Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.
Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?
Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?
Tujadili.
Nyerere amekufa miaka zaidi ya kumi iliyopita, na lingatuka madarakani miaka zaidi ya ishirini iliyopita na tangu aondoke madarakani wamekuwepo marais Ali Hassan Mwinyi (miaka 10), rais Benjamin Wiliam Mkapa (miaka 10) na Rais Jakaya Mrisho Kikwete (miaka tisa). Ukifanya Hesabu ya haraka mtoto aliyezaliwa siku nyerere anang'atuka madarakani hivi sana ana zaidi ya miaka 29.. huyu ni mtu mzima mwenye familia yake na possibly ana mtoto ambaye ashaanza darasa la kwanza... Tanzania sasa ina zaidi ya watu milioni arobaini na wote wana ubongo kama wa huyo marehemu baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere lakini hatuwezi kuutumia tunawaza misingi aliyoacha nyerere... hii ni aibu kubwaaa na kuwaza hivi ni dalili za kuchoka kufikirii.. Nini kilichofanya hao marais wengine wasiweke hiyo misingii?!! Leo tunajadili katiba mpya ambayo ndio msingi wa taganyika ijayo lakini baadhi ya watu wamekuwa wanafiki, wazandiki na kila wafanyalo wanaangalia maslahi yaona mtumbo yao na kulindana kwa misingi ya vyamaa... JIUNGE NA VUGUVUGU LA MABADILIKO JENGA TANGANYIKA IJAYO KWA AJILI YA WAJUKUU ZAKO NA MWACHE LATE MWL. JULIUS NYERERE RET IN PEACE PLEASE.
NOTE; Hoja zako nyingi zimeegemea katika ubaguzi wa kidini zaidi na si ajabu haya yote unayaona kwa sababu nyerere hakuwa wa dini yako...
On serius note; viongozi wa nchi sio mitume kiasi kwamba bado tuendelee kuabudu na kusoma hadithi zake za miaka elfu mbili iliyopitaa... nyerere alikuwa binaadamu ana alikuwa na mazuri yake na mabaya yake hivyo yale mazuri ni ya kutujenga hata yale mabaya yanatakiwa yawe funzo kwetuu.. Rais Kikwete yupo hai na anakusikia kwanini usimlamikie yeye aweke hiyo misingi unayoitaka umwache mzee wa watu apumzike huko alikoooo?!!!