NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
SIRI kwamba Profesa Ibrahim Lipumba amefungua akaunti mpya yenye jina la chama cha Wananchi CUF imefichuka. Wanaolaumiwa kutokana na kufichuka kwa siri hiyo ni watumishi wa benki ya NMB tawi la Ilala.

Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.

Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa pia huku Baraza Kuu la Uongozi la CUF likiwa limemsimamisha uanachama, amenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima, akilaani kitendo cha benki ya NMB kuvujisha taarifa za akaunti mpya ya Prof. Lipumba.

“Aulizwe Meneja wa NMB Ilala, kutoa siri za wateja, hayo ndiyo maadili ya kazi yake? Uko wapi usiri kati ya mteja na benki?” alihoji Kambaya.

Hata hivyo, MwanaHALISI online ilipomtafuta Kambaya siku ya jana ili kufafanua uanzishwaji wa akaunti hiyo, matumizi yake na kama yamezingatia matakwa ya Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama Vya Siasa, hakuwa tayari kufafanua akidai kuwa si wakati muafaka.

“Tutaeleza mambo hayo kwa wakati muafaka, kama kuna jambo tunakuwa accused (tunatuhumiwa), iulizeni ofisi ya msajili au benki husika, wao wana taarifa kamili,” amesema.

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza imenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Prof. Lipumba kwa benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo amedai kuwa ofisi ya msajili haijui matumizi ya akaunti hiyo.

Taarifa za kufunguliwa kwa akaunti mpya yenye jina la CUF kwa malengo yasiyojulikana zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii Alhamis ya tarehe 06 Septemba mwaka huu.

Uongozi wa CUF taifa kupitia kwa Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugezi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma umesema kuwa, utatoa taarifa rasmi juu ya suala hilo siku ya kesho Jumatatu, tarehe 10 Oktoba.
 
Kwani sio mwenyekiti wakweli maana umekuwa lawama kubwa ati Nani katoa siri
 
Hii 'Incidence' kama ni kweli imetokea basi haina tofauti na ile ya kufungua akaunti ya pili ya maafa wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera tena ilifanywa na viongozi halali wa Serikali..hii iansadikiwa imefanywa na matapeli wakijifanya wao eti ni viongozi wa Chama na Nchi nzima inatambua kuwa walishafukuzwa....kwa mantiki hii ni matarajio yangu kuwa tunapolizungumza swala hili mpaka sasa huyo Meneja wa tawi atakuwa ananyea debe Ukonga kama hajakamatwa basi hakuna haja ya kuwa utawala wa sheria na katika Nchi
 
Back
Top Bottom