Nurse Zai kutoka Kigoma umetoa fundisho

Nurse Zai kutoka Kigoma umetoa fundisho

Huyu mama ambaye wananchi wamemkatalia asihame kituoni kwake, kwa ajili ya ukarimu wake na moyo wa kuwahudumia watu kwa upendo.

Hadi umepewa uhamisho na wananchi kukukatalia usihame ili ubaki uendelee kuwahudumia.

Nakupa hongera na liwe fundisho kwa watumishi wote wanao wahudumia watu. Naimani siku ya wafanya kazi hautakosa zawadi kutoka kwa Rais

Magufuli. Big up.
Sasa hii Big up kwa magufuli au kwa nurse ??Magu kaingiaje hapo ??
 
Kazi hii ni kazi kama alivyo mchungaji au shehe kifanya kwa imani ..Na moyo ..Kulibeba tatizo na kulifanya lako kutoka jasho kwa ajili ya mtu ... Ni kazi ya kutoka ndani ya moyo.. ukiipenda kazi kwa moyo na imani ya kuhofu mungu utaifanya na majibu yake ndo haya sasa ....
 
Mungu ibariki nchi yetu mfano kama huu uwe kwa watumishi wengi wa afya tutaokoa wengi wenye matatizo... ... Hii ni nurse lakinj ni mfano kwa watumishi wote wanaohudumia jamii .. popote pale [emoji120]
 
Nurse amehakisi serikali ilivyo kuajiri watumishi kwa matakwa ya Umma... Hongera Chama tawala. Mbarikiwe,
 
Huo ni umasikini uliotukuka na watamfanya afe masikini... Kwahyo huyo nesi hataenda kusoma au kuwa promoted kisa wanakijiji wanampenda? What if huo uhamisho ulikua na lengo la kumpromote au kumpa chance ya kuonekana zaidi...
Inabid next tym afanye kimyaaaaa
 
Huo ni umasikini uliotukuka na watamfanya afe masikini... Kwahyo huyo nesi hataenda kusoma au kuwa promoted kisa wanakijiji wanampenda? What if huo uhamisho ulikua na lengo la kumpromote au kumpa chance ya kuonekana zaidi...
Alikuwa anasogezwa porini zaid
 
Huo ni umasikini uliotukuka na watamfanya afe masikini... Kwahyo huyo nesi hataenda kusoma au kuwa promoted kisa wanakijiji wanampenda? What if huo uhamisho ulikua na lengo la kumpromote au kumpa chance ya kuonekana zaidi...
Mr. Mtui, nadhani hata hapo ameonekana pia. Halafu kumbuka Jane Goodall alikuja na kuzama msituni huko Gombe akijifunza tabia za sokwe, lakini leo anafahamika kimataifa.
Kwahiyo siyo lazima ukae mjini au mahali gani ndipo uonekane, jitihada zako pekee ndizo zinazokufanya uonekane na ufanikiwe.
 
Nani kakwambia mfanyakazi bora ni yule anafanya kazi bora nooooo ni yule mtu anaependwa
 
duh ninavowafahamu manesi walio wengi wanastress hivi kwenye hii kada duh huyu anastahili kupewa zawadi ya pekee sana kama hao wananchi wanamkubali haswa.
Waambie wampatie pongezi huyo Zai
 
Mr. Mtui, nadhani hata hapo ameonekana pia. Halafu kumbuka Jane Goodall alikuja na kuzama msituni huko Gombe akijifunza tabia za sokwe, lakini leo anafahamika kimataifa.
Kwahiyo siyo lazima ukae mjini au mahali gani ndipo uonekane, jitihada zako pekee ndizo zinazokufanya uonekane na ufanikiwe.
Unachosema ni kweli.. But kumfananisha huyo nesi na Jane nahisi unakosea... Jane alizama msituni strategically kwa maana kwamba alikja anafanya utafiti... So kuna mashirika kadhaa yalikua nyuma ya mgongo wake yakimpa support kwa kile anachofanya.... Ikiwemo taasisi aliyokuwa anaifanyia kazi.. Kibongo bongo hatujafikia huko... Ukitupwa kijijini ujue ndo basi kwisha habari yako...Hatunaga utamaduni wa kuappreciate kitu mtu anafanya....
 
Nurse Zai . Anajua nini Maana ya taaluma yake , Pia Ana moyo wa uzalendo na kujari wengine .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom