Nyerere alimkosea nini Mungu?

Nyerere alimkosea nini Mungu?

Nyerere Alikuwa
Ana,Mabalaa mengi damu za watu wengi zinamlilia.
Nafsi Yake Haina Utulivu kuzimu

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais yoyote yule wa Africa lazima damu za watu zimlilie, kuna watu huuliwa na serikali ili nchi ipate amani, kwa mfano kule "kiberiti". hata Marekani Bush na yule aliyepeleka wanajeshi vietnam, wakifa watakutana na nafsi za watu zinawalilia
 
Twende Youtube tutafute channel ya Divistar Mata kuna aliyekuwa mkuu wa wachawi Tanzania sheikh Omari Mnyeshani wa Tanga ameeleza siri kuu kuanzia jina Tanzania,tambiko la nchi la kwanza la Bagamoyo lililoleta mwenge chini ya Foroje Gonze 'Master' ,Sheikh Yahya Hussein mnajimu na wengine na tambiko la pili la nchi la Lindi.
 
Mtoa mada unakosea Sana kusema Mandela Yuko above Mwalimu Nyerere, fatilia mahojiano au documentary ya huyo Mandela uone kamuongelea vipi mwalimu Nyerere

Wakati we umekaa hapa kupaza shingo kumtetea Mandela ila Mandela alikuwa anamuita mwalimu Nyerere kuwa ni Father of Africa
mandela was humble.
 
Watoto wa Nyerere hawana shida mnazo dhania ni ufahari.

Siasa ni shida kijana usione mtu yuko jukwaani.sijui UNO.Mara AU ana bwabwaja ukaona hewala. hawalali wale...ooohooo!!!

Mkituona tunapita na ulinzi mkaliii mnafurahia mnatamaniiii.sometimes wengine wanasema tunalinga.kujisikia nk.

Sometimes baada ya kupiga domo jukwaani Unaweza ambiwa usirudi huku. kaa hukohuko!! Km yaliyompata Nkurunzinza.. Obote nk

Sasa shida zoote hizi za nini hizi wkt nakula bure ,safari.heshima bure??

Zawadi na Ubora wa Nyerere.
kipaji.
uwezo.
maarifa.j
juhudi zinaweza tokea hata kizazi cha saba mbele huko..

Hawa wa sasa ni mayai mayai japo wanajitahidi sana.km Makongoro.fatma. Mwinyi mdogo nk muwaache!!ndiyo.

tuliwahi sema huko nyuma siasa mchezo mchafu tena mnooo!!!

Kipaji cha Babako kinaweza kisiwe chako au ukawa nacho pia.
omba Mungu akufunulie chako cha tofauti. Siyo muwe na mwendelezo huo tuuuuu.wote!!

Mleta mada usikariri. MWana marundi yuko wapi? kipaji chake alikufa nacho!!
Nani walirithi vipaji vya hawa wafuatao??.
Milambo Tabora.
Mkwawa, Iringa
Mangi sina wa Moshi
unawajua??

Elewa tu kipaji hakirithiwi, kinagunduliwa, waroto wa Nyerere ni wala mayai tangu kuzaliwa unataka wapigike kisiasa ?

Umaarufu wa siasa unagusa maisha ya watu. kuna hati hati nyingi sana. Ufe au upone!! Yaani unacheza na hatari.Kukimbia kimbia km Mbowe.

Sasa unakula bure mpaka kufa nika. Hatarishe maisha yangu kwa nini??

Siasa Duniani kote. ni mchezo hatari mno. km huamini muulize Lisu! Yaani Mpaka leo anachakaa bila kupigwa na jua.

Nyerere kapitia hatari ngapi mpaka leo mnamsifu kirahisi ivo.
km baba mwenye mapenzi atakubali mwanae acheze na hatari??

Wanae wanajua walivokuwa Matumbo joto kwa wkt mgumu wa kutaka kupinduliwa baba yao tena mara nyingi tu.leo wafanye hayo hayo??

Kwanza wamekuliamo hawaoni ni issue kiviile! Ila wewe...
Yaani waingie tu kichwa kichwa sababu ya kuendeleza historia wanayo ijua vyema??

Zanga Mobutu yuko wapi si kakimbia yule!! Kaacha mshahara.
Haile selasie watoto wote waliuawa tena Ndani ya London.kizazi kilifutwa kile.kiranga cha siasa.

Indira Gandhi huyu ni futa kabisa kizazi hicho.kamebakia katoto kajukuu. ka Rajivu Gadhi nako kanaogopa kuuawa na Masingasinga km kakithubutu kufanya siasa.

Wezi kaunda mjeda huyu: alikuja juu kisiasa mbona walimzima faster tu. Hata maji hakuomba.yuko wapiii kafa kitambooo! Alizaliwa ikulu akasomea nje shule classic.

Namibia wamemjengea kaunda nyumba bure na familia yake si angekaa huyu marehemu akala bata?

Ambitions za baba siyo zangu, mie ni mzee wa bata tu. Baba aliniandalie nife vizuri ..then nikajiue live??

Vitaibuka vitukuu huko mbele! vitafanya siasa.
mie zangu bata!! bata na mimi.

Bado watawala wa sasa wanatuheshimu Maisha yangu yote.then nikasotee siasa?? unaumwa wewe???

ukitaka somea mengine kabisa!! Hawa watoto wakienda nchi yeyote ya SADACC wanapewa kipaumbele sana. Hata tender ya kuuzia nchi husika siraha halali.

Museveni huyo hapo anamtunza Mama si kawaida na Marais weeengi wengine wanaheshimu familia yangu ajili ya Baba yangu.

Halafu km haitoshi nikajitoe sadaka kwa wachamba wima mweeee!!
Mwitongo patatunzwa na nani?

Leo Mwitongo ni mahala pa kumbukumbu kwa sababu tupo sisi vijana wa nyerere tuna toa miongozo ya kupatunza ili mje na wwngine waje.

Hii ikiwa ni pamoja na kutunza afya ya Mama.

Maana yangu ni kuwa Mama anajua hatari za Siasa kwanini nimuue mapema Mama yangu kipenzi ajili ya pressure za siasa weee!!

Mleta mada hujui uchungu wa Mama weye??? Fikiria Mama yake Binti F karume, au Lisu kwa yaliyo mpata mwanae!!! km hakuharisha, Bp yule bahati....

Sasa huyo ni ***** Lisu.Maria nyerere ameiishi siasa tangu akiwa kijana. Leo Akubali wanae waingie kwenye mchakamchaka tena akiwa bado hai.ili kuwa furahisha watu flani...
Haille kumbe ndio yaliyomkuta kizazi chake
 
Twende Youtube tutafute channel ya Divistar Mata kuna aliyekuwa mkuu wa wachawi Tanzania sheikh Omari Mnyeshani wa Tanga ameeleza siri kuu kuanzia jina Tanzania,tambiko la nchi la kwanza la Bagamoyo lililoleta mwenge chini ya Foroje Gonze 'Master' ,Sheikh Yahya Hussein mnajimu na wengine na tambiko la pili la nchi la Lindi.
Uko sawa kabisa mkuu ..huyo Gonze alitabiri Hadi tarehe na mwaka ambao Nyerere atakufa wakati huo ccm kukiwa na miaka kadhaa ..
 
Nyerere kaondoka Duniani akiwa kaacha heshima kubwa mno kimataifa.
Wanasiasa wa Tanzania wamekuwa hawaachi kumtaja huyu Mzee kila mara kwenye kampeni au hotuba zao.

Alimshauri rafiki yake mkubwa hayati Nicolai Cesesscue enzi za uhai wake akiwa Rais wa Romania aachie ngazi ili kulinda heshima yake ,Nicolai hakusikia matokeo akaja kuuawa kikatili yeye na mkewe.

Alimshauri Kaunda wa Zambia naye hakusikia, "mzee mwenzangu waachie Vijana ulinde heshima yako ".

Kaunda akapuuza ushauri wa Nyerere matokeo yake akaja kuondoka Kwa aibu ya kushindwa uchaguzi, badala ya kustaafu, yaani Rais wa kwanza wa nchi unagombea tena, what a shame?

Heshima ya Nyerere Kwa Africa inazidiwa na Mandela tu, ukimtoa Mandela hakuna Rais tena wa kufananishwa na Nyerere ktk bara la Africa.

Kwanza alikuwa akiaanza kuongea unatamani uendelee kumsikiliza tu muda wote hata Kama ulikuwa na stress Ukisikiliza hotuba za Nyerere stress zinapungua.

Ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Africa huwezi kuujadili bila kumjadili Nyerere ambaye ndo alikuwa key point ya Ukombozi Huo.

Ni katika Kipindi cha Urais wake Tanzania iliheshimiwa na hata kuogopwa na mataifa makubwa Duniani.

Pamoja na matatizo ya hapa na pale, lakini enzi zake uchumi wa Tanzania ulikuwa juu, pesa ilikuwa na thamani kubwa, noti ya mwisho Kwa thamani kubwa ilikuwa noti ya sh 100.

Elimu ilikuwa juu, siyo kama leo hii ambapo hata kiswahili tu kinawapa shida hata wahitimu wa vyuo vikuu, neno "hela " wanatamka "ela" neno "halafu "wanatamka "alafu " eti hao ni university graduates, kwenye English ndo unaweza hata kulia Kwa namna wanavyoboronga.

Enzi zake hata intelligence ya nchi ilitisha, TISS ya Nyerere haikuwa tofauti na CIA hutaki kuamini acha.

Wakati wa vita vya Kagera, TISS ilimzunguka Idd Amin Spain, alikuwa ameagiza makombora ya kisasa yenye nguvu lakini akajikuta anayakosa na yakaangukia mikononi mwa Tanzania.

Hatukuwa na silaha Kali Kama za Idd Amin, lakini tulikuwa na intelligence imara mno, hii ndo ilifanya tushinde vita bila msaada wa nchi yoyote, Idd Amin pamoja na kusaidiwa na Gaddafi bado tuliweza kumtwanga hadi akaikimbia Uganda.
Inahitaji Kitabu kuandika mambo mazito aliyofanya Nyerere.

Lakini alimkosea nini Mungu huyu mzee?
Mwandishi Munga Tehenani (RIP) aliandika Kitabu kiitwacho "Nyerere alikuwa mchawi ".
Kitabu hiki hakikukaa mitaani hata siku tatu kikawa kimepotea kimaajabu, ilikuwa ni kati ya mwaka 2001 au 2003.

Inadaiwa aliingia maagano na kuzimu na fimbo yake ndo ilikuwa muongozo wa mambo yake yote.

Maagano yoyote ya nguvu za giza humkasirisha Mungu na kukilaani kizazi cha mtu aliyeingia maagano hayo.

Mungu hulaani kuanzia watoto na hata vitukuu na vilembwe na hata kizazi cha nne.

Familia ya Rais Kennedy wa US aliyepigwa risasi mwaka 1963 imepukutika yote Kwa vifo vya ajali na kuuawa, hakuna alama yoyote ya Kennedy Marekani, yamebakia majina tu.

Nikiitazama Kwa jicho la tatu familia ya Nyerere haiko sawa, imefunikwa na giza nene, haing'ai, haionekani, it looks like Nyerere left no children to walk his ways,haya ni mambo ya Ulimwengu wa roho.

Hata ukuu wa wilaya tu imekuwa ishu? wanapata watu ambao wanaonea wivu wenzao wanaoinuliwa na Mungu, yaani mtu anataka ampangie hadi Mungu kwamba fulani anapaswa kuwa maarufu na mwingine hatakiwi.

Matendo yetu yawe mema au mabaya yana reflect maisha yetu ya baadaye.
Tuwe makini sana na tujae hofu ya Mungu .

cc:mshana jr

Makala ijayo😀ini ni Ugonjwa wa akili




Sent using Jamii Forums mobile app
wewe mwenyewe ulimkosea nini Mungu mkuu
kwanu uongozi ni suala la kurithishana au la ukoo
wewe ukoo wenu una nini katika muktadha wa uongozi au umaarufu katika nchi yako
 
Back
Top Bottom