... Mleta mada kabla sijaanza kuchangia mada hii naomba uombe RADHI kwa Watanzania na waafrika kwa ujumla kwa kumfananisha Mwalimu Nyerere na Nelson Mandela.
... Unafananisha mtu ambae alijitoa kwa ajili ya Waafrika na mtu ambae alikuwa kibaraka wa wazungu, unafananisha watu wawili kabisa, mtu aliyechukia ubaguzi na mtu aliyeacha nchi yake ikiwa na mizizi mikubwa ya ubaguzi.
... ANGALIZO: Ukiona Mzungu anakusifia sana wmafrika ujue una maslahi nae, Mandela alikuwa na Maslahi na Wazungu.
Hayati Julius Nyerere ni moja kati ya viongozi bora kuwahi kutokea katika Taifa hili na Afrika kwa Ujumla, achana na hawa wendawazimu wanaowahadaa watanzania mara sijui kutengua mikataba ya madini, kupambana na ufisadi, maisha bora, mara sijui viwanda n.k HAWA WOTE NI WEZI NA NI WANAFKI WAKUBWA, HAKUNA ALIYEMSAFI HATA MMOJA KATI yao kwa misingi ya Haki, Umoja, Upendo, Mshikamano, Uaminifu, Uwazi na Ukweli.
Ulimwengu umegawanyika katika sehemu Kuu mbili, Wa kiroho na Kimwili, Nyerere alijenga hii nchi katika weledi mkubwa uliotukuka kwa nchi kutokuwa na matabaka, ukanda, ukabila, dini, ubaguzi, ufisadi, unafki n.k na kitu ambacho Nyerere alifeli mpaka anaachia hii nchi ni katika mambo makuu mawili
1. KATIBA - Hayati alitambua kabisa kuwa Taifa lina katiba mbovu mbovu mbovu kupindukia ila akaona ni bora atuachie hiyohiyo wananchi na kwa kiongozi anayemfuata, kama yeye aliona aliweza kuiendesha katiba vyema, kwanini aamini wote watakaofuata nao watafuata nyayo kama zake? Aliwahi kutamka pia kwa katiba hii endapo akatokea mtu sio mwaminifu basi ataitumia vibaya, kama alilijua hili mapema, iweje asingeibadilisha kama alivyopoka uhai wa Tanganyika kwa amri na kuifanya kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Leo hii tuna Marais wa ajabu na wanaendesha nchi kiajabu kutokana na kuwa na Katiba MBOVU KABISA.
2. MISINGI IMARA YA UONGOZI NDANI YA CCM: Miaka ya nyuma kabla ya kuondoka duaniani aliwahi kuwakataa waatu hawa wawili waziwazi, JAKAYA MRISHO KIKWETE NA EDWARD NGOYAI LOWASA kwa kashfa ya WIZI {UFISADI}, Mwalimu alishindwa nini kuwaondoa hawa vijana ndani ya Chama? Leo hii haw watu wameingiza nchi ktk madeni na Umaskini wa kutisha huku Familia zao zikiend ulaya zitakavyo na kujimilikisha mali za kutisha na kuishi maisha ya anasa. Wanatujengea hospital wakati wao na familia zao hawatibiwa ndani ya hizo hospital, wanajenga shule wakati watoto wao wanasoma ulaya n.k HOVYO KABISA VIONGOZI WA CCM.
... Tukirudi katika upande wa kiroho, Mwalimu Nyerere katuingiza katika maagano ambayo kila mtawala wa Tanzania anapaswa kuenenda nayo na wanapswa kuenenda nayo sababu hawaingii kwenye kiti cha Urais kwa njia ya Mungu ila kwa ushirikina. Kitu chochote kwa kwanza ni kama lango ndani ya eneo husika au familia husika, iwe familia, nchi n.k kwa mujibu wa Imani ya Kikristo.
... Lango kazi yake ni kupitisha mambo flani, iwe ni mazuri au mabaya, je Mwalimu hayati alipitisha nini yeye kama Lango la Tanzania katika Ulimwengu huu wa Kiroho? Frankly Speaking hii nchi kiroho malango yake yanapitisha uharibifu mkubwa kuliko mema, kwa kuwa ni mambo ya kiroho ninaona nisizungumze mengi sababu ya wengi kutoamini mambo ya rohoni.
Eeeh Tanzania! Ewe Tanzania, kwanini wajivika shuka la amani ionekanyo kwa namna ya macho ila ndani mwako umebeba UHARIBIFU? HAUNA AMANI TANZANIA UNAYOJIVUNIA, Ulikotoka Muasisi hajataka kuacha maandishi, Uendako Tanzania wenye machoni ya rohoni wanatazama ni kubaya mno, tena sana na kwatisha haswa.