NSSF kutatua tatizo la umeme Tanzania

kuna ukweli... ila pia ujue they could have done better kama wasingejiingiz kwenye siasa

BTW, kumbuka kuna current pressure ambazo zinalazimisha certain organization kubadili approach, hayo ya uzazi yangekuwepo tu tena bila ya dau, ni global trend.... hebu niambie kwanini nssf wanashindwa kuendesha bima ya afya??
Je wajua kwamba kama mfanyakazi unapolipia huduma za bima ya afya kupitia NSSF ni kwamba unafanya double contribution?? Gharama ulizotibiwa nazo utakuja kukatwa wakati unakuja kudai mafao ya uzeeni.....Kwa nini usitumie haki yako yamatibabu kupitia NHIF ambapo unakatwa 3% ya mshahara wako kisheria?? NSSF hua hawawaambii wanachama wao ukweli kua hizi garama za matibabu kama zinakuja kukatwa kwenye mafao yao ya uzeeni.
Wanatumia propaganda ya huduma za bima ya afya ili kupata wateja wakati hata hawana vituo vilivyosajiliwa kisheria kutoa hizo huduma.
Kama wewe hauko NHIF siyo mbaya una haki ya kuwa NSSF.
 
Hawawezi hata uwaletee Bill Gates wacha hilo Dau lako

Ikiwa sababu za kuandamana ni kutisha wawekezaji basi nakubaliana nawe "hawawezi". Lakini ikiwa vyama vyote vitakuwa na itikadi ya amani na utulivu iliyozoeleka Tanzania na ndio chanzo kikubwa cha kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi, basi itawezekana.
 
Daraja la Kigamboni its the thing of the past, katika mchakato wa daraja ikaoneka si daraja tu linalohitajika, ni kuiboresha kigamboni yote na NSSF wana/wata play part kubwa sana. Hujui kuhusu New Kigamboni City? Unanishangaza sana.
naijua sana, na ni mdau sana tu... sasa niambie, ile notisi ya kutunyang'anya maeneo yetu iliyokwisha oct 31 2010 mmeshairinyuu??

ushabiki mandazi ni kitu kibaya sana
 
Ikiwa sababu za kuandamana ni kutisha wawekezaji basi nakubaliana nawe "hawawezi". Lakini ikiwa vyama vyote vitakuwa na itikadi ya amani na utulivu iliyozoeleka Tanzania na ndio chanzo kikubwa cha kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi, basi itawezekana.

Wit Rostam hand of course mon ami
 
Huu ni wizi mpya unapikwa, kibaya zaidi safari hii wataibiwa wafanyakazi wawekao akiba yao pale na taifa kwa ujumla.
NSSF inatakiwa ikae mbali kabisa na shughuli za kuzarisha nguvu za umeme si kazi yao. Hata kwenye masuala ya Ujenzi wa nyumba na ukodishaji inabidi wajitoe kabisa wao biashara yao ni pesa na si vinginevyo

Si kila mwenye pesa anajiingiza kufanya kila biashara



sifa kubwa ya mwafrika ni kuona mwafrika mwenzake anashindwa na hujitahidi kufanya kila awezalo kumkatisha tamaa! hao ndio waafrika
 
naijua sana, na ni mdau sana tu... sasa niambie, ile notisi ya kutunyang'anya maeneo yetu iliyokwisha oct 31 2010 mmeshairinyuu??

ushabiki mandazi ni kitu kibaya sana

Ha ha ha ha lol!!! Kweli huu ushabiki maandazi kama ulivyosema
 
Its a good move but taratibu na sheria zote zifwatwe, yasije yakatokea yale yalee tuliyozoea kuyaona na kuyasikia!
 
Why not now? If not now when?

Daraja as far as I know in few months time contractor atakuwa site

msimsikilize tule waziri anayeitwa POMBE alikuwa ana bwatuka tuuu bila kujua hali halisi...si mmeona kakaa kimya?

wewe ni nani huko NSSF? hebu jaribu kujibu haya mambo hapa chini please

icon1.png
Nssf ieleze wananchi sababu kutojenga daraja la kigamboni


Ndugu zangu,

naamini wote mmefuatilia kwenye vyombo vya habari jinsi Dr. Magufuli na Dr. Harrison walivyoanza kazi jana Jumapili, siku moja tu baada ya kuapishwa. Katika magazeti ya leo, ujenzi wa daraja la Kigamboni ni mojawapo ya vipaumbele vya makamanda hawa wawili. Dr. Magufuli anadai maelezo kutoka NSSF ya kutojenga daraja la Kigamboni hadi leo na kama hawawezi waseme hivyo ili yeye akope pesa BoT na kulijenga.

Mimi siyo msekaji wa Dr. Magufuli wala wizara ha ujenzi. Lakini naomba nitumie taarifa zilizo wazi kwa jamii (public) kuonesha ni kwa nini Magufuli anataka maelezo kutoka NSSF.

Ujenzi wa daraja la Kigamboni uko kwenye Ilani za Uchaguzi za CCM za mwaka 2000 na mwaka 2005. Sina nakala ya Ilani ya 2000 lakini ukirejea ukurasa wa 54 wa Ilani ya 2005 utaona hii ahadi. Lakini Hansard ya Bunge ya tarehe 3 Agosti 2007 inawakumbusha Wabunge na Watanzania kwamba ahadi ya ujenzi wa daraja hili ilikuwepo hata kabla ya Ilani ya 2000. Bahati mbaya Mbunge aliyetamka haya maneno hakutaja mwaka hasa ambao ahadi hii ilianzishwa na CCM.

Hansard mbali mbali za 2006 na 2007 zinaonesha Wabunge, hasa wa Dar es Salaam (Zungu na Msomi) wakiulizia maendeleo ya ujenzi huu mara kwa mara. Kila mara wanajibiwa majibu ambayo hasa hayana mshiko.

Lakini tarehe 3 Agosti 2007 Wabunge hawa wakiungwa mkono na wenzao wengi walitia pressure kubwa na serikali ililazimika kujibu kikamilifu.

Kwamba NSSF ilianza upembuzi yakinifu 2003 uliogarimu dola za kimarekani 20,000, ambazo zililipwa kwa Howard Humfrey. Mwaka 2004 wakafanya upembuzi wa kina kwa garama ya dola 230,000. Kisha serikali ikasema kwa kuwa CCM imeliweka daraja hili tena kwenye Ilani yake ya 2005, basi ni lazima litajengwa na mchakato umefika mahali pazuri.

Awali Hansard ya 1 Agosti 2007, Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana alijibu swali Bungeni kwamba daraja litajengwa kwa sababu tayari Waraka wa Baraza la Mawaziri umeshatayarishwa. Kwamba waraka huo umeshapita kwenye ngazi ya Sekretariati ya Baraza la Mawaziri. Kinachosubiriwa ni Waraka huo ufike kwenye Baraza la Mawaziri na ambalo kama likiridhika litamshauri Rais aagize kuanza ujenzi wa daraja hilo la Kigambani. Waziri alisisitiza kwamba daraja hili litajengwa kabla ya 2010, kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM ya 2005.

Mheshimiwa Zungu aliibana serikali zaidi ieleze gharama za hili daraja na kama ni kitu ambacho serikali kweli imeshindwa kujenga. Alijibiwa tarehe 3 Agosti 2007 kwamba garama za kujenga daraja la Kigamboni ni Euro millioni 45 ambazo ni sawa na Shilingi billioni 91. Pia akaarifiwa kwamba Euro milioni 22.5 zitatolewa kama msaada na serikali ya Uholanzi.

Baadaye NSSF walitoa Tangazo kwene magazeti wakialika makampuni binafsi yenye nia ya kuingia ubia na NSSF katika ujenzi wa daraja la Kigamboni. Baada ya hili tangazo (bado nalitafuta nitaweka tarehe yake hapa) sijaweza kupata taarifa zaidi kuhusu mchakato wa ujenzi wa daraja hili. NSSF hawakuweka bayana ni makampuni mangapi na uwezo wao walioomba ubia huo. Serikali pia haijazungumzia tena na pengine Wabunge pia hawaja uliza tena kwani kwenye Hansard sijaweza kupata taarifa yoyote.

Ni kwa sababu hizi hapa juu naamini kwamba NSSF wana maelezo kwa nini daraja hili halijajengwa. Pia ni kutokana na Dr. Magufuli kuwataka wajieleze natamani kuamini kwamba pengine serikali ilikwisha kabidhi ujenzi wa daraja hili kwa NSSF.

Kama NSSF hawahusiki, watueleze nani alikwamisha huu mradi. Kama kuna ufisadi ulijipenyeza, tunaomba Dr. Magufuli na kamanda wake msaidizi Dr. Harrison waweke mambo hadharani ili iwe rahisi kwao kulishuhulikia tatizo hili.

Nimalizie kwa kuwatahadharisha hawa makamanda wawili (Dr. Magufuli na Dr. Harrison) kwamba kama walitoa hii kauli kama mtaji tu wa kutafuta cheap popularity ya kuanzia kazi, kuna watu wanafuatilia, na tutalifuatilia kwa nguvu zetu zote. Lakini itoshe kuwahakikishia kwamba tunawaunga mkono katika hatua hii ya awali.​
 
Wanaona kuiba kodi zetu haitoshi na sasa wemeamua kuiba na akiba zetu. Grrrrr !

Unajua msiongee haya mambo kwa ushabiki tu ati kwasababu Tanesco wanamatatizo sasa hivi. Matatizo tunayoyapata yanaletwa na serikali kusini mikataba mibovu. Kama NSSF watashughulika na umeme, Nataka nikwambie hakuna returns nzuri na ya uhakika kama umeme. Inategemea wanataka kuinvest kwa staili gani. Nadhani wamefanya tathmini yakutosha mpaka kufikia hapo. Wewe mwanachama unachotakiwa kufanya ni kuona kama utalipwa mafao yako au la. Unajua tusipokua creative hakuna mabadiliko makubwa tunayoweza kuyapata. Hivyo tunapaswa kuwapongeza NSSF kwa ubunifu huu, Ila tu tuone ni jinsi gani tunaweza kuwashauri jinsi ya kuuboresha mpango huu.
1. Wasijihusishe na serikali hii labda ya baadaye katika kuimpliment mpango huu.

2. Wahakikishe wanachama wao wanafaidi mpango huu kwa kuwapa kipaumbele kwa kuwapunguzia gharama za umeme.

3. Wasiwatumie mawakala katika kutekeleza mradi yaani katk kuagiza au kuendesha mitambo yao.

Nidhahiri tukajaribu kushauri juu ya mfumo wao wakuendesha kuliko kushabikia kua ni changa la macho. Je lini tutakua na fikra mpya kama fikra mpya zote tunaziponda. Tafadhari WanaJF wenzangu, I know we are all patriots on this country, thats why we raise doubts for whatever news comming, let us investigate before commenting in the matter.
 
naijua sana, na ni mdau sana tu... sasa niambie, ile notisi ya kutunyang'anya maeneo yetu iliyokwisha oct 31 2010 mmeshairinyuu??

ushabiki mandazi ni kitu kibaya sana

Kama umepewa "notisi" basi fanya uondoke haraka sana, hakuna kurinyuu, kuna mama mkali huyo, kinachofuatia ni tinga-tinga. Shauri yako.
 
Je wajua kwamba kama mfanyakazi unapolipia huduma za bima ya afya kupitia NSSF ni kwamba unafanya double contribution?? Gharama ulizotibiwa nazo utakuja kukatwa wakati unakuja kudai mafao ya uzeeni.....Kwa nini usitumie haki yako yamatibabu kupitia NHIF ambapo unakatwa 3% ya mshahara wako kisheria?? NSSF hua hawawaambii wanachama wao ukweli kua hizi garama za matibabu kama zinakuja kukatwa kwenye mafao yao ya uzeeni.
Wanatumia propaganda ya huduma za bima ya afya ili kupata wateja wakati hata hawana vituo vilivyosajiliwa kisheria kutoa hizo huduma.
Kama wewe hauko NHIF siyo mbaya una haki ya kuwa NSSF.

Kama hawawaambii ukweli wewe ulijuwaje? au wewe ndie unaedanganya?
 
Hawa nssf wapuuuuuuuuuuuuuuuuuuzi tuuu, wameshindwa kuwawezesha wateja wao kuwa na maisha bora hata kuwajengea nyumba bora kwa mikopo nafuu -wanaishia kufanya biashara na mafisadi -biashara ambazo hazimnufaisha mwanachama anaechangia michango yake kila mwezi. Pesa za wanachama zinatumika kwa mambo ambayo hayana tija kwa mwanachama mojakwamoja huu ni unyanyasaji na uporaji haki. Huo umeme wataweka nyumba za mafisadi? Au mbavu za mbwa au nyumba za kupanga za wateja wao. Mifuko ya jamii tanzania ipo kinyonyaji saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana.
 
NSSF???? they might be liaring. in 2005 they promised us to build Kigamboni Bridge, now where it is? Today they are fumbling around with such great multmillion dollars project, I don't believe in NSSF plans/promises
 
Of course Rostam will invest and he will invite other big time investors, connections za Rostam wewe kwako hata kwenye ndoto hazimo.


hivi we zomba ni mtanzania mwenye uchu na nchi hii kweli?
 
Back
Top Bottom