Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Tatizo sio Nyerere bali ni sisi Watanzania kwa kila mmoja ana mchango wa kuharibu nchi. Hasa Wasomi ambao walishindwa kujitambua.

Kuna siku, zamani sana, nilikutana na msomi mmoja wa enzi hizo (sjuwi yuko wapi kwa sasa) anaitwa Dr. Mujuni, alikuwa katibu mkuu wizara ya viwanda enzi hizo. Alinambia kuwa "Mzee haambiliki wala hashauriki". Sikushangaa.

Ikiwa msomi anasema hayo, fikiri.

Tuwaombe tu watawala wetu wasirudie hayo makosa ya kutokushaurika na kutokuambilika.
 
Mshikamano wa kitaifa alioujenga Nyerere je, unathaminiwa na jamii? Je, Nyerere alisema nini kuhusu serikalki tatu? Je, wanasiasa na jamii ya leo inasema nini kuhusu serikali tatu? Je, alichofundisha Nyerere kinafanana na kinachosemwa na jamii?
Jamii ya Leo hatukubaliani na hesabu ya Nchi mbili kuungana alafu serikali zikabaki kuwa mbili. Ni Kati ya 1 au 3 haiwezi kuwa 2. Tuache unafiki. Tusi ji-BASHITEGE(0).
 
Hebu fafanua tuijadili vizuri hapo kwenye red, mimi naanza halafu wewe pinga hoja zangu......tujadiliane.

-Madini
Alikuachieni tena kwa ahadi kwamba mtavuna mkiwa teyari

-Elimu
wakati wake JK Nyerere, japo walifaidika wachache lakini wote masikini kwa matajiri walisoma shule za aina moja na waliofaulu waliendelezwa mpaka mwisho, leo hii watu binadamu fedha, walalahoi shule za kata hakuna chochote....

-Dawa za kulevya,
Wakati wa nyerere mlipata kusikia ujinga wa madawa haya kama ilivyo sasa na jinsi watanzania wanavyoteketea?

-Afya,
Pamoja na uchache wa dhahati na vituo vya afya, ukienda kutibiwa unapata dawa za uhakika, bure wahudumu na madakitari walifundwa na walikuwa wazalendo wa kweli.

-Polisi, jeshi na usalama wa raia,
Wakati wa Nyerere vikosi hivi vilitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu, uzalendo na ushilikiano kwa raia, walihifadhi siri za serikali kwa umakini mkubwa leo hii kila kitu ni upuuzi tu

-Mbuga za wanyama na maliasili

Mliwahi kusikia meli kusafilisha meno ya tembo?, Ndege kubebe twiga, Loliondo kupigwa mnada na akina Katabalo kuuwawa?

-Udini na mshikamano miongoni mwa raia wa tanzania
Mliwahikusikia watu kugawanyika kama ilivyo sasa kwa mitazamo ya udini, ukabila na ukanda? (Tulisifika duniani kote kwa jina moja - tuliitana Ndugu FaizaFoxy, Ndugu Red Giant nk)

Mnataka misingigani nyinyi??? unaweza kumpeleka punda hadi mtoni lakini jukum la kunywa au asinywe maji linabaki kuwa hiari yake sio mchungaji.
Huu uzi nimeupenda ghafla, umemaliza Mkuu.
 
Mkuu, unaelewa maana ya MSINGI lakini?

Fundi paa anaweza kuweka msingi?
ZeMarcopolo leo ndo nimekuona ukiongea point, kumbe Lumumba wenye akili timamu mpo ila basi tu mkipuliziwa moshi wa bangi mnajitoaga ufahamu.
 
Hoja yako hapa siokufundisha wachangiaji lugha, jibu hoja zetu tukitaka lugha tutaenda darasani

Kanisome vizuri post yangu halafu nioneshe ni wapi nimemfundisha?

Hivi mnachokisoma huwa hamuelewi au ni ujinga wa asili?
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

ukileta hoja ya namna hii usiongee juu juu kana kwamba unahubiri mapokeo...

unaposema 'alikuwa hana uzoefu wa kuongoza' bila kutia nyama kidogo au sana unakuwa hueleweki kama unaposema 'alikuwa hana muono' au hata pale unaposema 'alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani' haya si madai ya kuandika tu na kuyaacha yanaelea hewani tena madai mazito namna hiyo dhidi ya mtu aliyeacha legacy ya kupigiwa mfano duniani kama mmoja ya watu walioshiriki katika kupigania uhuru wa nchi za Bara la Afrika.

rudi tena kajipange uje upya.
 
Nyama weka wewe, mimi nimmelianzisha tu au uliza ujibiwe, hii ni open forum.

Hilo halina shaka kuwa alikuwa mpigania Uhuru mzuri sana na sababu alizitowa kwanini, wala hakuna ubishi katika hilo, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Lakini, jee ilikuwa na umuhimu wowote kwa Wananchi wake?

Nakumbuka Kenya walikataa kujiingiza katika mambo hayo lakini ukitazama hakuna walichokikosa na sisi hatuna tunachofaidika nacho, kama haitoshi pengine tunafukuzwa huko huko kwa tulio "wasaidia", juzi juzi tumesikia Watanzania wakifukuzwa kama mbwa huko Msumbiji na tumeshasikia kama hayo Afrika Kusini, kwa msaada wa hali na mali na roho za Watanzania zilizotoka, inanibidi nifikiri kuwa Wakenya walifanya vyeama kutojiingiza kichwa kichwa kama sisi, na ulikuwa ni uamuzi mbaya, au? Tumefaidika nini?
 
wengine hata hatuujui utawala wa Mwl
Lakini huu utawala wa sasa hivi, hadi watoto wa primary wanausema jinsi ulivyo na MAKOSA MAKUBWA SANAAAAAAAAAA
 
wengine hata hatuujui utawala wa Mwl
Lakini huu utawala wa sasa hivi, hadi watoto wa primary wanausema jinsi ulivyo na MAKOSA MAKUBWA SANAAAAAAAAAA

Kama yepi hayo "MAKOSA MAKUBWA SANAAAAAAAAAA" YA sasa ili tuliokuwepo tujikumbushe kama yaliwahi kutokea na tunayarudia au ni mapya kabisa.

Ndiyo lengo la huu uzi, tuyajuwe makosa ya kimsingi ambayo hayakutuletea tija ili tuwaombe viongozi wetu wasiyarudie.

Binadam hatuyajuwi yajayo lakini tunayajuwa yaliyopita na ndiyo mafundisho bora kabisa kujifunza kwa yaliyopita.
 
Who is He?......QUOTE="Mwanamutapa, post: 7317039, member: 62618"]Faiza, I respect you so much for many views and contributions you have done to this forum, but when it comes to Mwalimu Julius Nyerere you better leave him alone, Mwalimu laid foundations for this this nation as leader who was disciplinary and above corruption. Mwalimu Julius Nyerere's principles and values that he stood for, still arose deeply interest within and between the school of thoughts, scholars and intellectuals for many years after his death.

Don't compare Mwalimu with bunch of thieves like Ally Hassan Mwinyi, Ben Mkapa and the apex of all thieves Kikwete who has used his friends such as Lowassa, Rostam, Mkullo, Ngereja, Chenge, Karamagi, his son Ridhwan and others for plundering and looting our wealth and stash them abroad while leaving Tanzanians with high inflation rate, high unemployment rate, low GDP, low purchasing power parit and, poor balance of payment.

Right now CCM has nothing to offer except kutaja urefu wa barabara za lami as if ni muhimu zaidi ya ajira na mfumuko wa bei people can live without barabara za lami but they can't live without works that means kipato.[/QUOTE]
In TZ /Under the SUN no1 is UNTOUCHABLE. we just need to be honest.
 
Kama yepi hayo "MAKOSA MAKUBWA SANAAAAAAAAAA" YA sasa ili tuliokuwepo tujikumbushe kama yaliwahi kutokea na tunayarudia au ni mapya kabisa.

Ndiyo lengo la huu uzi, tuyajuwe makosa ya kimsingi ambayo hayakutuletea tija ili tuwaombe viongozi wetu wasiyarudie.

Binadam hatuyajuwi yajayo lakini tunayajuwa yaliyopita na ndiyo mafundisho bora kabisa kujifunza kwa yaliyopita.

1. Huyu mzee anakurupuka sana, hajui kukitumia kichwa chake hata kidogo kwa kufikiria jambo kabla ya kulitenda
2. Hashauriki huyu mzee, anachotaka yeye ndio hichohicho bila kujali madhara ya mbeleni
 
Who is He?......QUOTE="Mwanamutapa, post: 7317039, member: 62618"]Faiza, I respect you so much for many views and contributions you have done to this forum, but when it comes to Mwalimu Julius Nyerere you better leave him alone, Mwalimu laid foundations for this this nation as leader who was disciplinary and above corruption. Mwalimu Julius Nyerere's principles and values that he stood for, still arose deeply interest within and between the school of thoughts, scholars and intellectuals for many years after his death.

Don't compare Mwalimu with bunch of thieves like Ally Hassan Mwinyi, Ben Mkapa and the apex of all thieves Kikwete who has used his friends such as Lowassa, Rostam, Mkullo, Ngereja, Chenge, Karamagi, his son Ridhwan and others for plundering and looting our wealth and stash them abroad while leaving Tanzanians with high inflation rate, high unemployment rate, low GDP, low purchasing power parit and, poor balance of payment.

Right now CCM has nothing to offer except kutaja urefu wa barabara za lami as if ni muhimu zaidi ya ajira na mfumuko wa bei people can live without barabara za lami but they can't live without works that means kipato.
In TZ /Under the SUN no1 is UNTOUCHABLE. we just need to be honest.

I agree with you 100%, Mwalimu has done a lot but remember, he himself said we should not carry what he has done wrong.

If we do not discuss and just "leave" it, how shall we know what it is which was not right?

Don't you think its vital to for the nation to "leave" the wrongs and carry the rights?

You may open a new thread on the other leaders you have mentioned and we shall discuss about them, their wrongs and their rights. No problem. I think it is not right at all to compare them with Nyerere or even to humiliate them as it is not a secret, at least two of those leaders, namely Mwinyi and Mkapa were his chosen ones.

Talking about corruption, kindly read this article which appeared in the New York Times:

Still, his critics, who included free-market liberals and conservatives, condemned him for adopting paternalistic and coercive policies like ujamma. They deplored his insistence on one-party rule and price controls, which they said stultified Tanzania's economy, shrank agricultural production, encouraged corruption and led to vast squandering of foreign aid.

Yes, I thought the untouchables are found in India only but in Tanzania as well, good one.

Read more: Julius Nyerere of Tanzania Dies; Preached African Socialism to the World
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Kambarage siyo 'Kmabarage' wewe si ndiyo huwa unawasahihisha wengine kuandika kiswahili fasaha?
 
Tunaweza kumlaumu Nyerere....na ni kweli alishindwa kuwa na misingi thabiti kwa taifa...! lakini alishindwa kutokana na waliomuweka madarakani tena upo wakati bila yeye kujua kama anakwamishwa kwa yale aliyokua na dhamira nayo njema kwa taifa...lakini hakushindwa kwasababu ya utashi binafsi wa hama kujinufaisha au kwa namna yoyote ya maslai yake yeye kama yeye... na hiyo ndio tofauti yake na wote waliomfuatia.......
 
Kuna siku, zamani sana, nilikutana na msomi mmoja wa enzi hizo (sjuwi yuko wapi kwa sasa) anaitwa Dr. Mujuni, alikuwa katibu mkuu wizara ya viwanda enzi hizo. Alinambia kuwa "Mzee haambiliki wala hashauriki". Sikushangaa.

Ikiwa msomi anasema hayo, fikiri.

Tuwaombe tu watawala wetu wasirudie hayo makosa ya kutokushaurika na kutokuambilika.
Wasomi ktk Afrika ndo waloifikisha hapa ilipo, bado unaamini usomi wao. Tz ya Nyerere iliongozwa na wasomi wachache na ya leo hadi ngazi ya shule ya msingi na watendaji wa vijiji kuna wenye degree, bado tu unauamini usomi usiokuwa hata na maono.

Usomi ni nguzo ktk utawala lakini si lolote ktk uongozi. Hatukujua wapi twende, Nyerere alitucholea njia, sasa tunajua wapi twende tumeduwaa, lawama kwa aliyetucholea njia eti.

Nyerere ni miongoni mwa viongozi wema waliotukuka na kuwatendea kwa wema watu wake ktk ulimwengu huu. Wengineo ni mitume na manabii.
 
Nyama weka wewe, mimi nimmelianzisha tu au uliza ujibiwe, hii ni open forum.

Hilo halina shaka kuwa alikuwa mpigania Uhuru mzuri sana na sababu alizitowa kwanini, wala hakuna ubishi katika hilo, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Lakini, jee ilikuwa na umuhimu wowote kwa Wananchi wake?

Nakumbuka Kenya walikataa kujiingiza katika mambo hayo lakini ukitazama hakuna walichokikosa na sisi hatuna tunachofaidika nacho, kama haitoshi pengine tunafukuzwa huko huko kwa tulio "wasaidia", juzi juzi tumesikia Watanzania wakifukuzwa kama mbwa huko Msumbiji na tumeshasikia kama hayo Afrika Kusini, kwa msaada wa hali na mali na roho za Watanzania zilizotoka, inanibidi nifikiri kuwa Wakenya walifanya vyeama kutojiingiza kichwa kichwa kama sisi, na ulikuwa ni uamuzi mbaya, au? Tumefaidika nini?
Watu kama ninyi msingekuwepo enzi za Nyerere, yale mambo tungefaidika nayo saana. Kwakuwa mlikuwepo wenye uoni hafifu, ya mbeleni hamkuyaona. Ila ktk mahusiano ya kimataifa, kuwa na nguvu ktk diplomasia ni kuwa na nguvu kiuchumi na kijamii pia.

Tanzania ktk siasa za ndani ya Afrika na duniani, msingekuwepo akina ninyi ingekuwa kubwa kidiplomasia. Hata reli ya TAZARA na kiwanda cha URAFIKI na hata ushindi dhidi ya AMINI ni matokeo ya nguvu zetu ktk mawanda ya diplomatic. Nakushangaa, nilishawahi kusoma post yako na ukajinasibisha na usomi na kuishi sana nje, haya madogo kiaje usiyajue?
 
Kama yepi hayo "MAKOSA MAKUBWA SANAAAAAAAAAA" YA sasa ili tuliokuwepo tujikumbushe kama yaliwahi kutokea na tunayarudia au ni mapya kabisa.

Ndiyo lengo la huu uzi, tuyajuwe makosa ya kimsingi ambayo hayakutuletea tija ili tuwaombe viongozi wetu wasiyarudie.

Binadam hatuyajuwi yajayo lakini tunayajuwa yaliyopita na ndiyo mafundisho bora kabisa kujifunza kwa yaliyopita.
Kwwhyo utawala wa sasa na wa Nyerere, wa Nyerere ulikuwa ndo wenye makosa? Hata watawala wa sasa hilo hawawezi kulisema hivyo. Wanajua Nyerere alikuwa mtawala na kiongozi bora kuwahi kutokea nchini na hata kwa baadhi ya mataifa duniani.
 
Lawama zote ziende kwa CCM baada ya Mwalimu kung'atuka, takribani ni miaka 30 sasa tangu mwalimu akae pembeni lakini CCM hata hawajui nini priority kwa taifa, maadui watatu bado wanazidi kuwatafuna watanzania.
 
Kwwhyo utawala wa sasa na wa Nyerere, wa Nyerere ulikuwa ndo wenye makosa? Hata watawala wa sasa hilo hawawezi kulisema hivyo. Wanajua Nyerere alikuwa mtawala na kiongozi bora kuwahi kutokea nchini na hata kwa baadhi ya mataifa duniani.

Wewe unamjuwa zaidi Nyerere kuliko anavyojijuwa mwenyewe?

Nyerere kafanya mengi sana mazuri, lakini mwenyewe anakiri kuwa yeye si malaika na kuna aliyokosea, jee, ni yepi hayo?
 
Back
Top Bottom