Hivi ilikuaje mwl Nyerere hakumpa heshima hii Mugabe?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,971
Reaction score
14,538
Habari wanaJF wenzang

Mwl Julius K. Nyerere aliwapenda na kuwaheshimu wapigania Uhuru wote wa Bara letu la Africa.

Katika kuonesha heshima na upendo huo kwao, mwl Nyerere aliamua baadhi ya barabara na mitaa ya nchi yetu kuipa majina ya wapigania Uhuru hao wa nchi zetu za Africa.

Hapo chini ni baadhi ya barabara au mitaa iliyopewa majina ya wagombania Uhuru hao wa kiafrica.

Mandela road, Sam Nujoma road, Azikiwe road, Patrick Lumumba Street, Kwame Nkuruma road, Haile Selasah, Kaunda, Kenyatta nk. Lakini hakuna Robert Mugabe road au Street.

Je ni kwanini Mugabe hakupewa heshima hii waliyopewa wengine?

Tukumbuke ndani ya Harare Centre kuna barabara kubwa sana inaitwa Nyerere road. Ila kwetu hakuna Mugabe road. Je sababu ilikuwa ni nini yeye kuachwa, huku watu wa mbali kama kina Azikiwe wakiwekwa?
 
Habari wanaJF wenzang

Mwl Julius K. Nyerere aliwapenda na kuwaheshimu wapigania Uhuru wote wa Bara letu la Africa.

Katika kuonesha heshima na upendo huo kwao, mwl Nyerere aliamua baadhi ya barabara na mitaa ya nchi yetu kuipa majina ya wapigania Uhuru hao wa nchi zetu za Africa.

Hapo chini ni baadhi ya barabara au mitaa iliyopewa jina la wagombania Uhuru hao wa kiafrica.

Mandela road, Sam Nujoma road, Azikiwe road, Patrick Lumumba Street, Kwame Nkuruma road, Haile Selasah, Kaunda, Kenyatta nk. Lakini hakuna Robert Mugabe road au Street.

Je ni kwanini Mugabe hakupewa heshima hii waliyopewa wengine?

Tukumbuke ndani ya Harare Centre kuna barabara kubwa sana inaitwa Nyerere road. Ila kwetu hakuna Mugabe road. Je sababu ilikuwa ni nini yeye kuachwa, huku watu wa mbali kama kina Azikiwe wakiwekwa?
Sijui lakini mugabe alimkubali sana Nyerere mpaka kuandika kitabu kumshukuru
 
Ni kweli kabisa. Hakuna mtu ambae alipewa heshima kubwa na Mugabe kama Nyerere.

Ni Mugabe ndie aliehakikisha lile jumba la Umoja wa Africa kule Ethiopia linapewa jina la Julius Nyerere ili kumuenzi kwa mchango wake mkubwa wa kupigania Uhuru wa Africa.
 
Back
Top Bottom