Kama binadamu Nyerere amefanya makosa, lakini mazuri aliyoyafanya ni mengi kushinda makosa. Na nimesema makosa aliyoyafanya hakufanya kwa faida yake mwenyewe, haswa kwa elimu yetu, alifikiri wakati huo ndiyo itatufaa sisi Watanzania kwa kujitegemea sisi wenyewe. Wakati wa utawala wa Nyerere kulikuwa na mvutano wa siasa za communist na capitalism na Nyerere alikuwa hataki kufungamana na upande wowote, kwa hiyo aliona siasa ya kujitegemea bila kutegemea mataifa mengine ni bora kwa Watanzania.
Nakubaliana na wewe kabisa elimu ya kiwango cha kusoma na kuandika kilikuwa kikubwa Africa nzima na uhuru wa Watanzania kulalamika kuhusu Viongozi wao ulikuwa mkubwa, na kwa wakati huo elimu yetu ilikuwa ikienda na wakati huo.
Mambo yamebadilika , na Viongozi waliochukuwa kutoka kwa Rais Nyerere walikuwa na nafasi ya kuimprove education yetu kwenda na Wakati, badala yake wakaididimiza elimu yetu, wakauza benki zetu na viwanda, NBC ilikuwa ni benki yangu, na hii ilimuuma sana Rais Nyerere Wakati iliuzwa kwa bei ya kutupa, benki AMBAYO ilikuwa ikiendeshwa na Watanzania wenyewe. Nimeeleza wazi kuwa viongozi waliofuatia walikuwa na chance ya kuimprove education yetu, badala yake wakaivuruga nchi na nchi nzima ikakosa nidhamu. Wakati wa Rais Nyerere uonevu kwa watu wa kawaida ulikuwa hausikiki., cheo ni dhamana, kila mala Viongozi wakikumbushwa. Ukitumia Mali ya umma kwa manufaa yako mwenyewe hautaendelea kulala kwenye nyumba ya Serikali. Mwalim alikuwa sio selfish, he had Tanzania at heart.
Nakubaliana na wewe, kulikuwa Hakuna tofauti kubwa kati ya masikini na matajiri na ulikuwa huwezi kujitajirisha kutumia Mali ya umma wazi wazi kama tunavyoona Viongozi wa leo. Vitendo wanavyofifanya Viongozi wa leo, wizi wa wazi wazi wa Mali za umma, na bado wako bungeni na wengine bamoja na record mbaya ya kutumia ama kuiba Mali za umma bado wanadhikila nafasi zao, na wengine wako bungeni wakiendelea kututungia sheria, Wakati wa Mwalimu isingetokea.
Umeanza na kusema ni kweli Rais Nyerere kama binadamu alifanya makosa, kisha ukamalizia amefanya makosa gani? Narudia tena, Rais Nyerere hakufanya makosa kwa kusudi ili ajinufaishe mwenyewe, uamuzi wote alioufanya wakati huo alifikiri ulikuwa wa kuwanufaisha Watanzania. Na hii inagusa elimu yetu, vijiji vya ujamaa, na kadharika.