Kutatua tatizo la umeme, serikali ishirikishe wananchi kupatamaoni yao

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,041
Wadau nawasalimu.Nimekuwa nasoma maoni mbalimbali ya Wadau juu ya Tatizo kubwa la Umeme Nchini ila kila mtu Ana sababu zake wapo wanaowalaumu Tanesco wapo wanaoilaumu Serikali

Bila kupepesa MACHO anayejua TATIZO la UMEME Tanzania ni SERIKALI yenyewe tu na MTATUZI wa Tatizo hilo ni SERIKALI na sio VINGINEVYO.

Najaribu kujiuliza Maswali yafuatayo
1. Je Tatizo la Umeme ni UONGOZI wa Waziri au Mkurugenzi na Bodi ya Tanesco
2. Je Tatizo la Umeme ni Utalaamu wa Wafanyakazi wa Tanesco
3. Je Tatizo la Umeme ni Muundo wa Shirika
4. Je Tatizo la Umeme ni Vyanzo vya Umeme
5. Je Tatizo la Umeme ni Fedha
6. Je Tatizo la Umeme ni HUJUMA
7. Je Tatizo la Umeme ni SIASA
Majibu ya Maswali yote haya SERIKALI inayo.

Ili kumaliza TATIZO hili naiomba SERIKALI ikusanye MAONI na MAPENDEKEZO ya Wananchi juu ya UTATUZI wa TATIZO la Umeme kuna Watanzania wana mapendekezo mazuri tu yakichukuliwa na kufanyiwa kazi yanaweza kuwa SULUHISHO la Tatizo la Umeme nchini.

TANZANIA ni Yetu sote.
 
Back
Top Bottom