Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Lawama zote ziende kwa CCM baada ya Mwalimu kung'atuka, takribani ni miaka 30 sasa tangu mwalimu akae pembeni lakini CCM hata hawajui nini priority kwa taifa, maadui watatu bado wanazidi kuwatafuna watanzania.

Mimi nadhani adui yetu ni mmoja, sisi wenyewe ni maadui wa wenyewe.

Mwalimu aliposema kuwa yeye si malaika na kuna ambayo alikosea, jee ni yepi hayo? Pengine hao viongozi wetu wanayarudia makosa hayo hayo? Fikiri.
 
Watu kama ninyi msingekuwepo enzi za Nyerere, yale mambo tungefaidika nayo saana. Kwakuwa mlikuwepo wenye uoni hafifu, ya mbeleni hamkuyaona. Ila ktk mahusiano ya kimataifa, kuwa na nguvu ktk diplomasia ni kuwa na nguvu kiuchumi na kijamii pia.

Tanzania ktk siasa za ndani ya Afrika na duniani, msingekuwepo akina ninyi ingekuwa kubwa kidiplomasia. Hata reli ya TAZARA na kiwanda cha URAFIKI na hata ushindi dhidi ya AMINI ni matokeo ya nguvu zetu ktk mawanda ya diplomatic. Nakushangaa, nilishawahi kusoma post yako na ukajinasibisha na usomi na kuishi sana nje, haya madogo kiaje usiyajue?

Punguza ghadhab, diplomasia ya kuwa omba omba?

Hakuna wakati tume kuwa na diplomasia ya hali ya juu kama wakati wa Kikwete.

Kuishi kwangu nje kumenisaidia sana kuiona dunia na kujuwa nchi zingine zinaendeshwa vipi.

Ya tazara na urafiki ntarudi kukujibu.
 
Mwacheni Mwalimu apumzike. Kafanya yake aliyoweza, ameondoka. Mwacheni apumzike.

Naam, tunamuombea apumzishwe popote anapostahiki.

As a powerful leader tuna haki ya kum discuss, au hatuna haki hiyo?
 
Mtoa mada huja ainisha,, Makosa ya mwalimu hata mojawapo. NI MISINGI GANI ZAIDI ULIOITAKA???, kutofanikiwa KWA baazi ya mambo hakutokani na misingi,, Bali mambo mengine haywezi kufanikiwa KWA haraka, kwa sababu za kisera,, na sio misingi.
 
Kila nyanja ya uongozi wa nchi msingi wake mkuu ni katiba. Jee, katiba yetu tukiyonayo toka enzi za Nyerere inaturidhisha? Haina makosa? Kama jibu ni ndiyo, kwanini tunalilia katiba mpya?
 
Ikiwa tutaachana na marehemu waliotutanulia basi leo hii hata itabidi kila kitu tuanze kujifunza upya, sidhani kama hata kuvaa nguo tungeelewa, kwa kuwa wote waliovumbua nguo sasa ni marehemu.

Tulitazame suala hili "positively".

Ikiwa Nyerere mwenyewe kakiri kuwa yeye si malaika na kuna makosa aliyoyafanya katika uongozi wake, mimi nasema tuyatazame hayo makosa ili tusiyarudie.

Nyerere toka aliposema hata yeye amefanya makosa, tumeshawahi kukaa chini na kuona ni makosa yepi ili tusiyarudie?

Mimi nasema, kwa kufata kauli ya Nyerere mwenyewe, tuachane na makosa yake na tuchukuwe mazuri yake tuyaendeleze. Sasa swali linakuja, hayo makosa ni yepi? Naanza na hili moja, ingawa kwa upande wangu yako mengi sana niliyoyashuhudia.

Moja, mie nasema alikosea sana kwenye uchumi.

Wewe unasemaje?
Na ndo kinachoendelea kwa sasa huyo babu kidevu nae anarudia makosa yale yale ya Nyerere.
 
Wewe unamjuwa zaidi Nyerere kuliko anavyojijuwa mwenyewe?

Nyerere kafanya mengi sana mazuri, lakini mwenyewe anakiri kuwa yeye si malaika na kuna aliyokosea, jee, ni yepi hayo?
Hata Yesu na Muhamadi ungewauliza wangejibu hivyo, kwamba nao si wakamilifu. Hiyo ni lugha ya yeyote mwenye hekima. Tumekuuliza ni makosa yapi tuorodheshee hapa tuyajadili. Kila jicho huona kwa uwezo alionao mwenye jicho husika, hapa tuko wengi. Yalete, kuamini kuwa unachokijua wewe binafsi ndo cha kweli zaidi pia ni udhaifu mkubwa kupita yote.
 
Punguza ghadhab, diplomasia ya kuwa omba omba?

Hakuna wakati tume kuwa na diplomasia ya hali ya juu kama wakati wa Kikwete.

Kuishi kwangu nje kumenisaidia sana kuiona dunia na kujuwa nchi zingine zinaendeshwa vipi.

Ya tazara na urafiki ntarudi kukujibu.
Nimekwambia zile harakati njema hazikufanikiwa kwakuwa watu kama wewe mlikuwepo, siasa yetu ni ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA, huko kuombaomba kungetokea wapi hapo?
 
Tanzania na Watanzania tulijazwwa ujinga, amini usiamini, sikulielewa hilo mpaka nilipotoka nje ya Tanzania. Mpaka leo hii bado tunajazana ujinga.

Katika ujamaa tuliaminishwa mali ya umma ni kwa ajili ya wote, matokeo yake, tulipoona wananeemeka wachache, tukaanza kuiba, si mali ya umma? Wacha tujichotee. Matokeo?

Siasa ya ujamaa na kujitegemea haikuleta tija. Miaka 24 aliyotawala Nyerere ingeleta tija kubwa sana kama ilikuwa ina tija yoyote, matokeo yake tukawa masikini wa mwisho duniani, toka Mwingereza alipotuachia nchi tulikuwa wasafirishaji wakubwa wa bidhaa za mashamba nje ya nchi, tulikuwa wa kwanza katika Afrika, tukawa omba omba wa kwanza Afrika na tunajisifu.
 
Hata Yesu na Muhamadi ungewauliza wangejibu hivyo, kwamba nao si wakamilifu. Hiyo ni lugha ya yeyote mwenye hekima. Tumekuuliza ni makosa yapi tuorodheshee hapa tuyajadili. Kila jicho huona kwa uwezo alionao mwenye jicho husika, hapa tuko wengi. Yalete, kuamini kuwa unachokijua wewe binafsi ndo cha kweli zaidi pia ni udhaifu mkubwa kupita yote.

Naam, ina maana alikuwa anadananya kuwa kuna ambo hajayafanya sawa? Au unamaanisha nini?

Napenda uelewe kuwa Nyerere alikuwa ni kiongozi mmoja mzuri sana, wenye uelewa wa hali ya juu, mwenye kuweza kuongea na kumtoa nyoka pangoni na nyoka akatulizana, mwenye kuweza kuhutubia kutoka kichwani mwake na kuwafanya wote wanaomsikiliza wakubaliane nae, iwe msomi au kabwela. Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana ki akili, aongee na Watanzania au Wakubwa wa nje ya Tanzania basi utapenda unsikilize na atawakinasiha wote, kwa ufupi, kama Nyerere angekuwa ni "sales man" ningesema kuwa Nyerere anaweza kuwauzia Waeskimo barafu na wakainunua huku wanachekelea.

Hilo halina shaka kabisa. Lakini Nyerere hakuwa malaika, ni binaadam na binaadam ana makosa yake, hayo makosa ya great leader kama Nyerere ni yepi ili tusiyarudie?

Mojawapo, mimi nasema, ni la uchumi, Nyerere uchumi ulimshinda kabisa.

Msome Mwanasheria "msomi" hapa anasemaje: Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu!
 
Nacho kukubali bibi yangu ni kwenye hoja hata uandike ki kada kada hoja unanazo
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
As much as we hate to admit it, That is the realty and fact. Nyerere alikua kiongozi mzuri aliyefanya makosa makubwa sanaa. Na moja ya kosa kubwa ni kujilimbikizia madaraka na kuzuia namna yoyote ya kushauriwa au kukosolewa kwenye maamuzi yake. Na hii Katiba ya sasa ndio Ushahidi. Can you imagine katiba inasema raisi anaweza kumteua mtu yeyote kwa kadiri impendezavyo!! Maanake hapo hakuna kuangalia uzoefu, ubobezi wala historia na elimu ya muhusika. Na kumfukuza anaweza kumfukuza tu bila kuulizwa wala kushauriwa!!
Mbaya zaidi baada ya kumaliza madaraka na kuenjoy madaraka ya kifalme akatuambia "Kwa Katiba hii Kiongozi anaweza kua Dicteta!!" That was hypocrisy of the highest Degree.
 
Mwalimu alishatangulia mbele ya haki karibu miaka 18 iliyopita. Hawa walio hai ambao nyumba zao tunazijua zipo wapi, hawastahili kweli kubebeshwa mizigo ya lawama?.

Mmojawao alishakiri makosa makubwa yaliyofanyika kwenye ubinafsishaji, wengine wawili walitoa mianya kiasi kwamba wapigaji wakawa wanapitisha makontena mengi tu pale bandarini bila ya fedha yoyote ile kuingia kwenye akaunti za TRA. Hawa kweli hawastahili kunyooshewa vidole, mpaka anyoshewe mtu ambaye kwa sasa yupo ndani ya kaburi?.

Viongozi walioruhusu mazingira ya mfumo dhalimu wa kiuchumi yakawa na uhusiano wa moja kwa moja na CCM, wapo hai na ni rahisi kuomba muda wa kuwauliza maswali, kwani ni wastaafu ambao hutumia muda mwingi wakiwa huru pasipo kutingwa na majukumu ya kikazi.

Wafanya biashara ambao walifikia hatua ya kuwaweka viongozi wetu mifukoni mwao, walipata uwezo huo kwa sababu viongozi wa nchi waliomfuatia Nyerere walitengeneza mazingira ya kunyenyekea wenye fedha. Kwanini hawa tusiwanyooshe kidole na tunabakia kumsimanga Marehemu asiyeweza kujitetea?.

Nyerere alifanya makosa mengi sana, lakini alikuja kukiri makosa yake hadharani. Mtu wa aina hiyo kwetu tunaona anafaa kuwa sehemu ya mijadala yetu mpaka akiwa ameshatangulia mbele ya haki lakini wapigaji ambao wamekuja kumiliki migodi na biashara nyingine chafu, tunawaona ni watu wa kustahili kukanyaga zulia ili viatu vyao visichafuke.

Maandishi huwa yanadumu miaka na miaka, natumaini maandishi yanayoendelea kuandikwa, yatakuja kuleta mabadiliko fulani kwa vizazi vya miaka mingi ijayo.
 
binafsi sijawahi msifia Nyerere kwa kuleta maendeleo Tanzania. alishindwa vibaya. pia alikuwa hashauriki. likewise anaejaribu kufuata nyayo hizo atafeli tena vibaya. dunia haidanganyi.
 
As much as we hate to admit it, That is the realty and fact. Nyerere alikua kiongozi mzuri aliyefanya makosa makubwa sanaa. Na moja ya kosa kubwa ni kujilimbikizia madaraka na kuzuia namna yoyote ya kushauriwa au kukosolewa kwenye maamuzi yake. Na hii Katiba ya sasa ndio Ushahidi. Can you imagine katiba inasema raisi anaweza kumteua mtu yeyote kwa kadiri impendezavyo!! Maanake hapo hakuna kuangalia uzoefu, ubobezi wala historia na elimu ya muhusika. Na kumfukuza anaweza kumfukuza tu bila kuulizwa wala kushauriwa!!
Mbaya zaidi baada ya kumaliza madaraka na kuenjoy madaraka ya kifalme akatuambia "Kwa Katiba hii Kiongozi anaweza kua Dicteta!!" That was hypocrisy of the highest Degree.

Wanasema haya ni maneno yake mwenyewe:

"...according to his own words, “enough powers to make me a dictator",..."

Source: Tanzanian Affairs » PRESIDENT NYERERE AND THE STATE
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Kwangu mimi kosa kubwa alilofanya ni kutokutuunganisha na Rwanda, tukapata TANRWA, tungewafaidi wale watoto wa kinyarwanda
 
Back
Top Bottom