Nyerere alimkosea nini Mungu?

Nyerere alimkosea nini Mungu?

Hapa unachemka mkuu; usidhani unafahamu kila kitu ndugu, huu ni ulimwengu wa sayansi jamii; mitazamo, uzoefu na mazingira uliyokulia vina umuhimu mkubwa katika mjada uliouanzisha.

Watu wengi tunawakubali mashujaa wetu ambao kwa namna moja ama nyingine waliiletea heshima bara letu. Hili la Mandela vs Mwalimu, huhitaji kukaza misuli ya shingo, kuna ukweli mkubwa Mandela anaweza asimpate Mwalimu. Labda tuweke vigezo ndiyo tutaelewana. Huhitaji kutukana au kudhihaki ili uonekane bingwa, hapa tunajifunza tu. Mfano, wa vigezo ni:

1. Eneo ambalo kila mwanaharakati kati ya wawili hawa walifanya harakati zao. Kumbuka Nyerere ana mchango pia katika kuwasapoti kina Mandela. Mpaka leo waafrika kusini huja kuzuru kambi kama Mazimbu na Dakawa, zote zikiwa ni kambi za wanaharakati wao wakijipanga kwenda kukomboa nchi. Si, Afrika ya kusini pekee, ni nchi nyingi Tz ilifanya haya, mfano, Msumbiji, Zimbabwe n.k

Hapo juu unamshambulia mchangiaji wa mada yako eti Mandela ana nini cha kuwapa wazungu. Hujiulizi kwa hiki Nyerere alikifanya, kama kweli wazungu ni wakweli huoni Nyerere alipaswa kupata tuzo zaidi ya Mandela? Kwa kifupi, hatubezi juhudi za Mandela lakini ule umaarufu ulitiwa chumvi na wazungu kwa sababu zao binafsi. Kumbuka huyu ndiye alikuwa gaidi kwao hadi kumyima viza kuingia nchi zao lakini baada ya kukubaliana namna ya kuindesha Afrika ya kusini bila kuwadhuru wazungu na mali zao akageuka shujaa wa kimataifa.

2.Kigezo kingine ni kukaa madarakani huku ukiendeleza nchi yako na kusaidia wengine. Sote tunajua alichofanya Mandela, kuanzia muda aliokaa madarakani na hata kile alichokifanya ili kuwakomboa raia wa Afrika ya kusini kiuchumi. Fine, hapa hatuwezi kumlaumu kulingana na mazingira ya taifa lao, mpaka leo bado kiuchumi weusi wenyeji ni bilabila. Lakini huwezi kulinganisha na Tz, pamoja na wanasiasa kutufanya vibaya, bado hali zetu si sawa na wazulu. Ninarudia, hili si la kumlaumu Mandela, ni historia yao ndiyo imewafikisha hapo. Lakini kwakuwa tunalinganisha, basi tutumie kuwatathimini wote iwe ni sababu binafsi au za nje yao.

Aidha, pamoja na sifa nyingi tunazowapa watu hawa, huwa tunakosea sana kuona ama kufikiri hawa watu walikuwa peke yao. Wengi hulalamika kuhusu Mwalimu na namna alizima nyota za watu walioshiriki kuliletea taifa uhuru na heshima. Inashangaza sana vijana tunafunzwa na kukaririshwa Mwalimu peke wakati kuna wanaharakati wengi tu, wengine mwalimu aliwakuta wakiwa washakinukisha. Hata Afrika ya kusini ni hivyohivyo, wapo wengi saaaana waliofanya pengine hata zaidi ya Nelson. Lakini hao ndiyo nyota zao ziling'aa, wakatokelezea. Ni jukumu letu sisi wachambuzi, kuyajua haya na kuweka rekodi sahihi kuliko kushambuliana mradi tu fulani awe mshindi.

Kuhusu wanaharakati na kufaidi ama kutofaidi maisha kiasi cha kusema Mwalimu alimkosea nini Mungu, kuna ukweli kabisa ukiwa mtu si wa kutamani ufahari basi maisha yako hayawezi kuwa hivyo. Pamoja na mapungufu ya Mwalimu kama hayo niliyogusia hapo juu, kwa uoni wangu, hakuwa mtu mwenye tamaa ya maisha hayo pengine mimi na wewe tunaona ni ndiyo maisha.Lakini ujue, aliwajengea watoto msingi mzuri tu, namba moja ikiwa ni elimu. Sisi tunataka mtu kama yeye afuje mali, alazimishe watoto kuwa mawaziri na wakuu wa majeshi, wamiliki midege n.k, huku hatuna vitanda vya wagonjwa, hakuna sehemu za kina mama kuzalia, watu tunakufa njaa n.k., hapo ndiyo tunaona haki inatendeka kwa watu wa kaliba hiyo. Huu si uungwana!

Asante
Mkuu Nyerere na Mandela wote ni mashujaa wa Africa wenye historia na kazi tofauti ktk kuleta uhuru.
Sasa inashangaza humu kuona watu wanamdharau Mandela Kama Makonda hadi kusema hajafanya lolote

Bila Mandela South Africa ingekuwa huru?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naamini Baba wa Taifa ana rekodi nzuri zaidi kuliko Mandela hasa ukitilia heshima kubwa aliyojijengea duniani kote na katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa. Sioni kikubwa alichokifanya Mandela kumzidi Baba wa Taifa.
Huwezi linganisha kocha na mchezaji, inabidi kocha kwa kocha au mchezaji kwa mchezaji, mchezaji, wakati Mandela yuko jela huku Nyerere ni rais, halafu Nyerere kapambana kama nchi na sio kama individual wakati Mandela kapambana kama individual. Nyerere had nothing to loose yeye kama Nyerere maana resources zote zilizotumika ni za nchi, kwa hiyo credit ibabebwa zaidi na nchi tofauti na Mandela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Natofautiana na wewe, nchi haiwezi kubeba credit kwa sababu bila msukumo wa Baba wa Taifa nchi isingefanya lolote.

Inabidi kuwe na kiongozi wa kuhamasisha raia wa nchi yake ili kushiriki katika msukumo/kampeni ya kufanikisha jambo fulani vinginevyo bila huo uhamasishaji kampeni hiyo isingefanikiwa kwa kukosa msukumo.

Huwezi linganisha kocha na mchezaji, inabidi kocha kwa kocha au mchezaji kwa mchezaji, mchezaji, wakati Mandela yuko jela huku Nyerere ni rais, halafu Nyerere kapambana kama nchi na sio kama individual wakati Mandela kapambana kama individual. Nyerere had nothing to loose yeye kama Nyerere maana resources zote zilizotumika ni za nchi, kwa hiyo credit ibabebwa zaidi na nchi tofauti na Mandela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere kaondoka Duniani akiwa kaacha heshima kubwa mno kimataifa.
Wanasiasa wa Tanzania wamekuwa hawaachi kumtaja huyu Mzee kila mara kwenye kampeni au hotuba zao.

Alimshauri rafiki yake mkubwa hayati Nicolai Cesesscue enzi za uhai wake akiwa Rais wa Romania aachie ngazi ili kulinda heshima yake ,Nicolai hakusikia matokeo akaja kuuawa kikatili yeye na mkewe.

Alimshauri Kaunda wa Zambia naye hakusikia, "mzee mwenzangu waachie Vijana ulinde heshima yako ".

Kaunda akapuuza ushauri wa Nyerere matokeo yake akaja kuondoka Kwa aibu ya kushindwa uchaguzi, badala ya kustaafu, yaani Rais wa kwanza wa nchi unagombea tena, what a shame?

Heshima ya Nyerere Kwa Africa inazidiwa na Mandela tu, ukimtoa Mandela hakuna Rais tena wa kufananishwa na Nyerere ktk bara la Africa.

Kwanza alikuwa akiaanza kuongea unatamani uendelee kumsikiliza tu muda wote hata Kama ulikuwa na stress Ukisikiliza hotuba za Nyerere stress zinapungua.

Ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Africa huwezi kuujadili bila kumjadili Nyerere ambaye ndo alikuwa key point ya Ukombozi Huo.

Ni katika Kipindi cha Urais wake Tanzania iliheshimiwa na hata kuogopwa na mataifa makubwa Duniani.

Pamoja na matatizo ya hapa na pale, lakini enzi zake uchumi wa Tanzania ulikuwa juu, pesa ilikuwa na thamani kubwa, noti ya mwisho Kwa thamani kubwa ilikuwa noti ya sh 100.

Elimu ilikuwa juu, siyo kama leo hii ambapo hata kiswahili tu kinawapa shida hata wahitimu wa vyuo vikuu, neno "hela " wanatamka "ela" neno "halafu "wanatamka "alafu " eti hao ni university graduates, kwenye English ndo unaweza hata kulia Kwa namna wanavyoboronga.

Enzi zake hata intelligence ya nchi ilitisha, TISS ya Nyerere haikuwa tofauti na CIA hutaki kuamini acha.

Wakati wa vita vya Kagera, TISS ilimzunguka Idd Amin Spain, alikuwa ameagiza makombora ya kisasa yenye nguvu lakini akajikuta anayakosa na yakaangukia mikononi mwa Tanzania.

Hatukuwa na silaha Kali Kama za Idd Amin, lakini tulikuwa na intelligence imara mno, hii ndo ilifanya tushinde vita bila msaada wa nchi yoyote, Idd Amin pamoja na kusaidiwa na Gaddafi bado tuliweza kumtwanga hadi akaikimbia Uganda.
Inahitaji Kitabu kuandika mambo mazito aliyofanya Nyerere.

Lakini alimkosea nini Mungu huyu mzee?
Mwandishi Munga Tehenani (RIP) aliandika Kitabu kiitwacho "Nyerere alikuwa mchawi ".
Kitabu hiki hakikukaa mitaani hata siku tatu kikawa kimepotea kimaajabu, ilikuwa ni kati ya mwaka 2001 au 2003.

Inadaiwa aliingia maagano na kuzimu na fimbo yake ndo ilikuwa muongozo wa mambo yake yote.

Maagano yoyote ya nguvu za giza humkasirisha Mungu na kukilaani kizazi cha mtu aliyeingia maagano hayo.

Mungu hulaani kuanzia watoto na hata vitukuu na vilembwe na hata kizazi cha nne.

Familia ya Rais Kennedy wa US aliyepigwa risasi mwaka 1963 imepukutika yote Kwa vifo vya ajali na kuuawa, hakuna alama yoyote ya Kennedy Marekani, yamebakia majina tu.

Nikiitazama Kwa jicho la tatu familia ya Nyerere haiko sawa, imefunikwa na giza nene, haing'ai, haionekani, it looks like Nyerere left no children to walk his ways,haya ni mambo ya Ulimwengu wa roho.

Hata ukuu wa wilaya tu imekuwa ishu? wanapata watu ambao wanaonea wivu wenzao wanaoinuliwa na Mungu, yaani mtu anataka ampangie hadi Mungu kwamba fulani anapaswa kuwa maarufu na mwingine hatakiwi.

Matendo yetu yawe mema au mabaya yana reflect maisha yetu ya baadaye.
Tuwe makini sana na tujae hofu ya Mungu .

cc:mshana jr

Makala ijayo😀ini ni Ugonjwa wa akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu hachagui ukoo kutuma ujumbe wake bali huchagua mtumisihi wake.
 
Mkuu Nyerere na Mandela wote ni mashujaa wa Africa wenye historia na kazi tofauti ktk kuleta uhuru.
Sasa inashangaza humu kuona watu wanamdharau Mandela Kama Makonda hadi kusema hajafanya lolote

Bila Mandela South Africa ingekuwa huru?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi ninadhani wewe pia unakosea, wakati tunawapa heshima wanaharakati hawa, si vyema kuwachukulia kuwa wao ni kila kitu.Kwa mfano, mimi ninatifautiana na wewe unaposema bila Mandela South Africa isingekuwa huru. Ninaamini ingekuwa huru ,maana kuna wanaharakati wengi sana walifanya kazi pengine zaidi ya Mandela.Hebu fikiri miaka 20+ alipokuwa gerezani, nani aliendesha harakati? Harakati zilisimama?Japo kuna vigezo vingi vilivyochangia Mandela kutoka gerezani,unadhani fighters wenzake hawakuchangia kutoka kwake,japo kwa kelele na misukosuko?

So, hisia zetu juu ya watu hawa,zisitufanye tukatoka kwenye uhalisia, si Nyerere,Si Mandela, Si Obote, Si Kwame..n.k. wote hawa walifanya kazi kwa kushirikiana na watu fulani, sema kama ilivyokawaida mkiwa wawili na zaidi, mmoja atachomoka na kuonekana zaidi.
 
Nyie mnachekesha kweli? Hakuna la maana alilofanya Mandela Africa?
Kukaa jela miaka 27 unaona ni jambo la kawaida?
Mandela alipoteza mke, watoto na ndugu akiwa jela, aligoma ofa zote za makaburu akachagua kufia jela ili South Africa iwe huru, halafu leo useme hajafanya kitu?
Wewe ukifungwa miezi 6 utaomba pooo... Halafu leo umdharau Mandela?
Unachekesha kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Umewahi kujiuliza miaka michache alikaa Robin Island, Je Mingine alikuwa wapi? Kwanini alimtaliki Winne? Je yeye na Gracia walikutana lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanganyika ilipata uhuru wa mezani, nchi ilikuwa chini ya usimamizi wa muingereza ili tukiwa tayari tupewe uhuru wetu (wa mezani). Madiba ni chuma kweli kweli, nyerere huyuhuyu angekuwa msouth africa asingeweza kupigania uhuru wa kule, labda angekuwa mpigania uhuru wa level ya kati na sio kinara. Mkabulu alikuwa hatanii, ni majasiri hasa ndo walioweza kupambana nae. Na sio nyerere tu bali hakuna mtanzania yeyote ambaye angeweza kufurukuta mbele ya style ya upiganiaji uhuru ya afrika kusini labda tundu lisu.
Sasa kama jiwe na ndugai waswahili wenzetu tu wametubana na hatufuruti, hakuna cha mbowe, zitto, shein, makamba, maalim seif, Sirro, Bashiru, mabeyo, nk wote jiwe katukalisha tunafuata maelekezo yake badala ya sheria na tumekubali kuufyata. Sasa jiulize ungekuwa mziki wa mkaburu je?!
Jamani kufanya harakati za uhuru chini ya kabulu ilikuwa hatari mno, wao waswahili wa daressalaam wasingefua dafu. Mandela na wenzake walikuwa vyuma kwelikweli. Kwa kifupi wa afrika kusini wa zile siasa za kijasiri ndo maana walifanikisha, hata kichofanywa kwa rais mbeki na rais zuma kibongobongo haiwezekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikuita mjinga nitakupa hadhi, wewe ni mpumbavu hasa, Mandela aliwapa wazungu sh ngapi ili wampaishe?
Na wazungu walipata faida gani kumpaisha Mandela?
Pathetic zero brain!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa mada napenda nyuzi zako sana. Ila ushauri wangu usiwe mkali na kutukana watu unaona wapo against you.
Kuwa kama The Bold, yeye akisemwa mbovu mara nyingi hujibu kwa hekima tu, au hakujibu kabisa, anapita zake kujibu wengine
 
Mandela kapaishwa na wazungu huwezi mfananisha na Mwl.Nyerere hata kidogo
....kafanya nini cha maana kwa Africa huyo Mandela ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Things happen for a reason. Nyerere was ahead if his time. Europeans did not want Africans to have an emulated role models, with strong figures, with a well balanced mind like Nyerere
 
Mada hii imenipa picha kubwa mno ya ubongo wa kizazi hiki cha nyoka ndo maana kweli kuna ma PHD Holder wanaita Air hostess -Air hostage.
Kwa akili zenu hizo nchi haiwezi kufika popote ,yaani hujui mchango wa Mandela ktk bara la Africa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe mwenye ubongo ulio smart onesha huo mchango wa Mandela unaouzidi mchango wa Nyerere kwa bara la Afrika

Hapo ndo tutaweza kukutofautisha na kizazi unachokiita cha nyoka vinginevyo maneno pekee bila ushahidi nawe utaonekana kuwa miongoni mwa hao hao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ma zero brain mko wengi kiasi hiki?
Nyerere alipigania uhuru na nani? alipigania uhuru peke yake South Africa kisha akaenda South Africa na kuwa Rais wa huko?
Yaani mnam treat Mandela Kama mdoli flani hivi, kukaa gerezani miaka 27 siyo kupigania uhuru? alikuwa Hotel hiyo miaka 27 akila bata?
Nyerere angetoa wapi nguvu za kupigania uhuru bila kuongozwa na kina Mandela?
Nyerere alikuwa anatoa sapoti tu ya kupigania uhuru wa South Africa, huku Mandela aki risk maisha yake na wenzake wengi kuuawa.
Nyie watu vichwa vyenu zero brain kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana, kwa hiyo hapo ndo unajiona unaakili sana! Kwamba kwa vile Mandela alikaa gerezani ndo anamchango mkubwa kwa bara la Afrika kuliko Nyerere?

Dalili ya mtu asiye na akili ni kama hizi unazozionyesha hapa! Badala ya kutoa ushahidi umekazana kutoa matusi huku ukisahau wanaokusona wanaendelea kuthibitisha ubwege ulionao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa unachemka mkuu; usidhani unafahamu kila kitu ndugu, huu ni ulimwengu wa sayansi jamii; mitazamo, uzoefu na mazingira uliyokulia vina umuhimu mkubwa katika mjada uliouanzisha.

Watu wengi tunawakubali mashujaa wetu ambao kwa namna moja ama nyingine waliiletea heshima bara letu. Hili la Mandela vs Mwalimu, huhitaji kukaza misuli ya shingo, kuna ukweli mkubwa Mandela anaweza asimpate Mwalimu. Labda tuweke vigezo ndiyo tutaelewana. Huhitaji kutukana au kudhihaki ili uonekane bingwa, hapa tunajifunza tu. Mfano, wa vigezo ni:

1. Eneo ambalo kila mwanaharakati kati ya wawili hawa walifanya harakati zao. Kumbuka Nyerere ana mchango pia katika kuwasapoti kina Mandela. Mpaka leo waafrika kusini huja kuzuru kambi kama Mazimbu na Dakawa, zote zikiwa ni kambi za wanaharakati wao wakijipanga kwenda kukomboa nchi. Si, Afrika ya kusini pekee, ni nchi nyingi Tz ilifanya haya, mfano, Msumbiji, Zimbabwe n.k

Hapo juu unamshambulia mchangiaji wa mada yako eti Mandela ana nini cha kuwapa wazungu. Hujiulizi kwa hiki Nyerere alikifanya, kama kweli wazungu ni wakweli huoni Nyerere alipaswa kupata tuzo zaidi ya Mandela? Kwa kifupi, hatubezi juhudi za Mandela lakini ule umaarufu ulitiwa chumvi na wazungu kwa sababu zao binafsi. Kumbuka huyu ndiye alikuwa gaidi kwao hadi kumyima viza kuingia nchi zao lakini baada ya kukubaliana namna ya kuindesha Afrika ya kusini bila kuwadhuru wazungu na mali zao akageuka shujaa wa kimataifa.

2.Kigezo kingine ni kukaa madarakani huku ukiendeleza nchi yako na kusaidia wengine. Sote tunajua alichofanya Mandela, kuanzia muda aliokaa madarakani na hata kile alichokifanya ili kuwakomboa raia wa Afrika ya kusini kiuchumi. Fine, hapa hatuwezi kumlaumu kulingana na mazingira ya taifa lao, mpaka leo bado kiuchumi weusi wenyeji ni bilabila. Lakini huwezi kulinganisha na Tz, pamoja na wanasiasa kutufanya vibaya, bado hali zetu si sawa na wazulu. Ninarudia, hili si la kumlaumu Mandela, ni historia yao ndiyo imewafikisha hapo. Lakini kwakuwa tunalinganisha, basi tutumie kuwatathimini wote iwe ni sababu binafsi au za nje yao.

Aidha, pamoja na sifa nyingi tunazowapa watu hawa, huwa tunakosea sana kuona ama kufikiri hawa watu walikuwa peke yao. Wengi hulalamika kuhusu Mwalimu na namna alizima nyota za watu walioshiriki kuliletea taifa uhuru na heshima. Inashangaza sana vijana tunafunzwa na kukaririshwa Mwalimu peke wakati kuna wanaharakati wengi tu, wengine mwalimu aliwakuta wakiwa washakinukisha. Hata Afrika ya kusini ni hivyohivyo, wapo wengi saaaana waliofanya pengine hata zaidi ya Nelson. Lakini hao ndiyo nyota zao ziling'aa, wakatokelezea. Ni jukumu letu sisi wachambuzi, kuyajua haya na kuweka rekodi sahihi kuliko kushambuliana mradi tu fulani awe mshindi.

Kuhusu wanaharakati na kufaidi ama kutofaidi maisha kiasi cha kusema Mwalimu alimkosea nini Mungu, kuna ukweli kabisa ukiwa mtu si wa kutamani ufahari basi maisha yako hayawezi kuwa hivyo. Pamoja na mapungufu ya Mwalimu kama hayo niliyogusia hapo juu, kwa uoni wangu, hakuwa mtu mwenye tamaa ya maisha hayo pengine mimi na wewe tunaona ni ndiyo maisha.Lakini ujue, aliwajengea watoto msingi mzuri tu, namba moja ikiwa ni elimu. Sisi tunataka mtu kama yeye afuje mali, alazimishe watoto kuwa mawaziri na wakuu wa majeshi, wamiliki midege n.k, huku hatuna vitanda vya wagonjwa, hakuna sehemu za kina mama kuzalia, watu tunakufa njaa n.k., hapo ndiyo tunaona haki inatendeka kwa watu wa kaliba hiyo. Huu si uungwana!

Asante
Naamini atakuwa amekuelewa vizuri, tatizo ni pale mtu anaanzisha mada halafu anaamini anachokiamini yeye ndo mwanzo na mwisho

Ndugu yetu huyu anahisi kejeli anazomwaga hapa ndo zitafanya watu waamini anachokiamini

Facts kama hizi ndo zinatakiwa na sio bla bla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Nyerere na Mandela wote ni mashujaa wa Africa wenye historia na kazi tofauti ktk kuleta uhuru.
Sasa inashangaza humu kuona watu wanamdharau Mandela Kama Makonda hadi kusema hajafanya lolote

Bila Mandela South Africa ingekuwa huru?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujielewi wewe, watu hawajasema Mandela hajafanya lolote, watu wanakupinga unaposema Mandela anamchango mkubwa KULIKO Nyerere kwa bara la Afrika . Hapo ndo unapotakiwa kuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom