Wakati vijiji vya ujamaa vilipoanzishwa familia yangu ilikuwa mojawapo kuishi kwenye vijiji mbali mbali, baba yangu akiwa settlement officer. Nakumbuka hayo ingawaje wakati huo nilikuwa mtoto. Wana vijiji wengi walihama na kuacha mashamba yao kwa kupinga mwito huo. Wengine kwa fransration wakawa walevi. Wakulima wa pamba usukumani waliokuwa wakilima pamba na kuiuzua serikali, badala ya chama chao Nyanza cooperative wakaanza kucheleweshiwa malipo na walipolipwa, walilipwa na cheque AMBAYO wengi wao walikuwa hawana hata account, matokeo yake wengi walipoteza hundi hizo, kwaajili ya kukosa malipo, wengi walitupilia mbali kilimo wakawa walevi kwa frastration. Wazazi wakawa walevi, watoto wakaacha kuhudhulia shule, na wajinga tukawa wengi, ndiyo maana leo tuna Viongozi kama Bashite. Ujamaa ulikuwepo tangu zamani, watu walikuwa wakisaidiana kulimiana lakini kila mtu na shamba lake. China ilikuwa hivyo, na Mwalim alivutiwa na MTINDO wa China alipotembele huko. Ukiwa mgeni hauoni mabaya, wachina hawakumuonyesha maafa ya ujamaa, vijijini China watu walikuwa wakifa na njaa, lakini habari hizi Muchina alizificha zisijulikane. Wakati huo kila serikali ilitetetea MTINDO wa siasa zao. Hatuimbi kama kasuku, historia lazima ikumbushwe, ndiyo maana kila mwaka tunasherekea Uhuru.
Narudia tena, Mwalim alikuwa hana ubinafsi kabisa, alifikiri anachofanya kutawanufaisha Watanzania, Viongozi waliofuatia walikuwa na nafasi kubwa ya yakusahihisha makosa haswa kwa elimu, na kuyaendeleza mazuri, kwa ubinafsi wao wameididimiza elimu yetu, na kwa ubinafsi wao wamelitumia jina la Nyerere vibaya kwa manufaa yao. Tanzania ya leo sio ya Nyerere, pamoja na makosa aliyoyafanya, aliendelea kurekebisha mpaka hapo alipoachia madaraka. Walioshika madaraka badala yake wametugawa wakacreate matajiri wa kutupa wachache na masikini wengi wa kutupa. Pamoja na kuwa na fulsa ya kuibadilisha na kuimarisha education yetu, wameiteketeza, matokeo yake tunapata Viongozi kama Bashite. Hatujui tunaelekea wapi. Pamoja na nchi kuwa na maliasili nyingi, hatuna wa juzi wa kusisimia utajiri wetu. Kwa mufano tuambiwa kwenye macontainer Hakuna zaidi ya muchanga, mchanga huu, ni muchanga wa aina gani? miaka imepita , macontainer mengi yamepelekwa hatujuwi kama ni mchanga ama dhahabu. Umasikini wa elimu ni umasikini mbaya. Ni vigumu kuelewa kwa kuwa tumetosheka hatuna elimu na Viongozi wetu hawana haraka ya kuibadilisha, kwani ni rahisi kumutawala mtu asiye na elimu, lakini pia ni vigumu kuiendesha nchi ya watu wasiokuwa na elimu utegemee kuleta mabadiliko.