Nyerere alijua Katiba ni mbovu lakini hakutaka kuibadilisha. Ni wakati sasa umefika ili Taifa liendelee linahitaji Katiba Mpya

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Nyerere alikubali kutengeneza system ya kidikteta ambayo tumeirithi, system ambayo haijaandikwa popote kwenye katiba, kwamba ili rais awe na nguvu (power) lazima avae kofia mbili ya chama na ya serikali.

Nyerere aliwahi kusema katiba hii inamapungufu mengi inampa rais nguvu kubwa ya kuweza kuwa hata dikteta lkn pamoja na kuyajua hayo hakuwahi kuchukua hatua zozote za kutatua changamoto hizo.

Mfano, Katiba inataja mihimili mitatu Serikali, Bunge na Mahakama inayojitegemea lkn wakati huo huo Katibu wa bunge na majaji wa Mahakama wanateuliwa na rais.

Pamoja na mazuri ya katiba ya sasa lkn haikidhi kabisa mahitaji mengi ya msingi ya nchi na mwananchi, hasa kwenye eneo la utawala, matatizo tuliyonayo ya kiuongozi mengi yanasababishwa na ubovu wa katiba.

Hatuwezi kumlaumu sana Nyerere labda aliamua hivyo kutokana na hali halisi ya kisiasa ya wakati huo pengine hali hiyo kwa sasa haipo.

Ni wakati mwafaka sasa umefika ili taifa letu lisonge mbele kiuchumi, kijamii na kisiasa watanzania kwa pamoja lazima tuamue kuwa na katiba mpya na sio katiba mpya tu bali iwe katiba bora.
 
Nyerere alikubali kutengeneza system ya kidikteta ambayo tumeirithi, system ambayo haijaandikwa popote kwenye katiba, kwamba ili rais awe na nguvu (power) lazima avae kofia mbili ya chama na ya serikali.

Nyerere aliwahi kusema katiba hii inamapungufu mengi inampa rais nguvu kubwa ya kuweza kuwa hata dikteta lkn pamoja na kuyajua hayo hakuwahi kuchukua hatua zozote za kutatua changamoto hizo.

Mfano, Katiba inataja mihimili mitatu Serikali, Bunge na Mahakama inayojitegemea lkn wakati huo huo Katibu wa bunge na majaji wa Mahakama wanateuliwa na rais.

Pamoja na mazuri ya katiba ya sasa lkn haikidhi kabisa masuala mengi ya nchi, na matatizo tuliyonayo ya kiuongozi mengi yanasababishwa na ubovu wa katiba.

Hatuwezi kumlaumu sana Nyerere labda aliamua hivyo kutokana hali halisi ya kisiasa ya wakati huo pengine hali hiyo kwa sasa haipo.

Alichokifanya Nyerere ni kucheza na akili za watu anakupa kwa mkono wa kulia na kukupora kwa mkono wa kushoto, si kwa kwamba alikuwa hajui anachokifanya.
 
Ni kukosa weledi kutaka kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa yaliyofanyika enzi zake kwa yanayotokea leo. Ni wapi aliposema katiba haiwezi kubadilishwa? Ametoka madarakani muda mrefu, bado unatafuta njia ya kumleta leo ili uweze kutoa lawama kwake?

Hiyo katiba ilikuwepo kwa wakati huo, bila shaka kwa sababu maalum ambazo leo hazipo, bado wewe unang'ang'ania awe yeye ndiye abadilishe katiba inayofaa kwa wakati huu? Huoni upungufu wa hoja zako?
Hivi hawa wanaotawala sasa na wanaoshikilia hiyo katiba, wanatawala kwa niaba ya Mwalimu Nyerere?

Hata hivyo, tukiachana na hizo lawama zisizokuwa na msingi, tutengeneze katiba tunayoitaka, ni jambo jema, lakini pia ni kukosa dira kutegemea kwamba kuwepo tu kwa katiba nzuri ndipo tutakapopata maendeleo.

Katiba nzuri inakuwa nzuri inapotekelezwa matakwa yake; na sio lazima kuwepo tu kwa katiba hiyo ndipo maendeleo yawepo.
 
Katiba itabadilishwa siku jeshi litakapochukua nchi na kuwachinja madhalimu wote wenye vinasaba vya ccm, tukianza na Ndugai, PM, Mawaziri, manaibu nk, hivi hivi hawa ccm hawawezi kukubali vile wameshajua watanzania ni waoga wanatelezea humo humo
 
Nyerere alikubali kutengeneza system ya kidikteta ambayo tumeirithi, system ambayo haijaandikwa popote kwenye katiba, kwamba ili rais awe na nguvu (power) lazima avae kofia mbili ya chama na ya serikali.

Nyerere aliwahi kusema katiba hii inamapungufu mengi inampa rais nguvu kubwa ya kuweza kuwa hata dikteta lkn pamoja na kuyajua hayo hakuwahi kuchukua hatua zozote za kutatua changamoto hizo.

Mfano, Katiba inataja mihimili mitatu Serikali, Bunge na Mahakama inayojitegemea lkn wakati huo huo Katibu wa bunge na majaji wa Mahakama wanateuliwa na rais.

Pamoja na mazuri ya katiba ya sasa lkn haikidhi kabisa masuala mengi ya nchi, na matatizo tuliyonayo ya kiuongozi mengi yanasababishwa na ubovu wa katiba.

Hatuwezi kumlaumu sana Nyerere labda aliamua hivyo kutokana hali halisi ya kisiasa ya wakati huo pengine hali hiyo kwa sasa haipo.

Ni wakati mwafaka sasa umefika ili taifa letu lisonge mbele kiuchumi, kijamii na kisiasa watanzania kwa pamoja lazima tuamue kuwa na katiba mpya na sio katiba mpya tu bali iwe katiba bora.
Hakuna Mwanasiasa asiyeipenda hiyo katiba ya mwaka 1977. Hata CHADEMA ikitokea wakapata madaraka kupitia katiba hii hii, sahau katiba ya Warioba.

Katiba ya wananchi itapiganiwa na wananchi wenyewe kama ilivyotokea Zanzibar na Kenya. Hakuna mwanasiasa wala chama cha siasa kinachoweza kutoa katiba ya wananchi.

Kwa lugha rahisi hakuna mwanasiasa anayependa kumpa nguvu na madaraka mwananchi. Ukiona chama cha siasa au mwanasiasa analalamikia katiba iliyopo ni kwasababu tu haimpi faida yeye.

Nyerere alitengeza katiba mbovu kwa maslai yake kosa alilofanya ni kutokukumbuka kuibadilisha alipostaafu akiamini akili za watakaoongoza zitafanana.
 
Hakuna mahali mleta uzi amesemea kuwepo kwa Katiba mpya TU ndio kutaleta maendeleo. Sijui kwa nini hili angalizo la straw man argument linapendwa sana na wafahidhina wasiotaka kusikia kabisa suala la Katiba mpya.
Ni kukosa weledi kutaka kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa yaliyofanyika enzi zake kwa yanayotokea leo. Ni wapi aliposema katiba haiwezi kubadilishwa? Ametoka madarakani muda mrefu, bado unatafuta njia ya kumleta leo ili uweze kutoa lawama kwake?

Hiyo katiba ilikuwepo kwa wakati huo, bila shaka kwa sababu maalum ambazo leo hazipo, bado wewe unang'ang'ania awe yeye ndiye abadilishe katiba inayofaa kwa wakati huu? Huoni upungufu wa hoja zako?
Hivi hawa wanaotawala sasa na wanaoshikilia hiyo katiba, wanatawala kwa niaba ya Mwalimu Nyerere?

Hata hivyo, tukiachana na hizo lawama zisizokuwa na msingi, tutengeneze katiba tunayoitaka, ni jambo jema, lakini pia ni kukosa dira kutegemea kwamba kuwepo tu kwa katiba nzuri ndipo tutakapopata maendeleo.

Katiba nzuri inakuwa nzuri inapotekelezwa matakwa yake; na sio lazima kuwepo tu kwa katiba hiyo ndipo maendeleo yawepo.
 
Huo ndio ukweli halisi
Hakuna Mwanasiasa asiyeipenda hiyo katiba ya mwaka 1977. Hata CHADEMA ikitokea wakapata madaraka kupitia katiba hii hii, sahau katiba ya Warioba.

Katiba ya wananchi itapiganiwa na wananchi wenyewe kama ilivyotokea Zanzibar na Kenya. Hakuna mwanasiasa wala chama cha siasa kinachoweza kutoa katiba ya wananchi.

Kwa lugha rahisi hakuna mwanasiasa anayependa kumpa nguvu na madaraka mwananchi. Ukiona chama cha siasa au mwanasiasa analalamikia katiba iliyopo ni kwasababu tu haimpi faida yeye.

Hii katiba chakavu ni ya kidikteta haitupi sisi waajiri kuwashughulikia waajiriwa wasifuje pesa zetu,wasitumie vibaya madaraka,wasipeane pesa zetu zawadi, badala ya kufanya vipaumbele vya wananchi wanafanya vyao.Mwananchi gani alihitaji ikulu mpya, kuhamia dodoma,Chato international,nk.
Hata Mimi sidhani kama miongoni mwa matatizo makubwa ya nchi ilikuwa ni kupata Ikulu mpya.
 
Alichokifanya Nyerere ni kucheza na akili za watu anakupa kwa mkono wa kulia na kukupora kwa mkono wa kushoto, si kwa kwamba alikuwa hajui anachokifanya.
Na Kikwete nae akafanya hivyo hivyo! Ccm ni chama kisicho aminika kwa lolote.
 
Kwanini Lowassa wa CCM hakutaka katiba mpya lakini Lowassa wa CHADEMA alitaka katiba mpya?
Inawezekana kabisa ukiwa ndani ya ccm, akili zinawehuka. Na Membe nae akirejea ccm, utashangaa anayakana yale yote aliyo hubiri alipokuwa mgombea wa Urais kupitia Act Wazalendo.
 
Hoja kubwa sana hii na ndio utaona tofauti ipo wapi ya kuwa ICON au State Strongman!hapo SA hili Rais wao wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia aliliona hili na akalifanyia kazi,Mahakama ya kikatiba ndio Apex ya kila kitu na Majaji wake wanafanyiwa usaili wa juu ili kuweza kutumika kwenye mahakama hii,hapa kwetu Rais wetu wa awamu ya kwanza akiliona hili akaamua to sweep under the rug na kulisemea tu!!
 
Inawezekana kabisa ukiwa ndani ya ccm, akili zinawehuka. Na Membe nae akirejea ccm, utashangaa anayakana yale yote aliyo hubiri alipokuwa mgombea wa Urais kupitia Act Wazalendo.
Issue siyo kuwa CCM wala chama kingine.

Hapo issue ni MASLAHI.

Tanzania vyama vingi hasa vya upinzani ni ngumu kuja kuiobdoa CCM madarakani kwasababu vinaendeshwa kimaslahi sana utafikiri kampuni binafsi.

Vyama vingi hasa vilivyoko kwenye harakati vimekuwa kama sehemu ya MAPATO, AJIRA na STATUS.

Rejea harakati za Uhuru,

Kina Nyerere walipambana kwa kila namna kuhakikisha wanaunganisha makundi yote.

  • Vyama vya wafanyakazi
  • Wasomi vyuo vikuu
  • Jamii ya kimataifa ( Safari za UN)
  • Wananchi
  • Viongozi wa dini
  • Wanaharakati.

Sasa wanasiasa na wanaharakati wengi wa sasa hivi kazi kubwa ni kushutumiana, fulani msaliti, fulani hivi, fulani vile.

Ikifika wakati wa uchaguzi ikitokea chama fulani kimeona kimepata mgombea anayekubalika, basi hakitaki kabisa ushirikiano na wengine.

Kila mmoja anajiona yeye ndiye mwanaharakati au chama bora au sahihi zaidi kuliko mwenzake.

Mimi naamini mabadiliko ya nchi hii yataletwa na wananchi wenyewe.
 
Ni kukosa weledi kutaka kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa yaliyofanyika enzi zake kwa yanayotokea leo. Ni wapi aliposema katiba haiwezi kubadilishwa? Ametoka madarakani muda mrefu, bado unatafuta njia ya kumleta leo ili uweze kutoa lawama kwake?

Hiyo katiba ilikuwepo kwa wakati huo, bila shaka kwa sababu maalum ambazo leo hazipo, bado wewe unang'ang'ania awe yeye ndiye abadilishe katiba inayofaa kwa wakati huu? Huoni upungufu wa hoja zako?
Hivi hawa wanaotawala sasa na wanaoshikilia hiyo katiba, wanatawala kwa niaba ya Mwalimu Nyerere?

Hata hivyo, tukiachana na hizo lawama zisizokuwa na msingi, tutengeneze katiba tunayoitaka, ni jambo jema, lakini pia ni kukosa dira kutegemea kwamba kuwepo tu kwa katiba nzuri ndipo tutakapopata maendeleo.

Katiba nzuri inakuwa nzuri inapotekelezwa matakwa yake; na sio lazima kuwepo tu kwa katiba hiyo ndipo maendeleo yawepo.
Wazo la kuandika katiba mpya halijaanza leo lilikuwepo hata enzi ya Nyerere, 80s jaribio la mapinduzi na 90s wakati wa G55.

Nyerere alikuwepo enzi za Mwinyi na Mkapa aliyajua mapungufu yake sio kuyajua tu aliyasema waziwazi, alikuwa na uwezo wa kushawishi kuyaondoa lkn hakufanya hivyo. Sababu zinaweza kuwa nyingi lkn kubwa ni kutoona chama chake kinapunguziwa nguvu.
 
Wazo la kuandika katiba mpya halijaanza leo lilikuwepo hata enzi ya Nyerere, 80s jaribio la mapinduzi na 90s wakati wa G55, Nyerere alikuwepo enzi za Mwinyi na Mkapa aliyajua mapungufu yake na alikuwa na uwezo wa kushawishi kuandikwa katiba mpya lkn hakufanya hivyo. Sababu zinaweza kuwa nyingi lkn kubwa ni kutoona chama chake kupunguziwa nguvu.
Tatizo letu wabongo tunapenda sana vitu vizuri lakini hatuko tayari kuvipambania.

Tunataka kila kitu kizuri kije miguuni kwetu tukiwa tumekaa, tunakula bata.

Hapa tunataka Nyerere angemaliza kila kitu perfectly ndani ya utawala wake wa miaka 24 ili kazi yetu iwe ni kula bata tu mithili ya mwanaume wa Dar aliyeachiwa nyumba ya urithi.
 
Sio kweli, wanaotuangusha ni viongozi wetu na CCM hawapendi mabadiliko, unaikumbuka katiba ya Warioba ilikuwa kwenye hatua za mwisho watawala wakiongozwa na CCM wakaikwamisha.
 
Back
Top Bottom