NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

Uongozi wa CUF taifa kupitia kwa Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugezi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma umesema kuwa, utatoa taarifa rasmi juu ya suala hilo siku ya kesho Jumatatu, tarehe 10 Oktoba.

Kwani alikuwa anaenda kufungua akaunti yake binafsi mpaka iwe siri yake?
 
Huyo msajili wa vyama na lipumba yaan wote ni pumba tu. Tulimsikia wenyew kwenye midia anatangaza kujiuzulu.sasa wao wanamtambuaj kama mwenyekit. Na wew lipumba umeshakuwa mkubwa au sababu huna watot ndo unajion mtoto mwenyew. Acha kutumikishwa kisiasa
 
Lipunda ni propesa mwizi wait aka kuiba yeye na mutungi ili pesa zikipatikana wagawane limebuma watarukana
 
Hii 'Incidence' kama ni kweli imetokea basi haina tofauti na ile ya kufungua akaunti ya pili ya maafa wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera tena ilifanywa na viongozi halali wa Serikali..hii iansadikiwa imefanywa na matapeli wakijifanya wao eti ni viongozi wa Chama na Nchi nzima inatambua kuwa walishafukuzwa....kwa mantiki hii ni matarajio yangu kuwa tunapolizungumza swala hili mpaka sasa huyo Meneja wa tawi atakuwa ananyea debe Ukonga kama hajakamatwa basi hakuna haja ya kuwa utawala wa sheria na katika Nchi

Kivipi?
Iwapo yeye ndo aliehabarisha kwa nia njema...kwamba lipumba anampango kuiba fedha za chama unajuwaje?
 
SIRI kwamba Profesa Ibrahim Lipumba amefungua akaunti mpya yenye jina la chama cha Wananchi CUF imefichuka. Wanaolaumiwa kutokana na kufichuka kwa siri hiyo ni watumishi wa benki ya NMB tawi la Ilala.

Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.

Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa pia huku Baraza Kuu la Uongozi la CUF likiwa limemsimamisha uanachama, amenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima, akilaani kitendo cha benki ya NMB kuvujisha taarifa za akaunti mpya ya Prof. Lipumba.

“Aulizwe Meneja wa NMB Ilala, kutoa siri za wateja, hayo ndiyo maadili ya kazi yake? Uko wapi usiri kati ya mteja na benki?” alihoji Kambaya.

Hata hivyo, MwanaHALISI online ilipomtafuta Kambaya siku ya jana ili kufafanua uanzishwaji wa akaunti hiyo, matumizi yake na kama yamezingatia matakwa ya Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama Vya Siasa, hakuwa tayari kufafanua akidai kuwa si wakati muafaka.

“Tutaeleza mambo hayo kwa wakati muafaka, kama kuna jambo tunakuwa accused (tunatuhumiwa), iulizeni ofisi ya msajili au benki husika, wao wana taarifa kamili,” amesema.

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza imenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Prof. Lipumba kwa benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo amedai kuwa ofisi ya msajili haijui matumizi ya akaunti hiyo.

Taarifa za kufunguliwa kwa akaunti mpya yenye jina la CUF kwa malengo yasiyojulikana zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii Alhamis ya tarehe 06 Septemba mwaka huu.

Uongozi wa CUF taifa kupitia kwa Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugezi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma umesema kuwa, utatoa taarifa rasmi juu ya suala hilo siku ya kesho Jumatatu, tarehe 10 Oktoba.
Kila benk ina rules na procedures Za kufungua akaunti ya individual person, group, company na chama. Wanasiasa waache kuingilia taaluma Za watu. Wasilete siasa Kwenye biashara Za watu
 
Mbona wale waliofungua A/c kule Bukoba walikamatwa?

Huyu Lipumba na Mutungi kama baraka za Magufuli hapa basi wangekuwa na pingu mikononi kama wale wa Bukoba. Kwa mara nyengine hapa ndio ninapoona Unafiki wa Magufuli na TaKUKURU yake!
 
Msajili anataka kufanya money laundering kutumia pesa za ruzuku ambazo ni za umma.
Sheria ya vyama inaweka wazi kuhusu namna ya kufungua account na nani anahusika.
Hawa msajili ni wezi na lipumba. Kwa nini wamsaidie
 
watumishi wa CRDB tawi lile la Bukoba walioidhinisha kufungua akaunti feki Mkulu alisema wawajibishwe na vipi kuhusu hawa watumishi wa NMB walioshiriki kufungua akaunti feki ya CUF wanaachajwe? Huyo msajili aliyeandika barua ya utambulisho, je alijiridhisha sababu ya kufunguliwa akaunti ya pili kwa chama ambacho tayari kina akaunti? Serikali kupitia Msajili wa Vyama Vya Siasa, NMB na Polisi hawawezi kukwepa kujumuishwa kwenye hii kadhia ya CUF

Mkuu hapo huna haja ya kuzungumk mbuyu. Magufuli katoa Baraka zake kwa asilimia mia moja kutekelezwa huo uharamia! Halafu yeye anajidai kubana matumizi kumbe anafuga mijizi! Isije ikawa naye ni j..zi nambari moja?
 
Lowasa karuhusiwa lini na wapi kuwashukuru wapiga kura?

Lema aliruhusiwa afanye mkutano kwa masharti ya kutomkosoa JPM. Wenye akili wamekwisha anza kutekeleza mikakati mbadala ndani ya udikteta uchwara.

Hata hili la Lipumba wenye akili wamejipanga vizuri ataumbuka tu huyo rais wako
Jibu Kuntu!
 
Mkuu kwa sasa lipumba keshasahau alichokisoma ndiyo maana Abdalah kambaya kamwingiza kwenye Ushirikina kawa kama profesa maji marefu ndiyo maana wanafanya vioja wakiamini kuwa watawaroga watanzania wote wawaone kuwa wapo sahihi.

Walifungua hii Account ili serikali iwatumbukizie mamilioni kwa ajili ya 'Ziara' yao kule Ulaya!
 
MsemajiUkweli kuna mjadala nilikueleza kuwa Msajili ni sehemu ya mgogoro

Tulikueleza kuwa Msajili ambaye mgogoro wa UKUTA hakutueleza sheria zinazoruhusu marufuku ya mikutano 2020, ameingilia suala la CUF kwa nguvu na hamasa sana!

Tulikuambia kuwa anateuliwa na Rais wa JMT ambaye ni mwenyekiti wa CCM

Leo unaona, anaandika barua za utambulisho kwa Lipumba. Hivyo hiyo ni kazi ya Msajili?

Real, kwamba msajili sasa anasimamia uanzishwaji wa account za vyama!!

Bado mkuu huamini hakuna mgogoro, bali kuna kitu kinatengenezwa! ushahidi
 
Mkuu kujadiliana na huyo 'msemaji ukweli' itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gita! kwani kwake yeye nyeusi huwa ni nyeupe na nyeupe huwa ni nyeusi! alimradi yeye ni anahakikisha ya kwamba anakula yale makombo yaliyobakia kwenye meza kubwa!
 
Na wizi wake huu anaoutaka kuufanya umebarikiwa na Mwenyekiti wa MACCM mtakatifu wa Ikulu bila woga hata aibu ya kuruhusu uharamia huu ufanywe na mtu ambaye ameshafukuzwa uanachama CUF.

Kuficha taarifa ya mwizi ni kosa kisheria ila kufichua taarifa ya mwizi sio kosa kisheria ni ushujaa lipumba ni mwizi kama wezi wengine tu...
 
Na wizi wake huu anaoutaka kuufanya umebarikiwa na Mwenyekiti wa MACCM mtakatifu wa Ikulu bila woga hata aibu ya kuruhusu uharamia huu ufanywe na mtu ambaye ameshafukuzwa uanachama CUF.
Madalali wa siasa wa CCM wamelikamata vyema hilo Dili na wanajua mkulu anapenda kuona Ukawa ina sambaratika kabla ya 2020 hivyo wapo busy kubuni mbinu za kumchochea kila siku aendelee kutoa pesa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
MsemajiUkweli kuna mjadala nilikueleza kuwa Msajili ni sehemu ya mgogoro

Tulikueleza kuwa Msajili ambaye mgogoro wa UKUTA hakutueleza sheria zinazoruhusu marufuku ya mikutano 2020, ameingilia suala la CUF kwa nguvu na hamasa sana!

Tulikuambia kuwa anateuliwa na Rais wa JMT ambaye ni mwenyekiti wa CCM

Leo unaona, anaandika barua za utambulisho kwa Lipumba. Hivyo hiyo ni kazi ya Msajili?

Real, kwamba msajili sasa anasimamia uanzishwaji wa account za vyama!!

Bado mkuu huamini hakuna mgogoro, bali kuna kitu kinatengenezwa! ushahidi
msajili kala Dili na lipumba watafune pesa za CUF kwa kugawana pindi wakifanikiwa kuwapora CUF olijino ni Aina fulani ya ufisadi ambao wanjanja wanakula pesa za umma kwa njia haramu huku mkulu akiamini itamsaidia kudhoofisha ukawa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom