Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Naam, tunataka tuyachambue hayo ya kijinga ili tusirudie makosa. Maana naona imefikia mpaka yale ambayo hata mwenyewe alikiri ni "ya kijinga" sisi tunayakumbatia.
Na babaako alikuwa mmoja wa wasaidizi wa karibu wa nyerere. Ni mmoja wa waliochangia uharibifu kwa kushindwa kumsaidia ilivyopasa.
 
Na babaako alikuwa mmoja wa wasaidizi wa karibu wa nyerere. Ni mmoja wa waliochangia uharibifu kwa kushindwa kumsaidia ilivyopasa.

Si kweli, babangu hajawahi kufanya kazi serikalini.

Tatizo siyo waliokuwemo na wasiokuwemo, wengi tulikuwepo na tulimshangilia sana Nyerere enzi zake, baada ya kuiona dunia (exposure) tukaona mnhh, mbona hatuendi sawa kwetu? Si kitu.

Tatizo linakuja sasa, miaka zaidi ya 40 toka amalize utawala wake hatutaki kuainisha makosa ili tusiyarudie.

Wewe unadhani lipi lililopangika wakati wa Nyerere lisirudiwe kwa kuwa lilikuwa ni kosa. Mimi nimeainisha juu huko.

Pia unaweza kuweka mazuri yake ambayo unaona yangetufaa zaidi leo hii yaliyowachwa.
 
Ndivyo ulivyojazwa ujinga. Sikushangai.

Sasa fikiri, haohao unaosema wezi (nchi za kibepari) ndiyo tunawategemea watujazie kwa kutuchangia bajeti ya nchi yetu. Kulikoni?
labda unawategemea wewe. mimi naishi Vietnam.
 
He has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?

Tafadhali andika kiswahili.'has been died' maana yake ninini' Kwa nini unajifanya kutumia lugha ambayo huijui ?
 
NI vema tujikite katika kujadili mambo ya yanayojiri sasa badala ya kufukua makaburi.Mfano Tz itapata faida gani kupeleka watu saba EALA badala ya tisa?
 
Hoja yako hapa siokufundisha wachangiaji lugha, jibu hoja zetu tukitaka lugha tutaenda darasani

Mleta mada ana ugonjwa wa chuki dhidi ya Nyerere.Alitawala miaka 25,wakamfuata watawala wanne baada yake wewe u miongoni mwa wachache mlioona misingi ya hovyo iliyojengwa na Mwalimu ikibomolewa na waliomfuata.

Waliomfuata ni viongozi wangu.Madudu waliyoyaleta na madhara yake tumeyaona.Moja ya hiyo unayoidharau na inakuudhi ni Azimio la Arusha.Taja lililo jema zaidi ya azimio la Arusha.

Raha yako ingekuwa kuona tukibaguana kwa makabila yetu,dini zetu na tfauti ya vipato vyetu.
 
Katika mambo yote nitamlaumu nyerere kwa kulimbikiza madaraka mengi kwa raisi kiac kwamba raisi Tanzanis ni kama mungu mtu.

Nchi zote za Afrika baada ya kupata uhuru tuliendelea na katiba AMBAYO ilikuwa imempa wakati huo governor mamlaka yote. Katiba zimebadilika, Ghana wana katiba mpya, Rais hana mamlaka yote. Kenya katiba imebadilishwa, Kenyatta anapingwa kila siku maamuzi yote nje ya katiba. Hata hivyo Afrika tuna shida kubwa ya kuvunja sheria, hata kam
Si kweli, Kikwete ameacha nchi ina zaidi cubic feet trillion 15 za gas, utajiri wa ajabu.

Ameacha tuna akiba hazina kuliko wakati wowote wa kabla yake.

Ameacha nchi ina maghala ya taifa ya hifadhi ya chakula kingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha Tanzania inatowa misaada ya chakula kwa nchi jirani.

Ameacha nchi ina barabara za lami nyingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina shule nyingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina vyuo vikuu vingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina pato la utalii kubwa kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina umeme mwingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi inafanya upasuaji wa moyo hapa hapa nyumbani, hakuna kabla yake.

Niendelee?

Hayo yote unasema Kikwete kaacha unayaona wewe, pengine tuonyeshe kule ameficha. Mimi ninavyojuwa Kikwete ameacha madeni kibao, Rais Magufuli amechukua nchi hata mishara ya wafanyakazi wa serikali ya mwezi huo kulikuwa hakuna. Kikwete ameacha nchi ikatafunwa na kuwachwa mifupa mitupu. Kuna watu waliofaidi kwenye utawala wa Kikwete, ni wapiga dili.
Shule unazosema ameacha Kikwete ni shule duni, zenyekutowa mafunzo duni wenye fikra duni wasiofikiria. Wingi wa shule si kitu kama hazitowi quality education. Kikwete kwa miaka kumi angefanya mengi, lakini ameacha taifa lisilokuwa na nidhamu.

Kikwete ameacha wangojwa wanalala chini, ushahidi Magufuli alipotembelea Muhimbili, Kikwete aliendelea kuijenga Appolo hospital ya India iliyokuwa ikitibu wachache awapendao. Kikwete aliiachia nchi ikawa Soko la madawa, alipewa lisiti wanaohusika akaondoka nayo kibindoni, bila ya kuchukua hatua.
Kikwete aliikabithi nchi kwa mafisadi, bandarini mizigo ikipita bila ya kodi. Wizi wa ajabu wa fedha za walipa kodi, Hakuna , waliokuwa chukuliwa hatua, waliokuwa wakifungwa ni petty criminals watu wenye kuiba mandazi kwa kuwa wana njaa.

Safari za Kikwete pekee zimaacha deni kubwa. Fedha hizo zingejenga, hospitali na kuimprove maisha ya Watanzania. Watanzania walikuwa wakiishi kwenye false economy, gharama za nyumba haswa Dar es salaam zilifikia mamilioni, bei Mtanzania wa kawaida asingeweza kununuwa, waliokuwa wakinunuwa ni wapiga dili kwa pesa za serikali ambazo badala ya kuwa huduma wananchi, zilikuwa zikitumiwa na wachache. Mwenye kusifu uongozi wa Kikwete hajui haki ni kitu gani. Kikwete ameiacha nchi mifupa mitupu. Ingekuwa ni South Korea leo Kikwete angekuwa chini ya ulinzi, lakini Afrika pension inamungoja ingawaje hahitaji kwa utajiri inasemekana alionawo..
 
Kwa kweli FaizaFoxy leo hii ukimleta Mwl. Nyerere agombee uraisi dhidi ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete au hata Magufuli, Mwl. Nyerere atapita kwa kura nyingi mno, mimi mmoja wapo wakumpigia.
Legacy zake ni nyingi kwa kweli, na tulipotupa kule madhara yake ndio haya tunayoyaona :-
  • Uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, na cha kushangaza mpaka viongozi wa vyama vyote kudaiwa kuhusika
  • Wizi, ufisadi, ubinafsi, ulafi na ufujaji wa mali za umma
  • Kupendeleana kwa sababu za kidini na za kikabila.
  • Kutokuwajibika, hata kama serikali imekusomesha na kukufikisha hapo, kusoma tu na kukosoa mikataba kwa manufaa ya umma hakuna, tumeisahau nchi, tumbo na familia zetu kwanza.
  • Kutokufuata sheria bila shuruti, zamani ilikuwa na ajabu na kwa nadra kuona bastola zatolewa nje nje au hata askari kutembea na SMG mtaani, au kupiga tu risasi.
  • Kufoji foji makaratasi na maombi yawe ya kutaka kusafiri au kutibiwa serikalini, ni kinyaa, hapa kidogo kumepunguwa.
  • Viongozi kusafiri safiri kila wakati kisingizio wamebeba bakuli la kuomba hela kwa wazungu au nchi zilizoendelea, kumbe wanakoenda wana yao.
  • Udini kushika hatamu.
  • Utakatishaji wa fedha za umma, kina mzee wa vijisenti, huyu mzee siku nyingi angekuwa ananyea debe na mali zote kufilisiwa.
  • Utajiri usiokifani na usio jibu maswali ya upatikanaji wake, kina Rostam, Lowassa na wengine wengi tu
  • Kuzorota kwa elimu, ustawi wa jamii na afya, wahusika hata hawaeleweki wanafanya nini?! Shaghalabagala..
  • ..
  • ..
Na mengi mengineo, kwa kweli huyu mzee (Mwl. Nyerere) alikuwa wa kipekee..

Nakuunga mkono, Viongozi waliofuatia wamekula bila kufikilia kuna kifo. Utajiri wa ghafla haueleweki, wakati Watanzania wengi wanalala na njaa. Wizi sio wizi tena ni kuloot mchana wala sio usiku. Selective justice, wazi wazi. Kupendeleana na kuchungana inatisha. Asemaye haki ama mwenye kutetea haki anafukuzwa kazi, hii siyo Tanzania ya mwalim ni Tanzania ya man eat man society.
 
Si kweli, Kikwete ameacha nchi ina zaidi cubic feet trillion 15 za gas, utajiri wa ajabu.

Ameacha tuna akiba hazina kuliko wakati wowote wa kabla yake.

Ameacha nchi ina maghala ya taifa ya hifadhi ya chakula kingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha Tanzania inatowa misaada ya chakula kwa nchi jirani.

Ameacha nchi ina barabara za lami nyingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina shule nyingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina vyuo vikuu vingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina pato la utalii kubwa kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi ina umeme mwingi kuliko wakati wowote ule wa kabla yake.

Ameacha nchi inafanya upasuaji wa moyo hapa hapa nyumbani, hakuna kabla yake.

Niendelee?

Kwa haya uliyoaandika, inaonyesha jinsi gani ulivyo mjinga. Baada ya Miaka 20 Rais atakae kuja na kuiacha hii nchi, definately ataacha nchi yenye shule nyingi, umeme, vyuo nk kuliko wale wa nyuma yake.

Kila siku haya mambo yanafanyika na kujengwa kwa kuwa population inaongezeka. Kumbuka kipindi cha Nyerere population haikuwa kama ya leo.

Gas, gas, gas, eti Kikwete kaacha, yaani wewe kweli zero. Sasa hayo madini Nyerere aliyoyaacha mmepeleka wapi? Natural resources??? Kikwete kaacha.

Binafsi naona mnabishana na mtu mwenye chuki binafsi na si mwenye kuleta hoja zenye maana. Hivi Kweli kwa akili yako unamlinganisha Kikwete na Nyerere. This is a joke. Hiyo exposure yako unayo isema umeipata kukaa huko bado sana. Ujinga na chuki havijakutoka, na utasingizia eti ndo Misingi mibovu iliyoachwa.
 
Nchi zote za Afrika baada ya kupata uhuru tuliendelea na katiba AMBAYO ilikuwa imempa wakati huo governor mamlaka yote. Katiba zimebadilika, Ghana wana katiba mpya, Rais hana mamlaka yote. Kenya katiba imebadilishwa, Kenyatta anapingwa kila siku maamuzi yote nje ya katiba. Hata hivyo Afrika tuna shida kubwa ya kuvunja sheria, hata kam

Hayo yote unasema Kikwete kaacha unayaona wewe, pengine tuonyeshe kule ameficha. Mimi ninavyojuwa Kikwete ameacha madeni kibao, Rais Magufuli amechukua nchi hata mishara ya wafanyakazi wa serikali ya mwezi huo kulikuwa hakuna. Kikwete ameacha nchi ikatafunwa na kuwachwa mifupa mitupu. Kuna watu waliofaidi kwenye utawala wa Kikwete, ni wapiga dili.
Shule unazosema ameacha Kikwete ni shule duni, zenyekutowa mafunzo duni. Wengi wa shule si kitu kama hazitowi quality education. Kikwete kwa miaka kumi angefanya mengi, lakini ameacha taifa lisilokuwa na nidhamu.

Kikwete ameacha wangojwa wanalala chini, ushahidi Magufuli alipotembelea Muhimbili, Kikwete aliendelea kuijenga Appolo hospital ya India iliyokuwa ikitibu wachache awapendao. Kikwete aliiachia nchi ikawa Soko la madawa, alipewa lisiti wanaohusika akaondoka nayo kibindoni, bila ya kuchukua hatua.
Kikwete aliikabithi nchi kwa mafisadi, bandarini mizigo ikipita bila ya kodi. Wizi wa ajabu wa fedha za walipa kodi, Hakuna , waliokuwa chukuliwa hatua, waliokuwa wakifungwa ni petty criminals watu wenye kuiba mandazi kwa kuwa wana njaa.

Safari za Kikwete pekee zimaacha deni kubwa. Fedha hizo zingejenga, hospitali na kuimprove maisha ya Watanzania. Watanzania walikuwa wakiishi kwenye false economy, gharama za nyumba haswa Dar es salaam zilifikia mamilioni, bei Mtanzania wa kawaida asingeweza kununuwa, waliokuwa wakinunuwa ni wapiga dili kwa pesa za serikali ambazo badala ya kuwa huduma wananchi, zilikuwa zikitumiwa na wachache. Mwenye kusifu uongozi wa Kikwete hajui haki ni kitu gani. Kikwete ameiacha nchi mifupa mitupu. Ingekuwa ni South Korea leo Kikwete angekuwa chini ya ulinzi, lakini Afrika pension inamungoja ingawaje hahitaji kwa utajiri inasemekana alionawo..

Mkuu, huyu dada hajitambui. JPM kaingia madarakani mishahara hakuna. Bandarini wizi mtupu. Nchi ma deal kila mahala.
Huyu dada anachekesha sana.

While we agree kwamba Kikwete kafanya mambo mazuri, BUT it is a joke, kumlinganisha na Nyerere au eti kusema kuwa he was the best president of this country ever, may be kwa kuwa msikivu.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Hii ni moja wapo ya threads za kipuuzi kabisa kuwahi kuziona humu jamvini.

Alafu wewe ndio unakomaaga humu kutuaminisha kuwaJakaya ndio raisi bora kuliko wengine wote, unanishangaza sana.
 
Mimi nadhani kosa lao kubwa lilikuwa kumpa 100% trust Nyerere.
Naamini kwamba kosa kubwa la Mwalimu Nyerere ni katika Namna ya kupata viongozi...Ali tumia zaidi utashi wake kuliko misingi na madhara yake yameendelea hadi leo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom