Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Hapo juu kuna tatizo siamin kama nyerere alituongezea umasikin wakat nchi alichukua muda ambao uchum uliendeshwa kwa kutumia nguvu na forced labour:ulikuwa ni muda ambao alitakiwa kubadili MENTALITY ya watanzania ktk kuwajibika bola shurti kma mazoea yalivyokuwa...... ilikuwa ni lazm uchumi ushuke .....
Nyerere kafanya makuu mungu hasa ktk kuimarisha umoja na mshikaman na hii ilikuwa njia ambayo ilikuwa sahihi towards development
Tatzo tunashindwa kuelewa kuwa maendeleo sio kitu cha mwaka mmja ni lazm njia kwanza iandaliwe ili maendeleo yawe ''attained"" TUSHINDANE KWA HOJA SIO MATUSI
 
Ukiona kiwanda au benki imeuzwa ujuwe ilishindwa kujiendesha yenyewe na ilikuwa inangoja ruzuku kutoka serikalini.

Viwanda tulivyoweka na kujidai kuviendesha wenyewe wakati hatuna ujuzi lilikuwa ni kosa kubwa la kiuchumi. Tusirudie kosa hilo. Halikadhalika kwa benki.

Hayo mengine yote ni matunda ya misingi mibovu.

usijidanganye kuendesha viwanda lazima uwe na phd, kilichokosekana ni uzalendo tu, na kuanza kuwaona watz wengine siyo wenzenu mlipounda genge la wenye nchi hapo ndipo shida ilipoanza.kila mtu anataka kujirika kutokea ofisi za serikali.
 
usijidanganye kuendesha viwanda lazima uwe na phd, kilichokosekana ni uzalendo tu, na kuanza kuwaona watz wengine siyo wenzenu mlipounda genge la wenye nchi hapo ndipo shida ilipoanza.kila mtu anataka kujirika kutokea ofisi za serikali.

Si kweli. Viwanda vilikufa au vilikuwa hoi bin taabani wakati huohuo wa Nyerere.

Bakhresa ana PhD? Dangote ana PhD?

Hawana.

Huwezi kufanikiwa unapodhulumu.

Kosa kubwa lilikuwa ni hilo, lililopewa jina taifisha.

Au tuchukulie sababu yako ya "kukosa uzalendo". Una maanisha aliowateua Nyerere wote kuendesha viwanda walikuwa hawana uzalendo?

Unafunguwa kiwanda cha nguo huku unazalisha nguo low standard, nani atanunuwa? Ukiizalisha yenye standard bei yako inakuwa kubwa kuliko inavyouzwa duniani, nani atanunuwa?

Serikali kuanzisha wao wenyewe viwanda ilikuwa ni kosa kubwa la kiuchumi. Tusilirudie, tuwaache watu na mashirika binafsi yajifungulie viwanda kwa vigezo vyao, serikali iwape support panapohitajika na wasijiingize katika uendeshaji. Wawaachie wenyewe wakina Dangote waendesha wanavyoona sawa. Kama alivyofanya Magufuli juzi juzi kwa Bakhresa na Dangote. Vile ndivyo inavyotakiwa.

Nyerere alitaifisha akawapa wajomba, mtu anatoka misenyi huko hajaona kiwanda toka anazaliwa, hata choo kaja kukionea alipofika chuo kikuu, anahitimu unampa kiwanda aendeshe! Au unampeleka China anaenda kushangaa huko miaka miwili, anarudi unampa kiwanda aendeshe. Thubutu ufanikiwe.
 
Hizo zote porojo tu.

Hakuna engineer lakini barabara zilipitika, hakuna madaktari lakini watu walitibiwa.

Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kusafirisha mazao nje. Miaka miwili mitatu tu baada ya Uhuru tukaanza kuwa omba-omba wa chakula.

Tanganyika haijawahi kukosa amani na ndiyo maana nchi ikawa na sifa za peponi, mpaka Dar Es Salaam ikawa Dar Es Salaam, unajuwa kuwa Dar Es Salaam ipo kwenye Qur'an na ni peponi?

Ukweli tuuseme kuhusu makosa yaliyofanyika wakati wa utawala wa Nyerere, tutakuwa huru zaidi na kutorudia makosa. Hata Nyerere mwenyewe alikiri kuwa alifanya makosa, seuse sisi tuone hajafanya makosa. Inashangaza.

Mpaka leo tunalia tunataka katiba mpya, kama haina makosa kwanini tunataka katiba mpya? Ulishasikia nchi zenye katiba nzuri zikitaka katiba mpya? USA katiba yao ina miaka mingapi leo? Hiyo katiba ni ya nani? Au huo si msingi aliouweka?
Kila kitu ni udini tuuu,huko shule ulienda kusoma mini bashite wa kike!!
 
Bibi ana hasira na Baba wa Taifa utadhani alimtelekeza. In short sijaona cha kumlaumu JKN ambacho bwana wa FaizaFoxy JMK alishindwa kukirekebisha. Matokeo yake aliacha ya Nyerere ya maana akakomaa naya kijinga.
 
JKN aliweka misingi mizuri sana sana, tatizo lipo kwa waliofata na wanajamii kwa ujumla kwa kuwa na uelewa mdogo
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Nyerere is not a saint, he was human and yes he had his weakness.
But unavyosema kuwa aliongoza nchi kihisia... haha nakushangaa, una any proof kuwa aliongoza nchi kihisia?
The man is dead , why talk about him now?
Hata kama alifanya makosa huko nyuma.. hawa waliokuja baada yake hawakufanya?
 
Ikiwa tutaachana na marehemu waliotutanulia basi leo hii hata itabidi kila kitu tuanze kujifunza upya, sidhani kama hata kuvaa nguo tungeelewa, kwa kuwa wote waliovumbua nguo sasa ni marehemu.

Tulitazame suala hili "positively".

Ikiwa Nyerere mwenyewe kakiri kuwa yeye si malaika na kuna makosa aliyoyafanya katika uongozi wake, mimi nasema tuyatazame hayo makosa ili tusiyarudie.

Nyerere toka aliposema hata yeye amefanya makosa, tumeshawahi kukaa chini na kuona ni makosa yepi ili tusiyarudie?

Mimi nasema, kwa kufata kauli ya Nyerere mwenyewe, tuachane na makosa yake na tuchukuwe mazuri yake tuyaendeleze. Sasa swali linakuja, hayo makosa ni yepi? Naanza na hili moja, ingawa kwa upande wangu yako mengi sana niliyoyashuhudia.

Moja, mie nasema alikosea sana kwenye uchumi.

Wewe unasemaje?

Nchi iliharibika pale alipo achiwa mzaramo , wakaongezeka wapiga dili, makontena yanaingia hayalipiwi kodi, kukawa na easy coming kila kona uchumi ukawa fake mtu kutaja milioni 100 au kuzichezea kwenye birthday sio tatizo, that was totally fake
 
Kila wakati na majira yake, ukimsema Nyerere kama alishindwa basi wewe utakuwa naa matatizo makubwa. Uzi huu hauna maaana wala sioni cha kujadili. Ungesema tujadili mapungufu ya Mwl Nyerere ningeelewa lakini siyo kushindwa kwa Mwl
 
Ndio maana nimekuwa nikiwaambia washabiki wa serikali tatu kuwa likipitishwa hilo tu inabidi tujiulize Nyerere tunamuenzi kwa kipi maana Ujamaa na Kujitegemea tulishaupungia mkono siku hizi tunajivunia misaada na ubepari. Ndio maana tunaona vyama vinavyoahidi mabadiliko vikipokea rundo la pesa toka Ujerumani za kuendesha shughuli zake. Nyerere alihamasisha vyama viendeshwe na michango ya wanachama.

Umoja wa kitaifa ndio kilichobaki ambacho kwa kuleta serikali tatu tunakuwa tumeshauvunja rasmi umoja huo.

Uongozi kwa maslahi ya Umma siku hizi unaonekana ni ushamba na ujinga, uongozi siku hizi ni kwa maslahi binafsi hata wagombea Urais wanaweka vigezo kuwa wahakikishiwe pesa iwapo watashindwa uchaguzi la sivyo hawashiriki!

Je, legacy gani ya Nyerere itabaki?
Serikali 3 Ndo kuvunja Umoja?, mbona mbili hazijavunja?, kama umoja Ni NAMBA ungeshawishi iwe MOJA.....,kukataa serikali 3 kwa sababu ya umoja wa kitaifa hiyo Ni PROPAGANDA ya Chama cha masogange. Tusi-JIBASHITEGE(0) wakati tupo timamu.
 
Hebu fafanua tuijadili vizuri hapo kwenye red, mimi naanza halafu wewe pinga hoja zangu......tujadiliane.

-Madini
Alikuachieni tena kwa ahadi kwamba mtavuna mkiwa teyari

-Elimu
wakati wake JK Nyerere, japo walifaidika wachache lakini wote masikini kwa matajiri walisoma shule za aina moja na waliofaulu waliendelezwa mpaka mwisho, leo hii watu binadamu fedha, walalahoi shule za kata hakuna chochote....

-Dawa za kulevya,
Wakati wa nyerere mlipata kusikia ujinga wa madawa haya kama ilivyo sasa na jinsi watanzania wanavyoteketea?

-Afya,
Pamoja na uchache wa dhahati na vituo vya afya, ukienda kutibiwa unapata dawa za uhakika, bure wahudumu na madakitari walifundwa na walikuwa wazalendo wa kweli.

-Polisi, jeshi na usalama wa raia,
Wakati wa Nyerere vikosi hivi vilitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu, uzalendo na ushilikiano kwa raia, walihifadhi siri za serikali kwa umakini mkubwa leo hii kila kitu ni upuuzi tu

-Mbuga za wanyama na maliasili

Mliwahi kusikia meli kusafilisha meno ya tembo?, Ndege kubebe twiga, Loliondo kupigwa mnada na akina Katabalo kuuwawa?

-Udini na mshikamano miongoni mwa raia wa tanzania
Mliwahikusikia watu kugawanyika kama ilivyo sasa kwa mitazamo ya udini, ukabila na ukanda? (Tulisifika duniani kote kwa jina moja - tuliitana Ndugu FaizaFoxy, Ndugu Red Giant nk)

Mnataka misingigani nyinyi??? unaweza kumpeleka punda hadi mtoni lakini jukum la kunywa au asinywe maji linabaki kuwa hiari yake sio mchungaji.

Watawala tulio nao wako after Tumbo.Ndiyo walafi na mafisadi kupundukia.Kila anayekuwa Mtawala anatafuta pakupiga na kuweka watu wake ili ale vizuri.
 
lakini tukubaliane kuwa nyerere hajatufikisha popote na kweli hakuwa na maono. ni kweli alijenga mshikamano wa kitaifa lakini kungine kote alikuwa anaendeshwa na emotions zaidi kul.iko kuangalia ahalisia wa mambo na dunia inakokwenda.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni....yaani kweli hakuna alichofanya huyu hayati kwa taifa hili?
 
Serikali 3 Ndo kuvunja Umoja?, mbona mbili hazijavunja?, kama umoja Ni NAMBA ungeshawishi iwe MOJA.....,kukataa serikali 3 kwa sababu ya umoja wa kitaifa hiyo Ni PROPAGANDA ya Chama cha masogange. Tusi-JIBASHITEGE(0) wakati tupo timamu.

Mbili hazijavunjwa wapi kaka.Sasa hivi kuna UVCCM na Uchadema.Ukiwa Mpinzani utadhani wewe ni RAIA wa Somalia.Ukiwa unataka Ukanda wa Kaskazini utakuwa kama Mkimbizi toka Afghanistan.

Hakuna umoja ulishavunjwa siku nyingi.

Tanzania tunahitaji Kiongozi na si mtawala atakayekuwa na uwezo na nia ya kuwaunganisha watanzania.

Leo nikiwa na vita sidhani kama Jeshi litasaidiwa na RAIA.Nadhani RAIA ndiyo watakuwa wakwanza kuonyesha wamekimvilia wapi.

Hakuna bond kati ya jeshi na RAIA.Kuna msuguano na mauaji ya RAIA kila wakati.Hivyo umoja ulizikwa na JKN.Wakuufufua siyo Kiongozi toka CCM
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Tatizo sio Nyerere bali ni sisi Watanzania kwa kila mmoja ana mchango wa kuharibu nchi. Hasa Wasomi ambao walishindwa kujitambua.
 
Tatizo sio Nyerere bali ni sisi Watanzania kwa kila mmoja ana mchango wa kuharibu nchi. Hasa Wasomi ambao walishindwa kujitambua.

Ni kweli kabisa ni sisi Wenyewe kuendekeza ujinga.Hatutakiwi kufungua macho.Hatutakiwi kuelewa misingi mkubwa ya haki zetu.Hatutakiwi kujua mema na mabaya.Kila kitu ni unafiki tu.

Kuna watu Wa nadhani kupinga CCM ni sawa na kupinga JKN. Watu wana elimu zao lakini wanashindwa kukemea maovu.Wanabaki kuchekacheka na kupiga Makofi.

Tukiweza kuuutoa unafiki wetu tutafika mahali tu.
 
Hii ni kanuni tu ya ASILI, hakuna kinachokamilika kabisa pasi kuwa na mapungufu. Ni ujinga kutarajia serikali ya wanadamu tena wakawaida, kuanza tu na misingi imara isiyotetereka daima, wakati hata mitume wenyewe ktk uasisi wa dini zao hawakuziachia misingi thabiti,, makundi na vita viliibuka kwa kutokuwepo kwa misingi tu mizuri iliyoachwa.

Mungu na uumbaji wake pia "halijuta" according to Christianity, viumbe havikutenda kama matarajio yake, vilikengeuka, misingi iliwaruhusu kukengeuka. Nyerere nani hata asingeangukia huko?

Lakini lililo kubwa, huwa najiuliza, wapi Nyerere alikosea? Mi sipaoni labda ni la kung'atuka mapema. Mengine yote ambayo hayakutimia vyema kama ilivyopaswa kuwa, hatumbebeshi Mwl. Kwakuwa hakuyaleta kwa NIA OVU, makosa yana sehemu mbili, UTENDAJI WA VIUNGO NA UTENDAJI WA UBONGO. Wapi na ni ktk lipi Mwl. Nyerere alitenda jambo lenye hata kuashiria nia yake ovu kwa taifa?

Sera na itikadi zake, mataifa kadhaa wamezikopi na kuzipaste kwao, tunayajua hayo mataifa na yalikofikia leo? Tukubali, hawa wanaomkosoa leo ni vilembwe vya waliompinga jana, na ndo visababishi vya yote mazuri kufeli.

Tuwasamehe bure tu, wametuharibia nchi halafu wanajitia vipofu kukaa pembeni. Cha msingi tusiwape tena nafasi ya kufanya wayatakayo hawana maono ya mbali hawa, wamelilia "bill of rights" liingizwe ktk katiba, akina Nyerere the great wakawatahadharisha, vimacho vyao vya panya havikuona yaliyojificha, leo wanalialia na ushoga na usagaji, na mahakama itazitambua tu nyambafu.
 
Aliyeishi wakati WA utawala WA Nyerere atoe ulinganisho mambo aliyofanya mazur na mabaya yake. Pia atueleze madhara gani kama nchi ilipata kujiingiza katika vita vya ukombozi kusini mwa Afrika na vita vya kagera bila kusahau miaka 80 kuhusu uhujumu uchumi wakati WA Sokoine
 
Back
Top Bottom