NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

NMB yalaumiwa kutoa siri ya Lipumba

Acha aendelee kuumbuka kama hataacha chokochoko ataumbuka zaidi. Acheni Mungu aitwe Mungu.
 
Bodi ya wadhamini inapeleka documents gani ili akaunti ifunguliwe?

Je, kwenye mazingira kama haya ya mtafaruku ndani ya CUF, unategemea taasisi za fedha kama benki zitahitaji documents gani katika kupata ushahidi kama wale wameenda kufungua akaunti ya chama wanatambuliwa kisheria na taasisi za serikali kama ni viongozi wa vyama.
Mabenki yanatakiwa kuwasiliana na right organ, I mean bodi ya wadhamini.

Kama benki inaona kuna mtafaruku busara ni kuacha kufungua account hadi tatizo litakapokwisha.

Labda unieleze kidogo, ni chama gani kingine kilifungua account kwa kutumia msajili wa vyama?
Inawezekana ni utaratibu wa kawaida ndiyo maana naomba unifahamishe kwa mapungufu yangu

Hivi Lowassa angeenda kufungua account ni benki gani ingemkubalia?

Mkuu lazima tukubali jambo moja, msajili ameingilia hili jambo kwa hali isiyofahamika

Huu mgogoro wa Lipumba na CUF mbona upo wazi?

Lakini tukirudi nyuma kidogo, mgogoro wa Chadema na Serikali kuhusu UKAWA, msajili hakuonekana 'kusimamia' kama anayofanya sasa.

Hakuwahi kutueleza marufuku ya mikutano hadi 2020 yapo katika sheria gani ya msajili wa vyama?

Kilichonishtua Zaidi ni pale aliposhirikisha baraza la vyama vya siasa ambalo sasa halishirikishi bali ana act independently. Hizi naona ni double standards ambazo zinazua minong'ono

Huu mgogoro wa Lipumba na CUF aache usishe kwa njia za mhakama au chama.

Vinginevyo wanaohisi kuwa lipo jingine, wapo watu nyuma watapata hoja rahisi hata kama si kweli

Ukisoma barua ya CUF waliyomwandikia, CUF walionyesha wasi wasi kuhusu nafasi yake

Moja linalotakiwa kufafanuliwa ni hili la kufungua account.

Wananchi wapewe ufafanunuzi tu kuhusu mamlaka yake kwa hili, CUF washuhulikie mgogoro wao, wakimaliza wamtaarifu msajili.
 
Hawa dola nao ya nini kuhangaika na CUF ambayo naona haina madhara kwenye utawala wetu, hapa ilibidi wale sahani moja na peoples ili wasambaratike tuendeshe nchi kwa utulivu. Sijui wanawashindwa wapi hao CHADEMA
 
Mbona wakiomba misaada wanaweka details za akaunti hadharani?? Iweje taarifa za kufungua akaunti ziwe siri??
 
Back
Top Bottom