Mengine sio kweli.
Mimi natumia Camon 12 Pro, ina ram ya 6GB na Internal Memory ya 64GB.
Kila siku naijaza simu kukopy movies, series, setup files za windows, mac os, softwares na kadhalika. Napumulia 59GB hadi 63GB na inapush speed ileile. Haiyumbi. Haijawai ganda wala kustack hata siku moja.
Nina apps 128 nimeeka kwenye simu na zinafanya kazi fresh mno, zingine sijatumia zaidi ya mwaka na fresh tuu. Nacheza games, kwa speed nzuri tuu, ndogo na za kati (DLS21, Candycrush saga, Asphalt nitro)
Na pia napakua kwa speed ya hadi 5Mbps kwa line ya halotel na kupandisha (upload) kwa speed ya hadi 3Mbps.
Nliinunua dec 2019 na mpaka leo ipo good sana.
Asa io Camon 16 Premier ndio usibonyeze. RAM GB 8 na internal Memory ya 128 GB, processing speed ya (2×2.2 Ghz na 6×2.0 Ghz) ni soo.
Bei nafuu.
Sihangaiki kununua simu jina wala sifa za kijinga, za zamani, bali nanunua simu inafanya makubwa kwa bei chee. Na nachana boksi, hata kama ni laki mbili, ila mi ndo wa kwanza kuitumia.
Acheni nikue na Tecno