johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 787
- 811
Asubuhi hii, nimebahatika kuona mjadala wa wanasiasa kupitia UTV ambapo mwenyekiti wa ngome ya vijana ya ACT wazalendo, amemvaa vilivyo naibu katibu mwenezi wa CCM Zanzibar Khamis Mobeto.
Katika mjadala huo, Mwenezi huyo wa CCM amenukuliwa akisema Tume huru ya uchaguzi itaanza baada ya uchaguzi wa 2025.
Nimevutiwa na mwongozaji wa kipindi kwa kuwaita wahusika kutoka pande zote kushiriki mada hiyo lakini pia namna watangazaji walivyokuwa na uhuru wa kuingilia na kuhoji.
Huu ni ujumbe mzuri kwa wale wengine wanaoita watu wa upande mmoja na " kutoa mahubiri" ya upande wa wasifiaji na mapambio.