Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #661
Mchambuzi,
Unajua mimi huwashangaa sana watu wanaobeza Ujamaa hali wao wenyewe katika maisha yao ni Wajamaa. Na ktk Ujamaa wao wanakubali kabisa kwamba baba zao ni dikteta na wao kama wazazi ni madikteta vile vile. Ndio maisha ya kila Mtanzania mzazi ana sauti kubwa ndani ya familia na kuna sababu ya kuwa hivyo. Sasa kwa nini mzazi asimwache huru mtoto atafute riziki zake maadam kisha zaliwa na atakuwa na maisha yake aachiwe tu atafute maisha!...
Hata wanyama hawafanyi hivyo kuna kipindi cha mzazi kumwachia mwanaye hizi propaganda za nchi za Magharibi ambao kwa miaka zaidi ya 50 wamekuwa vitani hata baada ya Uhuru na wakiishi kwa amri za majeshi leo wanataka kutuambia sisi jinsi ya Kujitawala!. Hawa wazungu walilazimishwa kwenda vitani walilazimishwa kushiriki ktk ujenzi na hata kufanya kazi viwandani kutumikia majeshi yao na hakika mageuzi ya nchi hizi yalitokana na necessity za wakati wao ambao ulikuwa ni vita.
Hivyo Ujamaa ulikuwa na lengo zuri tu, sisi tulipopata Uhuru, asilimia 98 ya wananchi wake walikuwa maskini, middle class yenyewe walikuwa maskini vile vile maana hawakufika hata asilimia 5 na hawakuwa na uwezo wa hata kuendesha maisha yao wenyewe iwe elimu ama afya. Sasa hii nchi sii kama mtoto? na mtoto alitakiwa kulindwa kukuzwa na kufikia mahala anapoweza kujitegemea ndipo unampa uhuru wa kutafuta maisha yake mwenyewe lakini hatukutazama Uhuru wetu kwa jicho hilo bali kwamba sasa mkoloni kaondoka ni wakati wa kugawana utajiri na mamlaka walioacha. Ugonvi mkubwa baina ya Nyerere na viongozi wengi hasa hawa wanaomchukia ilikuwa mgawanyo wa kile mkoloni alichokiacha. Tazama nyumba zote walizokuwa nazo viongozi wetu ni zile za wakoloni.. kati ya mwaka 1961 hadi 1967 viongozi hawa hawa waliotuletea Uhuru ndio walikuwa wa kwanza kwenda kushika nyumba hizo maana hawa waliishi Kariakoo Ilala na Magomeni ghafla wote wamehamia Uzunguni..
Kwa hiyo wasiweke roho juu, Ujamaa ulikuja kwa nia njema kabisa lakini hauweza kufanikiwa kwa sababu sisi wenyewe hakukuwa tayari, tulitegemea kugawana utajiri waloacha mkoloni na haikuwa hivyo. Halafu basi ajabu ya Firaun tumeingia katika Ubepari watu wanawaita Chadema ni chama cha Kibepari?. Heee! itakuwaje dira ya Taifa iwe ya kibepari lakini tunabeza Chadema kama chama cha kibepari?... kwani nchi bado ipo ktk Ujamaa?... watakwambia hapana na hawataki kuusikia kabisa..
Hivyo kuna kushindwa watu kuelewa kwamba tupo ktk Ubepari na kwa kila baya na zuri linalofanyika leo linatokana na Ubepari lakini haina maana tunashindwa kwa sababu ya Ubepari isipokuwa itikadi zetu wenyewe ndizo hazina sera bora zaidi ktk kufikia malengo hayo ndani ya Ubepari lakini Ubepari ni tayari tumeubeba na sidhani kuna chama kinalaani Ubepari - a Socialist party - Hakuna!..Tumeshindwa hata kabla hatujaanza!
Mkandara,
Umeongea hoja za msingi sana. Kuhusu suala la u-dictator, Nyerere ni kweli alikuwa na hiyo element, but he wasn't a dictator per se, kwani hali ya udikteta means "expecting unquestioning obedience", this wasn't always the case; Nyerere hakuwa hivyo wakati wote, waliokuwa wanamwogopa ni wale waliokuwa na unafiki katika Ujamaa, otherwise kulikuwa na watu wanam challenge kwelikweli, and he liked it; Tumesikia mengi sana jinsi gani alivyokuwa anawatembelea wanafunzi wa UDSM mara kwa mara kwenda to debate with them kuhusu mambo mbali mbali ya ndani na nje ya nchi – kina Issa Shivji, Sitta na wengineo walikuwa wanapambana nae kweli kweli; Ugomvi mkubwa wa Mwalimu na UDSM wakati ule, Mh. Sitta akiwa ni mmoja wa vinara wa ugomvi ule, was sera ya kutumikia JKT kwa ulazima; Wengi wakiongozwa na Sitta hawakulitaka hilo; walikuwa na hoja, lakini ukiangalia mantiki ya JKT kwa miaka ile, haikuwa mbaya, kwani nchi nyingi mpaka leo kama Israel, Greece, etc, lazima mtu uende jeshini ikiwa sehemu ya kuwa raia madhubuti zaidi;
Pia kuna nyakati nyingi sana tulisikia jinsi gani Mwalimu alikuwa very democratic katika maamuzi ya Chama – kikubwa ilikuwa usimletee agenda za kuogopa Ujamaa in favor of Ubepari, hapo ilikuwa ni kumtafuta ugomvi; Otherwise demokrasia ndani ya chama, na yeye kukubali mawazo ya wengine ilikuwa ni jambo la kawaida sana, mfano, hata Salim A Salim mwaka 1985, Nyerere alikuwa na uwezo wa kusema liwalo liwe, nimesema yeye ndiye awe mgombea, lakini alishindwa na akaachana na hilo wazo; pia 1995, alimtaka Salim lakini bado hakuweza kufanikiwa kwa hilo; mifano ni mingi sana ndani ya CCM na serikali yake; Na kila alipokuwa anafanya maamuzi against demokrasia alikuwa anatoa maelezo – mfano, uchaguzi nadhani wa mwaka 1965 au 1970, Paul Bomani alianguka Ubunge; alipokuwa anahutubia bunge, akawaambia wabunge na wananchi, nimemteua Bomani kuwa mbunge ingawa wananchi mlimkataa lakini ninamuomba kwani namhitaji kwa hili na lile. Nani ambae anaweza sema kitu kama hiki miaka ya leo?
Wanaposema Nyerere alikuwa aambiliki, ni kweli lakini katika vitu vikuu viwili: Sera ya Ujamaa na Kujitegemea ambapo alikuwa hakubaliani na mawazo yoyote to give in kwa mabepari kwani alitaka itokee only when we are ready to participate on equal grounds; Suala la pili ambapo alikuwa haambiliki ni suala la serikali tatu katika muungano, hilo alipingana nalo mpaka anafariki, and in my opinion, this was one of his blind spots – muungano kuwa na serikali mbili; the idea was very good lakini it was and still is, very very very impractical.
Mkandara, leo hii unaposikia hoja juu ya maamuzi magumu, ukiangalia kwa undani, unaona kabisa kwamba watu wanataka kiongozi mwenye udikteta kidogo, au sio? Mara oh, tazama Kagame, mara ooh, sijui Mkapa angefanya hivi, mara ooh, tunahitaji mtu kama Mh Edward, lakini ukiangala kwa makini, yote hiyo ni ushahidi kwamba to many, elements za udikteta katika uongozi wa nchi kama zetu ni muhimu, ili mradi mhusika anaongoza kwa kuheshimu sheria, utawala wa haki, na kulinda haki za binadamu kwa ujumla wake;
Hoja yako kuhusu wenzetu wazungu na kuingia vitani, that's a very good point; ukiangalia matukio ambayo yanapelekea wao kutuma majeshi yao, maamuzi hayo yanakuwaga on what grounds? Na pia ndio maana hata mataifa yenye demokrasia iliyopitiliza, Rais ana kura ya VETO ili iweze kutumika katika mazingira fulani, especially kama yana maslahi kwa wengi. Kwa kweli Mwalimu hakufanya uamuzi wowote mkubwa kwa maslahi ya wachache au binafsi; angeshindwaje kujilimbikizia au kuweka ndugu zake kwenye madaraka? Watoto wake tulikuwa tunapishana nao barabarani, wengine katika hali kama vile wamerukwa na akili. Hata nyumba ya Msasani, alikopesha NBC kuijenga, lakini mkopo ukamshinda, so akaiuzia serikali ili alipe deni lake NBC; ile nyumba ilirudi serikalini kwa miaka mingi; alikuja kupewa bure miaka ya baadae alipostaafu; na alikuwa anasema always kwamba mimi Ikulu sio kwangu, sina hata raha kukaa katika jumba lile, ndio maana mara nyingi sana alikuwa anaishi msasani hata wakati wa urais wake;
Hoja yako ya viongozi wenzake baada ya uhuru kutaka kukamata alichoacha mkoloni stands very well; ni hawa ambao ndio walianza kushirikiana na mabepari wa nje to undermine Ujamaa; hata mashirika mengine ya umma ilikuwa ni sabotage tu going on, si jingine; WorldBank na wenzao walikuwa wanatokwa sana na mate kutaka hela yao ndiyo iwe yak u-finance projects, parastatals etc, coz that's how they make profit for its shareholders.
Kuhusu ubepari, you are right; mimi kwa mtazamo wangu ambao unaweza kuwa finyu, kinachotakiwa ni maandalizi ya watanzania kuingia katika mfumo huo wakiwa tayari, kwani mageuzi haya yaliwakuta kama vile walikuwa ugoni, na since then wamekuwa wana adjust kwa kudra za mwenyezi mungu; vinginevyo ubepari per se sio mbaya, issue to fair participation;
Hoja yako juu ya viongozi baada ya uhuru kutaka vya mkoloni na pia juu ya 98% ya wananchi walikuwa maskini, tena vijijini, kitu ambacho kilichangia sana Mwalimu kuamua kuja na Sera ya Ujamaa ili kujenga taifa lililo sawa na pia kulipa fadhila kwa wananchi waliopigania nchi yao kutoka makucha ya mkoloni.
On that note, ngoja nikuache with a quote ya Mwalimu from kitabu chake cha TANU NA RAIA (pp.6):
"Wakoloni walipokuwa hapa walipanga mishahara bila ya kujali uwezo wa watu wetu kulipa mishahara hiyo, na bila kuilinganisha mishahara hiyo na mapato ya watu wetu. Lakini wao ilikuwa ni ada yao kufanya hivyo. Serikali ya wageni haiwezi kujali maisha ya raia. Serikali yao ilikuwa ni serikali ya ubwana na ufahari; na walijitimizia ubwana wao na fahari yao, bila kujali uwezo wa watu wetu wa kugharamia ubwana huo na fahari hiyo;
Lakini baadhi yetu tulikuwa hatutambui jambo hilo. Waafrika wengi tulikuwa tumekwisha kusahau kwamba mzigo ule wa ubwana na fahari ni mzito mno na watu wetu hawawezi kuubeba. Kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana ule na fahari ile wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia sisi pia; Baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na fahari, bali tama yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na fahari; Tama yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia, iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo, bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, na bila ya kujali maisha ya watu wetu."
MWL J.K NYERERE< TANU NA RAIA - P.6.