Hakuna anepinga kuwa Nyerere ni Rais wa kwanza Tanzania, ninachosema ni kuwa Nyerere aliweka misingi mibovu ya kuongoza nchi na ndio chanzo cha Tanzania katika wakati wake kuwa wa mwisho kiuchumi, wa mwisho kielimu, wa mwisho ki michezo, wa mwisho ki diplomasia na wa mwisho ki mawazo. Aliharibu kila kitu. Niambie kimoja kilichofanikiwa.
Nimependa jinsi unavyoweza kukwepa maelezo yangu ili uone bado nina hoja ya kujibu.....! Km umeweza kusema WATU,ARDHI,SIASA SAFI na UONGOZI BORA villiuawa na yeye aliyeviamini kuwa ndio msingi wa maendeleo basi nimeamini sijadili siasa na wewe isipokua ni maoni yako na ufikiri wako tu wala si Siasa.....!
Ki UCHUMI...! Kama taifa tulijiwekea malengo ya kufikia kuwa taifa lenye viwanda, malengo haya yalikuwepo na yalitekelezeka kwa kiwango cha Serikali .... uendeshaji wake haukuwa wa mafanikio kwa sababu Watanzania walidhani ni lelemama na serikali iliviweka viwanda ili Watanzania waviendeshe wenyewe siyo tena Nyerere aendeshe ,...!
Ki elimu... Kabla ya Uhuru kulikua hakuna elimu ya utatu (UNIVERSITY)
wala utibabu vyoote hivi alivianzisha. Elimu ya msingi ilikua ni haki kwa kila raia, kukawepo na Polytechnic, kwenye mashirika ya uma kulikua na vyuo vya kuwaendeleza wafanyakazi na wengi waliweza kufikia hadi kiwango cha degree....kulikuwepo na Elimu ya Watu wazima..... mtu aliweza kujiendeleza hadi kufikia elimu ya "utatu". Elimu kwa njia ya Posta Tanzania nzima....! ambayo haikuweo ktk nchi zingine jirani....misingi hii iliruhusu kila aliyetaka kujiendeleza kielimu alisaidiwa kwa uwepo wa aina mbali mbali za kujiendeleza kielimu....hadi elimu ya Utatu....!
Ki michezo kwanza kulikua na timu za taifa za michezo zaidi ya mmoja....Mpira wa miguu, Mpira wa magongo, Mpira wa Kikapu, Mpira wa pete, Mpira wa Mikono, Mpira wa vinyoya, Mpira wa Meza, Mchezo wa Riadha ... michezo yote hii ilikua na ligi zake za ndani na pia zilishiriki mashindano ya nje kiumahiri... handball (Mpira wa Mikono) tulikua tuna sifika "zone" yetu, Riadha medali za dhahabu na shaba zilipatikan katika mashindano ya Commonwealth na Olympics...kwa sasa tuna timu ya taifa ya Mpira wa miguu peke yake... hatuna medali yoyote ya mashindano ya kidunia.... Labda majuzi "Cheka"
Kidiplomasia ....!Tanzania ndio nchi iliyopewa majukumu ya uhuru wa nchi za Kusini kwa Africa katika kitengo cha OAU
SALIM AHMED Salimini alikuwa mwenyekiti wa baraza la Usalama lililorudisha kura turufu ya Uchina ndani ya baraza hilo
Rais Nyerere, Neto wa Yugoslavia na wengine wa 4 walianzisha kundi la kidiplomasia la "Disarmament Group" lililojadili kuipunguzia silaha kali Duniani na leo ndio unasikia km juhudi za "non proliferation zone" ziki elekezwa kupunguza silaha.
kulifunguliwa ofisi za PLO Dar es salaam
Usuluhishi wa matatizo ya Burundi nk
Ki mawazo....!
Wazo la kuanzishwa kwa "nchi zilizo mstari wa mbele" ambazo ndiyo iliyokuwa chachu ya uhuru wa nchi za Kusini mwa Africa.
Uhuru wa Zimbabwe ulivyo buniwa na Nyerere...!
Hotuba ya Nyerere Indonesia iliyo amsha ari ya wananchi wa East Timor waliokuwa waki kandamizwa
Muundo wa South South Commission na hata Gettude Mongella kuwa katibu Mkuu wa Beijing Women Conference
Sijui km unanielewa au niache kujiele... Manake sioni km unalolote zaidi ya kupinga hata ambayo sijayasema