Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere katoka madarakani 1984 hadi leo kufeli kwa nchi mnamsingizia Nyerere. Huu ni upuuzi na chuki kijinga haijapata kutokea.
Mbona hata alivyokuwa madarakani nchi ilifeli kama ulikuwepo nadhani uliona au unaweza kutupa mafanikio ya Nyerere kiuchumi wakati yupo madarakani.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Sio Nyerere bali neo-colonialism. Nchi zote za kiafrika zilizotawaliwa zinafanana tu, sio east africa, central wala west africa kuliko na ahueni.
 
Kutoka kung'atuka kwake mpaka leo ni Miongo mingi imepita, Hatuwezi kumlaumu Yeye, maana kwa wakati wake alichokifanya na kukijenga kilitenda kazi yake, Tujilaumu wenyewe tunaoshindwa kujenga misingi sasa, na kwa wakati huu tulio nao kwa faida yetu na kizazi kijacho
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Misingi yote aliyoiweka ilikuwa imara na madhubuti ndio maana amani umoja bado unadumu mpaka leo. Hali ya utulivu tuliyonayo leo si tukio la nasibu ni misingi iliyowekwa na waasisi.
Ngoja tukumbushane nchi aliliyoipokea Mwl Nyerere, halafu tuone hatukuendelea? Katika hotuba moja ya Mwl Nyerere anasema kunamtaalam mmoja wa kizungu aliwahi kuifananisha nchi yetu na mdudu mmoja aitwaye kwa kiingereza bamboo bee. Anasema mdudu huyo hana sifa za kuruka/kupaa lakini anapaa. Na Tanganyika haikuwa na sifa za kuitwa nchi lakini ilikuwa nchi. Watu milioni tisa lakini injinia 2. Hapa unapata picha kuwa jamii yote ni kama ilikuwa haijaelimika vya kutosha. Mwalimu aliweka msingi wa kuelimisha watu na kupatikana wasomi wa mwanzo mpaka nawe ukapatikana sijui hapaswi kujivuna kwa msingi wake aliouweka kukuzalisha msomi wewe.
Kwa kuwa hukubainisha misingi ambayo Mwl Nyerere aliiweka na kushindwa. Niwe nimekuchokoza uitaje nipate kuitazama kwa jicholako na langu. Asubuhi njema
 
He has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?
umekurupuka,,,anaongelea misingi ambayo hutawala miaka na miaka,,like napoleon ,,,,washington,,,rosevelt,,,lincolin...na wengine,,,jadili kama huna maoni basi pita
 
Misingi yote aliyoiweka ilikuwa imara na madhubuti ndio maana amani umoja bado unadumu mpaka leo. Hali ya utulivu tuliyonayo leo si tukio la naibu ni misingi iliyowekwa na waasisi.
Ngoja tukumbushane nchi aliliyoipokea Mwl Nyerere, halafu tuone hatukuendelea? Katika hotuba moja ya Mwl Nyerere anasema kunamtaalam mmoja wa kizungu aliwahi kuifananisha nchi yetu na mdudu mmoja aitwaye kwa kiingereza bamboo bee. Anasema mdudu huyo hana sifa za kuruka/kupaa lakini anapaa. Na Tanganyika haikuwa na sifa za kuitwa nchi lakini ilikuwa nchi. Watu milioni tisa lakini injinia 2. Hapa unapata picha kuwa jamii yote ni kama ilikuwa haijaelimika vya kutosha. Mwalimu aliweka msingi wa kuelimisha watu na kupatikana wasomi wa mwanzo mpaka nawe ukapatikana sijui hapaswi kujivuna kwa msingi wake aliouweka kukuzalisha msomi wewe.
Kwa kuwa hukubainisha misingi ambayo Mwl Nyerere aliiweka na kushindwa. Niwe nimekuchokoza uitaje nipate kuitazama kwa jicholako na langu. Asubuhi njema

Hizo zote porojo tu.

Hakuna engineer lakini barabara zilipitika, hakuna madaktari lakini watu walitibiwa.

Tanganyika ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kusafirisha mazao nje. Miaka miwili mitatu tu baada ya Uhuru tukaanza kuwa omba-omba wa chakula.

Tanganyika haijawahi kukosa amani na ndiyo maana nchi ikawa na sifa za peponi, mpaka Dar Es Salaam ikawa Dar Es Salaam, unajuwa kuwa Dar Es Salaam ipo kwenye Qur'an na ni peponi?

Ukweli tuuseme kuhusu makosa yaliyofanyika wakati wa utawala wa Nyerere, tutakuwa huru zaidi na kutorudia makosa. Hata Nyerere mwenyewe alikiri kuwa alifanya makosa, seuse sisi tuone hajafanya makosa. Inashangaza.

Mpaka leo tunalia tunataka katiba mpya, kama haina makosa kwanini tunataka katiba mpya? Ulishasikia nchi zenye katiba nzuri zikitaka katiba mpya? USA katiba yao ina miaka mingapi leo? Hiyo katiba ni ya nani? Au huo si msingi aliouweka?
 
He has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?
Safi.
 
Semeni ukweli, na acheni porojo za kipuuzi. Kilichoshindwa katika nchi hii miaka yote ni mfumo uliojengwa na Chama chenu. Hajawahi kushindwa "Mtu" katika Taifa hili. Mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa raslimali za nchi uliojengwa na unaoendelea kusimamiwa na chama chenu ni hopeless, flawed and garbage, na ndio ulitufikisha hapa tulipo leo. Kama hatutauvunja mfumo huu, hao akina "Nyerere" mnaosema wameshindwa, wataendelea kupita na Tanzania itaendelea kuwa maskini daima. Be smart, don't argue like buffoons.
 
Hoja nzuri sana hii,

Kimsingi siasa yetu imebadilika. Siasa za siku hizi zinahitaji kiongozi kuinvest kwenye kupendwa na watu.

Mwanasiasa wa leo can not afford too many enemies, anatakiwa kujenga kundi la "marafiki". Hapo ndipo mambo yanapoharibika, kwa sababu kwenye urafiki kuna "kuvumiliana" na kuoneana aibu. Nakumbuka Nyerere alisema mtu akienda Ikulu inabidi awaambie marafiki zake kuwa Ikulu ni mahala patakatifu, that is not practical today kwa sababu bila kuwa na hao marafiki watakaompigania hata Ikulu mtu hawezi kuiwaza. Kuwageuka marafiki hao baada ya kuingia Ikulu is a political suicide.

Nyerere hakuhitaji "kambi" ndani ya chama ili aendelee kuwa kiongozi ili ashinde uchaguzi. Siku hizi bila kuwa na "kambi" mgombea haambulii kitu.

Vilevile viongozi siasa wa leo wanapatwa na changamoto zaidi ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Kwahiyo si sahihi viongozi hawa kuwafananisha kwa kutumia jedwali. By the way, kifalsafa hawa wote ni viongozi wa mfumo uleule. Mfumo wetu wa uongozi tangu Uhuru kimsingi haujabadilika.

You sound purely Machiavellian....
 
Kama kiongozi yeyote Hayati Nyerere alifanya makosa lakini pia kuna mazuri mengi aliyoyafanya. Na bahati nzuri hata yeye mwenyewe alikiri kuwa kuna makosa aliyoyafanya na akashauri kuwa waliomfuatia wayaondoe waendeleze yale mazuri.
 
He has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?
yaani yote unayoona ni matokeo ya makosa yake so lazima tuangalie pale tulipojikwaa sio hapa tulipoangukia
 
Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.

Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.
Hujuwi
Hujui.

Kumbe na wewe hua unakosea????
Tuambie ipi sahihi kati ya, hujui&hujuwi
 
Nataka nikubaliane na nyie mnaosema Nyerere alishindwa. Lakini Nyerere ameshaondoka kwenye utawala miaka mingi sasa, na in fact, ameshakufa na hayupo tena hapa duniani! Sasa nini kimetufanya tuendelee kushindwa miaka mingi hata baada ya yule aliyesababisha tushindwe kuondoka?? Use common sense please....
 
Uoga.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
huu uzi wa 2013 kuuleta tena 2017 haifanyi watu kubadilisha mtazamo wao kuhusu mwalimu nyerere.
 
Tumkosoe lakini tumheshimu sana Mwalimu. He remains to be the only visionary leader we ever had in this country. Actually, economic take off ya Tanzania ilikaribia kutokea wakati wa utawala wake. Ni wakati ule ambapo Tanzania ilikuwa moja ya nchi zilizokuwa zinazalisha kwa wingi Katani, Kahawa, Pamba, Chai, Korosho n.k huku ikiwa na viwanda vingi vya kutengeneza malighafi kutokana na mazao hayo. Ni wakati huo pekee nchi yetu ilikuwa na vyama imara vya ushirika vilivyokuwa na raslimali nyingi (Kagera , Ruvuma, Iringa, Nyanza, Mbeya RETCO etc). Ni wakati huo pia Tanzania ilikuwa na mashirika ya umma yaliyokuwa na ufanisi mkubwa (National Milling, SIDO, VETA BIMA etc), na viwanda vikubwa vya utengeneza zana za kilimo (UFI, Mbeya ZZK etc). Ni wakati huo pekee ambapo uwiano wa shillingi ya Tanzania na dola ya kimarekani ulibaki kuwa single digit. Narudia tena, ni wakati huo tu ndipo Tanzania ingeweza kusema inakaribia kuwa nchi ya viwanda (Kama nchi nchi yeyote katika Afrika inaweza kusema hivyo). Please leave this great man to rest in peace....
 
Back
Top Bottom