NSSF kutatua tatizo la umeme Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF kutatua tatizo la umeme Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Game Theory, Jan 10, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Wakati Pension Funds zingine zikiwa hazina Investment Policies zinayoeeleweka, NSSF on the other hand wameamua kwenda Kivyao na sasa wanaingia officially kwenye biashara ya investment ya Kuwa Independent Power Supplier Tanzania.

  Pension Funds zingine wamesema kuwa hili jambo wao wao bado ni kubwa mno na hawawezi kufanya maamuzi ya haraka kwani decision making Mechanism zao ni tofauti na NSSF (apparently ndio maneno ya ERIO wa PPF alipoulizwa lini wanaingia kwenye hii biashara)

  On the other hand Dr Dau kule NSSF washasema kuwa hawatokaa kusubiri na wameamua ku goa head na mpango wa kutuletea umeme kwani ni AIBU kwa taifa kufikisha miaka 50 huku tuko gizani

  For that I congratulate NSSF.


  Habari zaidi hapa:

  allAfrica.com: Tanzania: NSSF Set to Pour Funds in Electricity Generation


  This is the best news na naomba wawezeshwe maana to be honest its impressive na inatia moyo kuona kuwa kuna watu pamoja na matatizo yoote tulionayo kama taifa, bado tunao ma PATRIOTS


   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa kazi yao si ni kuinvest pesa za pensioners na kuzizalisha kwa wingi ili kuwanufaisha pensioners.... kwahiyo kazi yao sio kutoa service bali ni profit oriented....(kuangalia wapi wakiweka pesa itakuwa ina most returns) sasa kweli wamefanya homework na wameshaona return on investment au.....?
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hawa NSSF/PPF nitawaelewa kama wataelekeza investment zao kwenye kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya watu wa kawaida amabo ndio wateja wao wengi. haya mambo ya kujenga matower sioni kama yana faida kwa stakeholders.

  Kwa nini wasitenge bajeti ya kunjenga nyumba japo 50 kila mkoa kila mwaka na kuziuza kwa walimu,polisi na wafanyakazi wengine.

  Kama NSSF wanasaka faida hivyo sasa CRDB na EXIM wafanyaje.

  Nyumba ni best asset kwa pensioner kuliko pension ya mshiko.

  Mkuu sikubaliani nawe kwa hoja hii kwani Mission ,vision au core business ya NSSF inatakiwa kuwa nini.

  Usije ukajikuta unawasifu hata CCM au CDM wakitsema wanaleta mitambo kama hiyo just bcs kuna tatizo la umeme
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Creativity ni muhimu kwa maendeleo ya nchi! Hongereni nssf.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kuna haja ya ile regulatory body kuingilia hii mipango kwani siku haya mashirika yakipata hasara watakaoumia ni sisi tunaochangisha... we will have nothing when we retire/expire

  stakeholders involvement is also very important, ni pesa zetu kwa hiyo kila wanapoingia kwenye hizi ventures, our concurrence is vital... what if the venture fail? who will shoulder the loss?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,852
  Likes Received: 83,307
  Trophy Points: 280

  Umenena hapo Mkuu. Kutokana na mikataba ya kifisadi kila kona ya nchi yetu stakeholders inabidi wahusishwe katika maamuzi makubwa kama haya ili kuweza kupata idhini yao, vinginevyo management ya NSSF itakuwa inafanya maamuzi ambayo hawana haki ya kuyafanya bila ya kuwashirikisha wenye mali yao.
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Huu ni wizi mpya unapikwa, kibaya zaidi safari hii wataibiwa wafanyakazi wawekao akiba yao pale na taifa kwa ujumla.
  NSSF inatakiwa ikae mbali kabisa na shughuli za kuzarisha nguvu za umeme si kazi yao. Hata kwenye masuala ya Ujenzi wa nyumba na ukodishaji inabidi wajitoe kabisa wao biashara yao ni pesa na si vinginevyo

  Si kila mwenye pesa anajiingiza kufanya kila biashara
   
 8. v

  vassil Senior Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  I dont think there is anyone out there who knows whats in NSSF books I have a feeling future governments will have to bail it out ,they are not transparent they are getting ripped off big time in their real estate deals now they wanna get into what?utility please
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Eti wajenge nyumba zakuuzia polisi na waalimu..lol That is BS and those are not even investments, pensioners will die bila sumni
   
 10. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  hivi NSSF did they involve members to discuss this, je when business goes bankrupt what will they say? hivi huyu Dau na yeye anaamka tu
  na kutoka kwake na kutoa decision, seems one sided, wanachama uliwauliza? hela si zako hizo za wanachama, talk to them, let them
  seat down with board members wakikubali na uwezo upo then GO ahead, ila TAHADHARI hakuna mkono/ushauri toka kwa mafisadi
  ili mtupooze kwa DOWANS kulipwa, inaonekana kama mnataka kufukia mashimo wakati issue ya Dowans is HOOOT
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Afadhali na wewe umeshtuka. Niliuliza ivi posho za wakurugenzi wa nssf ni kiasi gani...hakuna mwenye jibu! Hizi ndo parastatal bodies zetu!
   
 12. T

  Taso JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  kazi yao inatakuwa kuwa ni mfuko wa Taifa ya hifadhi ya jamii, kwa mujibu wa sheria.

  Haya mashiriki ya umma, kila moja, linaanzishwa kwa sheria ya Bunge kwa kazi maalum.

  Hizi habari za NSSF kugeuka TANESCO ni uongo mtupu
   
 13. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Huko nyuma walisema wangewekeza katika ujenzi wa daraja la Kigamboni. Iliishia wapi? Hili ni changa jingine la macho.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kufuwa na kusambaza umeme ni investment kubwa inayolipa vizuri sana.

  Usione Tanesco invyokufa ukafikiri kuwa si biashara nzuri. Tanesco ni wenyewe wanaofanya madudu, wizi, ubadhirifu ndio unawafikisha pabaya, kama kawaida ya mashirika yote ya uma yaliyokufa.

  NSSF huwa wanaingia mikataba na mashirika binafsi na wao huinvest mifedha na huwaachia wenye uzoefu wa mambo hayo kuendesha hizo kazi, na kaka ujuavyo, kila kiwanda au shirika la uma linaposhindwa, likichukuliwa na watu binafsi linashinda.

  Nampa pongezi Dau kwa kuiona hii opportunity.
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wanaona kuiba kodi zetu haitoshi na sasa wemeamua kuiba na akiba zetu. Grrrrr !
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Why now????????? Kuna institution zingine zinachukulia hili suala la umeme dili kwao btwn NSSF wamefanya homework ya kutosha on this project maana wasije wakainvest pesa za pensioners halafu tukasikia habari nyingine. Vile vile suala la Daraja la Kigamboni wameishia wapi maana naona wanaruka form one project to another ili hali hakuna ambacho kimeishafanyika on the previous project ya Daraja la Kigamboni sijui tuwaelewe vipi????
   
 17. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Guys

  Naomba bora tuliangalie hili suala kwa marefu na Mapana maybe for once tungeacha ushabiki na kuwa walau objective kwenye kujibu au kuchangia hii mada. One would have thought kuwa kijireserach kidogo na hasa from someone who post ina forum that prides it members as GREAT THINKERS angeweza kuliangalia hili kwaupana zaidi. Issues za kutazama hapa ni zi fuatazo:


  -Current state ya Umeme Tanzania  -Makosa yaliyofanyika wakati wa liberalisation ya sekta ya Umeme  -Role ya NSSF kwenye hili itakuwa ni ipi?  -Je NSSF wanaruhusiwa na stakeholders wao kuingia kwenye hii biashara yak u generate umeme?  -Je kuna faida yoyote itapatikana kwenda NSSF?  -Je wenzetu wan je wanafanya vipi?


  Sasa majibu ya hapa yanaweza yakatoa mwanga walau kiasi mkaelewa why I support hawa jamaa kufanya mambo kama haya.
  Umeme Tanzania:


  Tanzania mwenye jukumu la generate, transmit and distribution ya umeme zamani ilikuwa exclusively TANESCO ambayo kama mjuavyo ni shirika la umma kwa asilimia 100 na wako responsible kupply asilimia 98 ya umeme Tanzania
  Statistics zinasema hivi:

  - Megawati 381 za umeme ambao tunatumia sasa hivi unatokana na vyanzo vya maji


  -Tanzania tuna uwezo wa kuzalisha mpaka Megawatt 5,000 ya umeme


  - Per capita electricity consumption yetu ni 46/KWh per annum, ambayo inakuwa kwa asilimia 11-13 au zaidi


  Hiyo ni moja kati ya sababu serikali inataka sana secta binafsi ziingie kwenye haya mambo ya kugenerate umeme. Mind you nchi ina watu milioni 40 na ni LESS THAN 10 % wako connected kwenye umeme. Serikali yetu pamoja na madudu mengi yanayotokea huwa ni competent kwa kujua matatizo ila tatizo huwa ni kwenye namna na njia ya kuyatatua hayo matatizo.

  Ndio maana kama mnakumbuka miaka ya 90's waliamua kulegeza masharti na kufanya reform kwenye hii sekta ya nishati na kuruhusu wazalishaji binafsi na hapo ndipo walipoingia the Songas na IPTL kwa nia ya kupunguza shedding, Of course it was not without controversy za akina RUGEMALILA (the same dude aliyeingia ubia na TRITEL) na mwishowe wakapelekana mahakamani, yaani IPTL na TANESCO lakini kujua haya yote inabidi uelewe connection kati ya EastCoast Energy v/s Independent Power Tanzania Limited (IPTL) v/s Songas v/s Ministry of Energy and Minerals (Wizara ya Nishati) v/s Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) v/s Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) v/s VIP Engineering Limited (VIP), v/s (TANESCO) v/s NETGroup Solutions vs SIDASida) na bila kuwasahau waheshimiwa wa pale World Bank.  Lakini ukiachilia hao wauzaji wakubwa kulikuwa na wauzaji wengine wadogo kwa TANESCO, kama vile Tanwat (2.5 MW), Kiwira Coal Mine (6.0 MW) na bila kuwasahau Kilombero Sugar (2.5 MW) Mindhali humu kuna GREAT THINKERS nashauri mtafute Economic Recovery Program (ERP) ya 1986-1989 kati yetu na jamaa wa World Bank na IMF ndio mtaelewa kiini cha yoote haya ya reform kwenye sekta hiina zinginezo

  MAKOSA TULIYOYAFANYA:  1. POOR COORDINATION: Victim mkubwa hapa alikuwa ni ESI nah ii ilisababishwa na poor coordination. Kupitia wizara mabali mbali (jambo ambalo mpaka leo linaendelea) bilakusahau wadau na wahisani wakati uleee wa kujadili mikataba ya Songas na IPTL. Kama taifa we PAID A HEAVY PRICE. Of course itakuwa ni jambo rahisi sana kukaa hapa na kuanza mambo ya finger pointing lakini haya ndio yale yale kuwa hatutaki kutatua mambo madogo madogo kama ya COORDINATION imagine HAZINA vs NISHATI vs TANESCO vs DONORS vs EVERYONE !!!  2.POOR PRIORITIZATION: Tusijindanganye, evitable consequence of poor coordination is that power sector reforms have been neither clearly prioritized nor implemented na Serikali yetu. Mfano mdogo hatuna clear policy framework for private sector investment katika secta hii, issue skama target percentage of private generation, standard investment incentives and contractual norms kwa jili ya PPA. Bila kusahau kuwa hatuna clear and feasible roadmap for how to make the main off-taker financially and technically viable. Matokeo yake Sekta hii ya Nishati Tanzana in the last 20 years has the sector has gone from dealing with crisis after crisis (kwanza kiangazi cha miaka ya 90 then issue ya high capacity charges, na mengineyo), hii yote imepelekea kudelay of the planning and execution of fundamental reforms necessary for the long-term sustainability of power supply and expansion kwenye nchi yetu na mbaya zaidi hatujui hata priority zetu ziko wapi when it comes to alternative energy!!!! Yaani tumekuwa kama motto mkiwa asiye na baba wala mama wala ndugu wa kumtazama.
  3. FAIR AND INDEPENDENT REGULATION: Bila hii hatutofika na hakuna investor atakaye taka kuja kuinvest kwenye hiii sektaka kama hatuna transparency . Imagine kama regulator angekuwepo enzi zile IPTL na Songas wameanza it means akina Mhavile and Co wangekuwa wako bize kuzalisha umeme badala ya kushinda Mahakamani na kwingineko. Sasa hivi tunao EWURA lakini hao wamekuwa kama vile PPRA hawana nguvu zozote zile na sote tunajua no one knows or lets just say its unclear when truly independent oversight will commence. This fact may have cost the country past and present investments and may ultimately impact on future investments.  Sababu zingine ni kutokuwepo kwa uwazi kwenye UNFAIR BIDDING PROCESS, ARBITRATION , CURRENCY DEVALUATION na mengineyo bilakusahau kuwa tunashindwa kua attract makampuni ya uhakika kama TATA kwa kuwa we are not interested na pili hawa washazowe mambo ya transparency sie hayo hatutaki...!  ROLE YA NSSF


  Kwenye hili as far as I know NSSF itakuwa ni IPP yaani independent power Producer kama walivyokuwa wengine ila kazi ya distribution ni ya Tanesco hivyo kama wataleta ma generator yao au watatengeza wa Jua au upepo au Gesi toka songo songo thats up to them


  JE SHERIA INAWARUHUSU NSSF KUFANYA HIVI:

  I would imagine NSSF sio PPF so I cant see them getting involved na jambo ambalo liko kinyume au sheria haiwaruhusu kulifanya. Sina sheria Mama ya ambayo naweza ku quote lakini kama kuna IPP zaidi ya 10 Tanzania sidhani kama wameenda kinyume na sheria. Nadhani hii ipo kwenye investment policy yao so this shouldn't be an issue. Pia si vibaya mkajua kuwa shirika hili lina BOARD ambayo wao ndio wenye maamuzi ya mwisho kwenye mambo kama haya na ndani ya bodi wapo wawakilishi wa wafanyakazi sasa sidhani kama maamuzi yanaweza kufanywa na mtu mmoja

  RETURNS:

  Kama watu wa investment as far as I know ni kuwa kwa Tanzania inasemekana return ya investment kwenye umeme ni 300% sasa surely hapa naona ni win win situation kwa NSSF


  WENZETU NJE WANAFANYAJE?

  Malaysia, Philipines,Brazil,Vietnam,India, Jordan, Egypt na kwingineko Pension Funds zao wameinvest kwenye umeme na wanapata returns kubwa sana
  Btw TANESCO washankatia umeme ntarudi baadae.
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wasiwasi wangu ni dhamira ya hao watu na kitakachotokea huko mbeleni. Mambo huanza hivi baadae unasikia wameingia ubia na hao wanyonyaji viona mbali halafu unasikia wameliwa tena au wanadaiwa mabilioni na huku hela za pensioners zimeondoka. Sijasahau sakata la Manji na majengo yake!
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Why not now? If not now when?

  Daraja as far as I know in few months time contractor atakuwa site

  msimsikilize tule waziri anayeitwa POMBE alikuwa ana bwatuka tuuu bila kujua hali halisi...si mmeona kakaa kimya?
   
 20. e

  eddy28 New Member

  #20
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  NSSF Wanafanya hivi kwa shinikizo la wakuu wa nchi na s lingine lolote. Wakuu wanataka wanekane kama wanalifanyia kazi suala la umeme lakini haileti maana kwa mfuko wa pension kuingia kwenye kuzalisha na kusambaza umeme. Wastaafu wataumia saana kama mambo yasipoenda vizuri.
   
Loading...