Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Katafute maana ya "protectorate" na "colony", ukiipata ndio uje kubishana.

Jee, Nyerere kafanya makosa makubwa ya kuweka msingi mbovu wa nchi au la, jibu utalotoa ueleze na kwanini umejibu hivyo. Mimi nasea aliweka msingi mbovu na ndio maana akaitoa nchi kutoka kwenye neema na kuiingiza kwenye umaskini wa mwisho duniani kabla hajang'atuka. Na huo msingi wake mbovu aliouwacha ndio kwanza umeanza kusambaratishwa na nchi inaanza kujengeka kwa kasi zaidi.

Yaliyokuwa haramu wakati wa Nyerere kwa sasa yote ni halali. Unalijuwa hilo?

Fauzy haya yote uyasemayo ni ya kufikiria tu.... ! kinachojengeka sasa hakina ustawi wa jamii ( human development) ila ni Hali ya kutafutia sifa ili wa onekani .... Kuistawisha jamii uakumletei sifa kiongozi ila huijenga jamii bila sifa za kuonekana ila jamii ikiimarika hakuna wa kuizuia kufikia maendeleo inayoyataka.....!

Nyerere aliamini mamlaka ya kiuchumi kusimamiwa na serikali kuu (njia kuu za uchumi kumilikiwa na serikali) ... mantikai ya hii yalijidhihirisha wakati wa Uchumi wa DUNIA kuanguka 2008

Serikali zote Duniani zikiongozwa na USA na UK ziliyafanya yale yote Nyerere aliyoyaamini ili kuunusuru uchumi wa DUNIA kwa serikali zao kumiliki Mabenki mkubwa ya nchi zao sera ambazo Nyerere aliyasema mwaka 1983 Cancun.
Sera za Azimio la Arusha ni moja ya mbinu zilizotumika kuuinua uchumi wa
Malaysia ... ushahidi wa hili ni wa kielimu na utafiti sina hakika ka ni Fauzy unatafiti hizi.... sera za uchumi wa nchi jirani zinaiga aliyoyaamini Nyerere na ushahidi upo bahati mbaya Mtoa mada hajajibidisha hata kidogo kujibidisha kujua hata machache...!

Kifupi sera za Nyerere ndiyo msingi wa utaifa wetu na maendeleo tuliyoyafikia leo.... hakuna maendeleo yaliyofikiwa na taifa hili nje ya CCM ambayo ni mojawapo ya dira za Nyerere km unaamini yapo maendeleo yaliyofikiwa leo ambayo yana kataa misingi ya Nyerere basi CCM haipo madarakani.
 
Wewe unaongea nini? sijui kustawisha sijui kujengeka jamii. Watu wako kwenye mengine kabisa. Huyo Nyerere alikustawisha na au kuijenga vipi jamii? wakati falsafa yake ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa ni ya kufikirika, imeshindwa kutimizwa toka 1967 mpaka anang'atuka. Matokeo? kila kitu hohehahe, si jamii, si watu, si nchi.
 
Unataka kujadili nini wakati, hutaki mabadiliko??? makosa ya Nyerere ni ya TANU NA CCM pia, ni yako pia maana unashabikia waliofanya makosa makubwa kuliko hata ya Nyerere, shame on you!
 
Makosa ya Nyerere ni ya Nyerere usihusishe chama, hata hao wenye vyama vingine wakati huo walikuwa hukohuko. Na thubutu kama waliweza kunyanyua hata sauti. Cheza na dikteta weye.
 
Wewe unaongea nini? sijui kustawisha sijui kujengeka jamii. Watu wako kwenye mengine kabisa. Huyo Nyerere alikustawisha na au kuijenga vipi jamii? wakati falsafa yake ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa ni ya kufikirika, imeshindwa kutimizwa toka 1967 mpaka anang'atuka. Matokeo? kila kitu hohehahe, si jamii, si watu, si nchi.

Nilichokihofia ndicho ninachokipata kutoka kwako... ufinyu wa uelewa.... Ustawi wa jamii ndio msingi wa sera ya Ujamaa na Kujitemea na wala siyo vinginevyo ....WATU, ARDHI,SIASA SAFI na UONGOZI BORA ndio msingi wa maendeleo ... hapa lisilo la kweli ni lipi? Kwamba hatuhitaji watu ili tuendelee? Hawa WATU ili wawe wenyetija USTAWI ni muhimu (yaani USTAWI WA JAMII) .... ndio maana nikazungzia ustawi wa jamii Budget kubwa ya awamu ya kwanza ilijikita katika ustawi wa jamii na siyo maghorofa au barabara za lami (nyingi zilikua za kiwango cha changarawe ili kupata fedha kiasi kusaidia USTAWI WA JAMII) kubwa lillilo endesha sera za Nyerere siyo hayo unayoyaita maendeleo Ujenzi wa Maghorofa nk. haya hua ni matokeo ya Ustawi wa jamii ... 1961 Ma-Engineer walikua hawafiki 10 katika watu Mil. 9 wapo waliosomeshwa nje ya nchi na ndani ya nchi mpaka leo hii wapo kwa maelfu....Rais Kikwete ni moja ya zao la Nyerere na amesome Digree yake UDSM chuo kilichojengwa kwa bajeti hiyo hiyo ya Ustawi wa jamii ..... nashangaa hauamini km misingi iliyoijenga Nyerere Ina tija sijui unawezaje kutenganisha yaliyopo sasa na aliyoyaanza Nyerere....!???!
 
Makosa ya Nyerere ni ya Nyerere usihusishe chama, hata hao wenye vyama vingine wakati huo walikuwa hukohuko. Na thubutu kama waliweza kunyanyua hata sauti. Cheza na dikteta weye.

Mbona unaamini kwenye makosa ya Nyerere na unataka tuamini kauli ulizozizalisha mwenyewe kuwa ndio msingi wa uelewa wetu? Uelewa wako ni potofu mno yaani ... unatishia kujua km kuna watu wana kuamini basi taifa hili halipo na km lipo basi kwa kuukataa ukweli hua anazaliwa mtu wa utenganishi na mwenye siasa za uzushi... Hivi kweli wewe unaweza kujisikia unatija kuliko Nyerere kweli umejikweza kiasi cha kutisha,
 
Nilichokihofia ndicho ninachokipata kutoka kwako... ufinyu wa uelewa.... Ustawi wa jamii ndio msingi wa sera ya Ujamaa na Kujitemea na wala siyo vinginevyo ....WATU, ARDHI,SIASA SAFI na UONGOZI BORA ndio msingi wa maendeleo ... hapa lisilo la kweli ni lipi? Kwamba hatuhitaji watu ili tuendelee? Hawa WATU ili wawe wenyetija USTAWI ni muhimu (yaani USTAWI WA JAMII) .... ndio maana nikazungzia ustawi wa jamii Budget kubwa ya awamu ya kwanza ilijikita katika ustawi wa jamii na siyo maghorofa au barabara za lami (nyingi zilikua za kiwango cha changarawe ili kupata fedha kiasi kusaidia USTAWI WA JAMII) kubwa lillilo endesha sera za Nyerere siyo hayo unayoyaita maendeleo Ujenzi wa Maghorofa nk. haya hua ni matokeo ya Ustawi wa jamii ... 1961 Ma-Engineer walikua hawafiki 10 katika watu Mil. 9 wapo waliosomeshwa nje ya nchi na ndani ya nchi mpaka leo hii wapo kwa maelfu....Rais Kikwete ni moja ya zao la Nyerere na amesome Digree yake UDSM chuo kilichojengwa kwa bajeti hiyo hiyo ya Ustawi wa jamii ..... nashangaa hauamini km misingi iliyoijenga Nyerere Ina tija sijui unawezaje kutenganisha yaliyopo sasa na aliyoyaanza Nyerere....!???!

Nayo hio no ni elimu sasa mbona tunaigopa kugungua vibali ili East african wafanye kazi popote
Si kwa sababu tunaogopa walosoma kweli ?
Yapo alofanya mazuri hatukatai lakini kiujumla nchi imekua kama ina ulemavu
 
Nilichokihofia ndicho ninachokipata kutoka kwako... ufinyu wa uelewa.... Ustawi wa jamii ndio msingi wa sera ya Ujamaa na Kujitemea na wala siyo vinginevyo ....WATU, ARDHI,SIASA SAFI na UONGOZI BORA ndio msingi wa maendeleo ... hapa lisilo la kweli ni lipi? Kwamba hatuhitaji watu ili tuendelee? Hawa WATU ili wawe wenyetija USTAWI ni muhimu (yaani USTAWI WA JAMII) .... ndio maana nikazungzia ustawi wa jamii Budget kubwa ya awamu ya kwanza ilijikita katika ustawi wa jamii na siyo maghorofa au barabara za lami (nyingi zilikua za kiwango cha changarawe ili kupata fedha kiasi kusaidia USTAWI WA JAMII) kubwa lillilo endesha sera za Nyerere siyo hayo unayoyaita maendeleo Ujenzi wa Maghorofa nk. haya hua ni matokeo ya Ustawi wa jamii ... 1961 Ma-Engineer walikua hawafiki 10 katika watu Mil. 9 wapo waliosomeshwa nje ya nchi na ndani ya nchi mpaka leo hii wapo kwa maelfu....Rais Kikwete ni moja ya zao la Nyerere na amesome Digree yake UDSM chuo kilichojengwa kwa bajeti hiyo hiyo ya Ustawi wa jamii ..... nashangaa hauamini km misingi iliyoijenga Nyerere Ina tija sijui unawezaje kutenganisha yaliyopo sasa na aliyoyaanza Nyerere....!???!

Huo Ujamaa ukaua hivyo vyote. Au unausikia tu? ulikuwepo wakati wa utawala wa Nyerere?
 
Mbona unaamini kwenye makosa ya Nyerere na unataka tuamini kauli ulizozizalisha mwenyewe kuwa ndio msingi wa uelewa wetu? Uelewa wako ni potofu mno yaani ... unatishia kujua km kuna watu wana kuamini basi taifa hili halipo na km lipo basi kwa kuukataa ukweli hua anazaliwa mtu wa utenganishi na mwenye siasa za uzushi... Hivi kweli wewe unaweza kujisikia unatija kuliko Nyerere kweli umejikweza kiasi cha kutisha,

Hakuna anepinga kuwa Nyerere ni Rais wa kwanza Tanzania, ninachosema ni kuwa Nyerere aliweka misingi mibovu ya kuongoza nchi na ndio chanzo cha Tanzania katika wakati wake kuwa wa mwisho kiuchumi, wa mwisho kielimu, wa mwisho ki michezo, wa mwisho ki diplomasia na wa mwisho ki mawazo. Aliharibu kila kitu. Niambie kimoja kilichofanikiwa.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Nayaheshimu sana mawazo yako japo sikubaliani nayo. Kwa nini? many people attribute success to resources such as gender, good family background, good school, good education, the right connections, good capital to do business, good job with hefty pay and other coveted things. Most of those who fail in whatever areas in life (mfumo mzuri wa siasa, taasisi, kiuongozi nk) usually blame it on lack of these attributes and strongly believe if they had those privileges, they would have succeeded (rejea mtazamo wako juu ya Nyerere). Hauko peke yako, watu wenye mitazamo hii wako wengi, mtaani/kazini si nadra kusikia kauli zifuatazo:

If only I was born different....

If only I had been born in a rich family...

If only I had capital to start a business I would not be in this stressful job...

If only I had an opportunity to go America or Europe...

If only I attended a good school I would have gone to university...

If only I have a godfather in the government or big corporations....

If only I had money I would not be living this kind of life....

If only I had an otherwise I could not be in this awful relationship...

If only I had free time I would attend evening classes and improve my career...

If only my circumstances were different..... etc
[List ni ndefu]

Such thoughts and beliefs are mere misconceptions and setbacks to success! hebu tujiulize, ni mara ngapi hatutimizi wajibu wetu wa msingi na kuishia kuwalaumu mambo kama poverty, corruption, and failure of leadership to mention a few, this is what many people believe to have caused problems in our communities. I personally believe very strongly that these are not the problem but are mere manifestations. THE REAL PROBLEM IS IN THE MIND. IF we can change our mentality, we can lead as others. You are in your present situation because of your mind-your thinking, your attitudes, world view and the actions you take based on them!Let's NOT spend more time wishfully thinking if we were born in different country or family, went to a different school, worked for a different company, and so on [kama Mwl. Nyerere angefanya lile na lile......!!!!??????] we would be better.
Nikutie moyo kuwa, some of the men and women who have transformed this world did so during hard economic times, the worst regimes the world has ever had, and in absolutely corrupt systems. The trouble is probably you have not known your true self. It is something to do with Psychology! NIKO TAYARI KUSAIDIA, Karibu sana
 
Kujenga umoja wa kitaifa, hali ya utulivu na amani kwa taifa na kukuza lugha ya kiswahili.

Nani alikwambia Tanganyika ilikuwa haina umoja? Mfano mzuri katazame majumba ya zamani yaliokuwa kila mji mkubwa na kijiji kikubwa uulize ya kina nani, utaambiwa, yale ya mmnyema, yale ya mnyamwezi, yale ya mwaarabu, yale ya mhindi, yale mzungu, yale ya mzaramo. Tuliona wakiishi pamoja Tanganyika nzima. Nyerere aliyakuta hayo wala msitake kumpa sifa ambayo si yake.
 
Kwani wakti wa ukoloni Tanganyika kulikuwa hakuna umoja? Je tanganyika wakti huo kulikuwa na vita vya koo na koo au makabila kwa makabila Nyerere akazuia na kuleta umoja na utulivu kitaifa?

Mimi naona si vizuri kumpa swifa asizo stahiki. Utulivu na amani ni tunu toka kwa Muumba kwa WaTz na sio Nyerere kavileta.
 
Hakuna anepinga kuwa Nyerere ni Rais wa kwanza Tanzania, ninachosema ni kuwa Nyerere aliweka misingi mibovu ya kuongoza nchi na ndio chanzo cha Tanzania katika wakati wake kuwa wa mwisho kiuchumi, wa mwisho kielimu, wa mwisho ki michezo, wa mwisho ki diplomasia na wa mwisho ki mawazo. Aliharibu kila kitu. Niambie kimoja kilichofanikiwa.

labda tudadavue mabo haya ambayo JKN aliyafanya mara baada ya uuhuru wa TGK
1. Africanization. hapa aliwatoa wazungu na kuweka waswahili katika nafasi nyingi za uongozi. hapa alifanikiwa/
2. Azimio La Arusha . hapa kwa kuwa alikuwa hajawaandaa wananchi wake hivyo Azimio hili liliua uchumi wa TGK.
Mind you alipopewa uhuru Dola moja ya marekani ilikuwa sawa na Shilini moja na sent ishirini ya Tanzania. Baa ya miaka kumi ya uhuru yaani 1972. Dola 1 ya marekani ilikuwa sawa na shilingi 28 za Tanzania.

Siasa ni Kilimo na vijiji vya ujamaa. siasa tupu havikufanikiwa kiuchumi bali ilikuwa ni lazima na kulazimisha watu na kumaliza kabisa uchumi mdogo wa mtu mmoja mmoja na kusababisha kukosekana kwa vitu hadimu na kusababisha maduka ya kaya na ulanguzi.

Na mengine mengi
 
Mkuu naona unajaribu kuelimisha makosa ya nyerere kwa watu wasiojielewa lakini bado watu wenyewe wapo gizani so kuwapa magazeti wasome ni kupata hasara tu,ni bora uwaache tu raiya hawa wasiojua hata tupo karne ya ngapi..wamesahau watu walipovaa magunia baada ya nguo kukosekana,wamesahau tuliponyimwa uhuru wa habari na kuwekwa radio 1 tu..
 
Nakubaliana na wewe kwamba Nyerere alifanya makosa makubwa ambayo ni:

1. Kuua vyama vingi na kuunda chama kimoja alichokiita ccm na kukifanya chama-dola. Maumivu ya uamuzi huo tunayo mpaka sasa
2. Kuleta sera ya Party Supremacy (Chama kushika hatamu) ambako kulifanya mihimili mingine ya dola kuwa inferior na kuonekana ni mkono wa chama. Jambo ambalo, hata baada ya miaka 28 ya Nyerere kuondoka madarakani na miaka 21 ya vyama vingi ccm bado inaota ndoto ya chama kushika hatamu

Pamoja na hayo, alifanya mengi mazuri kama ambavyo wengine wamefafanua kwenye uzi huu.

Kubwa kuliko yote alilofanya vizuri ni kukiri hadharani kwamba yeye siyo malaika hivyo yale mazuri aliyofanya yaendelezwe na yale mabaya yaachwe.

Tatizo hapa ni kwamba awamu zilizofuata baada yake zimefanya kinyume na nasaha hizi.
 
Umesahau kwamba wakati Nyerere anastahafu aliacha viwanda vya kuchambua pamba,Viwanda vya kusindika nyama,Viwanda vya zana za kilimo,Viwanda vya ngozi,Kiwanda cha Radio na betri cha National,Kiwanda cha Matairi cha General Tyre,Viwanda vya Nguo,Kiwanda cha kutengeneza Ndara,Shirika imara la Reli,Shirika imara la Ndege,Bomba la kusafirisha mafuta la TAZAMA,Je viko wapi vitu vyote hivi alivyowaachia Nyerere @ Faiza?Si wameviua hao hao unaowasifia.Sasa ni Misingi gani tena ya kiuchumi ulitaka Nyerere awaachie?
 
Nani alikwambia Tanganyika ilikuwa haina umoja? Mfano mzuri katazame majumba ya zamani yaliokuwa kila mji mkubwa na kijiji kikubwa uulize ya kina nani, utaambiwa, yale ya mmnyema, yale ya mnyamwezi, yale ya mwaarabu, yale ya mhindi, yale mzungu, yale ya mzaramo. Tuliona wakiishi pamoja Tanganyika nzima. Nyerere aliyakuta hayo wala msitake kumpa sifa ambayo si yake.

Oh! Kumbe! Sasa serikali ya CCM chini ya mtukufu Jakaya Mrisho Kikwete mbona uwa wanasema 'tutunze amani na umoja wa kitaifa ulioasisiwa na viongozi wetu wa kwanza wa taifa letu.'

Pia uwa anajitapa sana pamoja na wapambe nuksi kina Nape et al. kwamba bila CCM Tanzania hakuna amani na umoja wa kitaifa!

Kumbe amani na umoja wa kitaifa ulikuwepo kabla ya CCM na serikali yake?

Vivyo hivyo utakuwepo baada ya CCM na serikali yake.

Waambie wapambe nuksi na Mtukufu Jakaya, waache kuchukua sifa zisizo za kwao.

Amani na umoja wa kitaifa wa Tanzania ni tunu tuliyopewa na Mungu.

Asante kwa somo hili bidada.

Cc: Barubaru
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom