wanopinga wakameze wembe... turudi kwenye mada yetu.Kipande hiki nimekipenda sana na hakika nitachangia kwa wale wasiojua mahesabu ili wapate kujua kama kweli tulishindwa ama kulichangiwa sababu nyingine kabisa..
Nitawapa mfano mdogo sana:-
- Kuanzia mwaka 1972 hadi 1982, Tanzania tulikuwa na mashamba ya Kahawa Hectares 126,000 zikizalisha kahawa wastani wa tani 46,000kila mwaka - yields about 390 kilo per hectare...
- Na sasa hivi tuna hectares za kilimo cha kahawa zaidi ya 300,000 tunazalisha kahawa kwa wastani watani 60,000 kwa mwaka -yields ni about 320 per hectare...
Sasa waungwana kweli unaweza kusema leo hii tumeendelea kwa sababu tu leo hii Kahawa imepanda bei wakati uzalishaji ndio kama mnavyoona hapo juu.
Hivi kweli mama mpika vitumbua alokuwa akiuza vitumbua 1,000 kwa siku mwaka jana kwa bei ya Tsh 500 ana nafuu zaidi mwaka huu kwa sababu anauza vitumbua 600 kwa bei ya Tsh 1000? kwa sababu tu watu wanatazama pato la kutoka laki tano kwenda laki 7 bila kuzingatia matumizi na kupoteza wateja 300!...
Naomba wasomi wa uchumi mnielimishe..
Pili, productivity inasuta uwezo wetu bearing in mind technology imeongezeka duniani.