NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

Huyu Lipumba na Mutungi kama baraka za Magufuli hapa basi wangekuwa na pingu mikononi kama wale wa Bukoba. Kwa mara nyengine hapa ndio ninapoona Unafiki wa Magufuli na TaKUKURU yake!
Msajili hata akisema leo hii anaifuta CUF lazima mkulu atamwongeza cheo pengine anaweza kuwa jaji mkuu kwa sasa mkulu amependezewa na style mpya ya kuidhoofisha CUF na ukawa kwa ujumla anajua ruzuku ikipindishwa tu lazima vurugu kubwa itaibuka na ndipo watapata sababu ya kuifuta CUF pindi lipumba akiwa tayari kachukua pesa zote wamegawana na msajili na Madalali wa siasa.
 
Mkuu hapo huna haja ya kuzungumk mbuyu. Magufuli katoa Baraka zake kwa asilimia mia moja kutekelezwa huo uharamia! Halafu yeye anajidai kubana matumizi kumbe anafuga mijizi! Isije ikawa naye ni j..zi nambari moja?
Kumbuka Escrow ndiyo imemuweka madarakani. Huwezi kutumbua majibu wakati mwenyewe umenona usaha.
 
"Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama".

Nikisoma tu hii aya nabaki kucheka. [emoji23]
 
MsemajiUkweli kuna mjadala nilikueleza kuwa Msajili ni sehemu ya mgogoro

Tulikueleza kuwa Msajili ambaye mgogoro wa UKUTA hakutueleza sheria zinazoruhusu marufuku ya mikutano 2020, ameingilia suala la CUF kwa nguvu na hamasa sana!

Tulikuambia kuwa anateuliwa na Rais wa JMT ambaye ni mwenyekiti wa CCM

Leo unaona, anaandika barua za utambulisho kwa Lipumba. Hivyo hiyo ni kazi ya Msajili?

Real, kwamba msajili sasa anasimamia uanzishwaji wa account za vyama!!

Bado mkuu huamini hakuna mgogoro, bali kuna kitu kinatengenezwa! ushahidi
Mkuu Nguruvi3

Una maana gani unaposema kwa sababu Msajiri wa vyama vya siasa ameteuliwa na Rais basi atafanya kazi za Rais.

Kwa hiyo unataka kusema Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi taifa, James Mbatia alipoteuliwa na Rais kuwa Mbunge alikuwa anafanya kazi za Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM?

Kuhusu kufungua akaunti; Kwani taratibu za kufungua akaunti ya chama cha siasa ziko vipi?

Unafahamu kwa nini Prof. Lipumba ilibidi apeleke barua kutoka kwa msajiri wa vyama vya siasa.

Huoni labda inawezekana benki ilimtaka afanye hivyo kutokana na uwepo wa akaunti nyingine ya chama cha CUF au kutokana na mgogoro uliopo ndani ya CUF?

Jaribu kuliangalia hili suala kwa upana zaidi.
 
Akunti inafunguliwa na bodi ya wadhamini.

Bodi ya wadhamini ndiyo yenye chama.

Msajili anahusika vipi na kufungua akaunti za vyama?
 
sasa hapo kuna siri gani? anaelewa contractual relatioship btw a banker and customer? mimi pia naitaka kuijua hiyo namba yao niwatumie mchango wa kuendesha chama maana sijui watapata lini ruzuku. Basi na akaunti ya maafa inayotangazwa ni kosa pia. Kama vp hao benki waiweke wazi ili wanachama wapeleke michango kirahisi. kama ina jina la leprofesei hiyo wabakin ayo tu.
 
SIRI kwamba Profesa Ibrahim Lipumba amefungua akaunti mpya yenye jina la chama cha Wananchi CUF imefichuka. Wanaolaumiwa kutokana na kufichuka kwa siri hiyo ni watumishi wa benki ya NMB tawi la Ilala.

Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.

Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa pia huku Baraza Kuu la Uongozi la CUF likiwa limemsimamisha uanachama, amenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima, akilaani kitendo cha benki ya NMB kuvujisha taarifa za akaunti mpya ya Prof. Lipumba.

“Aulizwe Meneja wa NMB Ilala, kutoa siri za wateja, hayo ndiyo maadili ya kazi yake? Uko wapi usiri kati ya mteja na benki?” alihoji Kambaya.

Hata hivyo, MwanaHALISI online ilipomtafuta Kambaya siku ya jana ili kufafanua uanzishwaji wa akaunti hiyo, matumizi yake na kama yamezingatia matakwa ya Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama Vya Siasa, hakuwa tayari kufafanua akidai kuwa si wakati muafaka.

“Tutaeleza mambo hayo kwa wakati muafaka, kama kuna jambo tunakuwa accused (tunatuhumiwa), iulizeni ofisi ya msajili au benki husika, wao wana taarifa kamili,” amesema.

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza imenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Prof. Lipumba kwa benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo amedai kuwa ofisi ya msajili haijui matumizi ya akaunti hiyo.

Taarifa za kufunguliwa kwa akaunti mpya yenye jina la CUF kwa malengo yasiyojulikana zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii Alhamis ya tarehe 06 Septemba mwaka huu.

Uongozi wa CUF taifa kupitia kwa Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugezi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma umesema kuwa, utatoa taarifa rasmi juu ya suala hilo siku ya kesho Jumatatu, tarehe 10 Oktoba.
huko benki alipoenda inamaana hakukuwa na wateja wengine? kwanza kwa sasa yeye kujulikana anaenda benki anahatarisha pia usalama wa wateja wngine pamoja na benki yenyewe.
 
Akunti inafunguliwa na bodi ya wahdamini. Bodi ya wadhamini ndiyo yenye chama. Msajili anahusika vipi na kufungua akaunti za vyama?
Bodi ya wadhamini inapeleka documents gani ili akaunti ifunguliwe?

Je, kwenye mazingira kama haya ya mtafaruku ndani ya CUF, unategemea taasisi za fedha kama benki zitahitaji documents gani katika kupata ushahidi kama wale wameenda kufungua akaunti ya chama wanatambuliwa kisheria na taasisi za serikali kama ni viongozi wa vyama.
 
Ndio maana utashangaa unatoka bank dak mbl unatekwa na majambaz, unajiulza wanajuaje?
 
Mkuu Nguruvi3

Una maana gani unaposema kwa sababu Msajiri wa vyama vya siasa ameteuliwa na Rais basi atafanya kazi za Rais.

Kwa hiyo unataka kusema Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi taifa, James Mbatia alipoteuliwa na Rais kuwa Mbunge alikuwa anafanya kazi za Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM?

Kuhusu kufungua akaunti; Kwani taratibu za kufungua akaunti ya chama cha siasa ziko vipi?

Unafahamu kwa nini Prof. Lipumba ilibidi apeleke barua kutoka kwa msajiri wa vyama vya siasa.

Huoni labda inawezekana benki ilimtaka afanye hivyo kutokana na uwepo wa akaunti nyingine ya chama cha CUF au kutokana na mgogoro uliopo ndani ya CUF?

Jaribu kuliangalia hili suala kwa upana zaidi.
Hapa msemaji ukweli unatakiwa uangalie sheria inasemaje kishautajua nani yupo nje na aliye ndani ni nani.Inahitaji umakini kuliona kosa la Lee Pumba.
 
Bodi ya wadhamini inapeleka documents gani ili akaunti ifunguliwe?

Je, kwenye mazingira kama haya ya mtafaruku ndani ya CUF, unategemea taasisi za fedha kama benki zitahitaji documents gani katika kupata ushahidi kama wale wameenda kufungua akaunti ya chama wanatambuliwa kisheria na taasisi za serikali kama ni viongozi wa vyama.
Na katika mtafaruku huu lipumba anatambuliwaje?Vice-versa is true.
 
Msajiri tena jaji kushiriki kwenye sarakasi kama hizi ni kuishusha hadhi ya ujaji, Ni vizuri ukajitafakari vzur.
 
Hapa msemaji ukweli unatakiwa uangalie sheria inasemaje kishautajua nani yupo nje na aliye ndani ni nani.Inahitaji umakini kuliona kosa la Lee Pumba.
Mkuu Cham Bee

Sheria unayobainisha kwa sasa inabishaniwa na kwa sababu hiyo ndio maana mahakama imewaomba wapeleke malalamiko yao ili mahakama itoe tafsiri ya kisheria.

Nadhani hakuna maana sana ya kujadili sheria kwa sababu mahakama ipo mbioni kutoa tafsiri.

Kabla ya mahakama haijatoa tafsiri, Prof. Lipumba ataendelea kutambuliwa na Msajiri wa vyama vya siasa.
 
Ni sawa ataendelea kutambuliwa na msajili.Lakini suala la kufungua akaunti ya chama lipo katika upande wake au vipi?Anatambuliwa na msajili kama mwenyekiti sikatai.NMB inamtambua kama nani ili iweze kumkubalia kufungua account mpya ya chama?
 
Ninaamini NMB wana utaratibu wao wa kufungua akaunti ambao utakuwa unafanana au haufanani na benki zingine.

Siwezi kufahamu NMB watamtambua kama nani wakati kuna mgogoro ndani ya CUF. Hata hivyo ninaamini kama NMB watataka kufahamu Prof. Lipumba ni nani itawabidi waulize vyombo vya serikali ili kupata ukweli.
 
Ndio maana mpango wake umekwama.
 
Huu sio wizi, ni kwamba akaunti za chama zilizopo zinasimamiwa na katibu mkuu ambaye ni hasimu wake kwa sasa, inambidi afungue nyingine atakayoweza kuitumia. zile za zamani zote hana uwezo wa kuzitumia maana zipo chini ya katibu mkuu.
Mtu asiyekuwa kiongozi wala mwanachama wa chama husika anawezaje kufungua akaunti kwa jina la chama kwa utambulisho wa msajili wa vyama...ambaye ni kada wa CCM? Huoni kwamba huo ni uchochezi wa wazi?
 
Back
Top Bottom